Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Alliance Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

QUESTIONS

 1. UFAHAMU
  Soma makala yafuatayo kwa makini kisha ujibu maswali yanayofuata. (ALAMA 15)
  Katika ofisi yake moja alimfuma mpiga taipu akimwambia karani mwingine, "... kamnyoa yule yatima shilingi zake elfu mbili maskini..." Lakini maongezi yalikatika kwa kutokeza Salma, na Salma hakutaka kuambiwa nani 'kinyozi
  "Yupo?" aliuliza "Ke -keshaondoka, bibi," alibabaika mpiga taipu, "Kaelekea ofisi ya kati."
  Salma naye alielekea ofisi ya kati. Huko pia mlango wa ofisi yake aliukuta umefungwa, na watu kadha wakimsubiri nje.
  "Ameitwa na Mheshimiwa Waziri, tafadhali kaa umsubiri bibi," mwandishi alimwambia Salma, na Salma akapweteka juu ya kiti pamoja na wengine kumsubiri Karim.
  "Je, umesikia mambo hayo?" Sauti ilinong'ona karibu na Salma, miongoni mwa watu waliokuwa wakisubiri na kumfanya Salma, atege sikio. "Usifanye mzaha, mjomba wangu kafutwa. Shilingi mia nane ndipo alipopewa waraka wa nyumba yake. Mzee mmoja jirani yangu kasumbuliwa we-c-e, hata na kutahamaki kupanguswa haki yake yote. Na wangapi! Na wangapi! Basi na weye jihadhari."
  "Yatakwisha hayo! Hoja umoja wetu," mtu mmoja alieleza, "A-a-a! Na hawa wanaodhulumiwa haki zao hufanyaje?" Sauti nyingine iliuliza.
  "Wanalo?" Ilijibiwa. "Labda humjui mtu huyu weye. Mkuu wa Polisi nduguye kwa baba na pangu pakavu atapita wapi...?"
  "Hakuna pa kupita," Salma alijibu rohoni mwake, yeye akiwa ndiye mwenye kumjua kuliko wote.
  Hali kadhalika, Salma alijua kuwa pengine Karim hatarejea siku ile na hata angerejea kauli yake isingemrudi nyuma. Akiwaacha wale watu wakijadili juu ya haja iliyopo ya mabadiliko kwa nchi nzima iliyojaa dhuluma, Salma aliona afadhali aende tena kwa mama yake akamjaribu, ingawa tama haikuwapo.
  Alipoingia Mbiju na gari lake jekundu, alimkuta mamake na birika mkononi akitilia maji bustani yake ya maua, kavaa kanzu nyeupe, ya kukokota, rangi ya bahari. Alionesha mtu mzima tena, ingawa umaridadi ulimpa nuru.
  "Karibu," alisema huku akizungusha birika katika shina la mwasumini. "Leo pia hukumleta Karim."
  "Kashughulika na makazi yake," Salma alisema, mkono wake mmoja mfukoni na mwingine kashika mkoba wake uliokuwa ukining'inia chini ya ukwapa.
  ikumbuka kuliko Samir huko Ulaya. Hupita miezi sita hajaniletea barua, na anapoleta huwa kashikwa na haja. Hiyo huko ndani ya barua yake, nimeipata jana,
  laka shilingi elfu kumi. Ikiwa barua zenyewe za kutaka mapesa tu amonge huyo katiri wake wa Kizungu, afadhali asiniletee," Bibi Adili alisema huku akikung'uta birika tupu chini ya shina la mwaridi. Laiti angelizikata yeye mwenyewe ningempelekea japo nusu yake, lakini haja hizo zimeanza tangu kupambana na huyo kafiri wa Kizungu, anazitaka amhonge Mzungu wake, na sisi atufanye mahayawani kama yeye. Sipeleki hata senti moja"
  Salma ambaye hapo kabla hakuwa na tamaa ya kupata mradi wake, sasa alivunja moyo kabisa kabisa kwa maneno ya mama yake. Salma mwana mpenzi kuliko wote, atanyimwa alichotaka, seuze yeye Salma ambaye miezi miwili iliyopita alipewa shilingi elfu tatu.
  (Unukuzi kutoka Nyota ya Rehema, S.A Mohamed)
  1. Kwa kurejelea muktadha wa ofisini, fafanua aina sita za mabadiliko yaliyohitajika nchini kwa mujibu wa masimulizi haya. (alama 6)
  2. Thibitisha kwamba Salma hakuwa mgeni katika ofisi ya kwanza aliyozuru. (alama 4)
  3. "Haijambo wewe unanikumbuka kuliko Samir. Fafanua jinsi kauli hii haikuwa na ukweli kwa kumrejelea Salma. (alama 1)
  4. Taja mambo mawili yaliyomkatisha tamaa Salma kuhusu ufanisi wa ombi aliloendea kwa mama yake. (alama 2)
  5. kwa kuzingatia maana zilizo katika kifungu, andika vinyume vya matumizi ya lugha yafuatayo. (alama 2)
   1. Kutahamaki
   2. Pangu pakavu
 2. UFUPISHO (alama 15)
  Mikopo ni njia mojawapo inayotumiwa na watu wengi kwa lengo la kujiendeleza na kujikuza kiuchumi na kwa hivyo kukopa ni jambo lisilokwepeka. Mikopo inakubalika katika mataifa yote ya ulimwenguni na kwa sababu hiyo, mathalani, serikali nyingi hurasimisha ardhi za wananchi kwa ajili ya kutumika katika kukopa kutoka kwenye taasisi rasmi. Kutokana na uzoefu, na labda urahisi wa namna fulani, watu wengi hupendelea mikopo isiyo rasmi inayopatikana kwenye mikoba na vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa.
  Ikumbukwe kwamba haiwezekani kupata mkopo wa pesa kutoka kwenye taasisi rasmi bila kulipa deni. Ili kuonyesha uaminifu wake na uhakika wa kurejesha fedha za wenyewe, mkopaji hulazimika kuweka rehani nyumba, hatimiliki ya ardhi, mshahara wake kama yuko kwenye ajira rasmi au mali yake nyingine yoyote kama gari. Hii huwa ndiyo dhamana ya mkopo wake. Dhamana hii husimama kama mbadala wa mkopo ili kulipia deni taraa mkopaji atashindwa kurudisha fedha alizokopa.
  Watu wanaokopa mikopo wanaweza kukumbwa na hatari mbalimbali kutokana na kulemewa na kulipa madeni yao. Kushindwa kusimamia biashara au miradi wanayoanzisha kwa mikopo hiyo ni miongoni mwa hatari hizo. Wanaoshindwa kudhibiti biashara au miradi yao hukosa kupata fedha za kulipia madeni yao kwa sababu ya kuhasirika.
  Aidha baadhi ya wakopaji huwekeza kwenye miradi isiyozalisha faida na kwa hivyo mtaji wao unamomonyoka na hata kumalizika kabisa na kwa hivyo wanapata hasara mara mbili ya kupoteza mtaji ambao ni mkopo na kukosa fedha za kulipia mkopo wao. Kuna baadhi ya watu wanaoomba mikopo na kwenda kuitumia katika anasa na sherehe na kuishia kufilisika. Hawa ni wakopaji ambao hukopa bila mipango. Ole wao wanaoomba kwa njia hii!
  Kadhalika hatari nyingine ya kukosa kulipa madeni ni kwamba mali iliyowekwa rehani inaishia kwa mauzo ya kupigwa mnada. Aghalabu, hii inapotokea, wanaoathirika moja kwa moja ni wakopaji, familia zao, wafanyikazi na jamii inayomtegeme
  Kuna haja ya kutafuta namna ya kuwanusuru wakopaji kutokana na adha hii. Wakopaji wanafaa kushirikishwa katika namma bora za kutumia fedha za mkopo kwa ajili ya uwekezaji endelevu. Vilevile, wanafaa kuelimishwa kuhusu mbinu za kulipia madeni ili waepuke kufilisika. Kwa mfano, wanaweza kushauriwa waanze kulipa mikopo mara tu biashara yao inapoanza kushika japo kidogo kidogo ilmuradi bandu bandu huisha gogo.
  Baadhi ya wakopaji hushindwa kulipa madeni kwa sababu ya kukopa mikopo mikubwa sana kuliko uwezo wao wa kulipa. Hawa ndio wanaostahili kutathminiwa kwa kina kabla ya mikopo yao kuidhinishwa kama njia mojawapo ya kuwaepusha kujiingiza katika jinamizi la kushindwa kulipa madeni. Waama, baadhi ya mashirika ya kifedha hutoa mikopo kwa awamu kama namna ya kuwadhibiti wakopaji wasibadhiri fedha za mkopo. Imedbibitishwa kwamba mbinu hii imewafaa baadhi ya wakopaji.
  Kijumla basi, hamna shaka kwamba mikopo ni namna ya kujiendeleza kiuchumi na ni sharti watu wakumbatie uwajibikaji mbele ya mikopo ili kujiepusha kujiingiza katika lindi la rufukara
  1. Tumia maneno 80 kuandika mawazo yanayodokezwa katika aya mbili za kwanza. (alama 5, 1 utiririko)
  2. Kwa kurejelea aya za tatu hadi saba, eleza hatari zinazowakumba wakopaji na suluhisho kwa hatari zenyewe. (Maneno 80-85) (alama 8,1 utiririko)
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Andika ufanano mmoja kati ya sauti zifuatazo.
   1. /v/ na/th/
   2. /t/ na /l/
   3. /k/ na /f/
   4. /m/ na /z/
  2. Andika maneno yenye miundo ifuatayo.
   1. nazali, konsonanti, irabu ya juu nyuma, irabu ya kati nyuma
   2. Konsonanti, irabu ya mbele kati, kipua, kiyeyusho, irabu ya chini tandazwa.
  3. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wingi. Wembe alionunua kwenye duka umemsaidia kuukata ukucha. (alama 2)
  4. Andika neno lenye mofimu zifuatazo: Kikanushi cha nafsi ya kwanza umoja, hali timilifu, yambwa wingi, mzizi -p- na kiishio.
  5. Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa. Ng'ombe hawa na wale walivuka mto huo kwa utaratibu.
  6. Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo.
   1. Mwanafunzi aliadhibiwa kwa kuwa alikosea mwalimu. (Geuza maneno yaliyopigiwa mstari kuwa nomino) (alama 2)
   2. Nguo zilinunuliwa juzi. Nguo ziliuzwa kwa bei ghali. (Unganisha kuunda sentensi changamano) (alama 2)
   3. Mapambano baina ya mwanadamu na mazingira yalizua fasihi. (Anza kwa: Fasihi...)
  7. Tunga sentensi yenye kishazi tegemezi ambacho ni;
   1. kivumishi
   2. kiunganishi
   3. cha masharti
  8. Tunga senstensi moja yenye nomino katika ngeli ya U-I na kivumishi cha idadi isiyodhahiri(alama 1)
  9. Tunga sentensi yenye mpangilio ufuatao:
   RH+RH+Ts+N+V
  10. Geuza sentensi ifuatayo iwe katika hali ya mazoea.
   Kisu kinachonolewa ndicho kinachopata.
  11. Eleza matumizi ya 'kwa' katika senstensi ifuatayo. (alama 3)
   Moja kwa tano ya watu waliosafiri kwa gari la moshi walikula wali kwa mchuzi.
  12. Akifisha sentensi ifuatayo. (alama 1)
   kahindi alipanda matatu nambari saba kisha akamuuliza dereva gari hili litanifikisha ukunda.
  13. Kwa kutumia kitenzi kilicho katika mabano geuza sentensi iwe katika kauli uliyopewa. (alama 1)
   Mgonjwa huyu hawezi ....................chakula mpaka apate fahamu. (pa-tendeka) (alama 2)
  14. Andika katika hali ya ukatavu
   Sisi ndisi wanafunzi.
