Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - KCSE 2022 Mock Exams Set 2

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo

 • Jibu maswali manne pekee.
 • Swali la kwanza ni la lazima.
 • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki..
 • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

 

SEHEMU YA A: RIWAYA
Assumpata K. Matei: Chozi la Heri

LAZIMA

 1. “Sandarusi zenyewe mtu anazitafuta kwenye mlima taka zinazotolewa huko waishio waheshimiwa kuja kutuua huku”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Taja kwa kufafanua mbinu –ishi wakimbizi walizozizua kukumbana na chanagamoto zao.. (alama.12)
  3. Onyesha umuhimu wa msemaji katika kuzua sifa za wahusika wengine. (alama 4)

SEHEMU B: TAMTHILIA
Kigogo.Pauline Kea.
Jibu swali la 2 au la 3

 1. Mandhari ya soko la chapa kazi yamezua maudhui na sifa kadhaa za wahusika. Jadili’ (alama 20)
  AU
 2. “Mtalipa kila tone la damu mlilomwaga sagamoyo ;wewe na watu wako.”
  1. Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
  2. Eleza sifa za mzungumzaji (alama 4)
  3. Thibitisha kwa kutoa mifano kuwa maisha ya anayezungumziwa yametawaliwa na dhuluma. (alama 12)

SEHEMU YA C: HADITHI FUPI

 1. Kwa kurejelea hadithi ya Mapenzi ya kifaurongo, Mame Bakari,Nizikeni papa hapa na Mtihani wa maisha jadili mambo yanayowatatatiza vijana.(alama 20) (alama 20)

SEHEMU D: SHAIRI

 1. WASIA

  Huno wakati mufti, vijana nawausia
  Msije juta laiti, mkamba sikuwambia
  Si hayati si mamati, vijana hino dunia
  Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula

  Japo aula kushufu, na machoni vyavutia
  Dunia watu dhaifu, yaugua nasikia
  Vijana nawasarifu, falau mkisikia
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

  Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria
  Msije andama baa, makaa kujipalia
  Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria
  Uonapo yyang’aria, tahadhari vitakula.

  Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia
  Wajimwaie uturi, na mapoda kumichia
  Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia
  Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.

  Wawapi leo madume, anasa walopapia?
  Wamepita ja umeme, leo yao sitoria
  Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula

  Nambie faida gani, nambie ipi fidia
  Upatayo hatimani, waja wakikufukua
  Ila kufa kama nyani, kasoro yako mkia
  Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula.

  Vyatiririka tariri, vina vyanikubalia
  Alo bora mshairi, pa tamu humalizia
  Nahitimisha shairi, dua ninawapigia
  Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.

  Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia
  Wakingie wanarika, na anasa za dunia
  Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

  MASWALI:
  1. Ni ujumbe gani wanaopewa vijana kupitia shairi?. (alama 4)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (alama 2)
  3. Eleza bahari ya shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo. (alama 2)
   1. idadi ya vipande katika mshororo
   2. mpangilio wa vina katika beti.
  4. Eleza mbinu zozote mbili za kishairi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
  5. Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari (alama 4)
  6. Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
  7. Tambua: (alama 2)
   1. Nafsi neni
   2. Nafsi nenewa
  8. Eleza umuhimu wa mbinu ya kimtindo iliyotumika katika ubeti wa tano. (alama 2)
  9. Eleza maana ya msamiati: ‘aula’ (alama 1)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

 1.      
  1. Eleza maana ya miviga. (alama.2)
  2. Eleza sifa tano za miviga. (alama.5)
  3. Miviga ina udhaifu gani. (alama.3)
  4.  Fafanua vigezo sita vinavyotumiwa kuainisha methali. (alama.6)
  5. Jadili mambo manne ambayo huzingatiwa katika katika uchambuzi wa hadithi. (alama.4)

Mwongozo wa Kusahihisha

 1. “Sandarusi zenyewe mtu anazitafuta kwenye mlima taka zinazotolewa huko waishio waheshimiwa kuja kutuua huku”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   Masimulizi ya kaizari akimwelekeza Ridhaa wakiwa katika msitu wa Mamba akielezea jinsi maisha yalivyokuwa hapa.
  2. Taja kwa kufafanua mbinu –ishi wakimbizi walizozizua kukumbana na chanagamoto zao..
   1. Watoto wake kupata ushauri nasaha kukabiliana na udhalimu wa kubakwa.
   2. Kuchimba vyoo kukabaliana na tatizo la ukosefu wa misala
   3. Kukubali kupanga foleni ili kupata mgao wa chakula ulioletwa na mashirika tofauti tofauti.
   4. Kula miziz na matunda mwitu ili kuzima njaa ilipowazidi.
   5. Kujijengea vibanda ili kupata pahali pa kujisitiri.
   6. Wazazi kutafuta muda wa kuhusiana kimapenzi mchana wakati watoto wao walitoka kucheza.
   7. Kutobaguana kicheo au kitabaka katika kambi hii.
    hoja 6 x 2 = (alama.12)
  3. Onyesha umuhimu wa msemaji katika kuzua sifa za wahusika wengine. (alama 4)
   Kizani anauza sifa za
   1. Ridhaa – Mshauri mzuri anapowashauri wenzake kambini kuchimba misala
    Anakubali mabadiliko yaliompata kambini na kuamua kuendelea na maisha.
   2. Selume – Ana kihoro – anaposimulia chanzo chake cha kubagwaliwa na aila ya mumewe kwa msingi eti alimpigia kura Mwekevu.
    - Pia ana heshima – anapotambulisha ujio wake kwa kina Kaizani kabla akaribie kibanda chao.
 2. Mandhari ya soko la chapa kazi yamezua maudhui na sifa kadhaa za wahusika. Jadili’ (alama 20)
  •  Maudhui
   1. Ukosefu wa kazi – Sudi amesomea uanasheria lakini anachonga vinyango sokoni.
   2. Ufisadi – Ashua anasema wanalipa kodi lakini serikali ya Majoka anawaitisha kwa kutaka kitu zaidi.
   3. Uchafuzi wa mazigiria – wakati maji yanayopita mitaroni ni chafu na yananuka vibaya kutokana na kemikali inayotoka kwa kampuni ya Majoka and Majoka Company.
   4. Matumizi ya teknolojia – kusikizwa kwa habari kutoka kwa redio.Biashara – Ashuua anachuuza maembe , Boza ,Sudi naKkombe wanachonga vinyago.
   5. Ubadhirifu wa mali ya umma – Kenga anamshauri Sudi kuchonga kinyago na kumwahidi kumtunza kutokana na fedha ya ufadhili.
   6. Uongozi mbaya – kusherehekea uhuru kwa mwezi moja.
   7. Utu – Ashua kuwaletea Sudi , Boza na Kombe – chai ya mkandaa kwa maandazi.
  • Wahusika
   SUDI
   1. Mwepesi wa kukasirika. \
   2. Ana kipawa cha uchongaji
   3. Mzinduzi wa mambo – anapowaambia wenzake athari za kusherehekea uhuru kwa mwezi mmoja.
   4. Mwepesi wa hasira – Boza anapomkasirisha anataka kumpiga.
  • ASHUA .
   1. Mkarimu.
   2. Mtambuzi wa mambo – alitambua kuwa uongozi wa serikali kuitisha kitu zaidi ni kuwadhulumu wafanyabiashara.
   3. Ni mtani – anawaita Kombe shemeji
   4. wahusika wengine ni Boza na Kenga
    (mwanafunzi azingatie wahusika wawili kisha awatolee sifa tano tano kila mmoja. )

    AU
 3. “Mtalipia kila tone la damu mlilomwaga Sagamoyo ;wewe na watu wako.”
  1. Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
   1. Maneno ya ni Tunu.
   2. Akimwambia Majoka.
   3. Ofisini mwa Majoka
   4. Ashua alikuwa gerezani.
  2. Eleza sifa za mzungumzaji (alama 4)
   1. Sifa za Tumu.
   2. Mwanamapinduzi
   3. Msomi
   4. Mtetezi
   5. Mwajibikaji
   6. Mwenye mlahaka mwema na wahusika wengine.
  3. Thibitisha kwa kutoa mifano kuwa maisha ya anayezungumziwa yametawaliwa na dhuluma.
   • Majoka
    1. Kutoza kodi ya juu isiwasadi wafanyi biashara sokoni.
    2. Kando ya kulipa kodi wanalazimishwa kutoa kitu kikubwa juu ya kodi – kulingana na Ashua.
    3. Anafunga soko la chapakazi bila kuwapa wafanyi biashara njia mbadala ya kukidhi mahitaji yao.
    4. Anawalazimisha raia kusherehekea uhuru kwa mwezi mmoja.
    5. Anamtaka Ashua mapenzi anapoenda kwake kumtaka usaidizi.
    6. Anamlazimisha Sudi kuchonga kinyago bila hiari yake.
    7. Anawaongeza walimu na madktari mshahara pia anaongeza ushuru ili wasifaidike na nyogeza hiyo.
    8. Ana nia ya kujenga hoteli yake ya kifahari palipo soko la Chapakazi.
    9. Aliwaua wapinzani wake - Jabali.
    10. Anapanga kumwangamiza Tunu akiendelea kumpinga.
    11. Anaendeleza ukataji wa miti kuchangia uharibifu wa mazingira / ukame na njaa .
    12. Anatumia polisi vibaya kuwapiga na kuwaumiza waandamanaji.
     (alama 12)
 4. Kwa kurejelea hadithi ya Mapenzi ya kifaurongo, Mame Bakari,Nizikeni papa hapa na Mtihani wa maisha jadili mambo yanayowatatatiza vijana.(alama 20)
  1. Mambo yanayowatatiza vijana
   • Mapenzi kifaurongo
    1. unyanyapaa wa kutoka katika familia maskini – Dennis.
    2. Kutoelewa na masomo.
    3. Kudharauliwa na walimu.
    4. kutopata mahitaji yao ya kimsingi chuoni – Dennis.
    5. Shinikizo la vijana – kutaka kuwa na mavazi kama ya wanafunzi wenzi.
   • Mamake Bakari.
    1. kubakwa
    2. Usalama wa watoto waakiwa njiani kuelekea shuleni au kutoka shuleni.
    3. Kutokuwa na ufahamu mzuri kuhusu hatua za kuchukua iwapo amebakwa .
    4. Ukosefu wa uhusiano mzuri kati ya wazazi na watoto wao pamoja na waalimu.
    5. Elimu kukatizwa baada ya kupata uja-uzito.
    6. Kujiwekea siri zinazowaumiza na kuwaadhibu kisaikolojia.
   • Nizikeni papa hapa.
    1. Mapuuza – kujihusisha na mapenzi kiholela bila kujali matokea yake.
    2. Kutofuata ushauri wa marafikiri wanapokuwa na nia ya kutusaidia ili kuepukana na mashaka.
    3. Serikali kutokuwa na mpango wa kutambua, kuendeleza na kudumisha talanta za vijana mtaani.
    4. Kukosa usaidizi kutoka kwa jamii wanapoiihitaji zaidi.
    5. maoni yao kutosikiwa na kutiliwa maanani katika jamii.
    6. Kukosa kutafuta usadizi i wa matibabu wanapougua.
   • Mtihani wa maisha.
    1. Shinikizo la kupita mtihani ili kuyafikia matarajio ya wazazi.
    2. Mtoto kijana kutwikwa majukumu mengi katika jamii.
    3. Kufanya mambo ili kufurahisha marafiki – Nina.
    4. Kuwa na uhusiano mbaya na wazazi kunasukumia kuwa mwongo na kutaka kujiua.
    5. Kuchukuliwa kufeli masomo ya shuleni ndio mwisho wa maisha.
    6. Kutokuwa na ufahamu wa njia mbadala wa kuyaendeleza maisha baada ya kufeli masomo ya vitabuni.
 5. MASWALI:
  1. Ni ujumbe gani wanaopewa vijana kupitia shairi?. (alama 4)
   • Kujitahadharisha na vyote vinavyong’aa sababu vinadhuru.
   • Kujiepusha na zinaa.
   • Wasifikirie wanaovalia kinadhifu na kujipodoa ndio wazuri na kuwaandama.
   • Wasiandame / Kupapia anasa.
   • Kumcha Jalia.
   • Kuvumilia na kujikaza. (zozote 4 x1 = 4)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (alama 2)
   • Tabaini – si hayati , si mamati.
   • Msemo – Makaa kujipalia
   • Kaza kamba.
   • Mdokezo wa methali – si mlango nyumba nzuri (zozote 2x1 = 2)
  3. Eleza bahari ya shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo. (alama 2)
   1. idadi ya vipande katika mshororo
    Mathinawi - migao miwili katika kila mshororo. (alama 1)
   2. mpangilio wa vina katika beti.
    Ukara – vina vya ndani vinatofautiana lakini vya nje vinafanana. (alama 1)
  4. Eleza mbinu zozote mbili za kishairi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
   • Tabdilia – huno – huo.
   • Inkisani – Mkemba – mkaamba
   • Alo – aliye
   • Ngia – ingia ndani
   • -Utohozi – sitoria
   • Lahaja – hino
   • Kuboronga sarufi – makaa kujipalie. (alama 2x1)
  5. Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari (alama 4)
   • Ingawa vitu vitaonekana na kuvutia machoni, dunia ina udhaifu na maovu mengi. Vijana
   • nawasihi iwapo mtanisikia , tahadhari
   • na vyote vinavyong’ara kweli
   • vinawezeza kukudhuru.
  6. Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
   • Kushauri – mashauri anawashauri vijana kujihadhari na dawa za kuleya
  7. Tambua: (alama 2)
   • Nafsi neni – mshauri /mzazi /mhenga.
   • Nafsi nenewa – Vijana.
  8. Eleza umuhimu wa mbinu ya kimtindo iliyotumika katika ubeti wa tano. (alama 2)
   • Balagha – wawapi leo madume, anasa walopapia?
   • Umuhimu – kuibua hisia za nafsi nenewa kuhusu kupapia anasa na raha.
  9. Eleza maana ya msamiati: ‘aula’ (alama 1)
   Aula – bora nzuri.
 6.  
  1. Eleza maana ya miviga. (alama.2)
   • Ni sherehe za kitamaduni amabazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi maalum cha mwaka (1x2)
  2. Eleza sifa tano za miviga. (alama.5)
   • Huandamana na matendo Fulani – kama vile kupiga magoti, kunyolewa. n.k
   • Huongozwa na watu mahususi katika jamii.
   • Huandamana na utoaji mawaidha / ulumbi.
   • Maleba huvaliwa na wanaohusika.
   • Hufanyiwa katika mazingizira maalum.
   • Huambatana / Hufungamana na utamaduni wa jamii husika.
   • Hufanywa wakati wa kipindi maalum / wakati maalum.
   • Huwa na kutolewa kafara.
   • Huwa na kutolewa sadaka.
   • Kuna kula kiapo – wahusika huweka ahadi ya kutenda wema.
  3. Miviga ina udhaifu gani. (alama.3)
   Udhaifu katika miviga
   • Husababisha kudorora kwa maendeleo.
   • Huleta utengano kati ya jamii na majirani.
   • Huasi mabadiliko ya kiwakati (nyingine zimepitwa na wakati.
   • Madhara yanaweza kutokea hasa vifaa butu vinapotumika.
   • Huleta utengano wa kujinsia kumtukuza mwanaume na kumduinisha mwanamke. ( zozote 3x1)
  4. Fafanua vigezo sita vinavyotumiwa kuainisha methali. (alama.6)
   • Mandhari / mazingira – ukipanda pantosha , utavuna pankwisha.
   • Maudhui – ulezi – samaki mkunje angalia mbichi.
   • Fani / tamathali za usemi – Takriri haba na haba hujaza kibaba.
   • Jukumu – Kuonya – Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu.
   • Maana sawa – pole pole ndio mwendo -haraka haraka haina baraka.
   • Abjadi – Kupangwa kialfabeti zote zinazoanza na harufi A zinawekwa pamoja hadi Z. (zozote 6x1)
  5. Jadili mambo manne ambayo huzingatiwa katika katika uchambuzi wa hadithi. (alama.4)
   • Ujumbe. - Hadhira
   • Msuko/ ploti. - Fanani
   • Dhamira. - Kubainisha umuhimu wa formyula ya kufungua na
   • Wahusika. Kufunga hadithi.
   • Ugiligili
   • Tamathali za semi.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - KCSE 2022 Mock Exams Set 2.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?