Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 End Term 2 Exams 2023

Share via Whatsapp
MAAGIZO
  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima
  • Maswali hayo matatu mengine  yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani; riwaya,tamthilia ,hadihi fupi na ushairi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili
  • Andika nambari  ya maswali  uliyoyajibu

SWALI LA LAZIMA

  1. SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI
    1. Tofautisha kati ya hadhira ya Fasihi simulizi na Fasihi andishi.(alama 5)
    2. Fafanua mambo ambayo yanaweza kuchangia kubadilika kwa Fasihi Simulizi.(alama 5)
    3. Tambua wahusika katika Fashi simulizi na umuhimu wao.(alama 10)
  2. SEHEMU YA B:Riwaya ya Chozi la heri na  Asumpta Matei
    Lakini  itakuwaje ‘historical injustice ‘ nawe Ridhaa hapo ulipo sicho kitovu?
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
    2. Tambua mbinu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.(alama 2)
    3. Eleza sifa nne za mzungumzaji wa maneno haya.(alama 4)
    4. Eleza mambo matano yaliowakumba walioishi penye kitovu kisicho chao.(alama 10)
      AU
  3. Jamii ya Chozi la Heri ina taswira ya jinsi ukabila unavyoathiri bara la Afrika.(alama 20)

SEHEMU YA C; Tamthilia ya Bembea ya maisha na Timothy Arege

  1. Kila binadamu hukabiliana na mabadiliko katika maisha yake.Thibitisha kauli  hii ukirejelea Tamthilia ya  Bembea ya maisha.(alama 20)
    AU
  2. ”Mwanangu binadamu mchoyo  kwa lake lakini mkarimu ajabu kwa la mwenziwe.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
    2. Jadili namna msemaji na wenzake wa jinsia ya kike walivyosawiriwa kwa njia chanya katika tamhilia hii.(alama 6)
    3. Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya msemaji na msemewa katika tamthilia ya Bembea ya maisha
      (alama 10)

SEHEMU YA D.MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI ZINGINE

  1. Jinsia ya kike imesawiriwa kuwa dhaifu na inazidi kudhulumiwa kila uchao.Thibitisha kauli kuyoka hadithi zifuatazo:
    1. Nipe nafasi
    2. Sabina
    3. Fadhila za punda
    4. Kifo cha suluhu
           AU
  2. PAULINE KEA:Kila mchezea wembe
    1. Eleza nafasi ya mbinu zifuatazo za lugha katika kuendeleza hadithi:
      1. Barua                                                                                                 (alama 4)
      2. Majazi                                                                                                  (alama 3)
      3. Usimulizi                                                                                             (alama 3)
    2. Katika hadithi ya Msiba wa kujitakia na D.W.Lutomia athari za uteuzi mbaya wa viongozi zinaoenkana wazi.Zitambue(alama 10)
  3. SEHEMU YA E:SHAIRI (alama 20)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo:
    Nimeona ,milima na mabonde,misitu na nyika
    Nimeona, majani na umande, uliotandazika
    Nimeona ,mkulima yuenda , shambani

    Nimeona , uwanda na magugu, yalomkabili
    Nimeona, wajibu na vurugu, ‘wiano mkali
    Nimeona mkulima akiwa tayari

    Nimeona , kwa ari na juhudi, anatupa jembe
    Nimeona , kakaza ukaidi, kwa nguvu achimbe
    Nimeona, mkulima akiwa kazini

    Nimeona ,kijua kinawaka,kama jahanamu!
    Nimeona ,jembe lainuka, linapojuhumu
    Nimeona ,mkulima akiwa mbioni

    Nimeona, mvua yamiminika, naye hatohisi
    Nimeona ,kwa kani anatimka, bila wasiwasi
    Nimeona mkulima akiwa kazini

    Na sioni ,jasho linapomwaika ,yendapo mazao
    Na sioni ,hadhiye kutukuka ,ila kilio
    Kwa nini?Nauliza mkulima: kwani?

    Maswali
    1. Eleza ujumbe wa shairi hili.                                   (alama 4)
    2. Kwa kutolea mifano tambua mifano miwili ya uhuru wa mshairi.      (alama 4)
    3. Onyesha umuhimu wa matumizi ya ;
      1. Kihisishi                                                                                                   (alama 2)
      2. Kiulizi                                                                                                       (alama 2)
    4. Eleza mtindo wa lugha katika  shairi hili.                                                                 (alama 4)
    5. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi.                              (alama 4)