  15. Nyooka ni kwa pinda,___ni kwa dhahiri, na___ni kwa hakika (alama 2)
  16. Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya kasi na kazi. (alama 2)
  17. Tumia kivumishi kizalishwacho na kitenzi fisidi kutunga sentensi iliyo katika wakati ujao hali endelevu wingi
  18. Ainisha yambwa katika sentensi ifuatayo.
   Mwalimu aliwanunulia zawadi nzuri kwa shilingi elfu kumi.
  19. Onyesha kwa kutumia sentensi mbili jinsi neno shuleni linaweza kuwa nomino na kielezi (alama 2)
  20. Yakinisha katika umoja. Msipokuwa wenye bidii hamtayapata mafanikio maishani.
  21. Ainisha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia uamilifu wake.
   Funga majani matano matano kwa kila fungu. (alama 2)
  22. Tunga sentensi katika ngeli ya KI-VI kuonyesha kihusishi -na- ya mtendaji (alama 1)
  23. Tunga sentensi ukitumia kitenzi -p-katika kauli ya kutendana (alama 1)
 4. ISIMUJAMII(alama 10)
  Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali.
  "Baada ya mjadala mrefu kuhusu mswada huu na kuzingatia sheria za bunge hili tukufu, kifungu cha 4, kipengele cha 6, ibara ya 3, ndugu zangu ningependa kutangaza kupitishwa kwa mswada huu na sasa utawasilishwa kwa rais kusubiri sahihi yake. Kupitishwa kwa mswada huu kwa kauli moja ni tukio la kihistoria kwa bunge hili. Tutaweza kufikia the two third rule..."
  1. Sifa mbili za sajili ya bunge zinadhihirika katika kifungu hiki. Andika sifa zozote tano huku ukitoa mifano mwafaka. (alama 2)
  2. Fafanua vipengele vingine vitatu vya mitindo ya mawasiliano ambayo mbunge angetumia katika kufanikisha mawasiliano yake. (alama 3)
   Tamu sana! Very sweet! Very nutritious! Onja ujionee! Nunua. Nunua leo. Usikose mummy. Mchukulie mtoto. Fifty na Fifty! Hamsa. Fifty. Bure kwa bure! Bei ya starehe! Burudika.
  3. Tambua sajili hii (alama 1)
  4. Eleza sifa nne za sajili hii kwa kurejelea kifungu. (alama 4)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. UFAHAMU
  1. Mabadiliko yaliyohitajika 
   • Mayatima kunyanyaswa kwa kunyang'anywa pesa.
   • Kufunga milango ya ofisi za umma
   • Kuwepo kwa foleni ndefu za watu wanaosubiri kuhudumiwa katika ofisi za umma
   • Wanaostahili kuwahudumia raia kutokuwepo ofisini ili kuwahudumia.
   • Kutoa rushwa / mlungura ili kutimiziwa haki yako.
   • Wananchi kunyang'anywa/kuhiniwa haki zao.
   • Mapendeleo/ubaguzi katika uajiri, kuajiri watu kwa kuangalia ubusiano na kujuana. (hoja chanya au hasi zikubaliwe
  2. Salma hakuwa mgeni ofisini hapo kwa sababu zifuatazo:
   • Alipofika ofisini mazungumzo baina ya taipu na karani yalikatika ghafla kwani walimjua
   • Haulizwi jina na mpiga taipu anapofika ofisini.
   • Anapoulizwa kwa neno moja 'yupo anajibiwa kwa kuambiwa kuwa ameondoka. Hamtaji mhusika. .
   • Mpiga taipu anamjibu akibabaika kwa sababu anamjua Salma ni nani. 4 x 1-4
  3. Ziara za Salma Mbiju (kwa mamake) hazikuwa na lengo la kumjulia hali bali kumtaka mamakc ampe msaada / pesa.
  4. Samir, ambaye alikuwa mtoto mpendwa, hangetumiwa chochote na mamake seuze yeye? Wiki mbili zilizopita alikuwa amefika hapo na kupewa shilingi elfu tatu kwa hivyo hakutarajia kupewa chochote.
  5. Vinyume vya;
   1. kutahamaki - kutumia ; kusahau
   2. pangu pakavu -matajiri wakwasi.
 2. UFUPISHO ( ALAMA 15)
  1.    
   • Mikopo hutumiwa na watu wengi ili kujiendeleza kiuchumi.
   • Mikopo inakubalika kote ulimwenguni
   • Serikali nyingi hurasimisha ardhi za wananchi ili kutumika kukopa kutoka kwenye taasisi rasmi.
   • Watu wengi hupendelea mikopo isiyo rasmi.
   • Haiwezekani kukopa kutoka kwenye taasisi rasmi bila kulipa deni.
   • Wakopaji hutumia mali yao kama rehani wanapokopa.
   • Dhamana husimama kama mbadala wa mkopo.
  2. Hatari
   • Hushindwa kusimamia biashara / miradi wanayoanzisha kwa mikopo.
   • Hawa hukosa kupata pesa za kulipia madeni kwa kuhasirika.
   • Baadhi huwekeza kwenye miradi isiyozalisha faida na kupoteza kila kitu.
   • Wengine hutumia mikopo katika anasa na kufilisika.
   • Mali iliyowekwa rehani luuuzwa (hupigwa mnada)
    Suluhisho
   • Wakopaji wanafaa kushirikishwa katika namna bora za kutumia fedha za mkopo kwa ajili ya uwekezaji endelevu.
   • Wanafaa kuelimishwa kuhusu mbinu za kulipa madeni ili waepuke kufilisika.
   • Wakopaji wanastahili kutathminiwa kwa kina kabla ya mikopo yao kuidhinishwa.
   • Mashirika yanweza kutoa mikopo kwa awamu ili kuwadhibiti wakopaji wabadhirifu.
    Hoja za kuonyesha hatari 4 x 1-4
    Hoja za kuonyesha suluhisho 4 x1
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1.    
   1. vikwamizo
   2. Hutamkiwa kwenye ufizi / masine
   3. sauti sighuna
   4. sauti ghuna
  2.    
   1. nguo
   2. temwa
  3. sijawapa
  4. Nyembe walizonunua kwenye maduka zimewasaidia kuzikata kucha. 1 x 1=1
  5. Magombe haya na yale yalivuka jito hilo kwa utaratibu.
  6.        
   1. Adhabu ilitolewa kwa mwanafunzi na mwalimu kwa kufanya makosa au Makosa ya mwanafunzi kwa mwalimu yalimfanya apewe adhabu au Mwalimu alimpa mwanafunzi adhabu baada ya kufanya makosa.
   2. Nguo zilizonunuliwa juzi ziliuzwa kwa bei ghali au Nguo ambazo zilinunuliwa juzi ziliuzwa kwa bei ghali.
   3. Fasihi ilizushwa na mapambano baina ya mwanadamu na mazingira. 1 x 1=1
  7.      
   1. Nguo zilizoraruka zimeshonwa au Nguo ambazo ziliraruka zimeshonwa. 1 x 1-1
   2. Ijapokuwa nilienda kwake mapema sikufanikiwa kuonana naye au Maadamu umefika
    mapema tutaanza mkutano.
   3. Usalama ukiimarika watalii wengi watazuru humu au Angesoma kwa bidii, angepita vizuri.
  8. Miti michache ilikatwa.
  9. Miongoni mwa wanariadha wa Kenya kuna wanariadha hodari
  10. kisu kinolewacho ndicho kipatacho.
  11.      
   1. kwa tano-akisami /uakifishaji wa idadi
   2. kwa gari-kitumizi /kifaa
   3. kwa mchuzi -pamoja na
  12. Kahindi alipanda matatu nambari saba, kisha akamuuliza dereva, "Gari hili litanifikisha
   Ukunda?"
   Kahindi1⁄2. saba, dereva, 1⁄2,""1⁄2, Gari. Ukunda-1⁄2.?- 1⁄2-1⁄2 x 6=3
   Act
  13. kupeka
  14. Sisi si wanafunzi
  15. fiche, shaka.
