Kiswahili Paper 2 Questions - Maseno Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

QUESTIONS

 1. UFAHAMU (ALAMA 15)
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali
  Katika karne hii, juhudi zetu za kushughulikia changamoto za usalama zimeimarishwa Zaidi kwa matumizi ya teknolojia. Kuimarika kwa ufungaji milango, matumizi ya vifaa vya kamsa, njia za kisasa za utambuzi, utafiti na uchunguzi wa kiuhalifu ni baadhi tu ya maendeleo yaliyoafikiwa na jamii ili kujihami. Sasa hivi huduma zinazotolewa na polisi kwa umma zimewafikia watu kwa njia rahisi. Hata hivyo, maendeleo haya ya kiteknolojia yamehusishwa na hatari fulani. Baadhi ya mifumo inaweza kutumiwa vibaya au ikawa na athari zisizotarajiwa kama vile kumdhuru mtu asiyekusudiwa.
  Matumizi ya sayansi na teknolojia kuukabili uhalifu wa jinai si suala geni. Tangu kuvumbiliwa kwa kikosi cha askari polisi katika karne ya kumi na tisa, utendakazi na maendeleo yake yamepimwa kwa kigezo cha kuimarisha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika harakati za utoaji huduma kwa raia. Tumeshuhudia maafisa wetu wakitumia vifaa vya utambuzi kwa alama za vidole na matumizi ya vifaa visivyotumia nyaya katika mawasiliano. Lakini kutokana na kuimarika kwa ubunifu wa wahalifu pana haja ya vikosi vyetu kujipiga msasa zaidi ili kuzuia au kuzima kabisa njama za kihalifu. Matumizi ya teknolojia katika kuzuia visa vya uhalifu yameanza kukubalika na wanajamii kama sehemu ya maisha yao. Leo hii kuna vifaa vya kuchunguza iwapo mtu ana kifaa chochote cha chuma hususan silaha ndogondogo wakati aingiapo kwenye kumbi za umma au anapoabiri magari ya uchukuzi wa umma. Kifaa hiki kimezuia pakubwa uhalifu wa utekaji nyara uliokuwepo awali hasa miongoni mwa magari ya umma mijini. Aidha vifaa vya kudhibiti kasi ya magari vimeimarisha usalama barabarani. Uwekaji wa taa za umeme kwenye viunga vya miji huuhakikishia umma usalama wao na vilevile kuchangia kuwafichua wavamizi.
  Kamera za siri kwenye ofisi za kibinafsi, majengo ya umma na kwenye baadhi ya barabara za miji mikuu huwa hifadhi ya matukio anuwai na hivyo kuwa muhimu wakati wa kesi zinazohusisha uvamizi au uhalifu mwingine wowote. Vifaa vidogo vinavyotumia mawimbi ya kielektroniki na ambavyo hutiwa mifukoni ni muhimu wakati wa mawasiliano ya dharura.
  Huwasaidia sana watu wenye umri mpevu ambao huwa ni windo jepesi la wahalifu. Aidha huwapa hakikisho la kuwa huru kuyaendesha maisha yao kinyume na awali ambapo maisha yao yalitawaliwa na unyanyapaa baada ya kusikia au kuhusika katika visa vya uhalifu. Kwa sasa teknolojia inayotumia miale ya kufichua silaha haramu zilizofichwa au kutambua mtu anayenuia kupenyeza mihadarati kwa kumeza vidonge inagonga ndipo. Njia hii hufanya hivi bila kumkaribia mshukiwa na kuepuka hali ya kuhatarisha maisha ya afisa wa ukaguzi. Aidha huwezesha mshukiwa kutambuliwa mara moja na hatari husika kutandarukiwa bila ajizi.
  Licha ya ufaafu wa teknolojia ya kisasa katika kuzuia au kuzima kabisa visa vya uhalifu, athari zake hasi zimeweza kushuhudiwa. Kwa mfano matumizi ya vifaa vya kwenda kwa kasi kuwafuata wahalifu yanaweza kuwa hatari kwa mtumiaji, mshukiwa au hata raia asiyehusika. Kifaa cha kuzima kasi ya magari kwa mbali kinaweza kulisimamisha gari ghafla na kusababisha maafa makubwa. Matumizi ya mwangaza mkali au gesi kama njia ya kumdhibiti mhalifu yanaweza kusababisha ulemavu wa kuona au hata kupumua. Baadhi ya vifaa ambavyo hutumia miale vinaweza kuwa na athari ya kudumu na hata kusababisha maradhi ya kansa. Inapendekezwa kuwa matumizi ya teknolojia kuangamiza uhalifu yazingatie haki za binadamu. Aidha njia husika iwe nafuu, pawe na uwazi na uwajibikaji katika matumizi yake na vilevile matumizi yake yazingatie maadili.
