Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 2 Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

UFAHAMU ( ALAMA 15)

Rita na Evelyn walikuwa marafiki wa chanda na pete kwa muda mrefu. Waliishi katika mtaa wa Kibokoni jijini Mombasa. Evelyn alikuwa mwanafunzi wa masomo ya uhazili katika chuo kimoja pale mjini. Naye Rita alifanya kazi ya ukarani papo hapo mjini. Waliishi kidugu katika chumba kimoja walichopanga pale mtaani.

Ingawa marafiki hawa walishirikiana kwa kila njia katika shughuli za upishi, kupiga deki, kufagia, kufua na kazi nyinginezo za nyumbani, aliyekuwa akitoa msaada mkubwa zaidi alikuwa ni Rita. Rita alikuwa na mazoea ya kutunza pesa zake vyema. Aidha alijua maana ya haba na haba hujaza kibaba. Alijua kuwa Evelyn, kama mwanafunzi, hakuwa na uwezo wa kuyakidhi baadhi ya mahitaji yake. Alijitolea sabili hata kumnunulia Evelyn nguo, viatu na vim vingine alivyohitaji. Mara nyingine ilibidi Rita kulipa kodi ya nyumba peke yake kwa vile mwenzake hangeweza kupata pesa kwa wakati. Hakuwahi hata siku moja kumkera wala kumtesa Evelyn kwa jinsi yoyote ile. Fauka ya hayo, hakuwahi kumsemesha vibaya wala kuonyesha dharau kwake. Aliamini kama wanavyosema watu kuwa dunia rangi rangile, huenda siku moja atahitaji kusaidiwa yeye pia. Siku kama hiyo atamtegemea Evelyn, mwandani wake.

Evelyn alipomaliza masomo yake alikuwa na bahati ya mtende. Alipata kazi nzuri mara moja katika kampuni moja ya mafuta papo hapo jijini. Lakini muda si muda, mambo ya ajabu yalianza kutokea. Baada ya kupata kazi yenye kipato kizuri, kichwa cha Evelyn kilianza kufura mfano wa kaimati. Badala ya kumsaidia mwenzake katika kazi za pale nyumbani pamoja na gharama za maisha, alifuatilia raha za jijini kwa kuamini ule msemo wa ponda raha kufa kwaja. Rita alipomwuliza alimjibu kwa ukali, “Nikusaidie nini? Sasa si kama wakati nilipokuwa mwanafunzi. Kila mtu ana pesa zake.Ala!”

Rita hakumwelewa tena Evelyn. Isistoshe, alianza kumwibia Rita vitu vyake wakati alipokuwa hayupo nyumbani. Mara kwa mara Rita aligundua kuwa pesa alizokuwa ameficha sehemu fulani nyumbani zimedokolewa. Alipomwuliza, Evelyn alikuja juu, “Unafikiri mimi sina pesa? Unadhani ni wewe tu uliyeajiriwa?” Rita alizidi kushangaa, Muda wote alioishi na kumfadhili rafiki yake aliamini kuwa atamlipa mema. “Kumbe fadhila za punda ni mateke?” Alijiuliza Rita. Baada ya muda, urafiki wao ulivunjika na Evelyn akahamia mtaa wa Furaha alikoendelea na maisha yake ya starehe na ureda.

Hata hivyo mambo yalianza kumwendea mrama Evelyn. Wakubwa wake kazini hawakupendezwa na jinsi alivyoendesha shughuli zake pale ofisini. Mara nyingi alifika kazini akiwa amechelewa na kila wakati alitoa vijisababu mbalimbali ambavyo havikumridhisha yeyote. Aidha, alipokuwa ofisini hakufanya mengi isipokuwa kutembea kutoka ofisi hii hadi nyingine akiwasumbua watu kazini mwao. Mara kwa mara alionekana akisinzia wakati wenzake walipokuwa wakichapa kazi. Lakini lililowakera zaidi wakuu wa kampuni hiyo ya mafuta ni jambo fulani lililoanza kutendeka pale. Vitu vya watu vilianza kupoteapotea. Mara mfanyikazi huyu anapoteza saa yake, mara mwingine anapoteza pesa, mara hiki mara kile. Wakuu walipoyatupa mawazo yao nyuma wakagundua kuwa mambo haya yalianza kutendeka mara tu alipowasili Evelyn. Wakaamua kumwekea mtego. Evelyn alishikwa kimasomaso akidokoa mkoba wa msichana mwenzake. Mkoba huo ulikuwa umeachwa juu ya dawati kimakusudi ili kumvuta Evelyn. Evelyn alifutwa kazi papo hapo. Fauka ya hayo, alitiwa mikononi na kukabidhiwa polisi waliomtupa korokoroni. Kesho yake Evelyn alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la wizi. Alitozwa faini ya shilingi elfu tano au kifungo cha miezi sita. Hakuwa na pesa zozote za kulipia faini hii. Akawekwa rumande. Hata rafiki mmoja hakuwa naye wa kumuauni katika wakati huo wa majaribu.

Kwa bahati, Rita alisikia kuhusu kadhia hiyo.Hakupoteza muda. Akashika njia moja kwa moja hadi kituo cha polisi. Mpango ukafanywa na akamlipia Evelyn ile faini. Evelyn alipoachiliwa humo akashangaa. “Yaani nimesamehewa ama nini?”Aliuliza.“La. Hujasamehewa.Faini uliyotozwa imelipwa na msichana yule.” Evelyn akageuka na kumwona Rita. Alimtazama kwa muda bila kujua la kusema. Mwishowe alimsogea kisha wakakaribiana polepole na kukumbatiana. Machozi yakaanza kumdondoka Evelyn, nde! Nde! Nde! Akalia kilio cha uchungu na soni. Akamwomba Rita msamaha, “Nisamehe, sikujua nililokuwa nikifanya. Nilidhani kuwa baada ya kupata kazi sitahitaji tena urafiki wako. Haya yaliyonipata yamenifunza,” alisema kwa masikitiko. “Evelyn, kijengacho mtu ni utu na tabia,” alisema Rita.“Ni kweli rafiki yangu” alitamka Evelyn, Sasa nimejitia kwenye shida.Hata kazi yangu nzuri nimeipoteza.Sina mahali pa kuishi. Itabidi nirudi kijijini kwa baba na mama. Kwaheri rafiki yangu naasante kwa yote uliyofanya.”“La!
Hutaondoka”. Rita alimwambia kwa dhati, “Tutakwenda nawe nyumbani mwangu tukaishi pamoja kama zamani. Nitayagharamia mahitaji yako yote hadi utakapopata kazi”.
Basi Rita na Evelyn wakaungana tena na kuishi vizuri katika nyumba ile ile mtaani Kibokoni. Kweli akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.

MASWALI:

 1. Maisha ya Evelyn na Rita yalikuwaje kabla ya Evelyn kupata kazi? (alama 2)
 2. Kutokana na jinsi Rita alivyomtunza Evelyn, unafikiri yeye alikuwa ni mtu wa ama gani? (alama 2)
 3. Eleza baadhi ya mambo ambayo Rita alimtendea mwenzake. (alama 2)
 4. Baada ya kupata kazi Evelyn alikuwa mtu mkarimu. Je, unakubali?Eleza ilivyokuwa. (alama 2)
 5. Evelyn alipokuwa mwanafunzi hakuwa na tabia ya udokozi. Unafikiri ni kwa nini alianza tabia hiyo baada ya kuajiriwa? (alama 2)
 6. ‘Asiyefunza na mama hufunzwa na ulimwengu.’ Methali hii inahusianaje na Evelyn? (alama 1)
 7. ‘Akufaaye kiwa dhiki ndiye rafiki.’ Methali hii inahusianaje na Rita? (alama 1)
 8. Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika kwenye kifungu: (alama 3)
  1. marafiki wa chanda na pete
  2. enda mrama
  3. jitolea sabili

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA ( ALAMA 35)

 1. Pambanua sauti hizi kama ni ghuna au sighuna. (al 2)
  1. /t/
  2. /g/
 2. Kamilisha methali zifuatazo; (al 2)
  1. Mgaagaa na upwa ____________________________________________
  2. Mvumilivu________________________________________________________
 3. Andika visawe vya ; (al 2)
  1. Janibu
  2. Jadi
 4. Tunga sentensi zenye maneno yafuatayo; (al 3)
  1. N + V + T
  2. N + V + T + E
  3. I + N + T
 5. Onyesha viambishi awali na tamati katika sentensi hizi; (al 2)
  1. Alimkaribisha
  2. Umeogelea
 6. Onyesha matumizi manne ya koma. (al 4)
 7. Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani? (al 3)
  1. Mchungwa
  2. Mdudu
  3. Bonde
 8. Andika sentensi zifuatazo katika umoja. (al 3)
  1. Nyavu zimechanikachanika
  2. Nyuzi ziliingia matata
  3. Fito zilikatwakatwa
 9. Andika wingi wa; (al 3)
  1. Kiganja
  2. Cheo
  3. Kibindo
 10. Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika wakati ujao. (al 2)
  1. Mimi ninapenda mtoto mtiifu.
  2. Ninyi mnapendwa na wenzenu.
 11. Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali timilifu. (al 2)
  1. Safari hii itakuwa ndefu
  2. Shamba letu linalimwa
 12. Tunga sentensi ukitumia vitenzi hivi katika hali ya kutendewa. (al 2)
  1. Kata
  2. Pasua
 13. Eleza maana ya kirai. (al 1)
 14. Onyesha kundi Nomino na kikundi tenzi katika sentensi hii. (al 2)
  Hatibu hupaswa kuifahamu lugha
 15. Tegua vitendawili vifuatavyo. (al 2)
  1. Kisima kidogo kimejaa changararwe
  2. Namsikia lakini simwoni

ISIMU JAMII (Al 10)

 1. Eleza maana ya sajili ya shuleni. (al 2)
 2. Taja sifa nane za sajili ya shuleni. (al 8)

FASIHI SIMULIZI AL 10 

 1. Fafanua maana ya ; (al 2)
  1. Fasihi andishi
  2. Fasihi simulizi
 2. Onyesha tofauti zilizopo kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi. (al 8)

Mwongozo wa Kusahihisha

 1. Maisha ya Evelyn na Rita yalikuwaje kabla ya Evelyn kupata kazi? (al. 2)
  • Walikua marafiki wa chanda na pet
  • Walishirikiana kwa kila njia
 2. Kutokana na jinsi Rita alivyomtunza Evelyn, unafikiri yeye alikuwa ni mtu wa aina gani? (al. 2)
  • Alikuwa mwenye ukarimu
  • Alijawa na wema
  • Alikuwa na mapenzi ya dhati
 3. Eleza baadhi ya mambo ambayo Rita alimtendea mwenzake. (al. 2)
  • Alimnunulia mahitaji kama nguo na viatu
  • Alilipa kodi kwa nia baya Evelyn
  • Alimlipia faini alipokua kizuizini
 4. Baada ya kupata kazi Evelyn alikuwa mtu mkarimu. Je, unakubali?Eleza ilivyokuwa. (al. 2)
  • La. Evelyn alifuatilia raha za jijini na kukosa kumsaidia Rita katika kazi na gharama za maisha
 5. Evelyn alipokuwa mwanafunzi hakuwa na tabia ya udokozi. Unafikiri ni kwanini alianza tabia hiyo baada ya kuajiriwa? (al. 2)
  • Aliona kuwa alikuwa na pesa zake na angeweza kujikimu mwenyewe
  • Alidhani kuwa tayari alikuwa mtu mzima na hivyo hakuhitaji kuelekezw
 6. 'Asiyefunza na mama hufunzwa na ulimwengu.’ Methali hii inahusianaje na Evelyn? (al. 1)
  • Evelyn alikataa kumskiza Rita na baadaye akatenda kosa lililomtia korokoroni
 7. 'Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.’ Methali hii inahusiana aje na Rita? (al. 1)
  • Rita alimsadia rafikiye Evelyn alipokuwa mwanafunzi na hata baadaye alipokuwa korokoroni
 8. Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika kwenye kifungu: (al. 3)
  1. marafiki wa chanda na pete
   • Marafiki wasioachana kwa vyovyote vile
  2. enda mrama
   • Kuharibika
  3. jitolea sabili
   • Kuamua kikamilifu

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA

 1. Pambanua sauti hizi kama ni ghuna au sighuna. (al 2)
  1. /t/ - Sighuna
  2. /g/ - Ghuna
 2. Kamilisha methali zifuatazo; (al 2)
  1. Mgaagaa na upwa – Hali wali mkavu
  2. Mvumilivu - Hula mbivu
 3. Andika visawe vya ; (al 2)
  1. Janibu – Kipokeo, Mkarara, Kiitikio
  2. Jadi – Kale / zamani
 4. Tunga sentensi zenye maneno yafuatayo; (al 3)
  1. N + V + T
   • Watoto wawili wanatembea
  2. N + V + T + E
   • Mwalimu mrefu anaandika vizuri
  3. I + N + T
   • Lo! Juma amekuja
 5. Onyesha viambishi awali na tamati katika sentensi hizi; (al 2)
  1. Alimkaribisha
   • Awali – A – me – m Tamati – I - a
  2. Umeogelea
   • Awali – Tu – li Tamati - a
 6. Onyesha matumizi manne ya koma. (al 4)
  • Kuonyesha mambo yaliyo katika orodha
  • Kuandika tarehe Mei 2, 2008
  • Kuonyesha pumziko fupi katika sentensi iliyo ndefu
  • Kuandika anwani
  • Kutenga tarakimu za kiasi kikubwa 1,000,000
  • Kuonyesha maneno halisi yanayofuata
  • Katika nukuu. Akasema, “ Yule kondoo ni wangu”
 7. Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani? (al 3)
  • Mchungwa – U - I
  • Mdudu – A - WA
  • Bonde – Li - YA
 8. Andika sentensi zifuatazo katika umoja. (al 3)
  1. Nyavu zimechanikachanika
   • Wavu umechanikachanika
  2. Nyuzi ziliingia matata
   • Uzi umaingia utata
  3. Fito zilikatwakatwa
   • Ufito ullikatwakatwa
 9. Andika wingi wa; (al 3)
  • Kiganja - Viganja
  • Cheo - Vyeo
  • Kibindo - Vibindo
 10. Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika wakati ujao. (al 2)
  1. Mimi ninapenda mtoto mtiifu.
   • Mimi nitapenda mtoto mtiifu
  2. Ninyi mnapendwa na wenzenu.
   • Ninyi mtapendwa na wenzenu
 11. Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali timilifu. (al 2)
  1. Safari hii itakuwa ndefu
   • Safari hii imekuwa ndefu
  2. Shamba letu linalimwa
   • Shamba letu limelimwa
 12. Tunga sentensi ukitumia vitenzi hivi katika hali ya kutendewa. (al 2)
  1. Kata – Mti ulikatwa jana
  2. Pasua – Alipasuliwa mbao
 13. Eleza maana ya kirai. (al 1)
  • Ni fungu la maneno ambalo halijakamilika kimaana
 14. Onyesha kundi Nomino na kikundi tenzi katika sentensi hii. (al 2)
  Hatibu hupaswa kuifahamu lugha
  • KN – Hatibu
  • KT – Hupaswa kuifahamu lugha
 15. Tegua vitendawili vifuatavyo. (al 2)
  1. Kisima kidogo kimejaa changararwe
   • Kinywa na meno
  2. Namsikia lakini simwoni
   • Upepo

ISIMU JAMII (Al 10)

 1. Eleza maana ya sajili ya shuleni. (al 2)
  • Haya ni matumizi ya lugha katika muktadha wa shuleni.
 2. Taja sifa nane za sajili ya shuleni. (al 8)
  • Sentensi ndefu – (atoe mifano katika hoja zote.)
  • Huwa na mwanzilishi mkuu.
  • Misamiati ya taaluma mbalimbali.
  • kurejelea mawazo ya wengine.
  • Lugha ya heshima/adabu.
  • Kuna urasmi wa lugha
  • Lugha iliyo na mbinu au taratibu maalum

FASIHI SIMULIZI AL 10

 1. Fafanua maana ya ; (al 2)
  1. Fasihi andishi
   • Fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi.
  2. Fasihi simulizi
   • Fasihi inayowasilishwa kwa njia ya mdomo.
 2. Onyesha tofauti zilizopo kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi. (al 8)
  • Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
  • Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishi.
  • Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi.
  • Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa.
  • Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi.
  • Uwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara, nyimbo, makofi, kuimba, kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi hauandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhira.
  • Fasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe mbele ya hadhira.
  • Fasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani, arusini, n.k ilhali fasihi andishi haina mahali maalum.
  • Fasihi simulizi huandamana na shughuli fulani ya kitamaduni ilhali fasihi andishi haiandamani na shughuli ya kitamaduni.
  • Fasihi andishi huhitaji muda kutunga ilhali baadhi ya fasihi simulizi huzuka papo hapo k.m. semi, maigambo.
  • Fasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadilishwa na fanani anapowasilisha ufaraguzi) bali fasihi andishi haibadiliki isipokuwa mwandishi aiandike upya.
  • Fasihi simulizi ina historia ndefu kuliko fasihi andishi kwa kuwepo tangu mwanzo wa maisha ya binadamu
  • Fasihi simulizi huwasilishwa wakati maalum k.v. usiku, kipindi fulani cha mwaka ilhali andishi haina wakati maalum.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 2 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest