Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 Term 2 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

  1. Jibu naswali manne katika karatasi hii
  2. Swali la kwanza ni la lazima
  3. Maswali mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki

NB: Usijibu maswali mawili kutoka kitabu kimoja/ sehemu moja



MASWALI

SEHEMU YA A
USHAIRI

1. Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali

Mungu naomba subira, subira nayo imani
Imani iliyo bora, bora hapa duniani
Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani
Hiani pamwe ukora wenye kuhini.

Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu
Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili
Muwili hata kidari, kidari kuwa thakili
Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli.

Misuli kuwa hafifu, hafifu kama muwele
Muwele wa hitilafu, hitilafi ya nduwele
Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele
Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale.

Vishale vinitomele, vitomele vikwato
Vikwato pia maole, maole kufanya mito
Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto
Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto.

Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka
Kutamka wazi vino, vino subira kutaka
Kutaka imani mno, mno n'sipate wahaka
Wahaka wa matukano, matukano na mashaka.

Mashaka haya ya leo, leo yawe yarnepita
Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota
Nyota njema ingarao, ing'arao kunikita
Kunikita salamani, salamani nikadata.

  1. Kwa nini nafsi neni anaomba subira na amani. (al.2)
  2. Shairi hili ni la Bahari gani kwa kuzingatia;
    1. Mpangilio wa maneno. (Al. 4)
    2. Mpangilio wa vina.
  3. Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4)
  4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (al.4)
  5. Kwa kutolea mifano, elezea jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (Al.6)

SEHEMU YA B RIWAYA (Jibu swali la 2 au 3)
CHOZI LA HERI (Assumpta k. Matei)

2. “………Unatumia mantiki gani kusema kuwa sisi si watoto wa miaka hamsini?”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al. 4)
  2. Taja mbinu ya lugha inayojiotokeza katika dondoo hili. (al.1)
  3. Kwa kutumia hoja nane, thibitisha wazungumziwa walikuwa watoto wa miaka Hamsini. (al.8)
  4. Eleza wasifu wa msemaji wa maneno haya. (al.4)
  5. Eleza umuhimu wa msemewa wa maneno haya. (al.3)

3. Fafanua changamoto zinazoikabili jinsia ya kike katika riwaya ya chozi la heri. (al.20)
SEHEMU YA C: TAMTHILIA
KIGOGO (PAULINE KEA) – Jibu swali la 4 au la 5.
4. Tamthilia ya kigogo ni taswira kamili ya matatizo yanayokumba mataifa mengi barani Afrika. Fafanua ukirejelea tamthilia nzima . (al.20)

5. “Ukitaka kuwafurusha ndege, kata mti. Hawa wangekuwa sasa wametuliza nafsi zao.

  1. Eleza muktadha wa kauli hii. (al. 4)
  2. Tambua mbinu mbili za uandishi zilizotumika. (al.4)
  3. Onyesha jinsi wahusika kadhaa walivyofurushwa kama ndege. (al. 12)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI.
TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE – Jibu swali la 6 au la 7
6. Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi;

  1. Mame Bakari (al.10)
  2. Mapenzi ya kifaurongo (al.10)

7. Thibitisha ufaafu wa jina ‘mashaka’ katika hadithi ya Ndoto ya mashaka. (al.20)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
8.

  1. Taja aina mbili kuu za fasihi. (al.2)
  2. Fafanua tofauti baina ya fasihi ulizotaja hapo juu. (al.4)
  3. Tambua istilahi zifuatazo za fasili. (al.8)
    1. Fanani
    2. Jagina
    3. Maleba
    4. Miviga
  4.                      
    1. Eleza maana ya vitanza ndimi. (al.2)
    2. Fafanua sifa za vitanza ndimi. (al.4)


MARKING SCHEME

  1. SHAIRI
    1. Kwa nini  nafsi neni inaomba subira na amani. (al.2)
      • Ili asiwe na wasiwasi wa kutukanwa na kuhiniwa
      • Ili aepuke kufanyiawa mabaya (2 x2 =4)
    2. Shairi hili ni la Bahari gani kwa kuzingatia;
      1. Mpangilio wa maneno.  (Al. 4)
        Pindu/mkufu/nyoka
      2. Mpangilio wa vina.
        Ukaraguni
    3. Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4)
      • Tashbihi – hafif kama muwele/ tele mithili kitoto
      • Takriri / uradidi – subira- subura, kiburi – kiburi, neno – neno (2 x2 =4)
    4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.  (al.4)
      • Misulu kuwa dhaifu sana kama ya mgonjwa, hasa mgonjwa mwenye tatozo la uwele ambalo unasumbua daima na usiosikia dawa/ unaofisha/ usio na tiba
    5. Kwa kutolea mifano, elezea jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (Al.6)
      • Lahaja/ lugha kale – pamwe – pamoja na, matozi – machozi
      • Mazda – muwili – mwili
      • Inkisari – kitoto kilo vipele – kitoto kilicho na vipele n’sipate – nisipate 
         (3 x 2 = 6)
SEHEMU YA B RIWAYA (Jibu swali la 2 au 3)
CHOZI LA HERI (Assumpta k. Matei)
2. “………Unatumia mantiki gani kusema kuwa sisi si watoto wa miaka hamsini?”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.  (al. 4)
    • Ni mawazo yanayompitikia Ridhaa anapokumbuka maneno ya marehemu mwanawe Annatila (Tila)
    • Mjadala wenye unahusu mafarikio baada ya uhuru
    • Ridhaa yumo nyumbani kwake akitazama masozo ya aila yake, ambayo ni majivu
    • Hii ni baada ya kuawa kwa familia yake kinyama na mzee kedi alipoliteketeza jumba lake la kifahari.
  2. Taja mbinu ya lugha inayojiotokeza katika dondoo hili.  (al.1)
    • Balagha – pana matumizi ya swali lisilohitaji jibu.
    • Jazanda – watoto wa miaka hamsini kumaainisha kuwa bado waafuka wangali wanatawalimu na wakoloni kwa njia isiyo ya moja kwa moja; sifa za ukoloni zingali barani afrika.
    • Kinanya – waafrika wanaendelea kuwategemea wakoloni hata baada ya kupata uhuru.
  3. Kwa kutumia hoja nane, thibitisha wazungumziwa walikuwa watoto wa miaka Hamsini.  (al.8)
    • Baada ya miaka hassini ya uhuru, tumebaki kuwa watengemezi wa wakoloni wao hao waliotupa uhuru.
    • Baada ya miaka hamsini ys uhuru, mataifa mengi ya kiafuka hayajakuwa kiuchumi lakini yamebaki kuwa wategemezi wa wakoloni waliowapa uhuru.
    • Wakoloni walioondika Afuka, walowezi (settlers) na waafrika wenye uwezo walimiliki mashamba yaliyokuwa ya wakoloni na kufanya waafrika kuwa maskuota katika vituo usuli wao.
    • Wahokuwa wakoloni ndio wanawamua was fuka watakuza nini katika ardhi yao
    • Waafika wanaendelea kuwategemea wakoloni kwa lishe na ajira ambayo ni ya Kijungu jiko... huenda
    • Waafrika wana Kuza mazao madogo ambayo Kumfaidi huyo mkoloni aliyetupa uhuru. Hatyaweza Kujisagia Kahawa yetu ingawa mbegu. ni zetu, unachoka kulikuza lao lenyewe kisha tunawapelekea wahokuwa wakoloni walisage na Kuhuuzia kwa bei ya juu.
    • Mwafuka aliridhi umilikaji. hatimiliki kutoka kwa hah mzungu wa ardhi kwa Kutumia ambayo aliwafanya wengi ambao hawakuwa na uwezo wa kununus mashamba kuwategemea wenye uwezo.
    • Ubinafsi wa mkoloni ulrithiwa na mwafaka. Watoto waliosoma na Ridhaa walimwita mfuatamvua na Kukataa
    • Kucheza naye kwa madai aliwashunda mitihani. -Kupitia lawa maneno ya Tila kwa babake, tunaelezwa Kuwa machimbo ya mawe na hazina za mafuta. Zimepewa Kampuni za Kibinafsi ambazo ni za kigeni. -Huku nchini uchimbaj, mading. wahifadhi unafadhiliwa na wageni ambapo fedha zinazotokana na rasilimali hil huishia kwenye mifuko ya wageni kufaidi nchi
    • Kampuni za Kigeni zimewapa wenyeji (waafuka) ajira ambayo mshahara wake ni mdogo sana (mkia wa mbux) -Dongozi wa Killatili unaendelezwa, vijana wanavawa Kwa mitute ya bunduki wanapojaribu kujikomboa Kutokana na ukoloni
    • Waafrika wanategemea mahindi yahutolewa ili kuwa punguzia makali ya ambako Kunaingata nchi Kutotosheleza Chakula.
      (zozote 8x=8)
  4.  Eleza wasifu wa msemaji wa maneno haya (A14)
    • Msemaji ni Tila
    • Ni mkakamavu - Anazungumzia maswala ya sheria na Siasa kwa ukakamavu
    • Mwenye busara - Alifahamu kuwa hakung maendeleo ambayo walikuwa wamepats licho miaka hamsini ya uhu / hakuna ahyempiku kwa maswala ya Siasa
      (2x2=4)
  5. Eleza umuhimu wa Anatumiwa msemewa wa maneno haya (413)
    • Kuonyesha athari za ukabila mali yake yote yanateketezwa kwa ajili ya ukabila. 
    • Anaendeleza mandhu ya utu - anayadhamuni masomo ya wapwa wa Mzee Kedi'
    • Ni Kielelezo cha watu wenye bidii - Anasoma hadi kuwa daktari, anaweka anaanzisha hospitali.
      (zozote 3x1 = 3)
      (Mwalimu ahakiki "Jibu sahihi)

3. Fafanua changamoto zinazoikabili jinsia ya kike Katika viwaya ya Cho 2, La Heri (Al 20) · 

  1. Matusi na vitisho - Bwana Maya alipoulizwa maswali na mkewe alimpiga makondo, kumtisha na kumtusi.
  2. Kubakwa Sauna anabakwa Maya. Mamake naya anamsaidia Kuavya mimba huyo..
  3. Ndoa za mapema. Pete baada ya kupashwa to Larg ancozwa kwa mzee Fungo kwa lazima, Nyanyake. anajaribu Kumtelia lakini hakufaulu.
  4. kukatizwa elimu - Kiu cha Pete cha Kuendelea kusoma hukatizwa baada ya ndoa ya lazima kwa Bw. Fungu
  5. Waume zao kukosa uaminifu katika ndoa - mfano: Bwana Tenge anashiriki. ngono na wanawake wengi wakati B. Kimai Yuko Kiyini
  6. kunyimwa nafasi ya kuongoza - Mwekevu anadhalilishwa na mpinzani wake kwa kuandaa maquelamano ya kupinga Kuchaguliwa kwake.
  7. Kutelekezwa - Chandachems away anaondoka kwa jirani. yake baada ya Kulalamikia vitu vidogo viologo Kuonyesho Kutoridhika. Pia zohali anatelekezwa na wazazi wake.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 Term 2 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest