Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Lugari Constituency Joint Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp
                                                                                      SEHEMU YA   A 
                                                                            (FASIHI SIMULIZI)   ALAMA 20
  1. SWALI LA LAZIMA
    1. Eleza miviiga katika fasihi simulizi. (alama2)
    2. Fafanua sifa tano za miviga. (alama 5)
    3. Wewe ni mwigizaji wa michezo ya jukwaani, eleza mambo matano ambayo utazingatia ili kufanikisha uigizaji wako. (alama 5)
    4. Unaniuia kutumia mbinu ya maandishi kukusanya na kuhifathi habari kuhusu miviga ya tohara,
      1. Eleze manufaa ya kutumia mbinu hii? (alama 4)
      2. Eleza udhaifu wa kutumia mbinu hii? (alam4)

                                                                                     SEHEMU YA B

                                                     (MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI  ZINGINEZO

                                                                HADITHI YA FADHILA ZA PUNDA – ALAMA 20

    1. ''Nitapata wapi mwandani kama mkee wangu marehemu?“
    2. Eleza mukthatha wa dondoo hiili ? (alama 4)
    3. Fafanua sifa tatu za msemaji. (alama 6)
    4. Tambua na ufafanue maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
    5. Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa kwenye dondo hili. (alama 2)
    6. Eleza masaibu yanayomkumba Lilia katika hadithi hii. (alama 4)
                                               AU
  1. Kwa kuzingatia hadithi zifuatazo eleza namna maudhui ya unyanyasaji yanavyojitokeza  (alama 20)
    1. Fadhila za Punda
    2. Sabina
    3. Nipe Nafasi
    4. Pupa
    5. Toba ya Kalia

                                                                                        SEHEMU YA C 

                                                                       TAMTHILIA YA BEMBEA YA MAISHA 

  1. Ni mshtuko wa namna Fulani unaotokana na mtu kukabiliwa na hali ya maisha ya watu wengine ambayo inapingana na ile yake.
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili? (alama 4)
    2. Eleza namna ambavyo msemewa wa dondoo hili anavyojenga maudhui ya nafasi ya mwanamke. (alama 6)
    3. Onyesha namna maudhui ya ubabe dume yanavyodhihirika katika tamthilia hii.   (alama 10)
                                                                     AU
  2. Kwa kurejelea tamthilia hii eleza namna mila na destruri zinavyoweza kuzua migogoro katika jamii. (alama 20)

                                                                                         SEHEMU YA D

                                                                               RIWAYA YA CHOZI LA HERI

  1. Eleza namna wahusika mbali mbali walivyokabiliana na changamoto zilizowakumba riwayani. (alama 20)
                                                                            AU
  2. Binadamu aliumbwa kupambana na ulimwengu na kutumia rasilimali za Mungu kuyaboresha maisha yake.  
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili? (alama 4)
    2. Eleza umuhimu ya msemaji kwa kuijenga riwaya ya Chozi la Heri. (alama 4)
    3. Eleza ukitoa mifano riwayani namna binadamu anavyotumia rasimali anayopewa na Mungu kuyaboresha maisha yake. (alama 6)
    4. Kwa kutoa mifano riwayani, eleza namna ukiukaji wa haki za watoto ulivyojitokeza.  (alama 6)

                                                                                         SEHEMU YA E

                                                                                     USHAIRI     (ALAMA 20)

                                                                         Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

                                                                                        SABUNI YA ROHO

  1. Ewe tunu ya mtima kwa nini wanikimbia?
    Ndiwe suluhu za zama, waja wakumbilia,
    Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
    Ndiwe sabuni ya roho,ndiwe mvunja mlima.

  2. Ndiwe mafuta ya roho,walisema wa zamani,
    Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
    Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

  3. Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
    Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
    Sura zao mefufua, wanazuru kila Nyanja,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

  4. Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
    Watazame mayatima, kwao kumekuwa duni,
    Wabebe waliokuwa wainue walio chini,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

  5. Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
    Umezua uhasama waja kupata mizozo,
    Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

  6. Umevunja usuhuba, familia zazozana,
    Walokuwa mahabuba kila mara magombana,
    Roko zao umekaba, manyumbani wachinjana,
    Ndiwe sabuni ya roho ndive mvunja mlima.

  7. Nakutafuta kwa hamu sabuni unirehemu,
    Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
    Niondoe jehanamu, ya ufukara wa simu,
    Ndiwe sabuni ya roho ndiwe mvunja mlima

  8. Naondoka wangu moyo, nikwitapo itika,
    Fulusi wacha uchoyo, tatua walonifika
    Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika
    Ndiwe sabuni ya roho ndiwe mvunja mlima.

    MASWALI
    1. Tambua na udhibitishe nafsi neni katika shairi hili? (alama 2)
    2. Kwa hoja nne eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
    3. Tambua uhuru wa kishairi unaojitokeza katika shairi hili. (alama 2)
    4. Mshairi atatumia mbinu gani za lugha katika shairi lake. (alama 3)
    5. Tambua bahari zozote tatu zinazojitokeza katika shairi. (alama 3)
    6. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
    7. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)

                                                                              MWONGOZO WA KUSAHIHISHA 

  1. FASIHI SIMULIZI 
    1. Ni sherehe za kitamaduni zinazofanywa na jamii mbalimbali katika kipindi maalum xha mwaka. (Al 2)
      • Huandamana na matendo au kanuni flani.
      • Huongozwa na watu mahususi ambao huiendeleza.
      • Huandamana na utoaji mawaidha.
      • Maleba maalum huvaliwa na wanahusika ili kuwatofautisha.
      • Shugli za miviga hufanywa m,ahali sherehe inapofanyiwa.
      • Huambatana na utamaduni wa jamii husika.  ( zozote 5 x 1 = 5)
    2.  
      • Kuwa mchangamfu na mcheshi.
      • Kuhakikisha umefahamu utamaduni wa jamii husika.
      • Kufahamu hadhira na mahitaji yake.
      • Kutumia ufaraguzi.
      • Kuwa na kumbukumbu nzuri.
      • Kubadilisha kiimbo kulingana na mahitaji
      • Kutumia viziada lugha k.v ishara za uso.
      • Kushirikisha hadhira .
      • Kutumia lugha kwa uhodari ili kuipa mvuto.
      • Kuvalia maleba yanayooana na maigizo.
      • Kujenga mlahaka mwema na hadhira.  ( zozote 5 x 1 = 5)
    3.  
      • Si rahisi kwa data kusahaulika.
      • Huweza kufikia vizazi vingi.
      • Si ghali kama mbinu zingine.
      • Si rahisi kufisidiwa au kupotea. ( zozote 4 x 1 = 4)
    4.  
      • Hayaonyeshi baadhi ya mambo kama kiimbo, toni na ishara.
      • Si hai, hayawezi kwenda wala kusoma.
      • Baadhi ya waandishi wanayohitaji kwa wakati mahususi.
      • Huikwezesha fasihi simulizi taadhira asili (huondoa utangamano kati ya hadhira na fanani).

  2.  MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI  ZINGINEZO
    1. Muktadha: Pastor Lee Imani
      • Akijiwazia mwenyewe baada ya kupata shinikizo la mke mwingine baada ya kifo cha mkewe. Anaeleza kuwa kwa kuwa hayupo anayelingana na marehemu mkewe. (1x4)
      • Mcha Mungu - anaanzisha na kuendeleza kanisa
      • Mkarimu -  anampa mamake Luka jira
      • Mdasisi - anamwita Luka na kumuuliza nia yake kwa bintiye 
      • Mwenye mapenzi - alimpenda marehemu mkewe pia bintiye (Za kwanza 3 x 2 = 6)
        Tanbihi
        1. Kadiria majibu mengine ya mwanafunzi, maelezo ya sifa yao na sifa yenyewe.
        2. Akikosea msemaji katika (2a) asituzwe sehemu hii
    2.  
      1. Ndoa na mapenzi
      2. Kifo/mauti   (Za kwanza 2 x 2 = 4) 
        • alama 1 kutaja, 1 ufafanuzi wa kweli
    3.  
      1. Swali balagha
      2. Tashibihi               (Za kwanza 2)
        • Atolee maelezo ya kila mbinu, asipoeleza asitozwe chochote
  3.  
    1. FADHILA ZA PUNDA
      • Lilia kushurutishwa kuacha kazi
      • Lilia kupigwa na Luka kwa kosa la kutokeleza chumvi kwemnye chakula
      • Lilia kukosa usingizi kwa kumgoja Luka ambaye haji
      • Luka kumpiga Lilia kwa kosa la kumtembelea ofisini
      • Luka kumyanyasa Lilia kwa kuwa na mpenzi mwingine
      • Luka kumlazimisha Lilia kuanadmana naye kwenye kamepeni licha ya kuwa mjamzito    ( zozote 4 x 1 = 4)
    2. SABINA
      • Yunuke anamyanyasa Sabina kwa mumwachia kazi ya kuwachukua ng'ombe malishoni na kuwakama
      • Yunuke kumlazimisha Sabina kupeleka kisonzo shambani kabla ya kwenda shuleni
      • Sabina analazimika kuuza maziwa kwa soko la Itumbe kabla ya kwenda shuleni
      • Babake kumakana baada ya kuzaliwa kwake Sabina
      • Mjomba wake Ombati kutaka kumuoza mapema 
      • Yunuke kumyima Sabina fursa ya kudurusu akiwa nyumbani
      • Yunuke kumyima Sabina ushirikiano na wanawe
      • Yunuke kumtusi Sabina k.m anapomweleza kuwa amepokea barua    ( zozote 4 x 1 = 4)
                                 Kadira majibu mengine ya mwanafunzi
    3. NIPE NAFASI
      • Mamake msimulizi ananyanyaswa kwa kutotumia pesa za mumewe
      • Wazazi wa mumewe mamake msimulizi wananyanyasa mamake msimulizi kwa kuto sikiliza malalamishi yake kuhusu mumewe kuwa na mke mwingine 
      • Babake msimulizi kutumia pesa mkewe kupitia kwa nyanyake ambaye angeamua kumpa au kutompa
      • Mamake msimulizi kulaimiwa kwa kifo cha mwanawe na ukoo wa bwanake   ( zozote 4 x 1 = 4)
    4. PUPA
      • Bi mtego anamyanyasa Mwakuona kwa kumdanganya kuwa angefadhiliwa kwa kukubali kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja.
      • Wamiliki wa Chengaways wanawanyanasa wasichana kwa kuwaingiza katika ukahaba
      • Mwakuona ananyayaswa kimapenzi na mwanamme mke kwenye chumba alichopelekwa kule Changeways.
      • Wamiliki na walinzi wanawanyanyasa wasichana kwa kuwanyima uhuru wa kutembe. (Wanafungiwa baada ya kutoweka kwa Mwakuina.  ( zozote 4 x 1 = 4)
        Tanbihi: Mtahini akadilie hoja zingine.
    5. TOBA YA KALIA
      • Bwana Kalia anamyanyasa Jack kwa kubadilisha ushindi wake kweny mashindano ya Sayansi na kumpa mwanawe Siri
      • Wazazi wa Siri wanamyanyasa Jack kwa kutotimiza ahadi yao ya kumsomesha baada ya kifo cha wazazi wake
      • Wazazi wa Siri wanamyanyasa Jack kwa kutaka awape nusu ya faida aliyopata katika biashara ya kuuza viatu.
      • Jack ananyanyasawa kwa kupokonywa nafasi ya kupata ufadhili wa kupata masomo na familia ya Bi. Kalia na Bi. Mshewa
        ( zozote 4 x 1 = 4)     Kadiria hoja zingine
  4. TAMTHILIA YA BEMBEA YA MAISHA
    1. Msemaji - Asna
      Msemewa - Sarah
      Mahali - Hospitalini
      • Kiini - Alirejelea slivyoshangaa namna ambavyo Bunju alizingatia kushugulikia na familia yake, yeye mke na watoto bila kujali wengine/Alikuwa akitafsiri ujumbe wa '' culture shock'' kwa mamaye.  ( zozote 4 x 1 = 4)
    2. Msemwa ni Sarah
      • Anajenga maudhui ya uvumilivu
      • Anaendeleza mila mna tamaduni
      • Mwanamke ameajibika kulilinda jamii k.v kuwafunza wanawe 
      • Anashauri vyema k.v kwa wanawe
      • Mwanamke anaonekana ndiye wa kudhulumiwa katika ndoa.
      • Nafasi ya mwanamke ni jikoni na kumhudumia mumewe   ( zozote 6 x 1 = 6)
        Tanbihi 
        1. Kaadiria majibu mengine ya mwanafunzi
        2. Akikosea msemewa kwenye swali la (4b) asituzwe hapa
    3. Maudhui ya ubabedume
      • Kazi za nyumbani ni za mama
      • Mtoto wa kike kutoaminiwa k.v wananwe Sara kuonekana si muhimu
      • Panapotokea tatizo la uzazi mama ndiye wa kulaumiwa k.v Sarah
      • Mwanamke kumjuza mmewe kila kitu akifanyacho
      • Maomo ya mtoto wa kiume kuthaminiwa   ( zozote 5 x 2 = 10)
        Tanbihi akadirie majibu ya mwanafunz9i
  5. MILA NA DESTURI KUZUA MIGOGORO
    • Mwanamke kutoruhusiwa kulala nyumbani kwa mwanawe wa kike aliyeolewa ; Mgogoro ni Bunju na Neema kutofautiana
    • Mila ya kuwaamini watoto wa kiume kushinda wa kike - Yona anakuzwa na mgogoro wa nafsi na kuzama katika ulevi
    • Kutothamini mtoto wa kike - Mgogor kati ya Yona na Sarah
    • Mila inayomruhusu mwanamke kuwa ndiye wa kutekeleza majukumu ya nyumbani - Mgogoro kati ya Yona na Sarah, hasa Sarah anapokuwa mgonjwa.
    • Mila inayomlazimisha mwanamke kumtegemea, kumheshimu na kuwa mnyenyekevu kwa mmewe - Neema nakubali pendekezo la Bunju katika kila hali jambo linalomkosesha amani.
    • Mila inayopendekeza mtoto wa kike kuolewa anpoifika umri flani - Asha na mamake wanakosa kuelewana kwa hilo
    • Mila ya kuhalalisha ulevi ( Luka anapozungumza na Beni na Yona - inaleta mgogoro baina ya Yona na Sarah (katika ndoa)
    • Mila ya kumfunza mtoto wa kike kwa kuwa hana umuhimu (maelezo ya Luka) - Yona anakosa kujukumika kuwafunza wanawe.
    • Mila kuwa mtoto mkubwa katika familia wa kiume ndiye anayestahili kumtunza mamake - Neema na Bunju wanazozana wakati Neema alipopendekeza kumhifadhi mamake.  ( zozote 10 x 2 = 10)
      Tanbihi 
      1. Mtahini akadirie majibu mengine
      2. Mtahiniwa lazima lenge pande zote mbili nkatika maelezo yake la sivyo, asituzwe chochote.
  6. CHOZI LA HERI
    • Langa kiriri anapata dhiki ya kupoteza kazi katika Shirika la Maghala ya nafaka anaamua kufanya kazi ya ukulima
    • Baada ya Umu kuwapoteza ndugu zake Dick na Mwaliko anaamua kwenda kupiga ripoti katika kituo cha polisi ili kupata usaidizi
    • Petu alipopata hedhi yake ya kwanza aliamua kumjulisha bibiye ambaye anamtafutia tambara la blanketi kama sodo.
    • Baada ya Sauna kuhujiwa kimapenzi na Bw. Moya, anaamua kutoka nyumbani kwao na kutamba katika ulimwengu.
    • Kutokana na adhabu ambayo Dick angepewa na mwajiri wake, Buda anaamua kuingilia ulanguzi wa dawa za kulevya
    • Chandachema anaamua kuwasimulia kina Zohali, Umu na Mwanaheri ili kupunguza mlemeo wa matazio yake.
    • Chandachema anaondoka kwa jirani katini baada ya Satua mke wa jirani wake kuanza kumwona mzigo.
    • Zohali anapigana na majitu yaliyotaka kumhujumu utu wake na kumyanyasa kimapenzi
    • Baada ya mkewe Mwangeka, Lily kuaga dunia, Mwangeka anaamua kumuua Apondi ambaye amziba pengo hilo.
    • Neema na Mwangeka kw akukosa mtoto wanaamua kumpanga Mwaliko 
    • Mzee Mwimo Msubili baada ya ardhi yake kuwa ndogo kustahimili familia yake kubwa anaamua kuwahamish awake zake wawili wa mwisho katika msitu wa Heri.
    • Mamake Sauna anaamua kuavya mimba ili kujieupusha na aibu ambayo ingewakumba katika familia.
    • Sauna aliamua kuingilia ulanguzi wa watoto ili apate pato la kujikimu kimaisha.
    • Shomsi baada ya yote aliyoyapitia anaamua kuingilia unywaji wa pombe ili kupunguza mawazo
    • Baada ya mwanawe Mwangeka, Becky kuaga anaamua kumpanga Umu ili kuziba pengo.
    • Kutokana na upweke ambao Umu alikua nao katika mlima wa Simba anaamua kuondoka nyumbani kwano na kwenda kuanza maisha upya
    • Baada ya Neema kukuiokota kitoto ambacho hakijui anachukua anachukua hatua moja kwa moja mpaka kituo cha polisi na kisha kituo cha Benefactor.
    • Baada ya Ridhaa Kurejea nyumbani kwa kuitwa mfwata mvua, mamake anamrudisha shuleni na kuzungumza na mwalimu.
    • Kutokana na yale amabayo Zohali alifanyiwa na wazizi wake k.v. Kusimwaga anaamua kumdanganya mtawa Packa kwamba ni yatima
    • Kutokana na msongo wa mawazo wa Umu kwa kukosa wazazi anaamua kumwelekeza mwalimu ambaye anamtafutia wafadhili
    • Kutokana na ukosefu wa karo mamaye mamaye Kairu anaamya kuongea na mwalimu mkuu ili kumlipia karo kidogo kidogo
    • Kutokana na mawazo yake kuwa biashara yake ni uovu, Dick anaamua kuanzisha bisahra ya kuuza electroniki.
    • Pete anapoona kuwa anaenda kuwa na watoto watatu kwa umri wake mdogo, anaamua kujitoa uhai yeye pamoja na katoto chake.
    • Kutokana na hali duni ya maisha vyuoni, wanafunzi wanaamua kujihusisha katika unywaji wa  pombe haramu.
    • Tuama aliamua kupashwa tohara ili asitengwe na wenzake  (zozote 20, 1x 1)
      Tanbihi 
      1. Lazima mtahiniwa azungumzie kuhusu tatizo kisha mbinu aliyotumia kujinasu, la sivyo asituzwe chochote.
  7.  
    1.  
      1. Maneno ya Chandachema
      2. Akisimulia wenzake - Umu, Mwanaheri na Zohali
      3. Wako aktika shule ya upili ya Tangamano
      4. Chandachema anawasimulia wenzake dhiki alizopitia maishani mwake tangu utotoni
    2. Msemaji; Chandachema
      • Anawanjenga wahusika wengine; sifa ya Fumba (babake)
      • Swala la ukiukaji wa haki za watoto limejitokeza
      • Anaendeleza ploti ya riwaya
      • Anaibua swala la umaskini, anaajiriwa akiwa umri mdogo (1x1 = 4)
        Akikosea msemaji katika (7a), asitozwe chochote katika sehemu hii.
    3.  
      • Watoto wanatafuta kazi wakiwa umri mdogo ili kuyakidhi mahitaji yao - Chandachema
      • Watoto wanatumia kidogo walichonacho kuyanusuru maisha yao - Dick kuanzisha biashara ya electroniki
      • Kutia bidii katika biashara waliyonayo ili kukidhi mahitaji - Mamake Kairu
      • Kutia bidii masomoni ili kuyaboresha maisha - Umu
      • Ridhaa kujenga kituo cha afya cha Mwazno mpya ili kuendeleza huduma za matibabu
      • Pete kaujiriwa kwenye kiwanda cha sare licha ya kupata mshahara duni anaita bidii awalishe watoto wake (zozote 6)
    4.  
      • Watoto wanaajiriwa wakiwa umri mdogo - Chandachema
      • Watoto wanatumiwa vibaya na watu kuendelesha biashara zao - Dick
      • Watoto kuibiwa na kutekwa na kuuzwa. Sauna kuiba Dick na Mwaliko
      • Watoto wanaachiwa maleiz na wazazi wao - Naomi anawaachia wanawe malezi anapowatoroka na mumewe
      • Watoto wanaingizwa bishara haramu - Sauna na Bi. Knagara 
      • Watoto wanatishiwa na watuw wakubwa - Dick anatishiwa na Buda.
      • Watoto wanaozaliwa kutupwa - kitoto kilichookotwa na Neema
      • Watoto kuuwawa bila hatia - Lemi kusingiziwa wizi.
      • Watoto kubakwa - Lemi na Mwanaheri  (zozote 6  1 x 1)
        Kadiria majibu mengine ya mtahiniwa
  8. USHAIRI
    1. Makini/Mhitaji - ubet 7, msh. 3                    (1 x 2)
    2.  
      • Lina beti nane 
      • Kila beti una mishororo 4
      • Kila mshororo umegwawa viapnde viwili
      • Kila pande kina mziani 8
      • Shairi lina kibwagizo                  ( zozote 4 x 1 = 4)
    3.  
      1. Kuboronya sarufi/kubananga - mfano, madeni wakalipa, naondoka wangu moyo n.k
      2. Inkisari - sura za mefufua
      3. Vikule - mtima          (zozote 2 x 1)
      • Swali la balagha - Kwa nini wanikimbia?
      • Tashbihi - Sinilipue ja bomu
      • Tashhisi/uhuishi - Fuusi wacha uchoyo     (zozote 3 x1)

    4.  
      • Tarbia - mishororo minee katika kila ubeti
      • Ukaraguni - Vina tofauti kwa kila ubeti
      • Pindu - Mshororo wa mwisho ubeti wa nne, kiande cha mwisho kinatumiwa kaunzia mshororo wa kwanza ubeti wa tano
      • Sakarani - Lina bahari zaidi ya moja      (za kwanza 3 x 1)
    5. Toni ya kushawishi/kusihi   
      (ataje kuthibitisha)
    6. Wakwasi wanakutambua kwa sababu wameona uzuri wako. Umewangarisha na waatumia njia nyingi za kupata. Wanafurahia kutembea kila sehemu. Unapendeza roho na kufanikisha chochote. 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Lugari Constituency Joint Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?