Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Mid Term 2 2022

Share via Whatsapp

Maswali

UFAHAMU

 1. Soma taarifa kisha ujibu maswali yanayofuata. (alama 15)
  WENYE MATATU WASIRUHUSIWE KUPUNJA ABIRIA

                Taarifa zinazotolewa na makundi mbalimbalu ya matatu zaonyesha waziwazi hasira na dhiki za watu ambao wamerudi kutoka vitani wakiwa hoi baada ya kushindwa vibaya huku wakitafakari maafa na madhara yaliyowapata.
                Kama sivyo, basi ni kwa nini Chama cha Wenye Matatu (MOA) na Chama cha Maslahi ya Matatu (MWA) vinatisha Serikali na wananchi kwamba vitaongeza nauli kufidia hasara ambazo wanadai wamepata?
                Ndivyo, MOA na MWA vinateta kwamba imegharimu pesa nyingi kuweka mikanda ya usalama na vifaa vya kudhibiti mwendo katika matatu zao. Hivyo? Ni lazima wananchi wanyolewe wembe mkavu hadi warudishe pesa hizo.
                Hiyo si biashara. Ni upunjaji. Biashara inataka wepevu na busara na ndivyo maana serikali imefanya kuonya kwamba haitaruhusu nauli kuongezwa shaghala baghala bila kuzisimamia yenyewe.
                Ingawa matatu ni sehemu muhimu ya maisha, MOA na MWA havipasi kujidanganya kwamba wakenya hawawezi kuishi bila matatu. Sheria zikifuatwa, si tu na matatu, lakini pia wananchi, itagunduliwa kuwa matatu 40,000 zilizopo nchini hata bado hazitoshi. Matatu ambazo zinahudimia wananchi kwa heshima na staha hazihitaji kuongeza nauli kupata faida.
                Wananchi wengi wamevutiwa sana na matatu hizo kwa sababu wahudumu wa matatu hizo huwajali na kuwadhamini. Hii ndiyo maana wako tayari kuzingojea katika foleni ndefu, hata mvua ikinyesha jinsi gani, kwa sababu wanataka wasafiri raha mustarehe, kwa fahari na usalama. Pesa si hoja.
                Lakini vyama vya MOA na MWA vitapata kwamba ni shida kutekeleza nauli zao vinavyotisha kulipisha washa wasafiri kwa sababu vimelazimishwa kutii sheria. Je, vimefikiria mabilioni ya pesa ambazo hupotezwa kutokana na ajali ? Je, maisha ya wananchi ?
                Hivyo ikiwa MOA na MWA vinataka kuongeza nauli mwezi ujao viheshimu kwanza wananchi. Vitisho havitasaidia katika enzi za sasa. Ni afadhali maafisa wao waache kujidanganya tena.
                Kwa vyovyote vile, mradi tu kuna nidhamu na utaratibu wa sasa, magari mapya ya abiria yatamwagwa kwa wingi barabarani. MOA na MWA vihitaji wekevu zaidi na busara kushindana na matatu mpya na mabasi. Zipo tayari ?

  Maswali
  1.  Ipe taarifa hii anwani mwafaka. (al 2)
  2. Wenye matatu wanatishia kufanya nini? Kwa nini? (al 3)
  3. Ni nini hasa ndiyo malalamishi yao (MOA na MWA) (al 2)
  4. Serikali inafanya nini kuzima vitisho hivi? (al 2)
  5. Kwa nini wananchi wamevutiwa na matatu? (al 2)
  6. Ajali imesababisha hasara gani? (al 2)
  7. Mwandishi anatoa ushauri gani kwa jumla? (al 3)
 2. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 25)
  1. Toa mifano miwili ya vikwamizo vya ufizi/ masine. (al 2)
  2. Je sauti hizi zinatofautianaje? (al 2)
   1. /l/ na /r/
   2. /i/ na /u/
  3. Andika umoja wa sauti hizi. (al 2)
   1. Mahandaki haya yamechimbwa na wanajeshi hawa mahiri.
   2. Walifuata nyayo zake wakapatamanufaa makubwa.
  4. Andika udogo wa sentensi hii. (al 2)
   madege haya yalikula majichwa ya majijusi.
  5. Tunga sentence zenye kutumia vivumishi vya pekee vyenye kuonyesha: (al 2)
   1. Bila kubakisha/ kwa jumla
   2. Umilikaji/ hali/ tabia
  6. Andika methali unayoafiki maelezo haya: (al 2)
   Mtu anaweza kufanya jambo ambalo linaweza kumuumiza mwenyewe.
  7. Andika kauli ya kufanywa ya sentensi ifuatayo: (al 2)
   baba alifukia shimo lililojaa maji taka.
  8. Tambua virai vilivyopigwa mstari katika sentensi ifuatayo: (al 2)
   Watoto wadogo waliongea katika mto uliojaa maji pomoni
         (i)                                            (ii)              (iii)
  9. Andika sentensi hii kwa kutumia ‘O’ rejeshi tamati. (al 2)
   tunda lililooza lilitupwa jaani mwa taka.
  10. Tunga sentensi yenye muundo huu: (al 2)
   N+V+V+T+E+E
  11. Tunga sentensi moja kwa kila jozi ya maneno kuonyesha tofauti yake : (al 2)
   1. Zaa na saa
   2. Shoka na choka
 3. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
  1. Fafanua sifa zozote tano za sajili ya dini.

