Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 3 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote katika karatasi hi.
  • Andika majibu yako kwa lugha ya Kiswahili.

Kwa matumizi ya mtahini pekee

 Swali  Upeo   Alama 
 1. Insha  20  
 2. Ufahamu  15  
 3. Matumizi ya Lugha  35  
 4. Isimu Jamii  10  
 5. Ushairi  10  
 6. Fasihi Simulizi  10  
 Jumla    

 

  1. INSHA (Alama 20)
    Andika kisa kitakachothibitisha ukweli wa methali.
    “Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.”
  2. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Soma kifungu kisha ujibu maswali yanayofuata


    Lugha inaweza kuelezwa kwa jumla kuwa ni mfumo wa mawasiliano. Haiyamkiniki kwa mtu yeyote kueleza chanzo au kiini cha lugha na sote tunakubaliana kuwa matumizi yake yameanza tangu kuumbwa kwa binadamu kwani ni vigumu kukisia kuwepo kwa jamii ya watu bila lugha ya mawasiliano yoyote ile.

    Katika taifa lolote, huwapo na lugha moja au hata zaidi ya moja ambayo huwa ndicho chombo cha mawasiliano ya taifa katika nyaja za: elimu, maandishi, siasa na biashara. Kwa mfano, mataifa kama Kanada hutumia lugha mbili kwa usawa kama lugha za taifa na za kikazi. Maana ya lugha ya taifa ni lugha moja ambayo huteuliwa kutumika katika shughuli zote za taifa hasa katika nchi yenye lugha nyingi za kikabila. Lugha ya taifa ni muhimu sana kwa maisha na maendeleo ya taifa lolote lile. Lugha hii huwa ndiyo kiungo cha kueneza umoja na uelewano miongoni mwa jamii nyingi tofauti na huwa kama kitambulisho kwao kuwa wao ni ndugu wa jamii moja kubwa, yaani taifa lao.

    Kenya ni mfano mzuri wa taifa lenye lugha nyingi zinazozidi arobaini za vikundi vidogo vidogo vya kikabila. Hapo kabla ya miaka mia moja hivi iliyopita kila kimojawapo cha kikundi hivi kilijitambulisha kama kabila huru. Baada ya kuja kwa Serikali ya Kikoloni na hasa baada ya Kenya kujinyakulia uhuru, haja ya kuunganisha raia wote chini ya taifa moja lenye uongozi na shabaha moja ilikuwa ndilo jambo lililozingatiwa sana. Kwa itikadi tofauti. Utamaduni humaanisha jumla ya amali na tabia za watu wa jamii fulani. Amali hizi kujiimarisha, taifa huhitaji chombo hicho kuwasiliana na kuwaunganisha watu wake wenye asili mbalimbali. Chombo hicho huwa ni lugha ambayo siyo tu kwamba ni sehemu ya utamaduni ya jamii bali pia ni njia muhimu sana ya kutawanyia na kustawishia ule utamaduni.

    Katika taifa lenye lugha nyingi kama Kenya kwa mfano, lugha ya taifa inayozungumzwa na kueleweka na idadi kubwa ya raia ambayo imekiuka mipaka na tofauti za kikabila ni njia muhimu sana ya kuenezea maongozi ya taifa na kuleta ufahamikiano bora kote nchini. Kama zilivyo taasisi kama wimbo wa taifa, bendera ya taifa au bunge la taifa, ;lugha ya taifa ndicho kielelezo cha taifa lolote lile lililo huru. Lugha kama hiyo huvunja na kukomesha hisia za kibinafsi na kikabila na badala yake kuunda moyo wa uaminifu wa kitaifa.

    Zaidi ya kuwa chombo cha mawasiliano, lugha ni kielelezo cha fikira na hisia za binadamu. Lugha ya watu fulani haituelezi tu ujuzi au maarifa yao bali mtazamo wao wa kimaisha, falsafa na mawazo yao. Kwao ufupi lugha hutufahamisha namna akili za watu waizungumzayo ile lugha zinavyofikiri na kufanya maazimio. Lugha ni sehemu ya utamaduni wa taifa tulimozaliwa na lazima lugha hiyo ifunzwe katika muktadha wa maisha ya jamii ihusikayo. Utamaduni wa jamii hautenganiki na lugha yake.

    MASWALI
    1. Lugha ni nini kwa mujibu wa kifungu hiki? (alama 2)
    2. Ni kwa nini lugha ya taifa ni muhimu kwa nchi? (alama 4)
    3. Taifa la Kenya lina utamaduni uliochanganyika. Thibitisha. (alama 2)
    4. Lugha haiwezi kutenganishwa na utamaduni. Fafanua kauli hii kulingana na kifungu hiki. (alama 2)
    5. Tambua vielelezo vingine vinavyotambulisha taifa huru mbali na lugha ya taifa. (alama 3)
    6. Eleza maana ya maneno haya kulingana na taarifa hii. (alama 2)
      1. itikadi
      2. muktadha
  3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA      (Alama 35)
    1. Eleza sifa mbili za sauti /i/     (Alama 2)
    2. Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo.             (Alama 2)
      1. abudu
      2. tibu
    3. Andika wingi wa sentensi hii. (Alama 2)
      Umekwisha kumtembelea mgonjwa mwingine hospitalini?
    4. Yakinisha sentensi ifuatayo. (Alama 2)
      Hajaja kumsalimia nyanya yake.
    5. Onyesha mofimu katika neno hili. (Alama 3)
      Tuliwapikisha
    6. Andika sentensi hizi katika minyambuliko iliyo mabanoni. (Alama 2)
      1. Mama alimfanya mtoto ale (Kutendesha)
      2. Julia alifagia chumba vizuri (Kutendewa)
    7. Sentensi zifuatazo ni za aina gani? (Alama 2)
      1. Washindi wamefika uwanjani ili wapewe zawadi.
      2. Sakafu ile inateleza sana.
    8. Geuza sentensi ifuatayo katika usemi halisi. (Alama 2)
      Meja alishauriwa na Kasisi aache tabia ya ulevi.
    9. Nomino zifuatazo zimo katika ngeli gani? ( Alama 2)
      1. Marashi
      2. Chai
    10. Ghasia ni kwa fujo ilhali ndwele ni kwa …..  (Alama 2)
    11. Changanua sentensi ifuatayo kwa mstari. (Alama 4)
      Mtoto aliharibu kanda yangu.
    12. Andika kwa ukubwa. (Alama 2)
      Mwizi aliyekamatwa atafikishwa mahakamani kesho.
    13. Tunga sentensi ukitumia viakifishi vifuatavyo. (Alama 2)
      1. Vifungo
      2. Mkwaju
    14. Sahihisha sentensi hii. (Alama 2)
      Chakula tulizokula zilitushibisha.
    15. Eleza maana mbili za sentensi:
      Tumetengeneza barabara. (Alama 2)
    16. Onyesha tofauti kati ya vitate hivi: (Alama 2)
      1. Mzazi
      2. Msasi
    17. Weka shadda katika neno mtu. (Alama 1)
  4. ISIMUJAMII (ALAMA 10) 
    A:  Niaje bazenga?
    B:  Niko poa Timo.
    A:  Form ni gani?
    B:  Labda nicome kesho majioni. Leo niko busy siwezi patikana.

    Maswali
    1. Hii ni sajili gani? (alama 2)
    2. Toa sifa za sajili hii. (alama 8
  5. USHAIRI
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

    Daima alfajiri na mapema
    Hunipitia na jembe na kotama
    Katika njia iendayo kondeni
    Kama walivyofanya babuze zamani
    Nimuonapo huwa anatabasamu
    Kama mtu aliye na kubwa hamu
    Kushika mpini na kutokwa jasho
    Ili kujikimu kupata malisho.

    Anapotembea anasikiliza
    Videge vya anga vinatumbuiza
    Utadhani huwa vimemngojea
    Pia pepo baridi kumpepea
    Rihi ya maua zikimletea
    Nao umande kumbusu miguu
    Na miti yote hujipinda migongo
    Na yeye kuendelea kwa furaha
    Kuliko yeyote ninayemjua
    Akichekelea ha ha ha ha……….

    Na mimi hubaki kujiuliza
    Kuna siri gani inayomliwaza?
    Au ni kujua au kutojua?
    Furaha ya mtu ni furaha gani
    Katika dunia inayomhini ?
    Ukali wa jua wamnyima zao
    Soko la dunia lamkaba koo
    Dini za kudhani zamsonga roho
    Kuna jambo gani linamridhisha ?
    Kama si kujua ni kutojua
    Laiti angalijua, laiti angalijua!

    Maswali
    1. Hili ni shairi la aina gani ? (al.1)
    2. Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili. (al 4)
    3. Kwa kutoa mifano mwafaka taja aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumika (al.2)
    4. Toa mfano wa tamathali za usemi zifuatazo (al.2)
      1. Tashbihi
      2. Tashihisi
    5. Nani anayezungumziwa katika shairi hili ? (al.1)
  6. FASIHI SIMULIZI (ALAMA 10)
    1. Taja vipera viwili vya maigizo. (alama 2)
    2. Andika sifa tatu za michezo ya watoto. (alama 3)
    3. Eleza maana ya nyimbo zifuatazo. (alama 2)
      1. Wawe
      2. Kimai
    4. Taja majukumu matatu ya bembelezi. (alama 3)

MARKING SCHEME

  1. INSHA
    Mgaagaa na upwa hali wali mkavu

    Mwanafunzi aandike kisa kinachotoa maana kuwa anayefanya juhudi za kazi katika kutafuta mali hakosi kufanikiwa.
    • Mgaaga- Juhudi za kazi
    • na -Bidii
    • upwa- Kung’ang’ana
    • hali- mafanikio
    • wali- mavuno
    • mkavu- ufanisi
      Anayeandika kisa ambacho hakioani na methali atakuwa amepotoka.
  2. UFAHAMU
    1.  
      1. Lugha ni mfumo wa mawasiliano
      2. Ni kielezo cha fikira na hisia za binadamu.   (alama 2)
    2.  
      1. Kwa maisha na maendeleo ya taifa.
      2. Ndiyo kiungo cha kuenezea umoja na uelewano miongoni mwa jamii nyingi tofauti.
      3. Huwa kama kitambulisho kuwa wanajami huska ni ndugu wa jamii moja kubwa.
      4. Ni njia muhimu ya kueneza maongozi ya taifa na kuleta ufahamikiano bora kote nchini.   (alama 4)
    3. Utamaduni wa Kenya ni mchanganyiko wa tamaduni za watu wengi wenye mila, desturi, imani na itikadi tofauti.  (alama 2)
    4.  
      1. Lugha ni sehemu ya utamaduni
      2. Lugha ni njia muhimu ya kutawanyia na kustawishia utamaduni ule.   (alama 2)
    5.  
      1. Wimbo wa taifa
      2. Bendera ya taifa
      3. Bunge la taif                     (alama 3)
    6.  
      1. itikadi-imani
      2. muktadha- mazingira        (alama 2)
  3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
    1. Sifa za /i/ :
      • Ni ya juu
      • Ni ya mbele
      • Mdomo umetandaza    (alama 2)
    2.  
      1. abudu- ibada, maabadi, mwabudu
      2. tibu- tabibu, matibabu, utabibu    (alama 2)
    3. Mmekwisha kuwa tembelea wagonjwa wengine mahospitalini?  (alama 2)
    4. Amekuja kumsalima nyanya yake    (alama 2)
    5.  
      • Tu-li-wa-pik-ish-a
      • Tu- nafsi ya kwanza
      • li- wakati uliopita
      • wa- kitendwa
      • pik-mzizi
      • ish- kauli ya mnyambuliko
      • a- kiishio           (alama 3)
    6.  
      1. Mama alimlisha mtoto.
      2. Chumba kilifagiliwa vizuri na Julia.   (alama 2)
    7.  
      1. Sentensi ambatano
      2. Sentensi sahihi      (alama 2)
    8. “Acha tabia ya ulevi, ” Kasisi alimshauri Meja.   (alama 2)
    9.  
      1. Marashi- YA-YA
      2. Chai- I-I     (alama 2)
    10. ndwele ni kwa ugonjwa/maradhi      (alama 1)
    11. Mtoto aliharibu kanda yangu.
      S → KN + KT
      KN → N
      N → Mtoto
      KT  → T + N + V
      T → aliharibu
      N → kanda
      V → yangu
    12. Jizi lililokamatwa litafikishwa mahakamani kesho.   (Alama 2)
    13.  
      1. Vifungo/mabano-kufungia maneno yatoayo maelezo zaidi kuhusu maneno yanayotangulia.
        • Kubainisha nambari au herufi katika orodha.
        • Kutoa maelezo ya maelekezo katika mchezo wa kuigiza.
      2. Mshazari/mkwaju- kuonyesha nambari ya kumbukumbu.
        • Badala ya kiunganishi
        • Kutenga tarehe
        • Kuonyesha maneno yaliyotumika yana maana sawa.
        • Katika anwani ya mdahalishi.   (Alama 2)
    14. Chakula tulichokula kilitushibisha.    (Alama 2)
    15.  
      1. Tumetengeneza baraste/njia kuu
      2. Tumetengeneza vizuri    (alama 2)
    16.  
      1. mzazi-mama au baba wa mtu.
      2. Msasi-mwindaji     (alama 2)
    17. ‘mtu      (Alama 1)
  4. ISIMUJAMII (ALAMA 10)
    1.  
      1. Sajili ya mtaani
      2. Lugha ya vijana wa mjini    (1x2=2)
    2.  
      1. Imejaa maneno ya lakabu k.m bazenga
      2. Lugha isiyo sanifu k.m. majioni
      3. Huwa inachukuwa mwelekeo wa mkato k.m Timo
      4. Mada hutegemea kile kinachozungumziwa.
      5. Huwa yenye ucheshi mwingi.
      6. Kuchanganya ndimi k.m. nicome
      7. Sentensi fupi fupi.
      8. Kuna kukatizana kauli.     (8x1=8)
  5. SHAIRI
    1. Shairi huru. (Alama 1)
    2.  
      1. Mwenye matumaini/hamu kubwa.
      2. Mwenye bidii-huamka alfajiri na mapema
      3. anayafurahia mandhari- anapotembea anasikiliza ndege
      4. Mtulivu-kuna siri gani inayomliwaza?
      5. Anayedhulumiwa-soko la dunia la mkaba koo
      6. anayeridhika-kuna jambo gani linalomridhisha/halalamiki     (zozote 4x1=4)
    3.  
      1. Inkisari k.m babuze badala ya babu zake.
      2. Kuboronga sarufi-kubwa hamu badala ya hamu kubwa.   (Alama 2)
    4. Mfano ya tamathali za usemi. (Alama 2)
      1. Tashbihi- Kama mtu aliye na kubwa hamu
      2. Tashihisi
        • umande kumbusu
        • mti kumpapasa
        • upepo kumpepea    (2x1=2)
    5. Nafsi nenewa
      • mkulima
      • kibarua
      • mkata        (1x1=1)
  6. FASIHI SIMULIZI
    1.  
      1. Michezo ya jukwaani
      2. Vichekesho
      3. Najigambo/vivugo
      4. Michezo ya watoto
      5. Ngonjera
      6. Ngoma
      7. Miviga     (zozote 2x1=2)
    2.  
      1. Huigizwa na watoto
      2. Kila jamii ina michezo mahususi inayooana na shughuli za jamii hiyo.
      3. Maudhui ya michezo ya watoto hufungamana na shughuli za kitamaduni za jamii zao.
      4. Huhusisha pia nyimbo za watoto
      5. Huwa na miondoko mingi kama vile mwajificho.     (zozote 3x1=3)
    3.  
      1. Wawe-nyimbo za kilimo
      2. Kimai- nyimbo za uvuvi au shughuli za majini.     (zozote 2x1=2)
    4.  
      1. Kutumbuiza na kuongoa mtoto
      2. Kumsifu mtoto ambaye ni mtulivu.
      3. Huwasiri mfumo wa kiuchumi wa jamii husika.
      4. Huwasiri mahusiano katika jamii.
      5. Hutakasa hisia za mwimbaji.
      6. Humwelimisha mtoto
      7. Huwasiri mtazamo wa jamii kuhusu jinsia na matarajio ya jamii kwa jinsia fulani.
      8. Huwaonya watoto dhidi ya tabia hasi.      (zozote 2x1=2)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 3 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest