Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Kapsabet Pre Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA PILI:LUGHA

MAAGIZO:

 • Jibu maswali yote.
 • Andika majibu yote katika nafasi zilizoachwa.
 • Karatasi hii ina alama 80.
 • Hakikisha kurasa zote zimepigwa chapa.
 1. UFAHAMU (Alama 15)
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

  Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote mawili yaliyopita; wanawake makamu ya nyanyake na mamake mkuu.

  Yeye hutarajia kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia watoto na daima dawamu kuwa ‘mwendani wa jikoni’ akawapikia watoto na bwanake chakula; na akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani kuchanja kuni, mtoni kufua nguo na kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume. Akanyagapo mume naye papo huutia wayo wake.

  Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika masomo ya lugha, Historia, Jiografia, Hesabu, Sayansi na mengineyo, sawa na mwanamume.

  Mwanamke wa kisasa hutaka kufanya kazi za kibega, akazifanya. Akataka kuwa mwalimu, akawa.Akataka kuwa daktari, akafanikiwa.Almuradi, siku hizi mwanamke hufanya kazi yoyote ile afanyayo mwanamume. Kuna wanawake marubani wa ndege, masonara, waashi, wahandisi, madereva wa magari, mawakili mahakimu, mawaziri wakuu na hata marais wa nchi Hakuna kazi isiyofanywa na mwanamke siku hizi.

  Mwanamke wa kisasa hateswi akafyata ulimi. Anapohiniwa yeye hupigania haki yake kwa dhati na hamasa. Katu hakubali ‘mahali pake’ katika jamii alipotengewa na wanaume wenye mawazo ya kihafidhina yaliyopitwa na wakati.

  Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake iwapo ni mfanyi biashara, imepiga hatua ya kutomrudisha ukatani.

  Mwanamke wa kisasa haamuliwi katika jambo, lolote, bali hufanya maamuzi yake mwenyewe. Kwa upande mwingine, mwanamume wa ‘kisasa’, ambaye bado amefungwa pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akatamani ya kale, lakini wapi! Analazimika kumkubali mwanamke huyu kama mshiriki sawa maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni ya aushi.

  Maswali
  1.          
   1. Msemo ‘mwendani wa jikoni’ unadhihirisha hali gani ya mwanamke katika jamii?(alama1)
   2. Thibitisha hali uliyotaja hapo juu kwa kutoa hoja nne. (alama 2)
  2. Mwandishi ana maana gani anaposema ‘akanyagapo mume naye papo huutia wayo wake’ (alama 1)
  3. Tofautisha mwanamke wa kiasili na wa kisasa ukizingatia maswala ya ndoa na elimu. (alama 4)
  4. Eleza hoja sita zinazoonyesha kuwa wanaume wana ‘mawazo ya kihafidhina’ dhidi ya mwanamke. (alama3)
  5. Fafanua athari zinazotokana na mabadiliko ya mwanamke wa kisasa katika jamii kulingana na mwandishi. (alama2)
  6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika taarifa. (alama 2)
   1. Ukatani
   2. Aushi

 2. UFUPISHO (ALAMA 15)
  Soma kifungu kifauatacho kisha ujibu maswali.

  Mifuko ni muhimu sana katika maisha ya binadamu ya kila siku. Baadhi ya mifuko huundwa kwa namna ambayo inadumu na inaweza kutumiwa mara kadha wa kadha. Hii huweza kuhifadhiwa na kutumiwa kwa kipindi kirefu. Asilimia kubwa ya mifuko ya aina hii hutengenezwa kutokana na nguo au ngozi. Hata hivyo, ipo mifuko mingine ambayo si ya uashi, haidumu. Hii ni mifuko myepesi, rahisi kubebeka na inayopatikana kwa wingi sana. Hii ni mifuko ya plastiki.

  Mifuko ya plastiki hupatikana katika maeneo mengi sana. Mifuko hii sio ghali inapolinganishwa na ile ya nguo au ya ngozi. Hii ni ya gharama ya chni na hupendwa kutokana na wepesi wake. Hata hivyo, mifuko hii inaweza kuwa chanzo cha matatizo mengi. Matatizo haya hutokana na linalopasa kufanywa kuhusu mifuko hii baada ya kutumiwa kwake. Mifuko ya nguo ambayo inatupwa kwenye jalala huishia kuoza na kuwa sehemu ya uchafu wa jalala hilo. Kwa upande wake, mifuko huo. Hata inapofukiwa arthini haiwezi kuoza hata kama kufukiwa huko ni kwa miaka mingi. Aidha hata pale inapochomwa, haiwezi kuteketea hadi kuwa jivu kama ilivyomifuko ya karatasi.

  Upo umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa sera madhaubuti za kupambana na tatizo la mifuko hii. lazima zitungwe sheria ambazo zinakabiliana na uchafuzi wa mazingira kwa njia hii. kwa njia hii hatari zianzowakabili watu na wanyama zitapunguzwa kwa kiasi kikubwa. Kwa hakika njia mojawapo ambayo ingeweza kutumiwa ni kuharamisha matumizi ya mifuko hii katika upakiaji. Sheria zinaweza kupitishwa ambazo zinahimiza matumizi ya mifuko mbadala kama ile ya karatasi kubebea vitu vidogo Fauka ya hayo, pana haja ya kuwazia kuwepo kwa njia nzuri kuteketezea mifuko hiyo. Inawezekana kuhimiza watumiaji kuirejesha mifuko hiyo mahali Fulani kwa ajili ya uteketezaji huo. Hata hivyo, hali hii huenda ikawa ngumu kwa kuwa inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana kwa upand ewa watumiaji.
  1. Fupisha ujumbe wa aya tatu za mwanzo kwa maneno 105 – 110. (alama 10, 1 utiririko)
   Matayarisho
   Nakala safi
  2. Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika aya ya mwisho (maneno 50 – 55) (alama 5, 1 utiririko)
   Matayarisho
   Nakala safi

 3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
  1. Taja sauti mbili zinazotamkiwa kwenye kaakaa laini (alama 1)
  2. Eleza tofauti za sentensi zifuatazo (alama 2)
   1. Amerudi shuleni!
   2. Amerudi shuleni.
  3. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mstari.
   1. Afisa mkuu anafuata sharia sembuse wewe. (alama 1)
   2. Ameenda huko mbali sokoni (alama 1)
  4. Tambua aina ya vihusishi katika sentensi zifuatazo
   1. Jumba alifuatalo li mbele ya msikiti wa Musa (alama 1)
   2. Kisiwa cha Ginigi kimekauka (alama 1)
  5. Tambua hali katika sentensi ifuatayo.
   Vyungu vya aina hii vyafinyangwa na huyu. (alama 1)
  6. Toa maana mbili za neno lifuatalo (alama 2)
   Somo
  7. Kanusha
   Mama alimwambia sipo alime haraka (alama 1)
  8. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizowekwa katika mabano
   1. Lia (Kutendeshwa) (alama 1)
   2. -Ja (Kutendea) (alama 1)
  9. Andika katika hali ya wastani umoja
   Kigombe kile kiliumia kikwato ( alama 2)
  10. Akifisha sentensi ifuatayo.
   Je kuna manusura wowote yeye alitaka kujua. (alama 2)
  11.            
   1. Eleza maana ya kirai (alama 1)
   2. Onyesha aina ya virai katika sentensi ifuatayo.
    Nilimpata akilalama ndani ya darasa (alama 2)
  12. Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi.
   Mwelekezi wake alimwambia kuwa angeweza kuwa mwindaji mashuhuri ikiwa angeyafuata mashauri yake. (alama 2)
  13. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mishale.
   Mtoto mmoja aliyekuwa mgonjwa sana alitibiwa jana. (alama 4)
  14. Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia “o” rejeshi
   Mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo (alama 1)
  15. Ainisha shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo
   Wachimba migodi wanafanya kazi haraka ipasavyo. (alama 2)
  16. Tumia kivumishi kimilikishi nafsi ya pili wingi katika sentensi (alama 2)
  17. Onyesha viambishi katika fungutenzi hili ( alama 2)
   Sajilika
  18. Eleza matumizi ya “na” katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
   Ndovu aliuawa na wawindaji haramu nami nikawaripoti
  19. Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo ( alama 2)
   1. Takrimu
   2. Sakini
  20. Weka vitenzi hivi katika hali ya kuamrisha kulingana na maelezo katika mabano(alama 2)
   1. -nywa (umoja)
   2. Tubu (wingi)
  21. Weka neno lifuatalo katika ngeli mwafaka (alama 1)
   Nyasi
 4. ISIMU JAMII (ALAMAMA 10)
  Eleza sababu za vijana kutumia lugha ya sheng’ (alama 10)

MAAKIZO

 1. UFAHAMU
  1.                  
   1. Mahali pake mwanamke ni jikoni
    Kazi yake ni kuitumikia jamii
    Yoyote 1 x1 = 1 alama 1
   2.        
    • Kupikia wanajamii
    • Kulima shambani
    • Kuchanja kuni
    • Kufua nguo
    • Kuteka maji
     Zozote 4 x ½ = alama 2
  2. Afanyayo mwanamume, mwanamke pia huweza kufanya
   Alama 1
  3. Tofauti kindoa
   1. Wa kiasili aliolewa kwa lazima. Wa kisasa anaolewa kwa hiari
   2. Wa kiasili alilazima kuzaa watoto. Wa kisasa anazaa kwa hiari
   3. Alitumikishwa kwa lazima. Anafanya atakalo
   4. Aliamuliwa kila jambo. Anajiamulia mambo
   5. Alimtegemea mume. Anajitegemea kujikimu
   6. Alinyamaza alipoteswa. Hupigania haki na hujitetea
    Zozote 3 x 1= alama 3

    Tofauti kielimu
   7. Wa kiasili hakuenda shuleni. Wa kisasa huenda shuleni.
   8. Wa kiasili alikuwa na elimu ya kiasili. Wa kisasa ana elimu ya kisasa.
    Yoyote 1 x 1 = alama 1
   1. Mahali pake ni jikoni
   2. Akiteswa anapaswa kunyamaza
   3. Lazima aolewe na amzalie mume watoto
   4. Hapaswi kupelekwa shuleni
   5. Anapaswa kufanyiwa uamuzi
   6. Hapaswi kujitea/ anafaa kunyamaza
   7. Ana kazi maalum k.m kumpikia bwanake
    Zozote 6 x ½ = alama 3
  4.            
   1. Hampendezi mwanamume
   2. Ni mkaidi
   3. Ni mshindani wa mwanamume
   4. Ni mzushi
    Zozote 2 x 1 = alama 2
  5.       
   1. Ukatani – umaskini/ ufukara alama 1
   2. Aushi – maisha/ kudumu / milele/ daima / alfulela alama 1

 2. UFUPISHO
  1. Hoja
   1. Mifuko ni muhimu sana katika maisha ya binadamu
   2. Baadhi ya mifuko inadumu
   3. Asilimia kubwa ya mifuko ya aina hii hutengenezwa kwa ngozi/nguo
   4. Mifuko ya plastiki haidumu
   5. Mifuko hii ni nyepesi, rahisi kubebeka na hupatikana kwa wingi
   6. Hupendwa kutokana na wepesi na gharama yake ya chni
   7. Mifuko ya plastiki haiwezi kuoza
   8. Mifuko hii huchafua mazingira
   9. Mifuko hii ni hatari kwa maisha ya binadamu na wanyama
   10. Inapochomwa haiwezi kuteketea hadi kuwa jivu kama ilivyo mifuko ya karatasi. Zozote 9 , 1 mtiririko
  2.            
   1. Zitungwe sheria za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira
   2. Kuharamishwe matumizi ya mifuko ya plastiki
   3. Kuhimizwe matumizi ya mifuko mbadala
   4. Kuwazia kuwapo kwa njia nzuri ya kuteketezea mifuko ya plastiki
   5. Watumiaji wahimizwe kurejesha mifuko ya plastiki mahali Fulani kwa uteketezaji. Zozote 4 ,1 mtiririko

 3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
  1. /k/ /g/ng’/ gh/ (alama 1)
  2.      
   1. mshangao
   2. Maelezo/ taarifa
    (alama 2)

  3. Kiunganishi
   Kielezi cha mahali (alama 2)
  4.        
   1. Mbele ya –kihusishi cha ujirani/ mahali (alama1)
   2. Cha-kihusishi changamani / a-unganifu (alama 1)

  5. Vyafinyangwa- haliya ‘a’ / isiyodhihirika (alama 1)

  6. Somo- jina waitanalo watu walio na jina moja (alama 1)
   Funzo (alama 1)

  7. Mama hakumwambia Sipo alimeharaka (alama 1)

  8.    
   1. Lizwa (alama1)
   2. Jia (alama 1)

  9. Ng’ombe Yule aliumia uwato (alama 2)

  10. “Je , kuna manusura wowote?” Yeye alitakakujua. (alama 2) ( vitahiniwa vinnne kila moja 1/2 alama)

  11.               
   1. Kirai- Neno au fungu la maneno lisilodhihirisha maana kamilifu (alama 1)
   2. Ndani ya darasa –kirai kihusishi
    Nilimpata akilalama-kirai kitenzi( akiandika neno mojamoja atuzwe) (alama 2)
  12. “Utaweza kuwa mwindaji mashuhuri ikiwa utayafuata mashauri yangu,” alisema mwelekezi wake.
   Kila kitahiniwa ni nusu alama. Akiweka alama za usemi halisi apewe ½ alama (alama 2)

  13. S         KN+KT
   KN N+V+S
   N Mtoto
   V mmoja
   S aliyekuwa mgonjwa sana
   KT T+E
   T alitibiwa
   E jana (alama 4)

  14. Mwanafunzi aliyetumwa nyumbani juzi hajapata karo hadi leo. (alama 1)

  15. Migodi- Shamirisho kipozi (alama 1)
   Haraka - chagizo (alama 1)

  16. –ako -enu✓
   Mfano watoto wenu wananidhamu (alama 1)

  17. Sajili- mzizi (alama 1)
   k- kauli
   a-kiishio (alama 1)

  18. Na- kuenyesha mtendaji (alama 1)
   Na- ufupisho wa nafsi (alama 1)

  19. Takrima/ kutakrimu (alama 1)
   Maskani/ kusakini (alama 1)

  20. Kunywa! (alama1)
   Tubuni! (alama1)

  21. U-ZI (alama 1)

 4. ISIMU JAMII (alama10)
  1. Ukosefu wa ufasaha wa lugha/elimu
  2. kufahamu lugha zaidi ya moja
  3. kuficha siri
  4. kujitambulisha na kundi Fulani hasa vijana
  5. Kurithishwa na wazazi (vijana)
  6. Haina (sheng)masharti (lugha legevu)
  7. Uwezo mkubwa wa kukabiliana na mazingira (ubunifu wa hali ya juu) (Zozote 5x2) 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Kapsabet Pre Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest