Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Kangundo Subcounty Pre Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Jibu maswali manne pekee.
  2. Swali la kwanza ni la lazima.
  3. Maswali mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki.
  4. Usijibu maswali mawili kutoka kitabu moja.

USHAIRI

  1. Soma shairi kisha ujibu maswali
    Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki,
    Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki.
    Ukweli haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki,
    Mtu kuwa na tama, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Wengine watakuua, akiona una pesa, hata zikiwa kidogo,
    Hizo kwao ni maua, hupumiwa zikatesa, wakizifuata nyago,
    Hadi kwenye kwako ua, pasipo hata kupesa, wala kukupa kisogo,
    Mtu kuwa na tama, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Pindi kinuna kitu, hafurahi Shaitani, bali tajawa chukizo,
    Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwalo lako tekelezo
    Tamko lake ‘subutu’, kuondoa tumaini, na kukuulia wazi,
    Mtu kuwa na tama, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Aliye faraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kudai,
    Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui,
    Hana faida nyumbani, ni mtu akuchumbiye, mradi usitumai,
    Mtu kuwa na tama, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Kwa hakika ni balaa, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo,
    Bahati ni hadaa, kukupa alo sodawi, alibatili rohoyo,
    Mipangoyo kwake jaa, na nia ya ustawi,kuvunja kaniyo,
    Mtu kuwa na tama, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa,
    Ningetoa azimio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa,
    Ama nitumie mbio, faudini ninanena, akilini nazuiwa,
    Mtu kuwa na tama, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka
    MASWALI
    1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (ala 1)
    2. Eleza sababu ya mtungaji kulalamika katika shairi. (ala 3)
    3. Fafanua umbo la shairi hili. (ala 3)
    4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (ala 4)
    5. Taja mifano miwili ya tamathali za usemi. (ala 2)
    6. Eleza maana ya. (ala 2)
      1. zani
      2. faraghani
    7. Eleza kwa mifano mwafaka jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa katika shairi hili. (ala 4)
    8. Eleza bahari ya ushairi katika shairi hili. (ala 2)
    9. Taja nafsi neni katika shairi hili. (ala 1)

RIWAYA YA CHOZI LA HERI
JIBU SWALI LA 2 AU 3

  1. “Itakuwa kama kukivika kichwa cha kuku kilemba”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
    2. Fafanua athari zinazotokana na kuvikwa kilemba kichwa cha kuku. (ala 16)
  2. Eleza jinsi uozo unavyoshughulikiwa katika Riwaya ya Chozi la heri. (ala 20)

TAMTHILIA YA KIGOGO
JIBU SWALI LA 4 AU 5

  1. “Uliona nini kwa huyo zebe wako? Eti mpenzi.
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
    2. Eleza mbinu mbili za lugha katika dondoo hili. (ala 4)
    3. Taja hulka mbili za mnenaji katika dondoo hili. (ala 2)
    4. Mwanamke ni kiumbe wa kukandamizwa. Thibitisha kauli hii huku ukirejelea tamthilia ya Kigogo. (ala 10)
  2. Viongozi katika nchi zinazoendelea wamejawa na tamaa.
    Thibitisha kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya Kigogo. (ala 20)

TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI ZINGINE
JIBU SWALI LA 6 AU
7

  1. “Ndugu yangu kula kunatumaliza”
    “kunatumaliza au tunakumalizia”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
    2. Fafanua maana ya kitamathali katika kauli “kula tunakumaliza”
      Kwa kurejelea hadithi “shibe inatumaliza” (ala 10)
    3. Kwa mujibu wa hadithi hii kula kunawamaliza vipi. (ala 6)
  2.    
    1. Ubahaimu unaotendewa mwanamke una athari mbaya kwake. Fafanua kwa kutolea
      mifano huku ukirejelea hadithi ya “Mame Bakari” (ala 10)
    2. Mapenzi ni mateso, utumwa, ukandamizaji na ushabiki usio na maana.
      Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi “Masharti ya kisasa” (ala 10)

FASIHI SIMULIZI

  1.    
    1. Methali ni nini? (ala 2)
    2. Eleza sifa za methali. (ala 6)
    3. Andika methali zinazotumiia tamathali hizi. (ala 4)
      1. tashbihi
      2. takrikri
      3. tanakali za sauti
      4. istiari
    4. Eleza umuhimu wa vitendawili katika jamii. (ala 8)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Ushairi
    1. Kichwa mwafaka.
      • Unafiki wa binadamu.
      • Binadamu hatosheki.
      • Hatari ya tamaa ya binadamu.
        Yoyote 1x1 =1
    2. Sababu ya kulalamika kwa mtungaji.
      • Kusengenya/ kusema faraghani.
      • Kuuwawa.
      • Kunyang`any`wa pesa.
      • Kuchukiwa pindi anaponunua kitu.
        Zozote 3x1 =3
    3. Umbo la shairi.
      • Lina kibwagizo.
      • Mishororo ni 4 katika kila ubeti.
      • Beti ni sita.
      • Vipande vitatu kila mshororo.
      • Vina vya ndani na nje vinabadilika kila ubeti.
      • Idadi ya mizani inabadilika katika kila mshororo.
        Zozote 6x ½ =3
    4. Ukinunua kitu binadamu aliye kama shetani hafurahi bali atakasirika kwa kile kitendo.Maneno yake ni ya kutoa tumaini lako.Binadamu anayetamani vya wengine ni hatari kama nyoka.
      4x1=4
    5. Mifano ya tamathali za usemi:
      • Stiari –mf shetani
      • Misemo mf kukupa kisogo
        2x1=2 Kutaja ½, mfano
    6.    
      1. Zani- Baa
      2. Faraghani –Pembeni
        2x1=2
    7.    
      1. Kuboronga sarufi mf hafurahi shetani.
      2. inkisari mf Kinuna badala ya ukinunua.
      3. Tabdila mf rohoyo badala ya roho.
        Zozote 2x2=4
    8. Ukawafi – lina vigae vitatu.
    9. Nimkereketwa anayekerwa na unafiki wa binadamu.
      1x1=1

CHOZI LA HERI

  1.    
    1. Muktadha
      • Ni maneno ya Tetei katika usimulizi wa Kaizari.
      • Anamweleza Ridhaa na jamii ya Wahafidhina kwa jumla.
      • Wako kambini
      • Ni baada ya kutokea kwa vita vya uchanguzi kupinga kutawazwa kwa Mwekevu.
    2. Athari zinazotokana na kuvikwa kilemba cha kuku:
      • Mauaji – Baadhi walipoteza maisha kutokana na mashambulizi mf familia ya Ridhaa
      • Vilio – Vya kite vilihanikiza hewani wakati wa vita vya baada ya uchaguzi.
      • Ukimbizi – Watu waliacha makaazi yao na kukimbilia usalama mf Ridhaa, Kaizari,Selume nk.
      • Uporaji – Majangili waliingia madukani ya wahindi wakapora.
      • Uharibifu wa mali – Mifugo na majumba kama ile ya Ridhaa ziliteketezwa.
      • Ubakaji – Genge lilivamia boma la Kaizari na kubaka binti zake Lime na Mwanaheri.
      • Mateso ya kisaikolojia – Kaizari alibaki kuuguza majeraha ya maoyo aliyoyapata kwa kuona unyama wa kubakwa kwa wanawe.
      • Vita vya wenyewe kwa wenyewe – Familia ya Ridhaa ilishambuliwa kwa moto na jirani yake Kedi.
      • Ukosefu wa chakula na maji – Kule msituni wakimbizi walikula mizizi na matunda mwitu huku wengine wakifa njaa.
      • Magonjwa – Wakimbizi walipatwa na homa ya matumbo na kipindupindu kwa kunywa maji machafu.
      • Utengano wa kifamilia- Selume alitengana na familia yake kwa misingi ya tofauti za kisiasa. Zozote 8 x 2 = 16
  2. Uozo katika Chozi la Heri
    • Mashambulizi – familia ya Ridhaa ilishambuliwa kwa moto.
    • Ufisadi –Mabwanyenye walionekana wakitoa hongo hadharani kuzuia ubomozi wa majumba yao.
    • Ajira ya watoto – vijilunga vilinyakuliwa na kupelekwa maeneo mbali mbali kufanya kazi.
    • Unyanyasaji – Wakoloni walinyanyasa wafrika kwa kunyakua ardhi na kuwafanyisha kazi.
    • Ubaguzi – Ridhaa alitengwa na wanafunzi wenzake katika eneo la Msitu wa Heri.
    • Uongo- Vijana walidaganywa kuwa baada ya uchaguzi watapewa nyadhifa.
    • Kisasi – Umati wa wakimbizi ulitaka kumwadhibu askari kwani walimuona kuwa chanzo cha ukimbizi wao.
    • Umbeya – Wambeya walisema kuwa mumuwe Selume ameshaoa msichana wa kwao.
    • Taasubi ya kiume – Tetei anaamini kuwa uogozi kupewa mwanamke ni maoenevu.
    • Wizi – Madereva walivyonza mafuta kwa magari ya waajiri wao na kuyauza.
    • Wizi wa watoto- Sauna aliwaiba watoto Dick na Mwaliko.
    • Ulaghuzi wa dawa – Dick alishirikishwa katika ulaghuzi wa dawa na Mzee Buda.
    • Ukahaba – Sauna aliwahudumia waugwana katika majumba ya kuuza pombe.
    • Kuavya mimba – Mamake Sauna alitekeleza kitendo cha kumuavya mimba bintiye Sauna.
    • Kutupa watoto – Nehema anapata mtoto aliyetupwa kwenye takataka asubuhi akielekea ofisini.
    • Vitisho – Vikaratasi vilienezwa kutahadharisha wageni kuondoka baada ya kutawazwa kwa Mwekevu.
    • Ulevi –Shamshi ni mwandani wa chupa ya pombe.
      Zozote 20x1=20

KIGOGO

  1.    
    1. Muktadha
      • Maneno ya Majoka
      • Anamwambia Ashua
      • Ofisini kwa Majoka
      • Ni baada ya Ashua kumkataa Majoka kimapenzi. 4 x 1 = 4
    2. Mbinu za lugha
      • Swali la balagha mf uliona nini kwa huyo zembe wako?
      • Nidaa mf eti mapenzi! 2 x 2 = 4
    3. Sifa za mnenaji
      • Mwenye dharau – anamuita Sudi zembe.
      • Mpyaro anamtusi Sudi kwa kumuita zembe.
    4.    
      • Kupigwa- Ashua kupigwa na askari kule gerezani.
      • Kubezwa –Tunu anakejeliwa na Ngurumo na walevi wengine.
      • Wanatumiwa kama chombo cha kutumikia wanaume –Majoka anaagiza Husda kumpikia chapati na nyama.
      • Kufungwa – Ashua atiwa gerezani na Majoka.
      • Kunyimwa uogozi – Ngurumo asema kuwa ni heri ampe kura Paka kuliko Tunu.
      • Kunyimwa ajira – Ashua achuuza maembe katitka soko la chapa kazi licha ya kusomea ualimu.
      • Kuozwa bila hiari – Majoka ataka kumwoza Tunu kwa Ngao junior.
      • Kunyimwa fidia- Majoka alitaka kumnyima Hashma fidia baada ya kifo cha mumewe.
      • Kusalitiwa – Husda asalitiwa kimapenzi na Majoka anapomtaka mapenzi Ashua.
      • Wanatumiwa kama chombo cha mapenzi – Majoka anamtaka Ashua kimapenzi.
        Zozote 10x1 =10
  2. Tamaa ya viongozi.
    • Majoka anamuangamiza Jabali kutokana na tamaa ya kuongoza.
    • Majoka ataka kuridhisha Ngao junior uongozi.
    • Majoka ana tamaa ya anasa anaenda kuogelea katika hoteli yake ya Majoka and Majoka modern resort.
    • Majoka ana tamaa ya ulinzi kutoka kwa askari wake.
    • Majoka ana tamaa ya mapenzi na wake za watu mf Ashua.
    • Majoka ana tamaa ya kuungwa mkono na watu kama vile Ngurumo,Asiya,Boza nk.
    • Majoka ana tamaa ya kupata kodi – Anatoza wna bihashara kodi kwa manufaa yake.
    • Majoka ana tamaa ya kunyakua soka la chapa kazi ilikujenga hoteli ya kifahali.
    • Majoka ana tamaa ya kupata sifa – Ni lazima atangazwe kupitia vyombo vya habari.
      Zozote 10x2=20

TUMBO LISILO SHIBA NA HADITHI ZINGINE

  1.    
    1. Muktadha
      • Kauli ya kwanza ni ya Sasa.
      • Kauli ya pili ni ya Mbura.
      • Walikua nyumbani kwa mzee Mambo.
      • Ni baada ya kula na kushiba sana katika sherehe iliyoandaliwa kusherehekea motto wa kwanza kuingia nasari na Yule mwingine kumea pembe.
    2. Kula tunakumaliza:
      • Mzee Mambo kupata mshahara ilhali hana kazi yoyote.
      • Wafanyikazi wanafika kazini lakini hawafanyi lolote.
      • Wafanyiazi kama mzee mambo wanachota mshahara/hawapewi.
      • Mzee Mambo kuandaa sherehe kubwa inayoangaziwa na vyombo vya habari kwa garama kubwa.
      • Wizara moja inaendeshwa na mawaziri wawili mf Sasa na Bura katika wizara ya mipango na mipangilio.
      • Mawaziri kuendesha wizara kwa namna ya kujifaidi mf Sasa na Bura wasema kuwa wizara inawaendesha.
      • Magari ya serikari kutumiwa vibaya kwenye sherehe ya mzee Mambo kama vile kuleta maji,jamaa nk.
      • Wenye uwezo wanapapia mali ya umma jinsi Sasa na Bura wanavyobugia chakula upesi.
      • Matajiri hawajali lawama kutokana na wizi wao wa mali ya umma.
      • Dj kwenye sherehe hajali lawama kulipwa mabilioni ya pesa kutoka kwenye hazina ya uuma.
      • Dj ana duka la dawa ambalo mtaji wake ni bohari kubwa ya dawa za serikali.
      • Dj na wenzake wanapata huduma za afya huku rahia wakiumia. Zozote 10 x 1=10Kula kunawamaliza:
      • Magonjwa yanayosababishwa na lishe mf Saratani,Obesti,presha nk.
      • Kuna mauaji –Watu wanamalizana kutokana na unyakuzi wa mali ya umma.
      • Kuhalalisha wizi-Aliyepewa hapokonyeki.
      • Kuagiza bidhaa ghushi kutoka nje mf mchele huku wakulima wa hapa njini wakikosa wanunuzi.
      • Wananchi kula vyakula duni mf mchele ghushi.
      • Raia kuumia kwa kukosa huduma za kimsingi kwa sababu ya uporaji wa viongozi.
        Zozote 6x1=6
  2.    
    1.    
      • Kubakwa,Sarah anaambulia ubakaji alipokua akirejea shuleni kwa masomo ya ziada.
      • Kujeruhiwa –Sarah anajeruhiwa na kuvuja damu baada ya kubakwa.
      • Kuvunjiwa utu- Tendo la ubakaji lilimvunjia Sara utu na ujananjike wake.
      • Kukatizwa masomo –Mwalimu mkuu alimkabidhi Sarah barua ya kuacha masomo anapokuwa mja mzito.
      • Kudhulumiwa – Mwalimu mkuu anamdhulumu Sarah kwa kumwambia kuwa hiyo haikuwa shule ya wazazi.
      • Kuteseka kisaikolojia- Sarah anaingiwa na mawazo mengi jinsi ya kuukabili ujauzito wake.
      • Kupata adhabu ya wazazi – Sarah anahofu kwamba babake angemchinja kwa kupata mimba.
      • Kutoaminiwa-Sarah anaogopa kutoa taarifa ya kubakwa kwa kuwa babake hangemwamini.
      • Kuonekaka kama shetani/lawama Kila mara mwanamke anapobakwa yeye ndiye hulaumiwa huku mbakaji akibaki huru. Zozote 10 x 1=10
    2.    
      • Dadi anaumia kimapenzi kwa kumpenda Kidawa ambaye alichelea kumpenda Dadi.
      • Dadi ndiye mchuma riziki- Anachuuza samaki kuikimu jamii.Pesa za mkewe ni za kununua fasheni mpya na mapambo.
      • Dadi alazimika kufanya kazi za nje na za ndani mf upishi.
      • Kidawa na Dadi wana hiari kuzaa mtoto mmoja kutokana na athari za usasa
      • Dadi anajilazimisha/anaumia kumwona mkewe akitembeza bidhaa nje.
      • Dadi anashindwa kumweleza kidawa ugumu wa masharti yake.
      • Dadi ana hofu kuyavunja masharti ya mkewe kwa kuhofia kuvunja ndoa yao
      • Dadi ana wasiwasi kuwa kidawa huenda ana uhusiano wa mapenzi na mwalimu mkuu
      • Dadi alitarajiwa kuwa baada ya kula aviondoe vyombo mezani na kuvisafisha
      • Dadi avumaniwa akiwa katika harakati za kuchunguza mienendo ya Kidawa na mwalimu mkuu
        10x1=10

FASIHI SIMULIZI

  1.    
    1. Methali ni semi fupi yenye maana fiche 1x2=2
    2.      
      • Ni fupi
      • Huwa na urari wa maneno
      • Huwa na maana ya nje na ya ndani
      • Huwa na sehemu mbili
      • Hufunganishwa na jamii husika
      • Huwa na mpangilio wa kishairi
      • Hutumia tamathali za semi 6 x 1 = 6
    3.    
      1. Tashbihi- usichokijua ni kama usiku wa giza
      2. Takriri-Haraka haraka haina Baraka
      3. Tanakali –Kazi mbi! Si mchezo mwema
      4. Istiari- Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi 4 x 1 = 4
    4.    
      • Huburudisha jamii
      • Hufikirisha jamii
      • Huonya wana jamii
      • Hukuza ushirikiano katika jamii
      • Huhifadhi na kuendeleza utamaduni katika jamii
      • Huhifadhi historia ya jamii
      • Ni kitambulisho cha jamii
      • Huadilisha wanajamii 8x1=8
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Kangundo Subcounty Pre Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest