Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - ACK Diocese Mumias Joint Evaluation Mock 2022

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo Kwa Watahiniwa

 • Jibu maswali manne pekee
 • Swali la kwanza ni la lazima
 • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani Riwaya, Tamthilia, Hadithi fupi na Ushairi
 • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili pekee.

SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI
(SWALI LA LAZIMA ALA. 20)

 1. Soma utungo ufuatao kasha ujibu maswali yanayofuata.

  Nilipokukopoa,
  Cheko la mwivu wangu lilipaa sana
  Ukewenza ukamshawishi kuchukua buruji kueneza habari.
  “Njooni mwone jana la ajabu.”
  “Hajawahi kuonekana kama huyu
  Tangu kuumbwa kwa ulimwengu.”
  Ndivyo walisema walokubeza
  Kijiji kizima kilimiminika mwangu nyumbani
  Kuyatuma maozi kukutazama weye
  Uso na thamani walikwona,
  Wakaupa unyonge moyo wangu toto,
  Wakanituma kuola viungo vyako
  Wakanitanabahisha upungufu ulokulemaza!
  Chozi chungu likapukitika
  Likalovya change kidari
  Likalovya chaoko kipaji
  Tabasamu ukatoa kunihakikishia
  “Mimi si mjalana!
  Katu sivyo wasemavyo walimwengu!”
  Neno lako hili likanipa tulivu
  Nikaamua alakulihali kupambana na yangu jumuiya
  Ilpsema kwa moja kauli utokomezwe, chakani utupwe.
  Tazameni mahasidi mloteka
  Teko la dharau mlonimwaiya
  Mkanitia ukiwa usomithilika!
  Oleni! Tungeni macho!
  Mwana mlioambaa ukoma
  Ulomwinga ja nyuni wala mtama, tazameni
  Mekuwa malaika, anowaauni
  Kiguru mlomtajia hakimzuwii kufuma mishale!
  Maadui wamwonapo hutetema kama jani
  Mefagia vijiji vinane kwa pigo moja la kiganja chake
  Mepigana vita visohisabika
  Na Wetu mahasimu waliotupoka na mifugo.

  Jamii yetu sasa metawala kote
  Umekuwa nahodha mwenye kubwa saburi
  Akili yako nyepesi sumaku kweli kweli
  Hupakata yote ya neema na shwari
  Mwili wako japo lemavu,
  Mesheheni nguvu za majagina mia moja!
  Naposhika zana, maadui elfu huanguka!
  Umeifaa jamii hii, ilotaka kuangamiza
  Majagina wote, wakusujudia
  Walokufurusha wamebaki hizika
  Watukuka ewe shibli
  Mfano wa Shaka Zulu
  Alowayeyusha kama barafu.

  Limwengu mzima wakujua, mwana
  Alozawa kishika mkuki
  Ulosema na miungu, alfajiri lipoukumbatia ulimwengu
  Wla mwana jihadhari usaliti wao waja
  Wasije kutosa lindini kwa nduli kukukabidhi.

  MASWALI
  1. Ainisha utungo huu kimuundo na kimaudhui. (ala. 2)
  2. Eleza sifa tatu za mighani ambazo zinajitokeza katika utungo huu. (ala.6)
  3. Jadili fani katika wimbo huu. (ala.5)
  4. Jadili sifa za jamii iliyoizaa kazi hii. (ala. 2)
  5. Ni nani anayimba wimbo huu (nafsineni)? (ala.1)
  6. Eleza tofauti 4 kati ya mighani na visasili (ala.4)

SEHEMU YA B: CHOZI LA HERI
Jibu swali la 2 au 3.

 1. Fafanua jinsi riwaya ya chozi la Heri ililenga kuiadilisha jamii. (ala. 20)
 2. Usalama ni mojawapo ya mahitaji ya kibinadamu, kwa hakika, tunaweza kusema kuwa usalama ni mojawapo ya mahitaji ya kimsingi. Bila usalama binadamu hawezi hata kushiriki shughuli………”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (ala.4)
  2. Eleza umuhimu wa mzungumzaji katika kujenga ploti (ala.8)
  3. Mzungumzaji anazungumzia swala la usalama. Jadili matokeo ya ukosefu wa usalama ukirejelea matukio katika riwaya ya Chozi la Heri. (ala.8)

SEHEMU C: TAMTHILIA YA KIGOGO
Jibu swali la 4 au 5

 1. “Nusura roho inianguke mwanangu, wametutia woga mwingi sana. Twaishi kwa hofu…”
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al 4)
  2. Mnenaji wa usemi huu ana hofu gani? (al 2)
  3. Taja sifa tatu za mnenewa. (al 3)
  4. Bainisha mbinu moja ya lugha kutoka kwenye dondoo. (al 1)
  5. Wananchi katika maeneo haya wanapitia changamoto zipi? (al 10)
   AU
  1. Jadili athari za tabia zifuatazo kwa wananchi wa Sagamoyo.
   1. Ulevi. (al 3)
   2. Maandamano. (al 3)
   3. Usherati. (al 3)
   4. Kutegemea mikopo. (al 3)
   5. Tamaa. (al 3)
  2. Fafanua mbinu tano alizozitumia Majoka kufanikisha uongozi wake. (al 5)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
Jibu swali la 6 au 7

 1. “Ndugu yangu kula kunatumaliza.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
  2. Taja na ueleze sifa zozote mbili za mnenewa. (al 4)
  3. Eleza tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. (al 2)
  4. Kwa kurejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, thibitisha ukweli wa kauli ‘kula kunatumaliza’(al 6)
  5. Eleza umuhimu wa matumiziya nyimbo katika hadithi ya Shibe Inatumaliza. (al 4)
   AU
 2. (Mtihani wa maisha)
  ‘Leo mwalimu mkuu atajua kwamba mdharau biu hubiuka’
  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4)
  2. Taja mbinu ya lugha iliyotumika katika mktadha huu. (Alama 6)
  3. Eleza wasifu wa mzungumzaji wa maneno haya. (Alama 2)
  4. Jadili maudhui ya elimu kama yanavyojitokeza katika hadithi ya Ndoto ya mashaka (Ali Abdulla) ala. 8

SEHEMU YA E: USHAIRI

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yaliyofuata.

  Jambo lolote ni nia, kuweka yako azima,
  Hasa ukikusudia, kulepuka la lawama,
  Mola takusaidia, kila la ovu kuzama,
  Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

  Hakika si masikhara, wa kale waliyosema,
  Ni maneno ya busara, tena ni wasia mwema,
  Kuwa hasira hasara, ghadhabu zisizokoma,
  Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

  Mja katu haitaki, hasira kuziandama,
  Punguza zako hamaki, moyo uwe na huruma,
  Kwani zikizidi chuki, hapo huja uhasama,
  Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

  Na uhasama ujapo, uadui kukwegema,
  Hapo ndipo upatapo, kukufikia zahama,
  Mwisho ndipo ujutapo, ikabaki kulalama,
  Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

  La usawa sinyamai, kukweleza ni lazima
  Chuki nyingi hazifai, hebu tuliza mtima,
  Waweza tupa uhai, au nyingi darahima,
  Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

  Upunguze wako mori, mwana na mtu mzima,
  Upoze moyo wa hari, hasira zipate hama,
  Subira huvuta heri, ikaleta na neema,
  Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

  Kifaya nilipofika, hapa ndiyo kaditama,
  Sahibu wasia shika, hasira si kitu chema,
  Mtegemee Rabuka, atakulinda Karima,
  Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

  MASWALI
  1. Toa anwani mwafaka kwa shairi hili. (Al. 1)
  2. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia:- (Al. 4)
   1. Mishororo
   2. Vipande
  3. Fafanua umbo la shairi hili. (Al. 4)
  4. Dhihirisha matumizi ya idhini ya mshairi katika shairi hili. (Al. 3)
  5. Andika ubeti wa sita kwa lugha tutumbi. (Al. 3)
  6. Eleza toni ya shairi hili. (Al. 2)
  7. Ni nani nafsineni katika shairi hili? Eleza (Al. 1)
  8. Fafanua msamiati ufuatao kama ulivyotumika shairini. (Al. 2)
   1. Mtima
   2. Darahima

Mwongozo wa Kusahihisha 

 1.      
  1.  
   • Kimuundo ni shairi. Unaweza pia kuchukuliwa kama utendi (shairi la ushujaa) kwa sababu unazungumzia sifa za shujaa na vita alivyopigana.
   • Kimaudhui ni sifo/wimbo wa sifa- unamsifu shujaa
  2.  
   1. Matukio ya ajabu kama vile.
    • Kusema na miungu alipozaliwa.
    • anayesema ana nguvu za kipekee japo ni kilema.
    • Anayesema kazaliwa akishika mkuki
   2. Matumizi ya chuku kama vile:
    • maadui elfu kufa anaposhika silaha.
    • Kufagia vijiji vinane kwa pigo moja la kiganja chake.
   3. Utungo unahusu shujaa wa vita- amegpigana vita vingi visivyohesabika
   4. Anayesemwa amezungukwa na migogoro – mahasidi waliochukua mashamba na wasaliti.
   5. Utungo umechanganya historia na mambo ya kidini – anazungumza na miungu anapozaliwa – haya ni mambo ya kiimani.
  3.  
   1. kejeli/stihizai – anaitwa jana la ajabu.
   2. chuku:
    • Kijiji kizima kuja kuona mtoto
    • Maadui elfu kufa kwa anayesemwa kushika silaha
    • Mwili kuwa na nguvu za majagina mia moja
   3. ritifaa – anazungumza na mahasidi ambao hawapo kana kwamba wapo.
   4. tashbihi:
    • Maadui wamwonapo hutetemeka kama jani
    • Kuwayeyusha kama barafu
   5. sitiari:
    • umekuwa nahodha
    • Akili yako sumaku
   6. usambamba:
    • Likalovya change kidari
    • Likanavya chako kipaji
   7.  taswira:
    • Mama alivyolia na kujilovya machozi na kumlovya mwanawe
    • Alivyopigana na utawala wake au jamii yake. Kijiji kizima kinavyomiminika kwake nyumbani.
  4.        
   1. Waume huoa wake wengi – Anasema, Uke wenza ukamhimiza kuchukua buruji kueneza habari.
   2. vilema walitupwa kichakani – Ilosema kwa moja kauli utokomezwe chakani utupwe.
   3.  Ni wafugaji – Kutupoka mifugo.
  5. Anayeimba ni mama. Anasema nilipokuopoa.
  6. tofauti kati ya mighani na visasili;
   • Mighani husimulia kuhusu mashujaa, ilhali visasili husimulia asili ya vitu.
   • Mighani husimulia historia ya jamii, ilhli visasili husimulia mianzo ya vitu au mambo ulimwenguni.
   • Katika mighani, wahusika ni mijagina, ilhali katika visasili wahusika ni vitu tofauti kama vile miungu, wanyama na binadamu.
   • Mighani hueleza sifa za majagina , ilhali visasili hueleza mianzo ya desturi.
 2. Eleza maadili/ mafunzo katika riwaya
  • Kupitia kangara na Sauma, tunafunzwa kuwa uovu wa ulanguzi wa watu humfanya mtu afungwe jela.
  • Tunaadilishwa kuwa watu hawafai kutumia misala ua kupeperushwa. Wakimbizi wa msitu wa mamba wanakabiliwa na kipindupindu na homa ya matumbo; wengi wanakufa
  • Tunausiwa kuwa wanawake kama Naomi ambao hawapendi ndoa zao hujutia maamuzi yao baadaye.
  • Kupitia kwa aila ya Kaizari, tunausiwa kuhusu umuhimu wa kufunza mazingira.
  • Kpitia kwa wahusika kama lunga, tunafinzwa umuhimu wa watumishi wa umma kutumikia wananchi kwa uadilifu.
  • Kupitia kwa Pete, tunausi kuhusu shida wanazopitia wasichana wadogo wanaoozwa kwa mibaba; tunausiwa kuuepuka.
  • Kupta kwa Tuama, tunausiwa umuhimu wa kupigana na desturi ya zamani ya kukeketa wasichana.
  • Kupitia kwa Dickson, tunausiwa kuwa mui huwa mwema, kwamba vijana wanaweza kubadilisha tabia zao mbaya ya kulangua dawa za kulevya.
  • Kupitia kwa Dickson, tunaadilishwa kuwa vijana wanaweza kutatua tatizo la uhaba wa ajira kwa kujiajiri.
  • Kupitia Lemi, tunausiwa umuhimu wa kutochukua sharia mikononi mwetu; kwa upigaji kitutu wa watu unaweza kuua watu ambao hawana hatia.
  • Kupitia kwa Ridhaa tunausiwa umuhimu wa kupenda kazi na kujitolea kuwa msaada kwa ndugu zetu- anasanbaza naji ya mabomba kijijini.
  • Kupitia kwa Mwekevu, wanawake wanausiwa kuwa vijana hawafai kupigana na walinda usalama, ni kupiga ngumi ukuta!
  • Tunaadilishwa kuwa walimu hawafai kuwa na uhusiani wa kimapenzi na wanafunzi wao. Fumba anamringa Rehema na kuzaa Chandachema ambaye anatelekezwa.
  • Tunaadilishwa kwa mashariki kama CWA, Ansar Mwangaza na Shirika la Makazi Bora tunausiwa kuhusu nafasi ya mashirika ya kijamii katika maendeleo ya nchi.
  • Tunaadilishwa kuwa raia wanafaa wapende nchi zao. Annette na songoa wanahamia ughaibuni na kumsononesha Kiriri.
  • Tunafunzwa umuhimu wa kutambua makosa yetu na kupenda kazi. Naomi anatambua makosa yake na kujifunza umuhimu wa kufanya kazi kwa kujiajiri.
  • Tunausiwa kuzika tofauti zetu na kupanga maisha yetu upya. Ridhaa anakubali majaaliwa yake na kujenga nyingine katika mtaa wa afueni.
 3.    
  1.  ni maneno ya Apondi katika warsha ya walinda usalama. akiwahutubia walinda usalama akiwemo Mwangeka. Anatoa hotuba ya ufunguzi. Alikuwa anasisitiza umuhimu wa walinda usalama katika jamii. Baadaye alikutana na mwngeka na kuchumbiana naye kabla ya kufunga ndoa. Ala 4
  2. Umuhimu wa mzungumzaji katika kujenga Ploti
   Mzungumzaji ni Rachel Apondi
   • kupitia kwake tunapata kujua
   • Kukutana kwao – walivyokutana Mwangeka na Apondi
   • Kilichosababisha ujane wake
   • Alivyompanga umu
   • Ndoa yao na Mwangeka – Hatima ya ujane wa Mwangeka.
   • Tanaangaziwa uhusiano wa M. Dhababu na Apondi na alivyompanga.
   • Kupitia kwake na mwangeka Umu, Dick na Mwaliko wanakutana tena – Hatima ya utengano uliosababishwa na Sauna alipowaiba Dick/Mwaliko.
   • Mwangeka anaanza maisha mapya ya ndoa baada ya mkewe kufa kwa mkasa wa moto
   • Anaonyesha hatima ya msongo wa mawazo aliyokuwa nao. Ridhaa kuhusu mwanaye mwangeka kutokuwa na mke.
   • Anaonyesha hatima ya migogoro kati ya koo mbalimbali – anakubaliwa na Ridhaa baada ya kumzaa Ridhaa – licha ya koo zao kubaidika kama ardhi na mbingu.
   • Anaonyesha hatima ya donge chungu alilokuwa nalo UmulKheri tangu kuondoka kwa mama yake na akaanza kupona kutokana na pendo la Apondi na Mawangeka. 8x1=ala.8

    Matokeo ya ukosefu wa usalama
   • Vifo – Ridha kuipoteza familia yake – Terry mkewe, bintiye na mjukuu.Kutokana na ukosefu wa usalama, kuna vifo vinavyotokea, kutoka kwa vita vya baada ya uchaguzi, na maandamano – kuchomewa kwa nyumba ya Ridhaa.
   • Vita vya kikabila – vinasuka kutokana na uchaguzi na kutokubali matokeo ya kumtawaza kiongozi mwanamke Mwekevu.
   • Ubakaji – mabinti na mkewe wa kaisari kutendewa ubahaimu kwa kumpigia kura mwekevu.
   • Ukimbizi/wakimbizi – familia ya Ridhaa na kaizari kuhamia msitu wa mamba na kukaa kule kwa sababu ya ukosefu wa chakula.
   • Ukosefu wa chakula – katika msitu wa mamba, kuna ukosefu wa chakula na Ridhaa daktari mzima anaonekana kula mizizi hadi wanopoletewa msaada wa chakula na mashirika ya kidini.
   • Ukosefu wa makazi bora – Inawabidi kukaa katika kambi kwani hawakuwa na makazi bora.
   • Ukosefu wa misala – Hili unasababisha mkurupuko wa magonjwa kwa kutumia sadarusi kule katika mabanda ya sombera.
   • Usalama wa watoto - Umu, Dick na Mwaliko wanauzwa na Sauna aliyeaminiwa na mwajiri wake kuwatunza
   • Kuvunjika kwa ndoa – Subira
   • Uharibifu wa mali – kuvunja maduka, nyumba ya Ridhaa. Magari kuchomwa.
   • Upweke/ukiwa – Kufiwa na familia – kama Ridhaa anapoipoteza familia yake yote.
   • Kujeruhiwa – Subira kukatwa kwa sime
    (Zozote 8 x 1=ala. 8)
 4. ‘Nusura roho inianguke mwanangu, wametutia woga mwingi sana. Twaishi kwa hofu…’
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   • Ni maneno ya Hashima akimuelezea Siti.
   • Walikuwa nuymbani kwa hashima, baada ya kupokea vijikakaratasi na vitisho kwamba watawaua la sivyo wahame. 4×1= al 4
  2. Mnenaji wa usemi huu ana hofu gani ? (alama 2)
   • Kutishiwa kuhama.
   • Mwanawe tunu atawaua na vibaraka wa majoka.
   • Makaazi yake yatabomolewa. 1×2= al 2
  3. Taja sifa tatu za mnenewa (alama 3)
   • Mnenewa ni siti.
   • Mtetezi wa haki.-
   • Mdadisi. Anachunguza na kufahamu kiinI cha mauwaji ya vijana watano. 3×1= al 3
  4. Bainisha mbinu moja ya lugha kutoka kwenye dondoo. (alama 1)
   • Uhuishi – nusura roho inianguke.
   • Msemo- twaishi kwa hofu. 1×1= al 3
  5. Wananchi katika maeneo haya wanapitia changamoto zipi ? (alama 10)
   • Kupigwa na polisi wanapoandana.
   • Kuwaua wanapopinga uongozi.
   • Mazingira machafu.
   • Ukosefu wa shule nzuri ,watoto wa shule ya majoka and mojoka academy huiishia kuwa makabeji.
   • Vitisho vya kufukuzzwa kutoka sagamoyo.
   • Ardhi zao kunyakuliwa na viongozi.
   • Madeni yanayotokana na mikopo inayoombwa na viongozi na kulipwa na vizazi vingi.
   • Ahadi za uongo kutoka kwa viongozi.
   • Gharama ya Maisha kupanda kila kuchao., bei ya bidhaa kupandishwa juumara kwa mara.
   • Wafanyakazi kulipwa mishahara duni, mfano walimu na wauguzi.
   • Viongozi kupuuza malalamishi ya wananchi.
   • Wafanyabiashara kutozwa kodi ya juu.
   • Wananchi kutiwa gerezani kwa amri ya viongozi bila kupitia mahakamani kisheria.
   • Vyombo ya habari vinavyowafaa wananchi kufungwa kwa amri ya kiongomfano runinga ya mzalendo.
   • Maandamano ya wananchi kutajwa kuwa si halali ilhali wanaumia.
    10×1= al 10
 5.      
  1. Jadili athari za tabia zifuatazo kwa wananchi wa sagamoyo.
   1. Ulevi. (alama 3)
    • Vifo vya watu.
    • Watu wamepofuka.
    • Biashara haramu kuhalalishwa.
     3×1= al 3
   2. Maandamano ( alama 3)
    • Vifo- vijana watano.
    • Wafanyakazi kuongezwa mshara mdogo- wauguzi na walimu.
    • Yalileta mabadiliko ya uongozi baadaye..watu walimkataa majoka.
    • Yalizindua watu kuhusu haki zao.
     3×1= al 3
   3. Usherati.(alama 3)
    • Uliharibu ndoa- asiya ngurumo,boza.. Ndoa ya husda na majoka.
    • Ulimpa asiya kandarasi ya kuoka keki ya uhuru.
    • Ulimpa asiya kibali cha kuendeleza biashara yake ya kuuza pombe haramu. 3×1= al 3
   4. Kutegemea mikopo (alama 3).
    • Uliwekea wanasagamoyo madeni mengi.
    • Ulipandisha gharama ya Maisha juu, ili kujaribu kulipia madeni hayo.
    • Yalifanya wanasagamoyo kupinga uongozi wa majoka. 3×1= al 3
   5. Tamaa (alama 3)
    • Ilifanya majoka kujaribu kukatalia uongozini.
    • Ilimfanya majoka kunyakua arddhi za umma kwa manufaa yake..mfano ardhi ya soko la chapa kazi.
    • Tamaa ya ilimfanya husda kuoleka kwa majoka. 3×1= al 3
  2. Fafanua mbinu TANO alizotumia majoka kufanikisha uongozi wake. (alama 5)
   • Vitisho.
   • Mauaji.
    Matumizi ya vyombo vya dola.polisi,bunduki,vitoza machozi
 6. “Ndugu yangu kula kunatumaliza.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4)
   • Maneno haya ni ya Mbura akimwambia Sasa wakiwa nyumbani kwa Mzee Mambo katika sherehe. Mbura anamhakikishia Sasa kuwa kula kutawamaliza baada ya Sasa kumuuliza ikiwa anahitaji kuongeza vyakula. 4×1= al 4
  2. Taja na ueleze sifa zozote mbili za mnenewa (al 4)
   • Ni msomi- ni waziri wa mipango na mipangilio, wizara inayomhitaji mtu kusoma kwa kina vipengele vya jamii.
   • Mwenye bidii- hakuna sekunde iwapitayo akiwa na Mbura bila kufanya kazi
   • Mzalendo- wanajituma kwa uzalendo wa taifa lao.
   • Mwajibikaji- hufanya kazi kwa hiari yake ama kwa kuamriwa na huyu au yule.
   • Mtiifu- anafanya kazi kwa kuamriwa.
   • Mdadisi- anamsumbua Mbura na maswali mengi.
   • Mlafi- baada ya kupakua anaanza kula bila kunawa na kurudia kuongeza chakula chakula mara tatu. 2×2= al 2
  3. Eleza tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo (al 2)
   • Uhaishaji- kula kunatumaliza
   • Jazanda- kula kunatumaliza 1×2= al 2
  4. Kwa kurejelea hadithi ya Shibe inatumaliza, thibitisha ukweli wa kauli ‘kula kunatumaliza’ (al 6)
   • Mzee Mambo anachota mshahara ila hatosheki; anaendelea kuchota wananchi wakiteseka.
   • Mzee Mambo anapanga sherehe nyingi kwa pesa za umma ila hatosheki nazo.
   • Katika sherehe, watu wanakula na kula tena tokea jua lilipochomoza.
   • Watu wanakula tu bila kuuliza aliyepika chakula na jinsi chakula kilivyopikwa.
   • Sasa na Mbura wanakula hadi wanalala.
   • Sasa na Mura wanarudia chakula kwenye foleni mara tatu kabla ya kutafuta mahali pa kutulia kula bila aibu.
   • DJ bado anafanya kazi ya kuburudisha hata baada ya kuchota mabilioni ya pesa za serikali, nao wananchi wa kawaida wanateseka.
   • DJ na viongozi wengine wanapata huduma zote za msingi bure huku wananchi wa kawaida wakilipia huduma zote.
   • Mbura aneleza madhara ya kiafya yanayohusiana na kula kwa wingi bila kutosheka.
   • Viongozi wanajali maslahi yao na kunyakua mali kuliko utu na ubinadamu. 6×1= al 6
  5. Eleza umuhimu wa matumizi ya nyimbo katika hadithi ya Shibe Inatumaliza (al 4)
   • Zinatumiwa na viongozi kujitumbuiza baada ya kunyakua mali ya umma. (uk 37)
   • Zinatumiwa na viongozi kujiliwaza kuwa mali mtu hupewa na Mungu. (uk 37)
   • Zinatumiwa na viongozi kujiondolea lawama baada ya kuchota pesa za umma. (uk 43) Zinatumiwa kuonyesha kuwa wanaonyanyaswa na kutegemea viongozi wataamka na kuwakimbilia viongozi shida zikiwazidia. (uk 43)
   • Zinatumiwa kuonyesha kuwa wananchi wa kawaida wanasahau shida zao na viongozi wabaya pindi wanapopokea msaada mdogo. 9uk 43) 4×1= al 4
 7. Haya ni maneno ya Samueli matandiko anayejizungumzia.
  1. Yuko ofisini ya mwalimu mkuu. Amekuja kuchukua matokeo ya mtihani. (4x1)
  2.    
   • Uzungumzaji nafsi - Samueli anajizungumzia.
   • Kinaya - Ni Samueli aliyeaibika si mwalimu.
   • Methali - mdharau biu hubiuka (3x2)
  3.  
   • Ni mwongo - Alimdanganya Nina kuwa ni mwerevu shuleni.
   • Ni mwoga - Alitaka kutorokea babake.
   • Hana matumaini - Anataka kujiua.
   • Hana bidii - Anashindwa na masomo (2x1)
  4.  
   • Babake Samueli anauza mali yake ili asomeshe watoto.
   • Babake Samueli anathamini elimu ya Samueli kuliko dada zake kama mwajuma na Bilha.
   • Samueli anatembea muda wa kilomita sita ili atafute elimu.
   • Samueli anaogopa kuzungumza na babake kuhusu matokeo yake.
   • Mwalimu mkuu alimdharau Samueli kwa kumrushia matokeo yake.
   • Samueli hakutaka kuonyesha matokeo yake kwa wenzake alipoanguka.
   • Samueli hakutia bidii masomoni mwake kwani hata majibu yake si sahihi.
   • Samueli alipoanguka mtihani wake alikosa matumaini na kutaka kujiua. (zozote 8 x 1)
 8.    
  1. Hasira Hasara/Jua Hasira Hasara/Epuka Hasira 1 x 1 = Al. 1
  2.        
   • Tarbia – Mishororo 4 katika ubeti
   • Ukara – Vina vya utao vinatiririka|
    2 x 2 = Al. 4
    (Asipotoa sababu asituzwe)
  3. Fafanua umbo la shairi hili.
   • Shairi hili lina beti saba.
   • Mishororo 4 katika ubeti
   • Vipande 2 – ukwapi na utao
   • Mizani 16 katika mishororo
   • Vina vya mwisho wa mishororo vinatiririka
   • Shairi hili lina kibwagizo – “Ukiitaka salama, jua hasira hasara”
    Zozote 4 x 1 = Al. 4
  4.  
   • Inkisari – takusaidia (mshororo wa kwanza)
   • Kuboronga sarufi – ‘kuweka yako azima’ badala ya kuweka azima yako
   • Tabdila – Ubeti 5 – ‘Sinyamai’ badala ya ‘Simanyazi’
    Zozote 3 x 1 = Al. 3
  5.  
   • √√Mshairi anawasihi watu wazima na watoto kupunguza hasira. Mtu aulizapo moyo wake hasira zinapotea.
   • √√Anawashauri watu wawe na subira ili waipate na neema
   • √√Mtu akitoka salama akumbuke kuwa hasira ni hasara.
    1 x 3 = Al. 3
  6. Toni ya kushauri – anashauri dhidi ya hasira
   1 x 1 = Al. 1
  7. Mshairi/yeyote mwenye wosia
   1 x 1 = Al. 1
  8.  
   1. Moyo
   2. Pesa/Ngwenje/Fuhisi
    x 2 = Al. 2

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - ACK Diocese Mumias Joint Evaluation Mock 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?