  1. Kwa mujibu wa kifungu wahalifu bado wanazidi nguvu asasi za kiusalama katika jamii. Eleza. (alama 1)
  2. Onyesha jinsi teknolojia imeimarisha usalama katika sekta ya usafiri. (alama 1)
  3. Ni kwa njia gani teknolojia imesaidia kupatikana kwa haki? (alama 2)
  4. Eleza manufaa ya kutumia miale kama njia ya kuzuia uhalifu. (alama 3)
  5. Taja mambo mawili ambayo yanafaa kuingoza jamii wakati wa kuteua mbinu ya kuukabili uhalifu. (alama 2)
  6. Teknolojia ya kisasi katika kuukabili uhalifu imeelezwa kuleta changamoto zipi? (alama 3)
  7. Eleza maama ya msamiati huu kama ulivyotumiwa kwenye kifungu. (alama 3)
   1. Viunga
   2. Kuvumbuliwa
   3. Unyanyapaa
 2. UFUPISHO (ALAMA 15)
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali
  Kule kuubali Ukristo kulimaanisha kuuasi Uafrika pamoja na utamaduni wake. Kulimaanisha pia kuikataa miko na matambiko ambayo yalikuwa yanatuunganisha; kulimaanisha kuyakubali maisha na tabia za aina Fulani kutoka bara Uropa. Wamisheni walikuwa wameshambulia maisha ya jamii zetu na kushtumu mila na desturi za waafrika kama vile nyimbo na densi za kuvutia miungu mbalimbali; mambo ambayo yalitokana na misimamo yao kuhusu Imani kama hizi.
  Kwa sababu hii, nchini Kenya kwa mfano, huku Waafrika wakinyanganywa mashamba na rasilimali nyingine zilizotokana na jasho lao, wamisheni nao walinyanganywa roho zao. Hivyo basi mwili na roho ya mwafrika ilikatwakatwa kwa ahadi ya mazuri ya mbinguni Uropa.
  Elimu haikuwa jawabu kwa nyoyo za Waafrika zilizokuwa na njaa kwani ilitukuza maadili ya kikrosto ambayo yalikuwa yamedinda kushtumu kudhulumiwa kwa mwafrika-kimwili. Elimu ya kwanza aliyopata mwafrika ilikuwa ya kumwezesha kuisoma Biblia ili aweze kutekeleza majukumu rahisi kama msaidizi wa wamisheni. Ndipo baadaye elimu ikaanza kuchukuliwa kama kigezo muhimu cha kujipatia kazi nzuri, kuwa na mali na hivyo kuishi maisha mazuri, ingawa katika mfumo wa maisha ya huko Uropa. Mwafrika aliyekuwa amesoma na mkristo alikuwa tayari amejitenga na asili na utamaduni wake. Uhasama kati ya Wakenya na makanisa ya wamisheni; kuanzishwa kwa makanisa yenye misingi yake katika uafrika pamoja na maswala ya kidini ya vuguvugu la Mau Mau, yote yalikuwa mazao ya uhasama wa kitamaduni ulioasisiwa na haja ya wamisheni ya kumbadili mwafrika. Makanisa mbalimbali yalioanza yakiwa na uhusiano wa wamisheni na baadaye kujitenga yalijaribu kuanzisha mfumo wa maombi na elimu ambao ulikuwa sambamba na uliohusiana na matamanio ya jamii ya kiafrika huku yakijumisha baadhi ya tamaduni za kiafrika katika kuabudu na maisha ya kila siku.
  Siku hizi, kanisa nchini Kenya ni zao la wamisheni kutoka Uropa. Wamisheni walikuwa sehemu ya mchakato wa historia yetu- yaani majilio ya wakoloni, au kwa maneno mengine wamisheni, masetla na wazungu wengine walikuwa waajenti wa ukoloni. Imewahi kusemekana kuwa wanabiashara na masetla kutoka Ulaya walifuata miongozo iliyotolewa na wamisheni.
  Katika maeneo mengine barani Afrika, uongoci wa kisiasa uliasisiwa na ombi au shinikizo la wamisheni kutoka nchi ya wakoloni.
  1. Bila kupoteza maana, fupisha aya tatu za kwanza. (maneno 100-110) (alama 10, 2 za utiririko)
  2. Dondoa mambo muhimu yanayojitokeza katika aya mbili za mwisho.(maneno 50-55) (alama 5, 1 ya utiririko)
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Tunga neno linalosheheni sifa zifuatazo za sauti: kiyeyusho cha mdomo, irabu ya kati chini, kikwamizo cha mdomo-meno ghuna, irabu ya nyuma juu. (alama 2)
  2. Ainisha mofimu katika neno. (alama 3)
   lilimchwea.
  3. Tambua aina za viwakilishi katika sentensi. (alama 2)
   Je nyinyi mnafahamu yule?
  4. Tunga sentensi iliyosheheni maneno yafuatayo
   Nomino katika ngeli ya U-I, umoja, kivumishi kimilikishi nafsi ya tatu umoja. (alama 2)
  5. Ainisha vitenzi katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
   1. Mtoto analia akila.
   2. Yeye ndiye mwizi.
  6. Akifisha sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti bila kupoteza maana. (alama 2)
   Nilimfahamu Rebeka mwanaye shangazi kama msichana mwadilifu.
  7. Yakinisha sentensi ifuatayo (alama 1)
   Mwizi hakuiba, hakupigwa risasi wala kuaga dunia.
  8. Andika sentensi hii upya katika wakati ujao, hali ya kuendelea. (alama 2)
   Daktari aja hospitalini.
  9. Andika maneno yenye miundo ifuatayo (alama 2)
   1. IKKI
   2. KIIKKI
  10. Eleza matumizi ya kiambishi ji- katika sentensi ifuatayo.
   Walijisifu kutokana na uimbaji wao. (alama 2)
  11. Iandike sentensi upya katika kauli ya kutendea. (alama 2)
   Kijakazi alikula chakula cha babu.
  12. Nomino zifuatazo zinapatikana katika ngeli gani? (alama 1)
   1. Tohara…………………………………………………………………………………………..
   2. Nyembe…………………………………………………………………………………………
  13. Bainisha shamirisho katika sentensi hii. (alama 2)
   Shati la Wafula lilishonwa na Omari
  14. Tambua vishazi katika sentensi: (alama 2)
   Mfungwa aliyetoroka jela amenaswa na majasusi.
  15. Changanua sentensi kwa njia ya mistari. (alama 2)
   Sote tutapika chakula vizuri.
  16. Onyesha virai katika sentensi. (alama 2)
   Ukuta ule mrefu umebomolewa kwa tingatinga.
  17. Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa wingi. (alama 2)
   Simu hii iliharibika tulipokuwa tukipita vichakani
  18. Andika kinyume. (alama 2)
   Kubabaika ni kwa……….kama vile kutawanya ni kwa kukusanya na kulewa ni kwa…………
  19. Tunga sentensi moja kutofautisha kati ya kuna na ghuna. (alama 2)
  20. Andiika sentensi ifuatayo katika usemi halisi:-
   Mwalimu alitaka kujua walikotoka kuenda wanafunzi. (alama 2)
  21. Tambua kiima katika sentensi ifuatayo (alama 1)
   Shamba lililimwa na mama.
 4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
  Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu hapo chini.
  Bwana Spika, napinga hoja ilivyo na naomba kubadilisha hoja ili wanaume na wototo wa kiume nao wajumuishwe kwa maana wao pia hulawitiwa. Bwana Spika, visa vya watoto wa kiume kulawitiwa vimeongezeka na wanaotenda vitendo viovu kama hivi yapasa wahasiwe.
  1. Fafanua sifa tano za sajili zinazojitokeza katika kifungu ulichokisoma. (alama 5)
  2. Mbali na sifa ulizozitaja hapo juu, fafanua sifa nyingine tano zisizojitokeza katika kifungu. (alama 5)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions - Maseno Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?