Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Cekenas Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. SEHEMU YA A: HAMU YA HAMO
    Hamo alirauka majogoo kuanza maandalizi ya mapema. Hakutaka kukosa sherehe ya sikukuuu ya Jamhuri kama alivyokuwa amekosa ile ya mashujaa. Siku hiyo alipofika kwenye lango kuu la uga ambako sherehe zilitendeka, askari mmoja mwenye kofia nyekundu, miwani myeusi na bunduki kifuani alimnyoshea kidole na kumwambia, “Kwenda nyumbani kijana . Unafika hapa baada ya rais kuingia kwani wewe ni rais wa Marekani?” swali hilo lilimsumbua kwa siku kadhaa, akawachukia maafisaa wa usalama, na likamtwanga kwa nguvu sana asubuhi ya Jamuhuri. Alimaliza maandalizi  na kupiga milundi uwanjani.
    “Una kitambulisho?” Hamo aliona ajibu kwa kukitoa na wakati huu afisaa wa usalama alimruhusu aingie bila maswali zaidi. “Huyu amechoka sana. Hata sare yake ya bluu imechujuka jamani!” Hamo alijiambia akiingia uwanjani. Uwanja ulikula watu bila kushiba, kwani  kulikuwa na mapengo ya hapa na pale kama kinywa kilichong’oka meno. Bw. Hamo alitafuta nafasi karibu na jukwaa lakini katika sehemu iliyotengwa “wananchi wa kawaida.” Hayo maneno matatu yalikuwa yamemsumbua Hamo akijiuliza mbona wale wengine walijiona wasiokuwa wa kawaida. Hata, hivyo, hakutaka fikra hizo ziboronge hamu yake ya siku.
    Basi, bendi ya wanajeshi ilisikika na kiongozi wao akawa na fimbo fulani aliyoizungusha mkononi hapa na pale na wakati mwingine kuirusha juu, akakimbi kuidaka kabla ya kugusa ardhini. Vikosi vitatu vya wanajeshi waliovalia sare za rangi tatu tofauti: nyekundu, bluu na nyeupe viliingia kwa kupendeza. Kila mwanajeshi alikuwa ameishika bunduki  yake kwa mkono wa kulia, na kuurusha mkono wa kushoto mbele na nyuma kana kwamba hawakupendezwa na mikono yao, ila mikono hiyo ilirushwa kwa pamoja na kuunda safu nzuri, ungedhani mikono hiyo iliunganishwa na kufungwa. Kiongozi mmoja aliyekuwa na kitara mkononi alisimama katikati na kupaaza sauti kubwa ilyosikika kanakwamba alikuwa na kipaza sauti. Kwa pamoja wanajeshi waliichapa miguu yao chini kwa nguvu kana kwamba wakimuua nyoka na kutulia tuli! Haya yalimshangaza Hamo kwani alisikia ni kama kiongozi alilia “Hooooo ho!
    Muda ulizidi kuyoyoma na punde si punde rais aliingia kwenye gari lililompa uwezo wa kuwasalimu wananchi. Bw. Hamo alipiga kelele kama wananchi wengine na rais alipopita karibu naye, Bw. Hamo alimwambia “Nakupenda rais!” Rais alitabasamu na kuangalia upande huo huku akiweka viganja vyake pamoja na kuinua juu, ishara ya kwamba, “tu pamoja” , jambo lililomfurahisha Hamo aliyetabasamu nusura aonyeshe magego yake. Burudani iliendelea  pale na wanajeshi wakapendeza kwa vioja na viroja vyao; mara waangalie mbele, mara wapinduke ghafla kama walioumwa na siafu, mara wasukumane mikono na kujipanga vizuri zaidi, mara wawe wawili wawili, waunde ruwaza za kupendeza; haya yote baada ya kilio cha yule kiongozi ambacho Hamo hakusikia kikibadilika pahubwa, kwani kilicheza “Hoooho” na maneno mengine ambayo Hamo aliamini kuwa hayakuwa kwa mojawapo ya lugha alizozielewa.
    Kilele cha siku kilikuwa hotuba ndefu ya rais ya Kiingereza na japo Hamo hakung’amua chochote, alihisi kuwa ilikuwa siku iliyofana, na kwa kuwa rais alimjibu salamu zake kwa heshima kubwa, alijiona kuwa shujaa. Muhimu zaidi alikula yamini kuwa mwanajesi, ambaye ama awe Yule wa “hoooooho!” au Yule wa kurusha na kudaka fimbo kabla ifike ardhini.
    1. Mbona Hamo aliamka wakati wa majogoo (alama 2)
    2. Tofautisha maafisa wawili waliotajwa kwenye kifungu kihulka. (alama 4)
    3. Eleza sifa tatu za rais kulingana na taarifa. (alama 3)
    4. Mbona Homa alikuwa yamini kuwa mwanajesi. (alama 1)
    5. Thibitisha suala la utabaka kwa kurejelea kifungo. (alama 1)
    6. Toa mfano mmoja wa matumizi ya mbinu ya mbinu ya uhuishaji kutoka kwenye kifungo. (alama 1)
    7. Eleza maana ya maneno haya kulingana na taarifa: (alama 3)
      1. uga
      2. boronga
      3. kula yamini
  2. UFUPISHO
    Soma kifungo kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Mirundiko ya taka pamoja na utaratibu usiofaa wa uzoaji wake ni tisho kubwa kwa siha ya umma pamoja na mazingira . Hii ni kwa kuwa taka huwa ni makaazi ya wadudu na wanyama waharibifu kama nzi, mbu, kombamwiko na panya ambao hueneza magonjwa na kuharibu vitu vyenye dhamani. Maji taka nayo, pamoja na mifuko ya sandarusi huwa mastakimu ya wadudu na virusi vinavyoleta magonjwa mbalimbali.
    Mifuko ya sandarusi ina madhara kwa kuwa huziba mitaro ya maji na kuzuia upitaji wa maji. Madhara hutokeza wakati wa mvua za ngarika. Maji haya husababisha mafuriko ambayo huleta hasara ya mali na wakati mwingine ya uhai. Fauka ya haya, mifuko hii huwasakama tumboni wanyama sio wa nyumbani tu, bali wa porini na majini.
    Kwa sababu ya hatari zitokanazo na taka, pana haja kutafuta njia na teknolojia ya kwanza kukabiliana na tatizo hili ili kuyatunza mazingira na siha ya umma. Njia mojawapo ya  kufanya hivi ni kuelimisha na kuhimiza umma kuwa na uangalifu katika matumizi ya bidhaa na raslimali ili kupunguza uzalishaji wa taka. Matumizi ya bidhaa kwa njia ya ubadhirifu huwa chanzo cha uzalishaji wa taka kwa wingi. Kwa mfano, maji ni raslimali ambayo imeendelea kutumiwa kwa ubadhirifu na hiyo uzalishaji maji taka kwa wingi. Raslimali hii inaweza ikatumiwa kwa njia endelevu. Kwa mfano, badala ya kutumia bafu ya nyumbani kuoga mtu anaweza kutumia maji ya karai.
    Watu wengi huchukulia taka kuwa kitu kisicho na manufaa yoyote. Hawajui kuwa kwa kutumia teknolojia endelezi, taka nyingi zinaweza zikageuzwa na kuwa na manufaa mengi. Vijana wadogo sehemu za mashambani wanahitaji pongezi kwa kuwa na utambuzi huu. Wengi, kwa kukosa hela za kununulia mipira ya viwandani, hutumia teknolojia endelezi ambapo taka hugeuzwa na kuwa na manufaa.
    Baadhi ya wananchi wenye ubunifu nao wameanzisha miradi ya kuzoa takataka kutoka majumbani mwa watu kwa ada kisha huzipeleka taka hizi kule zitakakobadilishwa ili ziwe na manufaa. Mifuko na mabaki ya sandarusi hupelekwa katika viwanda vinavyotengeneza bidhaa za plastiki kama matangi, mitungi, sapatu na champali. Taka hizi huwa malighafi  ya kutengeneza bidhaa nungine.
    Taka za chupa na chuma nazo huuzwa katika viwanda vinavyozigeuza kuwa na manufaa tena. Taka za karatasi hutumiwa kutengeneza bidhaa  kama vitabu, katoni, shashi za chooni na magazeti.
    Taka zinaweza pia kugeuzwa kuwa zenye faida kwa kuzitumia kufanyia mboji. Ni muhimu kutambua kuwa si kila aina ya taka inaweza kutumiwa hapa. Taka zinazoweza kufanyiwa mboji ni zile ambazo huoza kwa haraka, kama vile: mabaki ya vyakula mboga na matunda. Kwa sadfa, hizi ndizo taka zinazozalishwa zaidi siku na hasa sehemu za mjini katika maeneo ya biashara kama mikahawa na hospitali. Mtu akiwa na nafasi anaweza kuchimba shimo ambalo atafukia taka ili kutengeneza mbolea. Hii ni njia isiyodhuru mazingira na yenye manufaa kemkem. Kwanza, kugeuza taka ambayo inaweza kuwa hatari na kuifanya iwe yenye manufaa. Kwa hivyo hutatua matatizo ya kiafya yanayoweza kutokana na mirundiko ya taka. Mchanga nao hufaidika kupata virutubishi. Mbolea kama hii inaweza ikatumika kukuzia mboga au maua katia bustani.
    Maji taka, hasa yanayotumika kuosha vyombo, nayo yanaweza kutumika kunyunyizia mashamba madogo ya mboga au bustani za maua. Maji taka haya yanahitaji kutayarishwa njia mahususi ya kuyaelekeza katika mashamba haya baada ya kutumiwa.
    Anglalabu watu wengi wana mazoea ya kuchoma taka. Ni kawaida kupata matanuri ya kuchomea taka  katika baadhi ya mitaa, shule na hospitali. Badala ya kupoteza moto huu bure bilashi, inawezekana pakawekwa birika kubwa au tangi la chuma ambalo litatuma moto huo kuchemsha maji. Maji haya yanaweza yakatumiwa katika shughuli za nyumbani.
    Hata hivyo ni muhimu kukumbuka kuwa kuna baadhi ya taka ambazo ni hatari na huenda zisigeuzwe ili kutumika kwa njia yenye faida.  Taka hizi ni kama vile mikebe au vifaa vingine vyenye kubeba sumu au dawa hatari. Ni bora kuvitupa vifaa hivi katika mashimo marefu au vyoo vya mashimo.
    Kwa vyovyote vile, si jambo muhali kwa  watu popote wanapoishi kulinda siha yao pamoja na kutunza mazingira. Ulinzi na utunzaji huo huhitaji uangalifu mkubwa katika utupaji taka.
    1. Fupisha ujumbe wa aya tatu za kwanza kwa maneno 100. (alama 8, 1 utiririko)
    2. Kwa kurejelea aya ya tano hadi ya tisa, onyesha manufaa ya taka (maneno 80) (alama 7, 1 utiririko)
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Unda maneno yenye muundo wa sauti zifuatazo: (alama 2)
      1. King’ong’o cha kaakaa laini, irabu ya nyuma wastani, irabu ya chini kati.
      2. Kikwamizo hafifu cha koromeo, irabu ya nyuma juu , kiyeyusho cha kaakaa gumu, irabu ya nyuma kati
    2. Andika neno moja lenye silabi za muundo ufuatao. (alama 1)
      irabu, konsonantii +konsonanti, irabu+konsonanti, irabu
    3. Bainisha matumizi ya ‘ki’ katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
      Akiendelea kukichezea, kichuma chake ki motoni.
    4. Unda vitenzi kutokana na nomino zifuatazo (alama 2)
      1. hasidi-
      2. tafakuri-
    5. Tunga sentensi yenye mpangilio wa maneno ufuatao: (alama 2)
      nomino katika ngeli ya U-zi wingi.
      Kivumishi cha pekee
      Kitenzi halisi
      Kielezi cha kiasi
    6. Ainisha viambishi: (alama 2)
      haujiki
    7. Tumia mzizi –ny- kukamiliisha sentensi hii (alama 1)
      Miti ya msitu huo ime ……. mvua katika jimbo hili
    8. Tumia mzizi ‘-ema’ katika sentensi kama: (alama 3)
      1. kivumishi
      2. kielezi
      3. nomino
    9. Mchezaji alipoona kiyu* aliya gugumia maji
      Kando na matumizi haya ya kinyota, taja matumizi mengine mawili ya kiakifishi hiki. (alama 2)
    10. Tunga sentensi ya swali ukitumia kiwakilishi nafsi ambata nafsi ya pili wingi  (alama2)
    11. Andika sentensi hii iwe katika usemi wa taarifa “Nyinyi nyote mkipita nitawanunulia mikate miwili kesho jioni, mwalimu alituambia. (alama 2)
    12. Andika kinyume cha sentensi hii:
      Tajiri wengi walikashifiwa baada ya  kuhamia msituni (alama 2)
    13. Ainisha shamirisho na chajizo: (alama 4)
      Mwanamke mzee alipikiwa chai tamu kwa sufuria kubwa leo asubuhi na mjukuu wake.
    14. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao: (alama 2)
      KN(S ̅  )+KT(t+KN_(2 ) (N+V))
    15. Mohamed alifuzu mtihani huo vizuri kwa sababu alisoma kwa bidii (maliza kwa mtihani huo vizuri) (alama 1)
    16. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielezo cha matawi.
      Lilikuwa limelimwa na wakulima hodari sana. (alama 4)
    17. Andika ukubwa wingi wa sentensi hii
      Mtoto alimuua nyoka mdogo kwa kumpiga kichwani (alama 1)
    18. Ainisha virai vinne katika sentensi hii:
      Vipya kabisa vilivyoagizwa jana sokoni vitanunuliwa na mtoto wa Juma (alama 2)
    19. Tunga sentensi moja kionyesha maana mbili za neno ‘funza’ (alama 2)
    20. Mkungu ni kwa ndizi, koja ni kwa …………….. na…………….. ni kwa mboga . (alama 1)
  4. ISIMUJAMII (ALAMA 10)
    1. Terry: Liandikwalo ndilo liwalo. “Since when has man ever changed his destiny?”
      1. Tambua mtindo wa lugha uliotumiwa na mzungumzaji wa maneno haya. (alama 1)
      2. Eleza sababu nne zinazopelekea wazungumzaji kutumia mtindo huu. (alama 4)
    2. Wewe ni mfanyikazi katika kiwanda cha kutengeneza mavazi. Eleza sifa tano za lugha utayotumia unapowasiliana  na wafanyakazi wenzako. (alama 5)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. MWONGOZO WA UFAHAMU
    1. Hakutaka kukosa sherehe ya sikukuu ya Jamuhuri kama alivyokuwa amekosa ile ya mashujaa (2x1=2)
    2. Wa kwanza - katili na mkali
      alimfunza Hamo na kumuuliz swali la kudhalilisha- kwani wewe ni rais wa Marekani.
      Wa pili - Mwajibikaji- aliangalia kitambulisho.
      Mwenye utu alimkaribisha Hamo (2x2=2)
    3. Mwenye mlahaka mwema - alijibu salamu za Homa
      Mnyenyekevu - alijibu salamu za Homa (mwananchi)
      Mchangamfu/ mwenye kufaha- alitabasamu anapo ambiwa na Homa anapendwa (3x1=3)
    4. Alipendezwa na wanajeshi kama aliyerusha fimbo na aliyekuwa kiongozi wa gwaride (1x1=1)
    5. Uwanjani kulikuwa na sehemu karibu na jukwaa iliyotengewa wananchi wa kawaida. (1x1=1)
    6. Uwanja ulikula watu bila kushiba (1x1=1)
    7.    
      1. uwanja
      2. haribu
      3. kuapa (3x1=3)
  2. UFUPISHO
    1.      
      1. Mirundiko ya taka pamoja na utaratibu usiofaa wa uzoaji wake ni tishio kubwa kwa umma.
      2. Taka huwa makazi ya wadudu na wanyama waharibifu.
      3. Maji taka na mifuko ya sandarufi huwa mastakimu ya wadudu na virusi.
      4. Mifuko ya plastiki huziba mitaro ya maji.
      5. Maji yanapozibwa husababisha mafuriko ambayo huleta hasara ya mali na uhai.
      6. Mifuko huwasakama tumboni wanyama.
      7. Pana haja ya kutafuta njia ya technolojia ya kukabiliana na tatizo hiyo.
      8. Njia mojawapo ni kuelimisha umma kuwa na waangalifu katika matumizi ya bidhaa na raslimali ili kupunguza uzalishaji wa taka. (zote 7x1=7)
    2.        
      1. Mifuko na mabaki ya sandarusi hutumika kama malighafi katika viwanda vinavyotengeneza bidhaa za plastiki.
      2. Taka za chupa na chuma huuzwa katika viwanda vinavyovigeuza  kuwa manufaa tena.
      3. Taka za karatasi hutumiwa kutengeneza bidhaa kama vitabu, katoni na shahi.
      4. Taka za hugeuzwa kwa kuzitumia kufanya mboji.
      5. maji taka yanaweza kutumika kunyunyizia mashamba madogo maji bustani za maua
      6. Moto unaotumiwa kuchoma taka unaweza ukatumiwa kuchemsha maji. (zote 6x1=6)
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1.      
      1. ng’o a
      2. huyo (2x1=2)
    2. abjadi, askari, abtadi, abtali (1x=1)
    3. Akiendelea – masharti
      kukichezea- yambwa /stamirisho ikitendewa
      kichuma- udogo
      ki motoni – kitenzi kishirikishi (4x½=2)
    4.        
      1. husudu
      2. tafakari
    5. Nyuzi (zote) zilikatwa mara nyingi.
      (zozote/zenyewe/ nyingine) (nyinginezo) (4x½=2)
    6. ha-               u ik                  -i
      ukanusho ngeli kauli                kiishio
      mnyambuliko (4x½=2)
    7. imenyesha 
    8.      
      1. kivumishi- mwanafunzi mwema ametuzwa.  
      2. kielezi- Mwanafunzi alicheza vyema.
      3. nomino- wema huozi
    9. Makosa ya kisarufi katika sentensi.   
      Kuonyesha neno la kigeni katika sentensi.
      Kuonyesha neno fulani limetolewa ufafanuzi –(chini ya kuraba).
      Kuficha maneno ya aibu.
    10. mmeenda?   
    11. Mwalimu alituambia kuwa sisi sote tungepita angetununulia mikate miwili siku ambayo inyefuata jioni (4x½=2)
    12. Maskini wachache walifisiwa kabla ya kuhama msituni. (2/0)
    13. Mwanamke mzee- kitondo
      Chai tamu- kipozi
      Sufuria kubwa- ala
      Kwa sufuria kubwa leo asubuhi- chagizo (4x1=4)
    14. Aliyekuja(KN)  kwetu/  ni mwizi(KT) sugu
    15. Kusoma kwa bidii kulimfanya muhammed kufuzu mtihani huo vizuri. (1/0)
    16.      
    17. Matoto yaliyaua majoka madogo kwa kumpiga majichwani.
    18. Vipya kabisa-RN
      Vilvyoagizwa jana sokoni-RV
      Vitanunuliwa na mtoto wa Juma-RT
      mtoto wa Juma-RN
      wa Juma-RH (4x½=2)
    19. Funza – mdudu mdogo kama kiroboto.
      Kufundisha
      Lea
      Darisi (2x1=2)
    20. Koja ni kwa maua
      kicha ni kwa mboga (2x½=1)
  4. UFUPISHO
    1.      
      1. Mirundiko ya pamoja na taratibu usiofaa wa uzoaji wake ni tisho kubwa kwa umma.
      2. Taka huwa makazi ya wadudu na wanyama waharibifu.
      3. maji taka na mifuko ya sandarusi huwa mastakimu ya wadudu na virusi.
      4. mifuko ya plastiki huzuia mitaro ya maji.
      5. maji yanapozibwa husababisha mafuriko ambayo huleta hasara ya mali na uhai.
      6. mifuko huwasakama tumboni wanyama.
      7. pana haja ya kutafuta njia au teknolojia ya kukabiliana na tatizo hili.
      8. Njia mojawapo ni  kuelimisha umma kuwa na uangalifu katika matumizi ya bidhaa na raslimali ili kupunguza uzalishaji wa taka. (zozote 7×1=7)
    2.      
      1. Mifuko na mabaki ya sandarusi hutumika kama malighafi katika viwanda vinavyotengeneza bidhaa za plastiki.
      2. Taka za chupa na chuma huuzwa katika viwanda vinavyogeuza kuwa na manufaa tena.
      3. Taka za karatasi hutumiwa kutengeneza bidhaa kama vitabu, katoni na shahi.
        Taka hugeuzwa kwa kuzitumia kufanya mboji.
      4. Maji taka yanaweza kutumika kunyunyizaji mashamba madogo maji au bustani za maua.
      5. Moto unaaotumiwa kuchoma taka unaweza ukatumiwa kuchemsha maji. (zozote 6×1=6)

ISIMU JAMII

  1.      
    1. kubadili lugha/ misimbo/ndimi/kuhamisha
    2. Kuficha siri/ kutenga wengine
      1. kuelewa/ kumudu matumizi ya lugha zaidi ya moja.
      2. Kutoimudu lugha anayoitumia sawasawa
      3. Kujitambulisha na kundi fulani.
      4. kuonyesah hisia.
      5. Uzoufu wa kuchanganya ndimi.
      6. Kufidia msemaji.
      7. Kutaka kujieleza/ kufafanua zaidi.
      8. Kutafsiri lugha.
      9. Ili kusisitiza jambo Fulani. (4x1=4)
  2.      
    1. Matumizi ya  kauli – kata jora.
    2. Hutaja vyeo vya watu kwa mfano, mkuu wa idara.
    3. Msamiati unaohusiana na mavazi au vifaa vya kiwandani kwa mfano cherehani.
    4. Ukiukaji wa sarufi kwa sababu ya viwango tofauti vya kielimu.
    5. Hutumia misimu ya kiwandani hicho ili kurahisisha  mawasiliano
    6. Lugha nyenyekevu hasa wadogo wanapozungumza na wakubwa wenye hadhi kwenye kumpuni.
    7. Kuchanganya/ kubadili misimbo kwa mfano leta mashini
    8. Lugha ya kuamrisha/ kuelekeza kutoka kwa wakubwa. 
      Panga jora hizi katika mafungi.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Cekenas Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?