Maagizo
- Andika insha mbili.
- Insha ya kwanza ni ya lazima
- Kisha chagua insha nyingine kutoka tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400
- Kila insha ina alama 20

Maswali
- Wewe ni chifu wa Kata ya Mwangaza. Umeandaa mkutano wa wanakata wako. Andika hotuba utakayo toa kuhusu mambo yanayoathiri utangamano wa kitaifa na hatua zinazoweza kuchukuliwa.
- Fafanua hatua ambazo zimechukuliwa nchini ili kukabiliana na tatizo la unyanyasaji wa jinsia ya kike.
- Andika insha itakayo dhihirisha maana ya methali hii.
Ukicheza ujanani utalipa uzeeni - Andika kisa kitakacho malizikia kwa maneno yafuatayo.
...sasa ninaelewa maneno yake kuhusu kufanya maamuzi ya busara. Sasa nimepata baraka za wazazi na ridhaa yakuishi pamoja.

Mwongozo wa Kusahihisha
- Wewe ni chifu wa kata ya Mwangaza. Umeandaa mkutano wa wanakata wako. Andika hotuba utakayotoa kuhusu mambo yanayoathiri utangamano wa kitaifa na hatua zinazoweza kuchukuliwa.
- JIBU
- Hii ni insha ya kiuamilifu
- kichwa kionyeshe; mada na hadhira lengwa
Neno hotuba sharti liwepo
- UTANGULIZI
- Huanza kwa kutaja watu kwa vyeo vyao na majina yao rasmi.
- Aliye na cheo cha juu zaidi hutambuliwa kwanza ukielekea chini/itifaki izingatiwe.
- Hufuatiwa na maamkuzi
- Baadaye lengo la hotuba yenyewe.
- MWILI
- Ndicho kiina cha hotuba
- Huanza katika aya ya pili
- Kila hoja hufafanuliwa katika aya yake.
- Ili hoja ya mtahiniwa ikamilike lazima mwanafunzi azingatie hatua zifuatazo:
- Ataje hoja,aieleze na ataje hatua zinazoweza kuchukuliwa kusuluhisha mambo yanayoathiri utangamano wa taifa(katika aya moja).
- HOJA
MAMBO YANAYOATHIRI UTANGAMANO WA KITAIFA- Ufisadi kama vile kuajiri watu kwa mapendeleo
- Ukabila
- Viongozi kueneza chuki/uchochezi
- Mafunzo hasi ya kidini/
- Ukosefu wa ajira/utabaka
- Kubagua maeneo Fulani kimaendeleo.
- Ukimbizi wa ndani kwa ndani
- Mashambulizi ya kigaidi/kikoo/kijamii
- Migogoro ya ardhi/mipaka ya kijamii
- Hatua zinazofaa kuchukuliwa
- Lugha ya taifa kuhimizwa
- Kukabiliana na ufisadi
- Usawa katika ugawaji wa raslimali
- Kuelimisha kuhusu umoja wa kitaifa/hamasisho
- Tamasha za kitamaduni
- Kutalii sehemu zingine za nchi
- Ndoa za makabila tofauti/ndoa za mseto
- Serikali ya muungano
- Viongozi wachochezi kuchukuliwa hatua kisheria
- HITIMISHO
Hatibu kuwashukuru wote waliohudhuria kwa muda wao na utulivu wao wakati wa kumsikiliza. - TANBIHI
- Alama za mtajo hazitumiki
- Hoja zisipungue nane
- JIBU
- Fafanua hatua ambazo zimechukuliwa nchini ili kukabiliana na tatizo la unyanyasaji wa jinsia ya kike.
- HOJA
- Hatua kali za kisheria kwa wanaowapiga na kuwabaka, na wanaotekeleza mila ya kuketa na ndoa za mapema
- Kufanya kampeni dhidi ya mila zinazochangia udunishaji wa wanawake
- Kuwashauri watoto wa kike waende shuleni
- Kuanzisha makao ya watoto wa kike wanaotishiwa na mila mbaya
- Kuelimisha mwanamke kuhusu haki zake
- Kuhimiza wanawake kupigania haki zao
- Serikali kutenga pesa za kuelimisha watoto wa kike
- Kuwepo kwa mashirika ya kutetea haki za wanawake kama FIDA na maendeleo ya wanawake.
- Hazina ya kutoa mikopo kwa wanawake kama K.W.F.T
- Kuwapa wanawake nafasi sawa za ajira
- Kutekelezwa kwa kipengele cha thuluthi mbili ya wanawake katika uongozi
- Kupunguza alama ambazo wasichana wanapaswa kufikisha ili kujiunga na vyuo vya elimu ya juu
- Kubuni sheria za kuwawezesha kumiliki mali
- TANBIHI
- Kadiria hoja za mwanafunzi
- Ili hoja iwe kamili, mtahiniwa ataje hoja na aitolee maelezo katika aya moja.
- HOJA
- Andika insha itakayodhihirisha maana ya methali hii
Ukicheza ujanani utalipa uzeeni.- MATUMIZI
- Hutumiwa kuwahimiza watu wajitahidi kujitengenezea maisha yao ya kesho/mustakabali wao wakiwa wangali na uwezo wa kufanya hivyo.
- TANBIHI
- Mtahiniwa sharti aandike kisa kitakachodhihirisha maana ya methali
- Kichwa kionyeshe pande mbili za methali:
- kucheza ujanani
- kulipa uzeeni
- Mtahiniwa atakayerejelea upande mmoja atakuwa amepungukiwa kimaudhui. Insha yake isizidi alama 10
- Atakayeandika kisa kisichohusiana na methali hii atakuwa amepotoka kimaudhui. Atuzwe alama 03.
- Atakayejitungia swali na kulijibu atuzwe BK 01
- Dhana ya kulipa uzeeni ijitokeze hata kama ni kwa aya chache/sentensi chache.
- Andika kisa kitakachomalizikia kwa maneno yafuatayo. ...sasa ninaelewa maneno yake kuhusu kufanya maamuzi ya hekima au busara.Sasa nimepata baraka za wazazi na ridhaa ya kuishi pamoja.
- MAJIBU
- Hii ni insha ya mdokezo
- Mtahiniwa ajihusishe na kisa (nafsi ya kwanza)
- mtahiniwa amhusishe pia aliyempa wosia(nafsi ya tatu)
- Ruwaza ya kisa idhihirike kwamba mhusika alikuwa amepotoka na kuvuruga uhusiano na wazazi wake LAKINI akapata mawaidha/mwelekeo/wosia kutoka kwa mhusika mwingine na uhusiano mwema ukarejeshwa baina yake na wazazi wake.
- Baadhi ya visa ni;
- Mhusika anayetoroka nyumbani kwa kukosana na wazazi ,apewe ushauri kisha aamue kurudi kuomba msamaha na kuendeleza maisha pamoja na wazazi wake.
- Mhusika anayetamauka kimasomo kwa sababu fulani .Jambo hili livuruge uhusiano na wazazi wake ,apewe ushauri na mwalimu au mwanafunzi mwenzake, asome afaulu na kufurahisha wazazi wake.
- MATUMIZI
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Bunamfan Cluster Pre Mock Exam 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates