Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Arise and Shine Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

 1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 3. Jibu maswali manne pekee
 4. Swali la kwanza ni la lazima
 5. Maswali hayo mengine yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki: yaani: tamthilia, Hadithi fupi, Ushairi na fasihi simulizi.
 6. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 7. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
 8. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Kwa Matumizi ya Mtahini Pekee

Swali

Upeo

Alama

1

20

 

 

20

 

 

20

 

 

20

 

Jumla

80

 

MASWALI

SEHEMU YA A: USHAIRI
Swali la Lazima

 1. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata:

  MKWARUZANO WA NDIMI

  Huyo! Mshike huyo!
  Hakuna bunduki wala kifani
  Bomu na risasi hata hawazijui
  Lakini mno wanashambuliana
  Kwa ndimi zilizonolewa kwa makali
  Vipande vya matusi silaha zao.

  Yu imara mmoja wao
  Akirusha kombora la neno zito!
  Limtingishe adui wake
  Na kumgusa hisia kwa pigo kuu
  Pigo linalochoma moyoni kama kichomi
  Kuchipuza joto la hasira na kisasi
  Katika mapigano yaso na kikomo

  Filimbi ya suluhu inapulizwa kuwaamua!
  Nani anayekubali suluhu?
  Roho zinakataa katakata
  Huku ukaidi ukinyemelea na kutawala kote
  Mapandikizi ya watu yakipigana
  Vita shadidi visivyo ukomo
  Vita vya ndimi!

  Magharibi sasa
  Jua linapungia mkono machweo
  Nalo giza likinyemelea kwa kiburi na kasi
  Sisikii tena sauti za misonyo
  Mate ya watesi yamekauka
  Makanwa yao yamelemewa na uchovu
  Sasa wameshikana mikono
  Ishara ya suluhu.

  Maswali

  1. Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. (alama 2)
  2. Eleza dhamira ya mshairi. (alama 2)
  3. Eleza kanuni za utunzi alizotumia mshairi. (alama 4)
  4. Fafanua mbinu zozote mbili za lugha katika ubeti wa mwisho wa shairi. (alama 2)
  5. Jadili toni ya mshairi katika beti tatu za awali. (alama 2)
  6. Tambua matumizi ya mistari mishata na utoe mifano miwili. (alama 2)
  7. Andika mishororo ya kwanza mitatu katika ubeti wa 4 kwa lugha ya nathari. (alama 3)
  8. Eleza athari tatu za vita vya ndimi (alama 3)

SEHEMU YA B: RIWAYA
CHOZI LA HERI - ASSUMPTA K. MATEI

Jibu swali la 2 au 3

 1. "Haiwezekani! Hili haliwezekani! Itakuwa kama kile kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike"
  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Eleza mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili. (alama 4)
  3. Jadili athari na dhiki zinazotokana na uongozi mbaya (alama 12)
 2.                      
  1. Changanua mtindo katika dondoo hili (alama 10)
   “Hawajui linalompa mama kutaka kujitoa roho huku akijua kwamba anawaacha wana wakiwa wawili. Hawajui, hawajui Kabisa. Na watajuaje na lao ni kushika zamu tu, kumlazimisha muwele huyu kumeza vidonge vichungu vya dawa, kufunga bendeji donda hili, kutia kitata mkono huo uliovunjika, kutazama zebaki ya kipima joto ikipanda na kushuka, kukishika kitoto kijoga viguu kidungwe, sindano, kuwatazama binadamu wenzao na kutoa jasho kupambana na Iziraili anapokuja kubwakura nafsi zao, na hatimaye kuwafunika shuka nyeupe waliotokwa na roho zao?"
  2. "Mabibi na mabwana," alianza Apondi," suala la usalama haliwezi tena kupuuzwa." Eleza mtazamo wa msemaji kuhusu suala la usalama kwa kurejelea hotuba yake. (alama 10)
 3. "Ama kweli, dunia gunia. Ilikumeza hindi bichi ikakuguguna, sasa inakutema guguta.
  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
  2. Eleza mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili (alama 4)
  3. Masaibu yanayowakumba wahusika katika Tamthilia ya Kigogo ni zao la matendo yao ya awali. Fafanua kauli hii kwa kutolea mifano mwafaka. (alama 4)
 4. Kwa Kurejela Tamthilia ya Kigogo, Jadili mbinuishi unazojifunza kutokana na Tunu. (alama 12)
 5. Huku ukirjelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki (alama 20)
 6. Mtihani wa Maisha na Eunice Kimal “…Leo mwalimu mkuu atajua kwamba madharau bihubiuka”
  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Fafanua tamathali' ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Eleza sifa za msemaji. (alama 6)
  4. Jadili maudhui ya elimu kama yanavyojitokeza katika hadithi hii. (alama 8)
 7.                    
  1. Nyumbani kuna kichuguu chenye. mashimo manne ambapo jogoo wetu hupenda kwenda kutagia mayai. Je, atagapo hayo mayai huanguka kwenye mashimo mangapi?
   1. ambua kipera hiki. (alama 1)
   2. Taja sifa nne za kipera hiki (alama 4)
   3. Eleza majukumu manne ya kipera hiki (alama 4)
   4. Kwa kutolea ithibati, tája shughuli yoyote ya kiuchumi inayotekelezwa na jamii inayorejelewa katika kipera hiki. (alama 1)
  2.                        
   1. Onyesha kwa hoja sita namna fanani wa maigizo anavyoweza kufanikisha uwasilishaji wake. (alama 6)
   2. Eleza njia zinazotumiwa na kizazi cha sasa kuendeleza utanzu huu wa maigizo. (alama 4)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.                          
  1. Shairi huru kwa sababu halina urari wa vina wala mizani. (alama 2)
  2. Kuonyesha jinsi kugombana ni kubaya na wagombanao huchoka na wakapatana
  3.                          
   1. Matumizi ya mshororo toshelezi na mshata
   2. Matumizi ya beti
   3. Matumizi ya mishororo
   4. Matumizi ya lugha ya mkato
   5. Matumizi ya mbinu za kishairi-yaso (inkisari) zozote 4 (alama 4)
  4. Tashihisi
   • Jua linapungia mkono machweo
   • Nalo giza likinyemelea kwa kiburina
    Takriri - sasa
    (alama 2)
  5. Toni ya kukerwa anaonyesha kuchukizwa na tabia ya kugombana kwa matusi (alama 2)
  6. Mapandikizi ya watu yakipigana
   Yu imara mmoja wao
   Lakini mno wanashambuliana
   Nalo giza likinyemelea kwa kiburi na (alama 2)
  7. Wakati wa jioni umefika. Jua linazama kwani ni wakati wa machweo. Giza linaingia kwa kishindo kikubwa. (3x1) (alama 3)
  8.                        
   1. Vinamtingiza adui (alama 3)
   2. Vinagusa hisia
   3. Vinachipuza joto la hasira na kisasi za kwaza 31=3
   4. Vinachochea mapigano yasiyo na kikomo
 2.                            
  1. Msemaji: Kaizari/ akirudia maneno ya Tetei
   Msemewa: Ridhaa
   Mahali: Kambini
   Sababu: Anasimulia kuhusu migogoro iliyotokea baada ya uchaguzi. Tetei hakupenda mwekevu kuchukua ule wadhifa wa uongozi. (4 X 1 =4)
  2. nidaa-haiwezekani! Kutaja 1 (2 X 2 = 4)
   Tashbihi - Itakuwa kama kile kisa mfan0 1
  3. (i) Hueneza uhasama uk 21
  4. Viongozi kulia machozi ya mamba kuonyesha jinsi wanavyowajali maskini
  5. Kunyakua mashamba ya walalahoi uk 22
  6. Viongozi kupokea milungula kwa mabwenyenye waliokuwa wamejenga sehemu zilizotengewa barabara uko Tononokeni uk 13
  7. Kutoona ripoti za uchunguzi wa mashamba ya walalahoi
  8. Tume za uchunguzi ambazo haziwajibiki.
  9. Wizara ya ardhi kupeana hati miliki ghushi baada ya kuuza shamba mara ya pili
  10. Viongozi katika hospitali za umma wanachukua dawa na kupeleka katika hospitali zao za kibinafsi
  11. Watoto wa matajiri wanapewa mikopo ya elimu iliyokuwa imetengewa watoto wa maskini
  12. Viongozi katika forodha wanapokea rushwa kuruhusu ulanguzi wa dawa za kulevya uk123
  13. Viongozi wanashindwa kuwapa vijana kazi baada ya masomo. Shamsi analalamika kwa kutopata ajira licha ya kupata shahada akiwa wa kwanza katika kijiji chao
  14. Viongozi wananyakua mali ya walalahoi huko msitu wa mamba bila kuwafidia kwa mfano Lunga
  15. Vijana saba wanakufa kwa mtutu wa bunduki kwa kutetea haki yao uk 24
  16. Wazungu walipoingia walinyakua mashamba yaliyotoa mazao mengi na kuchukua waafrika kuwa wafanyikazi wao.
   zozote 6x2=12
   Mwanafunzi athibitishe hoja zake kwa kutolea mifano katika riwaya ili atuzwe.
 3.                              
  1.                        
   1. Takriri – Hawajui
   2. Nahau/msemo - Kujitoa roho
    - Kushika zamu
   3. Uzungumzi nafsia – msemaji (pete) anajizungumzia
   4. Utohozi – bendeji
   5. Taswira Oni - Kutazama zebaki ya kipima joto.
    Taswira mwendo – anapokuja.
    Taswira mguso - kukishika kitoto kijoga viguu
   6. Tanakuzi - ikipanda na kushuka
   7. Balagha - na hatimaye kuwafunika kwa shuka nyeupe waliotekwa na roho zao?
    5x2 = 10
  2.                        
   1. Usalama mojawapo ya mahitaji ya kimsingi.
   2. Kila mja ana jukumu la kudumisha usalama.
   3. Polisi na wanajeshi wana jukumu kubwa zaidi la kudumisha usalama na amani.
   4. Polisi na wanajeshi wana ujuzi wa njia mwafaka za kutatua migogoro njia kupalilia maridhiano.
   5. Katahadhari kuhusu mauaji ya kiholela ya raia.
   6. Anawaonya walinda usalama dhidi ya kutaahiri kufika pahali palipotokea mkasa.
   7. Usalama hauji bila ya kujitolea mhanga na kujiaza dhidi ya njama za kifisadi na nyendo nyingine hasi.
   8. Mhalifu ana haki ya kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kabla hajapewa adhabu yoyote. 5x2=10
 4.                        
  1.                            
   • Msemaj ni majoka
   • msemewa ni Ashua
   • walikuwa katika ofisi ya Majoka.
   • Majoka alikuwa akimdhihaki Ashua kutokana na matatizo aliyopata kwa kutompenda. 4x1 = 4
  2. Taswira: Sasa inakutema guguta; dunia gunia
   • Tashihisi: Dunia ya kumeza
   • Kejeli/dhihaka: Majoka anamdhihaki Ashua kwa kutompenda.
    Zozote 2x2 = 4
  3.                    
   • Majoka anamuua Jabali kupitia ajali. Tunu anataka kuwaleta wachunguzi wa nje ili kuchunguza ajali hiyo hali inayomtia wasiwasi.
   • Majoka analifunga soko la Chapakazi, hali inayowachochea raia kuandamana na kumngatua mamlakani.
   • Ngao junior anatumia mihadarati, hatimaye inamuua kwenye uwanja wa ndege.
   • Majoka anawaruhusu wanafunzi katika shule yake kudungana dawa za kulevya, hivyo kuwasababisha wote kuanguka mtihani/ kuwa makabeji.
   • Boza anamruhusu Ngurumo kuuza pombe na mkewe mamapima, hatimaye Ngurumo anajihusisha kimapenzi naye.
   • Ngurumo anaunga mkono uongozi wa Majoka lakini uongozi huo unakuja kumuua hatimaye. Anauliwa na kundi la watu analolitumia Majoka kuwaua wapinzani wake.
   • Hali ya mumewe Bi. Hashima kutokuwa na bima karibu ifanye familia yake ikose fidia kutoka kwa Majoka alipokufa akifanya kazi katika kampuni yake.
   • Majoka ana Kampuni kubwa zaidi inayozalisha dawa za kulevya ambazo zinakuja kumuua mwanawe Ngao Junior.
   • Kitendo cha Husda kutokuwa na mapenzi ya dhati kwa mumewe Majoka kinamfanya kuaibishwa na Majoka hadharani kwamba hampendi.
   • Majoka anafungulia biashara ya kukata miti, hali inayotishia mvua kutonyesha jimboni, hivyo kuathiri maisha ya raia.
   • Majoka anampa Mamapima kibali cha kuuza pombe haramu ambayo hatimaye inawaua na kuwapofusha raia.
   • Мајока anawaua raia wengi, hali inayomsababisha kujiona akiwa amefungwa mikono kwa minyororo ndani ya ziwa la damu anapozirai.
   • Chopi anakubali kutumiwa na Majoka kuwaua wapinzani wake kama Tunu lakini naye anapokosa kumuua Tunn alivyoagizwa, Majoka anaanza kupanga mauaji yake.
   • Kombe anaunga mkono mrengo wa Majoka unaowadhulumu raia badala ya kumpinga. Majoka anaanza kusambaza vijikaratasi vinavyolitaka kabila lake Kombe kuhama Sagamoyo kwa madai kuwa si kwao.
   • Wafanyibiashara kama vile Kombe na Boza walihamia ulevini Majoka alipofunga Soko badala ya kushirikiana na raia wengine katika maandamano in kuupinga udhalimu huo, hali inayomsababiaha Majoka kudinda kulifunga soko.
    Zozote 6x2 = 12
 5. Kwa kurejelea tamthilia ya Kigogo, jadili mbinu- ishi unazojifunza kutokana na Tunu.
  Mbinu-ishi ni mikakati ya kukabiliana na hali ngumu za maisha.
  1. Ujasiri. Majoka amapotaka kumuoza kwa mwanawe Ngao Junior, Tunu anajijasirisha na kumwambia kwamba hawezi kuolewa katika familia ya wahuni.
  2. Kujidhibiti. Licha ya kutembea na Sudi ambaye ameoa hakuvuka mpaka wa uhusiano wao na kuwa mpenziwe jinsi mkewe Sudi alivyokuwa akidhani. Lao lilikuwa ni kutetea haki za wanyonge.
  3. Bidii. Alijibiidisha katika harakati zake za kuwapigania raia. Licha ya kutembea kwa kiti c magurudumu, aliwatembelea hata walevi na kuwaomba kuhudhuria mkutano ambao ungefanyika katika soko la Chapakazi.
  4. Msimamo thabiti - Majoka anamshawishi kumuoza kwa mwanawe lakini anakataa katakata kumjibu kuwa atasubiri ili aolewe na mwanume ampendaye.
  5. Mbinu za kushawishi - anapotembelea walevi kule Mangweni anawashawishi kuacha kun pombe kwa kuwaeleza madhara yake - anawaambia kwamba ilikuwa imewaua na kuwapofusha wengi.
  6. Ushirikiano. - anashirikiana na Sudi na raia wengine katika kupinga kufungwa kwa soko Hali inayosababisha kung'atuliwa mamlakani kwa Majoka.
  7. Ustahimilivu licha ya kupigwa na kuumizwa mguu na kumbidi kutembea kwa magongo kwa miezi mitatu, Tunu anavumilia masaibu haya yote na kuendelea kupinga kufungwa kwa soko.
  8. Kutokata tamaa- licha ya kupigwa na wahuni na kuumizwa mfupa wa muundi, hakukata tamaa katika harakati zake za kupigania haki za raia wanyonge.
  9. Kutolipiza kisasi- licha ya kufahamu kwamba Ngurumo alihusika katika kumshambulia na kumvunja mfupa wa muudi, hakulipiza kisasi.
  10. Kusoma - Majoka alipowadhulumu kwa kutaka kuwanyima fidia baada ya kifo cha babake kwa madai kwamba hawakuwa na bima, Tunu aliamua kusomea uanasheria ili kuwasaidia wengine.
  11. Kujitolea. Alipofuzu masomo ya chuo kikuu, aliapa kujitolea kupigania haki za wanasagamoyo hata kama ni kwa pumzi zake za mwisho.
  12. Usemehevu - mamapima anapoacha kupika pombe haramu na kuendelea kwake kuomba msamaha, anamwambia kwamba yeye hana kinyongo naye.
  13. Uzalendo - umuhimu wa uzalendo katika jamii hasa vijana.
  14. Huruma-kuwahurumia wana wa Sudi, Pendo na Pili. Kuwahurumia walevi.
  15. Kujithamini - anakataaa kuolewa na Ngao Junior.
  16. Busara - ni muhimu kuwa na busara maishani. Inamwezesha kusoma hadi chuo kikuu.
  17. Mwadilifu - ni vizuri kuwa na maadili- hapendi ulevi licha ya kufuatiana na Sudi kila mara, hawana uhusiano wa kimapenzi.
  18. Mshauri mwema- anaowashauri Ngurumo na walevi wenzake dhidi ya matumizi mabaya.
  19. Shukrani - kumshukuru Siti kwa kuwa alikuja kumjulia hali. Anamshukuru kwa kukubali kuwalinda wananchi badala ya kuwatawanya kama walivyofanya awali.
  20. Utambuzi - alitambua sauti ya mmoja wa majangili waliomvamia. (zozote 10 X 2 = 20)
 6. Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki. (al.20)

TUMBO LISILOSHIBA.

 1. Viongozi kuweka vitego na vikwazo vya sheria ili watu wadogo wasiweze kutetea mali zao.
 2. Kutowahusisha maskini katika maamuzi muhimu yanayoathiri maisha yao.
 3. Kunyakua ardhi ya madongoporomoka ambapo watu maskini waliishi.
 4. Kupanga njama za kuwapatia wanyonge visenti vichache ili waondoke madongoporomoka.
 5. Jitu la miraba minne kula chakula chote bila kubakishia wateja.
 6. Wanamadongoporomoka kubomolewa vibanda vyao na mabuldoza.
 7.  Askari wa baraza kutimua watu waliokuwa wanabomolewa.
 8. Jeshi la polisi kulinda askari wa baraza wakibomoa vibanda vya wanamadongoporomoka.
 9. Askari kuwapiga virungu watu.
  Zozote 5 X 2 = 10

SHIBE INATUMALIZA.

 1. Mzee mambo kulipwa kwa vyeo viwili alivyovifanyia kazi.
 2. Waajiriwa kwenda kazini na kukosa kufanya kazi.
 3. Viongozi kuibia wananchi kwa kujipakulia mshahara
 4. Waajiriwa wawili kufanya kazi moja-Sasa na Mbura ni mawaziri wa wizara moja.
 5. Mzee Mambo kuandaa sherehe ya kuingiza watoto nasari kwa kutumia pesa za umma.
 6. Mzee Mambo kuandaa sherehe kwa kutumia rasilmali za nchi.
 7. Sasa na Mbura kula vyakula vyao na vya wenzao.
  Zozote 5 X 2 = 10

7. 

 1.                                  
  1. Ni maneno ya Samueli
  2. Samueli anajizungumzia.
  3. Yuko ofisini mwa mwalimu mkuu.
  4. Amekuja kuchukua matokeo ya mtihani. 4x1 = 4
 2. Methali- Mdharau bihubiuka.
  Kinaya - Ni Samueli aliyeaibika si mwalimu mkuu. Taja -1 1x2 = 2
  Mfano - 1
 3.                                
  1. Ni mwongo – Anadanganya Nina kuwa ni mwerevu shuleni.
  2. Ni mwoga – Anamhofu babake.
  3. Mwenye kukata tama – Anataka kujiua
  4. Mzembe – Hasomi kwa bidii shuleni
  5. Mjinga - Hajui maswala kijiografia na Historia. Zozote 4x1=4
 4.                                  
  1. Babake Sumueli anauza mali yake ili asomeshe watoto.
  2. Babake Samueli anathamini masomo ya Samueli kuliko dada zake.
  3. Samueli anatembea kilomita sita ili atafute elimu
  4. Samueli anaogopa kuzungumza na babake kuhusu matokeo yake.
  5. Mwalimu mkuu alimdharau Samueli kwa kumrushia matokeo yake.
  6. Samueli hakutaka kuonyesha matokeo yake kwa wenzake alipofeli.
  7. Samueli hakutia bidii masomoni mwake kwani hata majibu yake si sahihi.
  8. Samueli alipoanguka mtihani wake alikosa matumaini na kutaka kujiua. Zozote (4X2 = 8)

8. 

 1.                                
  1. Kitendawili 1 X 1 = 1
  2.                          
   • Hubuniwa na mtendaji akilenga hadhira maskin. Maalum.
   • Huwa maelezo marefu yanayoficha kitu kilichofumbuliwa.
   • Kufumbua huhitaji uchunguzi na kufikiria kwingi.
   • Hayana mpangilio maalum.kiumbo/kimtindo.
   • Jibu lake hufahamika katika jamii husika
   • Hubuniwa kulingana na hali ya muungano baina ya vitu/mambo.
    Za kwanza 4x1 = 4
  3.                      
   • Huburudisha wanajamii.
   • Huongea na kutoa mawaidha
   • Hukuza stadi ya udadisi
   • Huwapa wanajamii mazoezi ya kufikiri
   • Njia muhimu ya mawasiliano.
   • Huimarisha uwezo wa kukumbuka za kwanza 4 x 1 = 4
  4. ufugaji wa kuku yoyote 1x1=1
 2.                    
  1.                          
   1. Avael Maleba
   2. Atumie miondoko ya mwili na ishara za uso.
   3. Atumie sauti inayosikika
   4. Aelewe utamaduni hadhira.
   5. Ashirikishe hadhira katika uwasilishaji wake.
   6. Atambue hali za hadhira
   7. Achekeshe hadhira / Atumie lugha ya ucheshi
    zozote 6x1=6
  2.                    
   • Kupitia Tamasha za muziki
   • Sherehe za jamii/kitamaduni
   • Sarakasi za wasanii
   • Ngoma za Kienyeji kwa mfano isukuti katika hafla ya siasa.
    Zozote 4x1=4

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Arise and Shine Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?