  16. Dereva yeyote atakayeendesha gari kwa kasi atapoteza kazi yake. (kadiria) 2x1=2)
  17. Viongozi fisadi watakuwa wakifishwa mahakamani.
  18.    
   • yambwa tendewa/ kitondo -aliwanunulia
   • yambwa tendwa/ kipozi -zawadi nzuri
   • yambwa ala /kitumizi-shilingi elfu kumi
  19. Shuleni mwetu mna majengo mapya. (nomino)
   Mashindano ya kandanda yanafanyika shuleni. (kielezi)
  20. Ukiwa mwenye bidii utapata fanikio maishani.
  21. Sentensi agizi
  22. Kiti kilibebwa na seremala.
  23. Watoto walipana chakula
 4. ISIMUJAMII (alama 10)
  1. Matumizi ya sentensi ndefu. Sentensi ya kwanza ina zaidi ya maneno 30.
   • Matumizi ya msamiati maalum. "mswada, bunge"
   • Vifungu vya sheria vinarcjelewa. "kifungu cha 4..."
   • Matumizi ya lugha sanifu. "sentensi ya kwanza ina lugha sanifu"
   • Matumizi ya lugha kavu. "lugha inayotumiwa haina mapambo"
   • Matumizi ya lugha ya heshima. "sheria za bunge hili tukufu..."
   • Kuchanganya ndimi. "kufikia the one third rule..."
   • Lugha ya kuibua utangamano. "ndugu zangu" (zozote mbili)
  2. Matumizi ya uradidi/urudiaji. "mheshimiwa spika"
   • Matumizi ya viziada lugha au ishara za mwili au uso
   • Kutajwa kwa wahusika kwa majina. " Mheshimiwa Tunu"
   • Wabunge kukatizana kalima.
   • Matumizi ya lugha ya mzaha na kukejeliana.
   • Lugha ya maswali na majibu
   • Matumizi ya utohozi. "spika, bajeti"
   • Matumizi ya lugha amrishi hasa na spika. "Mheshimiwa... keti!"
   • Mtindo maalum wa kuanzisha na kuendeleza mjadala. "Mheshimiwa Bwana Spika"
   • Lugha ya kushawishi. "ndugu zangu waheshimiwa naomba"
    (zozote tano za kwanza 5x1=5)
    TANBIHI: Kila sifa iandamane na mfano au maelezo.
    Sifa bila mfano, alama nusu, mfano bila sifa sufuri.
    Tamu sana! Very sweet! Very nutritious! Onja ujionee! Nunua. Nunua leo. Usikose mummy. Mchukulie mtoto. Fifty na Fifty! Hamsa. Fifty. Bure kwa bure! Bei ya starehe! Burudika.
    1. Sajili ya biashara/ sokoni:Anasema nunua leo
    2. Eleza sifa nne za sajili hii kwa kurejelea kifungu.
     • Lugha ya kuvutia hutumiwa, bure kwa bure ili kuvutia wateja.
     • Lugha shawishi mno hutumiwa, mfano bei ya starehe sana/ usikose mummy ili kuwavutia wanunuzi.
     • Kuna matumizi ya takiriri nunua, nunua leo
     • Kuchanganya ndimi, very sweet ili kuvutia wateja wengi.
     • Huwa na ucheshi na porojo ili kuwavutia wateja. Mfano, bure kwa bure Lugha nyepesi hutumika ili kuwasilisha. Bei ya starehe
     • Ubora wa bidhaa husisitizwa, ili kuwavutia wateja. Tamu sana
     • Kuna upigaji chuku mwingi ili kuwavutia wateja. Mfano bure kwa bure.
     • Sentensi fupi fupi hutumika kurahisisha mawasiliano. Mfano nunua, nunua leo.
     • Lugha ya mafumbo-fifty na fifty (ni mia)
     • Mwanafunzi akitoa hoja kisha akose kusema ili, au akose kutoa sababu, alama zake ni nunge.

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Alliance Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?