Mwongozo wa Kusahihisha

 1. UFAHAMU
  Maswali
  1.  Ipe taarifa hii anwani mwafaka. (al 2)
   • Matatizo katika usafiri wa matatu
   • Dhiki za wanamatatu/ wenye matatu
   • Malalamishi ya wanamatatu/ MOA na MWA
  2. Wenye matatu wanatishia kufanya nini? Kwa nini? (al 2)
   •  Kuongeza nauli
   • Kwa kufidia hasara waliopata
  3. Ni nini hasa ndiyo malalamishi yao (MOA na MWA) (al 2)
   • Wanaleta kwamba imegarimu pesa nyingi kuweka mikanda ya usalama na vifaa vya kudhibiti mwendo.
  4. Serikali inafanya nini kuzima vitisho hivi? (al 2)
   • Inasema kuwa haitaruhusu nauli kuongezwa shaghalabaghala bila kuzisimamaia yenyewe.
  5. Kwa nini wananchi wamevutiwa na matatu? (al 2)
   • Wahudumu wao hawajali na kuwadhamini.
   • wanataka wao wasafiri raha mstarehe, kwa fahari na usalama.
  6. Ajali imesababisha hasara gani? (al 2)
   • kupoteza kwa mabilioni ya pesa.
   • kupoteza maisha
  7. Mwandishi anatoa ushauri gani kwa jumla? (al 3)
   • Kuwa MOA na MWA havipasi kujidanganya kwamba wakenya hawawezi kuishi bila matatu
   • Maafisa wao waache kujidanganya tena.
   • Biashara inataka wepevu na busara kushindana na matatu na mabasi.
   • MOA na
 2. MATUMIZI YA LUGHA
  1. /S/ an /z/
  2.      
   1. /l/ haikwaruzi ufizi ila sauti /r/ linakwaruza/ ufizi kwa haraka
   2. /sauti i/ linatamakwa kama mdomo imetandanzwa na kwa upande wa mbele wa ulimi ilhali sauti /u/ linatamkwa kwa kuviringa mdomo na kwa upande wa nyuma wa ulimi
  3.       
   1. handaki hili limechimwa na mwanajeshi huyu mahiri
   2. Alifuata wayo wake akapata manufaa makubwa
  4.  videge hivi vilikula vijichwa vya vijijusi
  5.    
   1. Mwanafunzi anapaswa kutunga sentensi akitumia -ote
   2. Mwanafunzi anapaswa kutunga sentensi akitumia -enyewe/ enye
  6. Mwanafunzi anapaswa kujibu na methali inayoamabatana na maagizo:|
   Mf; Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe
  7. Shimo lililojaa maji taka lilifukiwa  na baba
  8.     
   1. kirai nomino
   2. kirai kihusishi
   3. kirai kielezi
  9. tunda liozalo lilitupwa jaani mwa taka
  10.  Mwanafunzi anapaswa kutunga sentenzi iliyo na vivumishi viwili na vielezi viwili kulingana na maagizo  
  11. Mwanafunzi anapswa kutunga sentensi zinazoonyesha tofauti za maneno aliyopewa
 3.       
  1. Hutumia msamiati wa kidini kama vile
   • Bibilia
   • maombi
   • mbinguni
   • jehanamu
   • Madhabahu
   • Paradiso
   • Mbinguni
   • Mwenyezi Mungu
   • Mwokozi
  2. Ni lugha inayonukuu sana hasa wazungumzaji wanaporejelea Kitabu kitakatifu
  3. Lugha yenye heshima, upole na unyenyekevu
  4. Lugha sanifu
  5. Ni lugha iliyojaa ahadi nyingi kwa wanaoandamana na mafunzo ya kidini na vitisho kwa wanaoenda kinyume na mafundisho
  6. Huwa imejaa matumaini
  7. Ni lugha yenye kutoa maneno ya sifa, kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Mid Term 2 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest