Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kassu Jet Pre Mocks 2022

Share via Whatsapp
MAAGIZO
  1. Andika jina lako na nambari ya usajili kwenye nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  3. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  4. Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  5. Kila insha isipungue maneno 400.
  6. Kila insha ina alama 20.
  7. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  8. Insha zote sharti ziandikwe katika nafasi ulizoachiwa kwenye kijitabu hiki cha maswali.
  9. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo. 
Kwa matumizi ya mtahini pekee 

Swali

Upeo

Alama

1

20

 

 

20

 

Jumla

40

 



MASWALI

  1. LAZIMA
    Chamko la ugonjwa wa Korona lililemaza shughuli za michezo nchini. Wewe ni katibu wa jopokazi lililoteuliwa na Waziri wa Michezo kubuni mikakati ya kufufua michezo katika taasisi za elimu nchini. Andika kumbukumbu za mkutano huo.
  2. Vijana wamekuwa wakichelea kuhusika katika mchakato wa uchaguzi. Jadili vyanzo vya hali hii huku ukiwapendekezea vijana umuhimu wa kubadili msimamo huu. 
  3. Tunga Kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:  Achanikaye kwenye   mpini hafi njaa.
  4. Andika insha itakayomalizikia kwa:
    ...nilipotua nchini, nilishusha pumzi, nikamshukuru Jalia kwa kuponea chupuchupu katika uvamizi huo.


MWONGOZO

  1. Chamko la ugonjwa wa Korona lililemaza shughuli za michezo nchini. Wewe ni katibu wa jopokazi lililoteuliwa na Waziri wa Michezo kubuni mikakati ya kufufua michezo katika taasisi za elimu nchini. Andika kumbukumbu za mkutano huo.
  2. Vijana wamekuwa wakichelea kuhusika katika mchakato wa uchaguzi. Jadili vyanzo vya hali hii huku ukiwapendekezea vijana umuhimu wa kubadili msimamo huu.
  3. Tunga Kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo: Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
  4. Andika insha itakayomalizikia kwa …nilipotua nchini, nilishusha pumzi, nikamshukuru Jalia kwa kuponea chupuchupu katika uvamizi huo. 

Hii ni insha ya kumbukiumbu. Utaini wake ujikite katika vipengele viwili vikuu:

  1. Muundo
  2. Maudhui

 

  1.  Muundo
    1. Kichwa kionyeshe:
      1. Kundi linalokutana
      2. Mahali pa mkutano
      3. Tarehe ya mkutano
      4. Wakati wa mkutano
    2. Waliohudhuria-vyeo na nyadhifa zao zidhihirishwe
    3. Waliokosa kuhudhuria kwa udhuru
    4. Waliokosa kuhudhurria bila udhuru
    5. Waalikwa/Katika mahudhurio- hawa ni wale waliohudhuria mkutano japo si wanachama ( si lazima)
    6. Ajenda za mkutano
    7. Kumbukumbu zenyewe/ kiini cha mkutano:
      1. Utangulizi/ kufunguliwa kwa mkutano
      2. Wasilisho la mwenyekiti
      3. Kusomwa na kuthibitishwa kwa kumbukumbu za mkutano uliopita/uliotangulia
      4. Yaliyoibuka kutokana na kumbukumbu hizo
      5. Masuala mapya yaliyoadiliwa/masuala mapya( kulingana na ajenda za siku)
      6. Masuala mengineyo
      7. Hitimisho
        1. Sahihi, jina la mwenyekiti na tarehe
        2. Sahihi, jina la katibu na tarehe
  2. Maudhui
    Mtahiniwa adhihirishe majadiliano yalivyofanywa na hatima ya mjadala huo- yaani uamuzi ulioafikiwa na wanachama kuhusu suala zima la ufufuzi na uhaishaji wa shughuli za michezo katika taasisi za elimu nchini.

Zifuatazo ni baadhi ya hoja:

  1. Mikakati ya kutambua na kukuza talanta mashinani
  2. Mikakati ya kuwamotisha wa wanamichezo
  3. Uteuzi wa wasimamizi/viongozi katika michezo mbalimbali
  4. Shughuli za urekebishaji wa muundo msingi-viwanja
  5. Ufadhili wa shughuli za michezo
  6. Kuandaliwa kwa semina za uhamasisho kuhusu michezo katika magatuzi mbalimbali
  7. Mikakati ya kuzuia maenezi ya korona viwanjani
  8. Jinsi ya kukabiliana na visa vya kutumia muku miongoni mwa wanariadha na wanamichezo wengine
  9. Kuandaliwa kwa warsha za mafunzo kwa makocha na wasimamizi wa michezo mbalimbali
  10. Upanuzi wa mawanda ya michezo kwa kujumuisha tasnia nyingine zisizokuwepo
  11. Ushiriki katika michezo ya ndani na nje ya nchi

Tanbihi
Hii ni kumbukumbu wala si ripoti, sharti maadiliano yadhihirike na uamuzi ulioafikiwa kuonyeshwa 

2.Vyanzo vya vijana kutohusika katika mchakato wa uchaguzi/ sababu ya kutohusika kwa vijana katika mchakato wa uchaguzi.

  • Mchakato itahusisha kujiandikisha kama wapiga kura na vilevile,kampeni,kuelimisha wapiga kura,kuwania viti na kupiga kura kwenyewe. Yaani vyanzo vya vijana kutohusika kabisa.
  • Vyanzo:
  • Ukosefu wa Akira
  • Wizi wa kura/ tetesi za wizi wa kura
  • Ukosefu/uhaba wa pesa za kuwania viti
  • Wazee kutawala hali mchakato mzima
  • Uvivu/uzembe miongoni mwa vijana
  • Vijana kutoelewa umuhimu wa kuhusika
  • Uhaba wa elimu miongoni mwa vijana/ uhaba wa elimu ya juu (shahada na kuendelea) itakayowawezesha kuwania viti.
  • Mzozo ya uchaguzi/vita

HAKIKI MAJIBU
Umuhimu wa kubadili msimamo huu/umuhimu wa kuhusika katika mchakato wa uchaguzi/umuhimu wa uchaguzi

  • Kuchagua viongozi bora/wenye maadili/kukabiliana na uongozi mbaya
  • Kupata maendelea kama vili muundo msingi iletwayo na uongozi bora
  • Kupata kuchagulia kuwa viongozi na kuhusika katika maamuzi muhimu nchini/kuamua mustakabali wao
  • Kuelimisha wapiga kura kuhusu umuhimu wa uchaguzi
  • Kupata nafasi za ajira
  • Kuepuka vita vya baada ya uchaguzi/kutumiwa vibaya na wanasiasa

HAKIKI MAJIBU
3.Achanikaye kwenye mpini hafi njaa
Hii ni insha ya methali
Mtahiniwa abuni kisa kitakachodhihirisha maana ifuatayo:

  1.  Anayechoka akifanya kazi kwa jembe shambani hakosi chakula
  2. Ataabikaye akifanya kazi ijapokuwa ngumu hatimaye atafaidika kwa kuwa kazi hiyo itamnufaisha au itamridhisha.

Matumizi ya methali hii.

  1. Hutumiwa kumtia moyo mtu afanye kazi kwa bidii ili afanikiwe
  2. Hupigiwa mfano mtu aliyetaabika akitafuta hadi mwishowe akafanikiwa na pengine hata kupata maendeleo makuu
  3. Methali inaweza kutumiwa katika mktadha ifuatayo; mkulima anayefanya bidii, mwanafunzi anayejitahidi masomoni mwishowe afaulu, mwanasiasa anayefanya kampeni kwa bidii hadi akateuliwa na kadhalika

Mtahini anastahili kutunga insha ya masimulizi inayodhihirisha maana na matumizi ya methali hii.
Mtahini aonyeshe sehemu mbili ya methali
Mapambo ya lugha yawepo
Mwongozo wa kudumu urejelewe katika utuzaji.

4.MUHIMU.

  • Hii ni insha ya mdokezo
  • Mtahiniwa sharti amalizie kisa kwa maneno haya.
  • Mtahiniwa atumie mbinu rejeshi ili kumrejesha msomaji kwenye matukio ya awali
  • Mtahiniwa akiacha au aongeze neno moja au mawili atakuwa amejibu swali ila lichukuliwe kama kosa dogo tu la kimtindo
  • Akikosa kuanza kwa mdokezo aliopewa atakuwa amejitungia swali D- 02/20
  • Mtahiniwa aandike kichwa cha insha ingawa asipoandika si huja.

Taswira zifuatazo zinaweza kuzingatiwa;

  1. Kisa kisimuliwe kuhusu mhusika ambaye anarejea nchini kutoka nje
  2. Mhusika huyu yumkini alikuwa ameenda ngambo kwa shughuli za kimasomo,kikazi au ziara
  3. Asimulie matukio yaliyofanyika katika nchi alikokuwa kiasi yeye kukushurtika kurejea nyumbani
  4. Anaweza kusimulia kuhusu uvamizi wa nchi moja dhidi ya nyingine kama ule wa Urusi dhidi ya Ukraine ambapo wageni wanakimbilia usalama
  5. Yumkini mhusika huyu alikuwa akisafiri kurejea nyumbani baada ya kipindi cha masomo, ziara au kikazi kupitia cnhi fulani ambapo mashambulizi yanachipuka
    • Usahihishaji wa insha ukadiriwe kulingana na viwango vya usahihishaji.
    • Mtahiniwa asiondolewe alama za urefu badala yake mwongozo ufuatao wa kudumu uzingatiwe

Robo maneno 174
Nusu maneno 175 hadi 274
Robo tatu 275 hadi 374
Kamili 375 na zaidi.

Tanbihi:
Utahini ufanywe kwa kuzingatia mwongozo wa kudumu wa usahihishaji wa insha Kitaifa

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kassu Jet Pre Mocks 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest