KISWAHILI PAPER 2 - KCSE 2019 JOINT PRE MOCK EXAMINATION NAMBALE

Share via Whatsapp

UFAHAMU:        (ALAMA 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Mawasiliano ni upashanaji habari kwa namna tofautitofauti. Njia za mawasiliano zimebadilika sana katika historia ya binadamu. Kwa mfano, zamani ingechukua siku nyingi kupitisha ujumbe baina ya watu wanaoishi sehemu mbalimbali. Siku hizi ujumbe hupitishwa katika sekunde chache katika masafa marefu.

Ugunduzi wa simu uliofanywa na Alexander Graham Bell mwaka wa 1876 ulifungua ukurasa mpia katika mawasiliano. Nchini Kenya, miaka ya sabini na themanini, ilikuwa vigumu kupata huduma za simu. Mtu alihitajika kusafiri masafa marefu ili kupata huduma hizo hasa kwa wale walioishi mashambani. Aidha kutokana na ukosefu wa huduma hizo katika sehemu nyingi, mtu alihitaji kupiga foleni ili ahudumiwe ama ajihudumie.

Baadaye, simu tamba zilivumbuliwa na mawasiliano yakarahisishwa. Mwanzoni, simu tamba zilikuwa vidude vikubwa ambavyo havikutoshea mifukoni. Hata hivyo, usumbufu huo ulitafutiwa suluhu. Siku hizi simu tamba ni ndogo na hivyo huwa rahisi kuzibeba. Aidha, kampuni za kutoa huduma za mawasiliano na kufanya gharama ya kupiga simu kuenda chini.
Barua pia ni njia ya mawasiliano na imetumika kwa muda mrefu. Baadhi ya nchi kuliko tumiwa barua katika enzi za zamani ni Misri na Uyunani. Matarishi walitumwa kupeleka barua. Barua zilichukua muda mrefu kufikia aliyeandikiwa. Aidha kutokana na kwamba si watu wote waliojua kusoma na kuandika, wachache waliokuwa na maarifa hayo waliwandikia na kuwasomea. Katika enzi hizi matumizi ya barua yamepunguzwa kwa kiwango kikubwa na tarakilishi na simu tamba. Kwa kutumia tarakilishi unaweza kutuma barua pepe. Aidha, kwa kutumia simu tamba unaweza kutuma arafa.

Waajiri wengi hupendekeza wanaoomba kazi watume maombi yao kwa kutumia baruapepe. Njia hii huondoa uwezekano wa wanaoomba kazi kutumia ufisadi ili wapate kazi. Aidha, njia hii husaidia kutunza mazingira kwani karatasi hazitumiwi. Katika elimu tarakilishi zinatumiwa shuleni kufundishia hivyo kurahisisha mawasiliano kati ya mwalimu na mwanafunzi. Aidha, kupitia tarakilishi iliyotandawizwa ama kuunganishwa kwa mtandao, watu huweza kujuliana hali na kupashania habari mbalimbali kutoka pembe zote za dunia. Changamoto katika hatua hii ni ukosefu wa nguvu za umeme hasa mashambani. Aidha,gharama ya kununua tarakilishi ni kali mno hasa kwa mataifa yanayoendelea ikizingatiwa kuwa yana changamoto za kimsingi kama vile kutojua kusoma na kuandika, magonjwa na umaskini.

Vilevile, redio ni chombo muhimu ambacho huchangia sana katika mawasiliano. Kwa sasa, hiki ndicho chombo cha pekee kinachomilikiwa na karibu kila familia. Hali hii inachangiwa na ukweli kwamba kunazo redio ndogo ambazo hutumia betri. Chombo hiki huwapitishia matangazo na habari kuhusu yanayotendeka kutoka pande zote za ulimwengu. Redio hufahamisha, huburudisha na kuelimisha. Wizara ya Elimu imekuwa ikitumia redio kufundishia masomo mbalimbali hasa katika shule za msingi.

Nani asiyejua kuhusu runinga? Chombo hiki pia hutoa mchango mkubwa katika mawasiliano. Runinga hushirikisha hisi za kusikiliza na kuona, kwa hivyo mawasiliano yake hufanikiwa sana. Hata hivyo, ni asilimia ndogo ya watu ambao wanaweza kuimiliki kutokana na gharama yake na pia si wengi wanazo nguvu za umeme majumbani mwao.

Mwalimu ni muhimu sana katika maendeleo ya jamii oyote. Ni dhahiri shahiri mwasiliano ni sehemu muhimu katika kuimarika kwa uchumi. Vile vile huwezesha watu kutangamana na kubadilishana mawazo. Binadamu si kama visiwa vinavyosimama peke yavyo. Binadamu huhitaji kutangamana na binadamu wengine katika maisha na kwa hivyo mawasiliano ni muhimu.

  1. Eleza kini cha taarifa hii.           (al. 1)
  2. Toa sababu mbili za waajiri kuhimizi matumizi ya barua pepe.      (al. 2)
  3. Kwa nini redio ndicho chombo kinachotegemewa zaidi katika mawasiliano.
    Eleza sababu nne.                                                                                           (al. 4)
  4. Kwa mujibu wa kifungu hiki eleza udhaifu wa tarakilishi.                    (al. 3)
  5. Eleza faida mbili za tarakilishi.                    (al. 2)
  6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa.           (al. 2)
    1. Kupiga foleni
    2. Matarishi

UFUPISHO: (ALAMA 15) 

Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali yafuatayo

Lugha ndio msingi wa maandishi yote. Bila lugha hakuna maandishi. Kila jambo tufanyalo kuhusiana na lugha husitawisha ufahamu wetu wa mambo tusomayo. Mazoezi katika kuandika husitawisha ufahamu katika kusoma kwa sababu katika kuandika ni lazima kuyatumia maneno vizuri na kufahamu ugumu wa usemi. Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine wakizungumza. Lugha tusomayo ni anina ya lugha ya masungumzo.

Kuna ujuzi mwingi katika kuzungumza kama vila michezo ya kuigiza, hotuba, majadiliano na mazungumzo katika darasa. Haya yote husaidia katika uhodari wa matumizi ya lugha. Ujuzi wa kila siku utasaidia katika maendeleo ya kusoma na usitawi wa msamiati. Ikiwa mwanafunzi amemwona ndovu hasa, atakuwa amejua maana ya neno ndovu vizuri zaidi kuliko mwanafunzi ambaye hajawahi kumwona ndovu bali ameelezwa tu vile ilivyo. Vilevile ujuzi wa kujionea sinema au michoro husaidia sana katika yaliyoandikwa. Ikiwa mwanafunzi ana huzuni au ana furaha, akiwa mgonjwa au amechoka au amefiwa, haya yote ni ujuzi. Wakati juao mwanafunzi asomapo juu ya mtu ambae amepatikana na mambo kama huyo hana budi kufahamu zaidi.

Karibu elimu yote ulimwenguni huwa imeandikwa vitabuni. Hata hivyo, lugha zote hazina usitawi sawa kuhusu fasihi. Kwa bahati mbaya lugha nyingine hazijastawi sana na hazina vitabu vingi. Fauka ya hayo , karibu mambo yote yanayohusiana na elimu huweza kupatikana katika vitabu kwenye lugha nyingine.

Inambidi mwanafunzi asome vitabu au majarida juu ya sayansi au siasa au historia, lakini haimbidi kusoma tu juu ya taaluma fulani anayojifunza . Inafaa asome juu ya michezo, mambo ya mashairi na juu ya mahali mbalimbali ili kupata ujuzi wa mambo mengi.

  1. Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65 (alama 10, 1 ya utiririko)
  2. Kwa kuzingatia habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho
    (Maneno 30) (alama 5 utiririko)

         

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1. Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya vielezi viwili vya silabi moja.           (al. 2)
  2.  
    1. Eleza maana ya sauti za likwidi.                                                                         (al. 1)
    2. Toa mifano ya sauti za likwidi.                                       (al. 1)
  3. Ainisha mofimu: Lililoliwa                                                           (al. 3)
  4. Eleza huku ukitoa mifano matumizi mawili ya kiambishi ‘ji’.                              (al. 2)
  5. Huku ukionyesha upatanisho wa kisarufi katika sentensi, weka nomino zifuatazo katika ngeli mwafaka.      (al. 2)
    1. Uwele
    2. Vita
  6. Tumia ‘O’ rejeshi tamati kuunganisha sentensi zifuatazo.                              (al. 1)
    Tawi limekauka                         
    Tawi limeanguka
  7. Tambua vivumishi na uonyeshe ni vya aina gani.                              (al. 3)
    Wanafunzi wawa hawa waliochelewa watafanya kazi ya sulubu kama adhabu.
  8. Kanusha: Msichana ambaye amefika ametuzwa.                              (al. 1)
  9. Onyesha aina za virai katika sentensi hii:                                       (al. 2)
    Wale wazazi wetu watawasili kesho saa tatu.
  10. Unda nomino kutokana na kitenzi ‘Haribu’                                       (al. 1)
  11. Tambua aina za vitenzi katika sentensi.                                       (al. 2)
    Hawa sio wachezaji bali wamekuwa wakichezea timu hii.
  12. Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya viunganishi vya kulinganua.           (al. 1)
  13. Eleza matumizi mawili ya ‘ka’ . Toa mifano katika sentensi.                              (al. 2)
  14. Andika visawe ya maneno yafuatayo                                                 (al. 2)
    1. Daawa
    2. Ainisha
  15. Onyesha kwa kauli ulizopewa                                                 (al. 1)
    Ja (tendewa)
  16. Andika kinyume: Tajiri aliyesifiwa amelaaniwa.                                       (al. 1)
  17. Chananua sentensi hii kwa kutumia vishale.                                                 (al. 4)
    Yule mgeni aliyefika jana ameondoka leo.
  18. Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo                              (al. 2)
    Oyula atapendwa na wengi ikiwa atashinda leo.
  19. Eleza majukuma mawili ya chagizo huku ukitoa mifano.                              (al. 2)
  20. sikiliza bwana mdogo siku hizi tunaishi katika jamii ambayo imebadilika hayo mawazo yako ya zama kongwe hayatakufikisha popote kumbuka
  21. Andika ukubwa wa sentensi katika wingi. Nyundo imo ndani ya kibweta.           (al. 1)
  1. ISIMU JAMII (ALAMA 10)

    Eleza matatizo matano yanayowakabili wazungumzaji wa Kiswahili.        (al. 10)


MARKING SCHEME

  1.  
    1. Eleza kini cha taarifa hii. (al. 1)
      Dhima ya mawasiliano katika nyanja mbalimbali
      Njia mbalimbali za mawasiliano.
      Teknolojia ya kisasa katika mawasilano.                                 (1x1=1)
    2. Toa sababu mbili za waajiri kuhimizi matumizi ya barua pepe. (al. 2)
      Huondoa uwezekano wa wanaomba kazi kutumia ufisadi ili wapate kazi.
      Husaidia kutunza mazingira kwani karatasi hazitumiki.                                     (2x1=2)
    3. Kwa nini redio ndicho chombo kinachotegemewa zaidi katika mawasiliano.
      Eleza sababu nne.                                                                              (al. 4)
      Ndicho chombo cha pekee kinachomilikiwa karibu na kila familia.
      Ni rahisi kutumia.
      Zina gharama ndogo.
      Wizara ya elimu hutumia redio kufundisha masomo mbalimbali.                                (4x1=4)
    4. Kwa mujibu wa kifungu hiki eleza udhaifu wa tarakilishi. (al. 3)
      Ukosefu wa nguvu za umeme hasa mashambani.
      Gharama za kununua tarakilishi ni ghali.
      Kutojua kusoma na kuandika.                                                    (3x1=3)
    5. Eleza faida mbili za tarakilishi. (al. 2)
      Hutumiwa shuleni kufundisha.
      Husaidia katika mawasiliano.                                       (2x1=2)
    6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa. (al. 2)
      1. Kupiga foleni ……… Simama katika mstari
      2. Matarishi …………… Wanaotumwa kupeleka ujumbe / habari.
  2.  
    1. Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65 (alama 10, 1 ya utiririko)
      Matayarisho                                                 
      • Kila jambo tufanyalo katika lugha hustawisha ufahamu wake.
      • Mazoezi ya kuandika hustawisha ufahamu wa kusoma.
      • Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine.
      • Lugha iliyoandikwa ni ya aina ya mazungumzo.
      • Ujuzi mwingi katika kuzungumza hupatikana shuleni.
      • Ujuzi wa kila siku husaidia katika maendeleo ya kusoma na msamiati.
      • Husaidia kufahamu yaliyoandikwa.
      • Hali ya mwanafunzi kujionea sinema ni ujuzi.
      • Matatizo na shida ambazo wanafunzi hupitia pia ni ujuzi.
    2. Kwa kuzingatia habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho
      (Maneno 30) (alama 5 utiririko)
      Matayarisho
      • Karibu elimu yote imeandikwa vitabuni.
      • Lugha zote hazina ustawi mwingi.
      • Nyingine hazina vitabu ama zina vitabu vingi.
      • Mwanafunzi anayesoma anafaa kusoma mengi kando na taaluma anayoisoma.
        a – 09
        b – 04
        Ut - 02
  3. MATUMIZI YA LUGHA        (ALAMA 40)
    1. Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya vielezi viwili vya silabi moja. (al. 2)
      Po ya wakati – alipowasili tulifurahi.
      PO-KO-MO – Anapoishi panapendeza.
      Vyo ya jinsi – hivi ndivyo alivyo
      (2x1=2)
    2.  
      1. Eleza maana ya sauti za likwidi.            (al. 1)
        Ni sauti zinazotamkwa kukiwa na mkondo wazi katika ala za kutamkia.
        (1x1=1)
      2. Toa mifano ya sauti za likwidi.                                     (al. 1)
        Kimadende - /r/
        Kitambaza - /l/
    3. Ainisha mofimu: Lililoliwa                                                             (al. 3)
      Li - Ngeli
      li – wakati uliopita
      lo - kirejeshi
      l- mzizi
      iw – kauli ya kutendwa
      a – kiishio
      (6x1/2=3)
    4. Eleza huku ukitoa mifano matumizi mawili ya kiambishi ‘ji’. (al. 2)
      • Kuleta dhana ya ukubwa – jibwa
      • Kuonyesha mtendaji / uzoefu wa kutenda – mkimbiaji
      • Kuonyesha yambwa ya kujitendea – anajikuna.
      • Kiambishi awali cha ngeli ya LI-YA – Jicho, jibu n.k
        (zozote 2x1=2)
    5. Huku ukionyesha upatanisho wa kisarufi katika sentensi, weka nomino zifuatazo katika ngeli mwafaka.                    (al. 2)
      1. Uwele…… U-ZI
        Uwele umemzidia – Ndwele zimewazidia
      2. Vita ….. VI-VI
        Vita vimechacha
    6. Tumia ‘O’ rejeshi tamati kuunganisha sentensi zifuatazo.                         (al. 1)
      Tawi limekauka                         
      Tawi limeanguka
      Tawi likaukalo huanguka.
    7. Tambua vivumishi na uonyeshe ni vya aina gani.             (al. 3)
      Wanafunzi wawa hawa waliochelewa watafanya kazi ya sulubu kama adhabu.
      Wawa hawa – visisitizi
      ‘o’ – kirejeshi.
      Ya – a - unganifu
    8. Kanusha: Msichana ambaye amefika ametuzwa.             (al. 1)
      Msichana ambaye hajafika hajatuzwa
    9. Onyesha aina za virai katika sentensi hii:                         (al. 2)
      Wale wazazi wetu watawasili kesho saa tatu.
      Wazazi wetu – kirai nomino
      Watawasili kesho – kirai tenzi
      Kesho saa tatu – kirai elezi.
      (zozote 2x1=2)
    10. Unda nomino kutokana na kitenzi ‘Haribu’                         (al. 1)
      Uharibifu
      Kuharibu           (2x1/2=1)
    11. Tambua aina za vitenzi katika sentensi.                         (al. 2)
      Hawa sio wachezaji bali wamekuwa wakichezea timu hii.
      Sio – kishirikishi kipungufu
      Wamekuwa – Kisaidizi
      Wakichezea – kikuu.                                                      (zozote 2x1=2)
    12. Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya viunganishi vya kulinganua. (al. 1)
      Lakini/ila/ijapokuwa/ingawa/ijapo/bali/ilhali/sembuse/seuze                    (1x1=1)
    13. Eleza matumizi mawili ya ‘ka’ . Toa mifano katika sentensi. (al. 2)
      Kuonyesha mfululizo wa vitendo – alicheza, akaoga, akala.
      Kuonyesha wakati ujao – atakaponiita nitaenda.
      Hali ya kufanyika kwa kitendo – kinalika.
      Kama kihisishi – ka! Kumbe ni mjamzito.
      Katika usemi halisi – “Njoo hapa,” akasema. (zozote 2x1=2 )
    14. Andika visawe vya maneno yafuatayo                                     (al. 2)
      1. Daawa ……… Fitina/madai/kochokocho
      2. Ainisha ………Onyesha/panga/bainisha/chambua. (2x1=2)
    15. Onyesha kwa kauli ulizopewa                                     (al. 1)
      Ja (tendewa)
      Jiwa                                       (1x1=1)
    16. Andika kinyume: Tajiri aliyesifiwa amelaaniwa.                         (al. 1)
      Tajiri aliyekashifiwa/aliyelaumiwa/alishutumiwa amebarikiwa
    17. Chananua sentensi hii kwa kutumia vishale.                                     (al. 4)
      Yule mgeni aliyefika jana ameondoka leo.
      S         KN +KT
      KN       V+N+S
      V         Yule
      N        mgeni
      S         aliyefika jana
      KT       T+E
      T         ameondoka
      E         leo.                                (8x1/2=4)
    18. Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo                         (al. 2)
      Oyula atapendwa na wengi ikiwa atashinda leo.
      Oyula atapendwa na wengi – huru
      Ikiwa atashinda leo – tegemezi.                                                (2x1=2)
    19. Eleza majukuma mawili ya chagizo huku ukitoa mifano.             (al. 2)
      Hueleza jinsi kitendo kilivyofanywa – Amecheza vibaya sana.
      Kueleza wakati – Aliwasili jana jioni
      Kueleza mahali – Tutachezea huko Nambale.
      Kueleza idadi – Alimchapa mara tatu (2x1=2)
    20. (al. 3)
      Sikiliza bwana mdogo, siku hizi tunaishi katika jamii ambayo imebadilika. Hayo mawazo yako ya zama kongwe hayatakufikisha popote. Kumbuka.         (6x1/2=3)
    21. Andika ukubwa wa sentensi katika wingi. Nyundo imo ndani ya kibweta.(al. 1)
      Majundo yamo ndani ya majibweta.                       (1x1=1)
  1. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Eleza matatizo matano yanayowakabili wazungumzaji wa Kiswahili. (al. 10)
      • Athari ya lugha ya kwanza.
      • Kutumia msamiati visivyo.
      • Kuchanganya ndimi.
      • Kubadili msimbo.
      • Athari za sheng’
      • Kutoendeleza sentensi inavyofaa.
      • Hali za kiafya za wahusika.
      • Mapuuza ya kuongea Kiswahili sanifu.
      • Kutumia ishara za lugha visivyo.
      • Mtazamo hasi kuwa Kiswahili ni lugha duni.
      • Kupendelea kingereza.
        (zozote 10x1=10)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 2 - KCSE 2019 JOINT PRE MOCK EXAMINATION NAMBALE.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest