Kiswahili Form 1 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

Kiswahili Form 1 End Term 2 Exams 2021 with Marking Schemes

 1. INSHA: (Alama 20)
  Andika barua ya kuomba nafasi ya kujiunga na shule ya upili baada ya kupita mtihani wa darasa la nane.
 2. UFAHAMU

  Soma taarifa ifuatayo halafu ujiu maswali

  UMOJA NA UTANGAMANO WA KITAIFA

  Taifa ni jamii ya watu wanaoishi pamoja na kuunganika kihistoria na kitamaduni chini ya serikali moja. Muunganiko huu hutokea kinasibu na watu kujikuta chini ya himaya moja. Umoja na utangamano katika taifa hutokana na mambo kadha wa kadha.

  Kwanza kabisa ni ushirikiano baina ya wanajamii wenyewe. Umoja wao huletwa na lugha wanayotumia. Hapa nchini Kenya Kiswahili kimechangia pakubwa katika kuleta utangamano. Luhga ya Kiswahili inazungumzwa kote nchini. Wananchi kutoka sehemu tofauti za nchi wanaweza kuwasiliana bila shida yoyote.

  Pili, utawala wa serikali ya kitaifa huleta utangamano wa jamii katika nchi. Huduma za serikali hutolewa kwa wote bila ya ubaguzi. Nchi inapokuwa chini ya kiongozi aliyechaguliwa na wananchi hufanikisha umoja.

  Jambo lingine ambalo huleta utangamano wa kitaifa, ni kuweko kwa sera inayoongoza maazimio na malengo ya taifa. Viongozi na wananchi wote hujitahidi kuchangia katika kuyafikia maazimio na malengo ya taifa lao.

  Utamaduni wa nchi nao ni muhimu katika kuleta umoja wa kitaifa. Mila, itikadi na kaida zenye manufaa na zinazokubalika na jamii hufanikisha kutambulisha taifa. Hivyo wananchi kupigania kwa jino na ukucha kuhifadhi utamaduni wao. Kwa mfano: sanaa za uigizaji na uimbaji nchini Kenya husaidia kutomelea umoja huu. Tamasha hizi ni chombo muhimu cha utangamano. Mfumo sawa wa elimu nchini ni njia nyingine ya kuimarisha umoja wa kitaifa.

  Wafanyibiashara wanaposafiri kutoka sehemu moja ya nchi hadi nyingine hutangamana na wananchi wenzao wanapouza au kununua bidhaa na huduma. Utangamano huo hukuza umoja wao.

  Maswali
  1. Eleza maana ya taifa. (al 2)
  2. Eleza umuhimu wa Kiswahili nchini Kenya. (al2)
  3. Taja mambo manne ambayo huleta umoja wa kitaifa. (al4)
  4. Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa kifungu hiki. (al 2)
   1. Utangamano……………………………………………….
   2. Utamaduni ………………………………………………..
 3. Matumizi ya lugha (al. 30)
  1. Taja sifa mbili mbili za sauti zifuatazo. (al. 4)
   1. /u/…………………………………………
   2. /e/……………………………………
  2. Taja sauti mbili mbili ambazo ni, (al. 6)
   1. Vipasuo……………………………
   2. Nazali…………………………………
   3. Vikwamizo…………………………
  3. Pambanua aina za maneno katika sentensi ifuatayo. (al. 21/2)
   Maharagwe yalivunwa na kutiwa ghalani.
  4. Panga maneno haya vizuri ili yaunde sentensi sahihi. (al. 2)
   Hodari Yule mwanamuziki nchi amezuru nyingi Afrika za.
  5. Tunga sentensi moja moja kubainisha maana ya maneno yafuatayo; (al.2)
   1. Paa
   2. Shuka
  6. Kanusha sentensi ifuatayo; (al. 2)
   Mwalimu anasahihisha kitabu cha mwanafunzi.
  7. Andika sentensi ifuatayo upya ukizigatia maagizo kwenye mambano. (al. 2)
   Mazingira yamehifadhiwa. (hali ya mazoea)
  8. Maneno yafuatayo hupatikana katika ngeli zipi? (al. 2)
   1. Manukato……………………………………
   2. Sukari…………………………………………
  9. Tofautisha sentensi hizi. (al. 4)
   1. Gari liliibwa
   2. Gari liliibiwa
  10. Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia vitenzi vilivyo katakia mambano.(al. 2)
   1. Suti hii ili ……………..na fundi wa kihindi. (shona)
   2. Yuko wapi Yule mgonjwa aliye………….. hapa? (leta)
  11. Eleza maana ya msamiati ufuatao wa ushairi. (al. 21/2)
   1. Ubeti
   2. Mizani
   3. Mshororo
   4. Ukwapi
   5. Dhamira
 4. ISIMU JAMII (al 10)
  1. Eleza maana ya;
   1. Isimu
   2. Jamii
   3. Isimu jamii
   4. Sajili
   5. Lafudhi
 5. FASIHI SIMULIZI. (al 10)
  1. Eleza maana ya fasihi. (al. 2)
  2. Toa sifa nne ili kutofautisha fasihi andishi na fasihi simulizi. (al. 8)

Mwongozo wa Kusahihisha

 1. INSHA
 2. UFAHAMU
  1. Taifa ni jamii ya watu wanaoishi pamoja na kuunganika kihistoria na kitamaduni chini ya serikali moja.
  2. Kiswahili kimechangia katika kuleta umoja na utangamano.
  3.  
   • lugha inayotumiwa na jamii
   • utawala wa serikali
   • sera inayoongoza maazimio na malengo ya taifa
   • utamaduni wa nchi
  4.  
   1. maingiliano, mahusiano
   2. mila, desturi, imani
 3. MATUMIZI YA LUGHA
  1.  
   1.  
    • Irabu ya nyuma kati
    • midomo huwa imevingirwa
   2.  
    • Irabu ya mbele kati
    • midomo hutandazwa
  2.   
   1. /P/, /b/, /t/, /d/, /k/, /g/
   2. /m/, /n/, /ny/, /ng'/
   3. /f/,/v/,/th/,/dh/
  3. maharagwe - nomino, yalivunwa - kitenzi, na - kihusishi, kutiwa - kitenzi, ghalani - kielezi cha mahali
  4. Yule mwanamuziki hodari amezuru nchi nyingi za Afrika.
  5.  
   1. paa - kwenda juu
    -mnyama - mbuzi mwitu
    -sehemu ya juu ya nyumba
   2. shuka -kuteremka kutoka juu
    -kitambaa cha kutandika kitandani
  6. Mwalimu hakusahihisha kitabu cha mwanafunzi
  7. Mazingira huhifadhiwa
  8.  
   1. ya - ya
   2. I - I
  9.  
   1. Gari lote limechukuliwa na mwizi.
   2. Sehemu ya gari imechukuliwa.
  10.  
   1. shonwa
   2. letwa
  11.  
   1. Ni aya au stanza ya shairi.
   2. Ni silabi/mapigo yanaounda maneno ya shairi
   3. Ni mstari wa shairi
   4. Kipande cha kwanza katika mshororo wa shairi
   5. lengo/kiini/kusudi/madhumuni ya kufanya jambo
 4. ISIMU JAMII (al 10)
  1.  
   1. Ni sayansi ya lugha/Ni taaluma inayochunguza lugha kisayansi
   2. Ni kundi la watu wanaoishi na kuendesha shughuli zao pamoja
   3. Ni matumizi ya lugha katika jamii/Ni taaluma inayochunguza uhusiano baina ya lugha na jamii
   4. Ni matumizi ya lugha katika muktadha fulani / Ni namna mbalimbali lugha inatumika katika muktadha ya jamii
   5. Ni upekee wa mtu kimatamshi kutokana na athari za lugha ya kwanza / Ni tofauti kimatamshi kwa wazungumzaji wa lugha moja.
 5. Fasihi Simulizi
  1. Ni sanaa inayotumia lugha kuchambua vipengele mbalimbali vya maisha ya binadamu.

  2. Fasihi Andishi Fasihi Simulizi 
   1. Ni mali ya mtu binafsi
   2. Inahifadhiwa vitabuni
   3. Si rahisi kubadilishwa
   4. Huwa na hadhira lengwa
   5. Hadhira yake ni tuli
   6. Hugharimu wakati na pesa
   7. Ubora wake hutegemea ujuzi wa mwandishi
   Ni mali ya jamii nzima
   Inahifadhiwa akilini
   Ni rahisi kubadilishwa
   Haina hadhira mahususi
   Hadhira yake ni tendi/hai
   haina gharama
   ubora wake hutegemea ujuzi wa fanani 

Download Kiswahili Form 1 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest