MASWALI
- Ukiwa waziri wa Elimu nchini, umealikwa kuwazungumzia wanafunzi wa Kidato cha nne katika shule ya Ufanisi. Andika tawasifu utakayowasilisha.
- Wananchi ndio wakulaumiwa kutokana na kuzorota kwa usalama nchini Kenya. Jadili
- Andika insha itakayoafikiana na methali
Baniani mbaya kiatu chake dawa - Tunga kisa kinachomalizia maneno yafuatayo:
.....Nilijitolea kafara na msaada wangu ukazaa natija kwa wengi.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA INSHA
- Zingatia lugha ya mririko
- Kujitambulisha
- Jina
- Kuzaliwa/Eneo/Kaunti n.k
- Malezi yake
- Elimu –Msingi
- Sekondari
- Vyuo mbalimbali alivyosoma
- Tajriba
- Kazi aliyofanya/alizofanya kabla ya kuwa waziri
- Atajika kwa jambo /mambo gani
Mfano - Elimu ya juu – shahada kadhaa
- Miradi ya maendeleo
- Ziara alizofanya
- Uwajibikali wake/maadili kazini
- Falsafa yake ya maisha
- Changamoto alizopitia
- Ruwaza/maazimio yake
Lugha – mtahiniwa atumie nafsi ya kwanza
Usemi taarifa
Lugha rasmi itumiwe
- Kujitambulisha
- Wananchi ndoo wa kulaumiwa kufuatana na kuzorota kwa usalama nchini Kenya . Jadili
Kuunga
- Chuki na uhasama baina ya makabila/vita vya kikabila
- Uundaji wa kivikundi haramu vya vijana
- Tamma ya kutajirika km; wizi wa mifugo
- Wachochole kuingilia uhalifu kwa madai ya kujitafutia
- Wananchi kukataa kufichua wahalifu miongoni mwano/wanawaficha
- Umiliki wa silaha hatari na baadhi ya wananchi
- Mitazamo hasi ya wananchi kuhusu maafisa wa usalama/hawashirikiani nao
Kupinga - Usalama umekoseshwa na kutokuwepo kwa nafasi za kazi/wasio na kazi hulazimika kuingilia uhalifu ili wapate ajira
- Uhaba wa pesa za kuendeleza uimarishaji wa usalama.
- Idadi ndogo ya maafisa wa usalama
- Vifaa vya kuendeleza shughuli za usalama mf. Magari , silaha havitoshi.
- Kiwango cha chini cha mafunzo kwa walinda usalama
- Magaidi wanaotatiza usalama nchini kutoka nchi za kigeni
Tanbihi - Mtahiniwa asiwe na hoja chini ya saba
- Hoja zote zijadiliwe kikamilifu
- Mtahiniwa anaweza kuwa na idadi sawa na hoja katika pande zote, almuradi aonyeshe msimamo wake
- Akishughulikia upande mmjoa tu bila kugusia upande wa pili asipite kiwango cha C+
- Zingatia hoja zozote nyingine mwafaka
- Baniani mbaya kiatu chake dawa
Maana
Kiatu cha baniani - Kitu au watu ambao umewachukia au kudharau
Dawa - Kitu au watu husika huenda wakawa ndio jibu au jawabu au suluhu kwa tatizo fulani maishani mwa mtu au katika jamii
Tanbihi
- Mtahiniwa aandike kisa kuthibitisha matumizi haya ya methali
- Pande zote za methali zishungulikiwe. Anayeshughulikia upande mmoja asipate zaidi ya alama C – 08/20
- Anayekosa kulenga katika kisa chake amepotoka kimaudhui alam D -03/20
- Mtahiniwa lazima atunge kisa kitakachoafiki mdokezo huo. Kisa lazima kionyeshe kujitolea kafara(kujitolea kwa vyovyote licha ya vikwamizo) na kuzaa natija (kufaidika) kisa cha mtahiniwa kinaweza kuafiki hali zifuatazo
- Safarini anayejitolea kuwanusuru wengine wakati chombo au gari lilikuwa linaenda mrama.
- Kiongozi wa wafanyakazi kuwatetea wnzake licha ya pingamizi kutoka kwa mwajiri hatimaye hali yao ya kufanya kazi inaboreshwa.
- Yeye akiwa mtoto aliyeajiriwa kuwasaidia ndugu zake na wazazi wakafaidika.Singatia hali nyingine zinazoafikiana na dondoo
Tanbihi - Akikosa kumalizia kwa dondoo alilopewa lakini kisa kiafikiane nalo, amepungukiwa kimtindo
- Akiongezea maneno baada ya dondoo au katikati achukuliwe kuwa ana upungufu wa kimtindo
- Lazima kisa kimhusu yeye mwenyewe. Asipojihusisha amepotoka kimaudhui na atuzwe D – 03/20
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Momaliche Joint Pre Mock Exams 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students