Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mokasa II Joint Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  1. Lazima
    Wewe ni katibu wa Gatuzi la Tuokoeni. Kumekuwa na misukosuko ya kiuchumi ambayo imewaathiri wazazi. Andika kumbukumbu za mkutano wenu wa kwanza kujadili namna ambavyo hali hii imemwaathiri mwanafunzi kimaadili.       (alama 20)
  2. Wewe ni mtaalamu wa masuala ya uchukuzi na umealikwa kuwahutubia vijana kuhusu namna ambavyo mfumo wa usafiri wa bodaboda umeathiri jamii nchini.    (alama 20)
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Mchezea tope humrukia.
  4. Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno yafuatayo:
    Niliketi chini ya kivuli cha mzambarau, mkononi nikiwa na bilauri ya maji ya matunda. Niliyanywa polepole nikitazama kitalu cha matunda nilichostawisha katika safari yangu ya kupanda kilele cha ufanisi......................

MARKING SCHEME

Swali la Kwanza - Kumbukumbu

  1. Mtahiniwa azingatie sura ya kumbukumbu.
    1. Fungu la muktadha (kichwa)
      • Jina la kikundi
      • Mahali pa mkutano
      • Tarehe
      • Saa
    2. Mahudhurio
      1. Waliohudhuria
      2. Waliotuma udhuru wa kutohudhuria
      3. Waliokosa kuhudhuria
    3. Ajenda
      Athari za kupanda kwa gharama ya maisha.
      1. Wanafunzi kukosa kuhudhuria masomo
      2. Kuongezeka kwa visa vya wizi shuleni
      3. Kuongezeka kwa visa vya ulaghai na utapeli shuleni au katika eneo.
      4. Kusheheni kwa wizi au upokonyaji wa kimabavu.
      5. Visa vya wanfunzi kushiriki ngono kunakosababisha magonjwa na mimba za mapema.
      6. Vijana/wanafunzi kuacha shule na kuanza kufanya kazi zaBsuluhu/kutumikishwa.
      7. Matumizi ya mihadarati
    4. Mambo/shughuli nyinginezo
    5. Mtahiniwa aandike yaliyojadiliwa kwa kufuata ajenda akianza na wasilisho kutoka kwa mwenyekiti.
      Kumbukumbu zipewe nambari
      Amalizie kwa nafasi za sahihi ya mwenyekiti na katibu,
      INDHARI
      1. Mtahiniwa asionyeshe/asirejelee sehemu ya kusomwa na kuidhinishwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia.
      2. Mtahiniwa ataondolewa alama 4 za sura kama amekosa vipengee vyote vya muundo wa kumbukumbu. Akikosea kipengee kimoja au viwili lichukuliwe kama kosa la kimtindo.
  2. HOTUBA
    Hii ni hotuba. Vipengele viwili vikuu vya hotuba vizingatiwe.
    1. Maudhui
    2. Sura
      1. Muundo
        1. Anwani
        2. Mwanzo
          • Salamu. Hatibu atambue waliohudhuria kwa vyeo, kuanzia kwa aliye mashuhuri zaidi; kuzingatia itifaki.
          • Katika ayah ii hatibu abainishe kiini cha hotuba
        3. Mwili
          Hapa ndipo mtahiniwa atajadili kuhusu athari za mfumo huu wa usafiri wa bodaboda.
          Kila hoja ujadiliwe kwa kina kwa mtindo ufaao. Mtahiniwa azumgume moja kwa moja na hadhira lengwa.
        4. Hitimisho
          Mtahiniwa ahitimishe hotuba kwa kubainisha msimamo wake kuhusu mfumo huu wa usafiri. Ayah ii ibainishe fomyula ya kuhitimisha/kufunga hotuba, hususan awashukuru waliohudhuria.
      2. MAUDHUI
        Mtahiniwa adadavue kwa kina athari hasi na chanya za mfumo huu wa usafiri.
        Umuhimu
        • Imechangia kupatika nwa ajira miongoni mwa vijana ambao wamekamilisha masomo yao na wasio na ajira.
        • Sekta hii imechangia kupungua kwa visa vya uhalifu, ambapo wengi wanaitumia kama wenzo wa kuzumbulia riziki badala ya kukaa tu.
        • Ni mfumo ambao uhahakikisha usafiri wa haraka hususan mijini na mashinani.
        • kufanikisha kilinio.
        • Uwezo wake wa kupenya hata kuliko na msongamano wa watu na magari unaifanya kuwa njia ya kutegemewa ya usafiri.
        • Ufumo huu wa usafiri ni wenye gharama nafuu ikilinganishwa na usafiri wa magari na reli.
        • Kungezeka kwa pato la nchi kupitia kodi inayotozwa uagizaji wa pikipiki.
        • rahisi kupatisha
          Hasara
        • Kuongezeka kwa visa vya uhalifu mijini na mashambani ambapo wahuni wanatumia pikipiki kuwapora watu
        • Imechochea vijana wengi kuacha shule ili kuingilia biashara hii
        • Imechangia uchafuzi wa mazingira kupitia kwa kelele na moshi
        • Kuvunjika kwa ndoa au mahusiano katika jamii
        • Kupujuka kwa maadili ya kijamii, wasichana wengi wameishia kutungwa mimba
        • Imechangia katika ongezeko la visa vya ajali nchini
        • Ni mfumo ambao unaweza kutumika katika safari za masafa mafupi tu.
        • Si njia mwafaka ya usafiri katika msimu wa masika n ahata maeneo yanayoshuhudia baridi nyingi.
        • Misongamano barabarani.
        • Imechangia migogoro ya kijamii
          Tanbihi
          Hii ni insha ya kiuamilifu
          Utahini wa insha hii unajikita katika sura na maudhui
          Mtahiniwa ajadili maudhui yasiyopungua manane
          • Ikiwa mtahiniwa atakosa sehemu moja tu ya sura ya hotuba, atakuwa amepungukiwa tu kimtindo
          • Ikiwa mtahiniwa atatumia nafsi ya tatu, yaani aripoti, aondolewe alama 4 sura 
          • Alama za kunukuu zinaweza kutumiwa ilmradi ziwekwe mwanzo na mwisho. Ikiwa ataweka upande mmoja tu-kosa la sarufi.
          • Ikiwa tanukuu kila aya, lichukuliwe kama kosa la sarufi pia.
          • Suala hili lina pande mbili, athari hasi na chanya-ziangaziwe kikamilifu.
          • Katika kuhitimisha, hatibu anaweza kutoa kauli ya kuhamasisha umma kuhusu namna ya kuboresha na kuhakikisha ufanifu wa usafiri wa mfumo huu.
  3. METHALI
    Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Mchezea tope humrukia.
    Anayejiingiza/jihusisha katika jambo la hatari lazima atadhurika.
    Mamba ya kuzingatiwa:
    1. Mtahiniwa atunge kisa kinachofafanua maana ya methali hii,
    2. Kisa cha mtahiniwa kidokeze pande mbili za methali: Kucheza na tope na kule kurukiwa.
    3. Kujihusisha katika jambo/shughuli zenye hatari na namna anavyodhurika halafu.
      Mifano ya mikondo ya visa
      1. Anayejihusisha/shiriki mapenzi kiholela (kucheza na tope) mwishowe kumbukizwa maradhi au kuambulia ujauzito (tope kumrukia)
      2. Anayejihusisha katika wizi wa mitihani shuleni (kidato cha kwanza hadi cha nne) na anapojaribu hila ananaswa (tope kumrukia)
        Utuzaji
        1. Asiyetininga kisa atakuwa amepotoka atuzwe alama D03/20
        2. Asiyezingatia pande mbili za methali atakuwa amepungukiwa kimaudhui, asipite C+ 10/20
  4. INSHA
    Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno yafuatayo:
    Niliketi chini ya kivuli cha mzambarau, mkononi nikiwa na bilauri ya maji ya matunda. Niliyanywa polepole nikitazama kitalu cha matunda nilichostawisha katika safari yangu ya kupanda kilele cha ufanisi.
    1. Hii ni insha ya mdokezo wa kuanzia. Mtahiniwa aanze insha yake kwa maneno haya.
    2. Mtahiniwa aonyeshe juhudi za mhusika katika kukua hadi anapofikia ufanisi wake kama vile wa kupata mali au kustawi katika lolote alilolifanya. 
    3. Nafsi ya kwanza itumike kusimulia kisa.
    4. Hata hivyo, kwa vile msimulizi huenda akakumbana na wahusika wengine, anaweza pia kuchanganya nafsi ya kwanza na tatu.
    5. Katika kutuza, mwngozo wa kudumu urejelewe. 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mokasa II Joint Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?