Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Mid Term 2 Exams 2023

Share via Whatsapp
Instructions
  • Fanya maswali yote
  1. Soma shairi hili kisha ujibu maswali.(alama 20)

    Nitampa nani, sauti yangu ya dhati, 
    Kwa kipimo gani, ingawa kiwe katiti, 
    Amefanya nini, la kuleta umati, 
               Kipimo ni kipi?

    Yupi wa maani, asosita katikati, 
    Alo na maoni, yasojua gatigati,
    Atazame chini, kwa kila ule wakati, 
                Kipimo ni kipi? 

    Alo mazalendo, atambuaye shuruti
    Asiye mafundo, asojua mangiriti 
    Anoshika pendo, hata katika mauti, 
                Kipimo ni kipi?

    Kipimo ni kipi? Changu mimi kudhibiti,
    Utu uko wapi, ni wapi unapoketi,
    Nje kwa Mkwapi, au ndani kwa Buheti, 
               Kipimo ni kipi?

    Maswali
    1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka.(alama 1)
    2. Eleza bahari nne za shairi hili. (alama 4)
    3. Taja tamathali moja ya usemi na kisha utoe mfano wake kutoka kwa shairi.(alama 1)
    4. Mshairi ana uhuru wa uandishi anapotunga shairi. Taja na ueleze mifano yoyote miwili ya matumizi ya uhuru huo kisha utolee mifano kabambe. (alama 4)
    5. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
    6. Eleza muundo/umbo la shairi hili.(alama 4)
    7. Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika ushairi. (alama 2)
      1. Katiti _________________________________________________
      2. Gatigati __________________________________________________
  2. MATUMIZI YA LUGHA.
    1. Andika tofauti moja kati ya sauti zifuatazo. (alama 2)
      1. /v/ na /f/
      2. /r/ na /l/
    2. Bainisha silabi katika neno:   (alama3)
      Sikumpiga.
    3. Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo.(alama 2)
      Mtoto alishonewa nguo na mama yake vizuri sana.
    4. Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo.(alama 2)
      Ingawa mshahara wake si mkubwa anaikimu familia yake.
    5. Eleza maana ya shadda.(alama 1)
    6. Onyesha panapotokea shadda katika neno:    (alama 1)
      Mteremko  _______________________
    7. Bainisha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi hii.(alama 2)
      Babu ametengenezewa kiti kizuri na mjukuu wake.
    8. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo.(alama 3)
      Mwanafunzi yule hupenda kutembea katikati ya barabara kila wakati.
    9. Yakinisha sentensi ifuatayo.(alama2)
      Nisingemuona nisingetimiza ahadi yako.
    10. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.(alama 4)
      Watoto wote wamelala na wazee wanakunywa pombe.
    11. Andika sentensi hii katika hali ya kuamrisha wingi.(alama2)
      Ondoka hapa._________________________________________
    12. Geuza sentensi zifuatazo kulingana na maagizo.(alama 2)
      1. Maimuna anapika wali.(wakati usiodhihirika).
      2. Wao walisoma riwaya hiyo.(wakati timilifu)
    13. Onyesha miundo miwili ya nomino za ngeli ya A-WA.(alama 2)
    14. Unda nomino mbili kutokana na kitenzi:    (alama 2)
      Soma.____________________________________

MARKING SCHEME

  1. Maswal
    1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka.(alama 1)
      • kipimo ni kipi?
    2. Eleza bahari nne za shairi hili. (alama 4)
      • tarbia:kila ubeti una mishoro mine
      • mathnawi:lina vipande viwili
      • msuko:kibwagizo kimefupishwa
      • ukara: vina vya kati vinabadilikabadilika lakini vina vya nje vinafanana.
    3. Taja tamathali moja ya usemi na kisha utoe mfano wake kutoka kwa shairi.(alama 1)
      • swali balagha:kipimo ni kipi?
      • Uhuishi/tasihishi:utu uko wapi ,ni wapi unapoketi
    4. Mshairi ana uhuru wa uandishi anapotunga shairi. Taja na ueleze mifano yoyote miwili ya  matumizi ya uhuru huo kisha utolee mifano kabambe. (alama 4)
      • Inksari:asosita badala ya asiyesita.alo badala ya aliye,anoshika badala ya anayeshika.
      • Tabdila:maani badala ya maana.
    5. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
      • mshairi anasema kwamba aliye mzalendo ni apendaye nchi yake na kufuata sharia zake.ni asiyechukia watu wala kudanganya,au yule ashikaye pendo hadi kifoni.atajulikanaje au atapimwaje?
    6. Eleza muundo/umbo la shairi hili.(alama 4)
      • shairi hili lina mishororo mine katika kila ubeti.
      • Vina vya kati vinabadilikabadilika ilhali vya nje vinafanana.
      • Lina kibwagizo kifupi
      • Lina jumla ya beti nne.
      • Kila mshororo umegawika kwa vipande viwili.
    7. Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika ushairi. (alama 2)
      1. Katiti-kidogo 
      2. Gatigati –ubaguzi/upendeleo
  2. Matumizi ya lugha.
    1. Andika tofauti moja kati ya sauti zifuatazo. (alama 2)
      1. /v/ na /f/
        • Sauti /v/ ni ghuna ilhali /f /ni sighuna/hafifu
      2. /r/ na /l/
        • Sauti /r/ni kimandende ilhali sauti /l/ ni kitambaza.
    2. Bainisha silabi katika neno:   (alama3)
      Sikumpiga.
      • Si-kiambishi kikanushi cha nafsi ya kwanza umoja
      • Ku-kiambishi cha wakati uliopita
      • m-kiambishi awali cha mtendwa/yambwa
      • pig-mzizi
      • a-kiishio
    3. Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo.(alama 2)
      Mtoto alishonewa nguo na mama yake vizuri sana.
      • Kiima-mama yake
      • Chagizo-vizuri sana.
    4. Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo.(alama 2)
      Ingawa mshahara wake si mkubwa anaikimu familia yake.
      • Kishazi tegemezi-ingawa mshahara wake si mkubwa
      • Kishazi huru-anaikimu familia yake
    5. Eleza maana ya shadda.(alama 1)
      • Ni mkazo unaotiwa kwenye silabi au herufi ili kutoa maana nayokusudiwa.
    6. Onyesha panapotokea shadda katika neno:    (alama 1)
      • Mtere’mko .au ‘m’
    7. Bainisha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi hii.(alama 2)
      Babu ametengenezewa kiti kizuri na mjukuu wake.
      • Babu-shamirisho kitondo
      • Kiti kizuri-shamirisho kipozi
    8. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo.(alama 3)
      Mwanafunzi yule hupenda kutembea katikati ya barabara kila wakati.
      • Kirai nomino-mwanafunzi yule
      • Kirai kitenzi-hupenda kutembea
      • Kirai kihusishi-katikati ya barabara
      • Kirai kielezi-kila wakati
    9. Yakinisha sentensi ifuatayo.(alama2)
      Nisingemuona nisingetimiza ahadi yako.
      • Ningemuona ningetimiza ahadi yako.
    10. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.(alama 4)
      Watoto wote wamelala na wazee wanakunywa pombe.
    11. Andika sentensi hii katika hali ya kuamrisha wingi.(alama2)
      Ondoka hapa. Ondokeni hapa!
    12. Geuza sentensi zifuatazo kulingana na maagizo.(alama 2)
      1. Maimuna anapika wali.(wakati usiodhihirika).
        • Maimuna apika wali.
      2. Wao walisoma riwaya hiyo.(wakati timilifu)
        • Wao wamesoma riwaya hiyo.
    13. Onyesha miundo miwili ya nomino za ngeli ya A-WA.(alama 2)
      • m-mi:mtume -mitume
      • ch-vy:chura- vyura
      • ki-vi:kiboko- viboko
      • m-wa:mtoto-watoto
    14. Unda nomino mbili kutokana na kitenzi:    (alama 2)
      • Soma.-  Msomi
      • somo - kusoma
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Mid Term 2 Exams 2023.

Tap Here to Download for 50/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest