Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Maranda Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  2. Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  3. Kila insha isipungue maneno 400.
  4. Kila insha ni alama 20.
  5. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

MASWALI

  1. Insha ya lazima
    Umepata fursa ya kumhoji Waziri wa Ugatuzi nchini kuhusu mikakati ya kukabiliana na umaskini nchini. Andika mahojiano yenu.
  2. Mitandao ya kijamii imeleta hasara nyingi kuliko faida. Jadili.
  3. Andika kisa kinachodhihirisha maana ya methali:
    Mti mkuu ukigwa, wana wa ndege huyumba.
  4. Andika insha itakayomalizikia kwa maneno yafuatayo:
    Nilijitolea mhanga na msaada wangu ukazaa natija kwa wengi.

MWONGOZO

  1. Insha ya lazima.
    Umepata fursa ya kumhoji Waziri wa Ugatuzi nchini kuhusu mikakati ya kukabiliana na umaskini nchini. Andika mahojiano yenu.
    Hii ni insha ya mahojiano. Yafuatayo yazingatiwe;
    1. Anwani-ibainishe wahusika na kiini cha mahojiano k.m MAHOJIANO BAINA YA MWANAFUNZI NA WAZIRI WA UGATUZI KUHUSU JINSI SERIKALI NA JAMII ZINAVYOCHANGIA KUONDOA UMASKINI NCHINI
    2. Utangulizi-uwe na maelezo kuhusu mandhari.(yawekwe kwenye mabano)
    3. Mwili-maudhui yajitokeze hapa. Mfumo wa kitamthilia utumike ambapo majina ya mhoji na mhojiwa au vyeo vyao vijitokeze hapa na viandikwe upande wa kushoto wa karatasi na yatenganishwe kwa koloni.Hoja za kuzingatiwa na kama zifuatazo:
      • Uimarishaji wa afya ya umma ili kuwepo na jamii yenye afya
      • Kuwahimiza wananchi kuchukua mikopo inayopanua shughuli mbalimbali za maendeleo
      • Kuimarisha maendeleo mashinani
      • Kipiga vita ufisadi na kuwachukilia hatua kali wanaohusika
      • Taasisi za dini kusaidia wasiojiweza katika jamii
      • Wazazi kuwawekea watoto wao msingi mzuri wa kiuchumi
      • Vyombo vya habari kutumiwa kuendeleza elimu ya uwekezaji
      • Vilabu mbalimbali vya michezo kuwasaidia vijana kujikimu maishani
      • Vyama vya watu mbalimbali kujiunga pamoja uili kijiendeleza kiuchumi
      • Wakulima kusaidiwa na pembejeo ili kuwe na chakula cha kutosha
      • Miradi ya kuleta maendeleo mashinani kuanzishwa
      • Kuwapa wazee pesa za kujiendeleza
      • Kuwajibika katika matumizi ya pesa za maeneo bunge
      • Misaada kwa wanaohitaji hasa kupitia mashirika mbalimbali
      • Kuhimiza benki kutoa mikopo kwa riba za chini ili kuawezesha wananchi kushiriki shughuli za kimaendeleo
    4. Hitimisho-Hapa, mhoji amwuulize mhojiwa kutoa ushauri, rai au himizo kuhusiana na mada. Mahojiano yahitimishwe kwa mhoji kumshukuru mhojiwa, maagano na kutakiana heri.
      Tanbihi : mhoji aulize masawli naye mhojiwa atoe majibu. Mahojiano yasitawaliwe na mhusika mmoja sana. Mhoji aulize maswali ya kudadisidadisi.
  2. Mitandao ya kijamii imeleta hasara nyingi kuliko faida. Jadili.
    Hii ni insha ya mjadala. Iwe na muundo ufuatao;
    1. kichwa –Mtahiniwa abuni kichwa mwafaka kulingana na swali
    2. utangulizi- Mtahiniwa atangulize insha yake kwa kufafanua suala la ugatuzi akirejelea sekta ya afya/matibabu. Anaweza pia kufafanua maana ya na mifano ya mitandao ya kijamii.
      Ikumbukwe kwamba utangulizi huu si lazima bali ni upekee wa mtahiniwa.
    3. Mwili- Maudhui yajitokeze hapa. Mtahiniwa aandike hoja za kuunga mkono kauli hii na zile za kupinga.
      • Kuunga mkono (Hasara/ubaya/changamoto)
        1. Ulaghai/utapeli kwa kushawishiwa kupitia mtandao
        2. Kueneza /kusambaza/kuhimiza ukabila
        3. Ajizi
        4. Kupotosha watu
        5. Filamu ziazohimiza watu kuwa wazinifu.
        6. Matangazo ya vileo/mihadarati inayoathiri kihasi
        7. Kueneza chuki na propaganda
        8. Kuiga utamaduni wa kigeni usiofaa k.v. mavazi, talaka
        9. Gharama kali ya kununulia vifaa/ada ya kuingia mtandaoni
        10. Kutopata muda wa kushauri watoto na kuomba kwa kuwa mtandaoni kila mara.
        11. Wanafunzi kutosoma jioni/kupoteza muda
        12. Kuvunja uchumba
        13. Vifaa vya mtandaoni kama simu/kompyuta huleta magonjwa ya macho na kansa
      • KUPINGA (Umuhimu)
        1. Kupasha habari za taifa na kimataifa
        2. Kuelimisha k.m. kuhusu afya
        3. Kuburudisha k.m. vibonzo
        4. Matangazo ya biashara
        5. Ajira k.m. wahariri, wauzaji
        6. Mapato kwa serikali
        7. Kutangaza nafasi za ajira
        8. Elimu k.m. uchambuzi wa vitabu vya fasihi na mashairi
        9. Mpwito wa wakati
        10. Kukuza umoja(kurasa za fesibuku na wazapu)
        11. Kurahisisha utafiti
    4. Hitimisho- Mtahiniwa ahitimishe insha yake kwa kutoa msimamo wake kwenye aya ya mwisho.
      Tanbihi : Mtahiniwa lazima ajadili pande zote za swali.Akijibu upande moja pekee asipite alama 10.
  3. Andika kisa kinachodhihirisha maana ya methali;
    Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
    Hii ni insha ya methali.Yafuatayo yazingatiwe:
    1. Kichwa/anwani- iwe methali yenyewe
    2. Utangulizi-Hapa mtahiniwa anaweza kufafanua maana ya methali na matumizi yake. Maana ya methali ni kwamba mtu wa kutegemewa katika familia au sehemu yoyote ile akitoweka, waliokuwa wakimtegemea huteseka.
      Ikumbukwe kwamba utangulizi huu si lazima. Mtahiniwa anaweza kuanza kisa chake moja kwa moja bila utangulizi huu.
    3. Mwili-Hapa, mtahiniwa abuni kisa kinachothibitisha maana ya methali hii. Kisa kiangazie sehemu zote mbili za methali. Pawe na mhusika ambaye kwa sababu ya cheo/hadhi/mamlaka au mali na uwezo, wengine wanamtegemea.Pia aonyeshe jinsi waliomtegemea wanateseka baada ya kutoweka kwake.
    4. Hitimisho- Mtahiniwa ahitimishe insha yake ifaavyo kutokana na kisa chake.
  4. Andika insha itakayomalizikia kwa maneno yafuatayo:
    …Nilijitolea mhanga na msaada wangu ukazaa natija kwa wengi.
    Hii ni insha ya mdokezo/masimulizi. Yafuatayo yazingatiwe:
    1. Kichwa-Mtahiniwa abuni kichwa mwafaka. Kisizidi maneno sita.
    2. Abuni kisa kinachoafiki mdokezo huu.
    3. Kisa lazima kionyeshe kujitolea mhanga(kujitolea kwa vyovyote vile licha ya vikwamizo au hali ngumu) na kuzaa natija(kufaidika). Kisa kinaweza kuafiki hali zifuatazo miongoni mwa nyingine;
      • Safarini ,anayejitolea kuwanusuru wengine wakati chombo au gari lilikuwa linaenda mrama
      • Kiongozi wa wafanyakazi kuwatetea wenzake licha ya pingamizi kutoka kwa mwajiri hatimaye hali yao ya kufanya kazi inaboreshwa
      • Yeye kama mtoto aliyeajiriwa kuwasaidia ndugu zake na wazazi wakafaidika.
        Zingatia hali nyingine zinazoafikiana na dondoo.
        Tanbihi
        Mtahiniwa lazima ajihusishe kwenye masimulizi.Asipojihusisha amepotoka kimaudhui na asipite kiwango cha D. Akikosa kumaliza kwa dondoo alilopewa lakini kisa kiafikiane nalo, amepungukiwa kimtindo. Akiongezea maneno baada ya dondoo au katikati achukuliwe kuwa ana upungufu wa kimtindo.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Maranda Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?