MARKING SCHEME

  1. SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI
    1. Tofautisha kati ya hadhira ya Fasihi simulizi na Fasihi andishi.(alama 5)
       HADHIRA YA FASIHI SIMULIZI  HADHIRA YA FASIHI ANDISHI
      1.Huwasiliana moja kwa moja
      2.Huchangia katika uwasilishaji wa fasihi simulizi
      3.Huonana na mwasilishaji
      4.Ni kubwa kwani huhusisha wanaojua kusoma na wasiojua kusoma
      5.Ni hai-inajulikana na fanani
      6.Hainunui kazi inayowasilishwa
      7.Yaweza kumiliki kazi ya fanani
      1. Sio lazima iwasiliane na mwandishi
      2. Haichangii katika uandishi
      3. Si lazima ionane na mwandishi
      4. Ni ndogo- huhusisha wanaojua kusoma na kuandika pekee
      5. Si hai-msomaji hajulikani na mwandishi
      6. Hununua kazi iliyoandikwa
      7. Haiwezi kumilili kazi ya mwandishi
      Zozote 5*1=5
    2. Fafanua mambo ambayo yanaweza kuchangia kubadilika kwa Fasihi Simulizi.(alama 5)
      • Kuwasilishwa vibaya
      • Fanani kusahau na kubadilisha yalioma na mtiririko
      • Mabadiliko ya mandhari /mazingira
      • Mabadiliko ya wakati
      • Mabadiliko ya vizazi na maingiliano
      • Ubunifu wa fanani
      • Maendeleo ya TEKNOHAMA –Hasa kama njia ya uhifadhi wa fasihi simulizi ambayo huua baadi ya taathira na uhalisia wake.
        Kutuza-zozote 5*1=5
    3. Tambua wahusika katika Fashi simulizi na umuhimu wao.(alama 10)
      • Fanani-anatunga na kuwasilisha fasihi simulizi
      • Hadhira-kusikiliza,kutazama,na kushiriki katika uwasilishaji wa Fasihi simulizi
      • Wanyama-wanaotenda kama binadamu ili kuwakilisha sifa kama ujanja, ulaghai, tamaa, ujinga –ingawa kuna wale wanaobakia kuwa wanyama tu
      • Binadamu
      • Maziwa na majitu-viumbe vyenye matendo na maumbile ya kutisha ,tamaa iliyokithiri
      • Vitu visivyo na uhai-hutumiwa kuibua sifa za Imani za kidini na ushirikina
      • Mizimu-roho za waliokufa-kuendeleza itikadi na Imani za jamii
      • Miungu-viumbe wenye uwezo mkubwa Zaidi ya wa binadamu-kuonyesha udhaifu wa binadamu na unyenyekevu wake kwa nguvu hizi
        Zozote 5*2=10(kutaja alama 1. Mfano au maelezo alama 1)
  2. SEHEMU YA B: Riwaya ya Chozi la heri na Asumpta Matei
    1. Lakini itakuwaje ‘historical injustice ‘ nawe Ridhaa hapo ulipo sicho kitovu?
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
        • Ridhaa anajisemea akilini mwake
        • Anarejelea majadiliano yao na bintiye Tila
        • Baada ya kuteketezwa kwa nyumba yake na mali pamoja na aila yake
        • Akiwa eneo lililochomekea nyumba
      2. Tambua mbinuza lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.(alama 2)
        • Swali la balagha-…sicho kitovu?
        • Kuchanganya ndimi-historical injustice(kutaja alama 1 ,mfano alama 1)
      3. Eleza sifa nne za mzungumzaji wa maneno haya.(alama 4)
        Mzungumzaji ni Ridhaa
        • Ana mapenzi-alisaidia jamii kupata maji
        • Mvumilivu-alivumilia uchungu wa kuipoteza aila yake
        • Mwenye maadili-alimwadhibu Tila na Mwangeka walipoiga mazishi ya Dede mdogo wao
        • Msomi-ana shahada ya uzamili
        • Mfariji-alimfariji mwanawe Mwangeka
          Za kwanza 4*1=4
      4. Eleza mambo matano yaliowakumba walioishi penye kitovu kisicho chao.(alama 10)
        • Kukejeliwa na kuitwa “mfuata mvua”
        • Kutengwa-wanafunzi wengine wanamtenga Ridhaa kwa kuwa ni ‘mfuata mvua’
        • Kuchomewa nyumba zao kama vile Ridhaa
        • Kuharibiwa mali zao-majumba ya Ridhaa yanaharibiwa eti amejengea mahali palipotengewa barabara
        • Kufanywa kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani
        • Kuishi kama maskini ukimbizini
        • Selume kupoteza ndoa yake
        • Watoto wao kubakwa kama watotot wa Kaizari
        • Masomo ya watoto ya wakimbizi kuathirika –kama watoto wa Kaizari
          Hoja za kwanza
          AU
  3. Jamii ya Chozi la Heri ina taswira ya jinsi ukabila unavyoathiri bara la Afrika.(alama 20)
    • Ridhaa alibaguliwa na wanafunzi wenzake kwa kutokuwa wa jamii yao jambo linalomfanya Ridhaa kulia sana na kutaka kuacha shule
    • Subira analia kilio cha ubaguzi unaotokana na mamamkwe
    • Mamamkwe anamlaumu kuwa yeye ndiye anasababisha kuharibikiwa na mali yao
    • Ukabila huu unasababisha ndoa ya Subira na Kaizari kuvunjika
    • Watoto wa Subira wanawachwa bila mama yani Lime na Mwnaheri
    • Ukabila ulichangia kifo cha aila ya Ridhaa
    • Kuharibiwa kwa mali na nyumba yake kuchomwa
    • Kaizairi kuaga mapema baada ya kuachwa na mkewe Subira
    • Selume kutengwa na bintiye Sara kwa sababu ya ukabila
    • Ndoa ya Lucia Kangata kupingwa kwa kuwa anaolewa kwa jamii ambayo si yao.
    • Lime na Mwanaheri kubakwa mbele ya baba yao
    • Tila kufa akiwa bado mdogo kabla hajatimiza ndoto yake ya maisha ya kuwa jaji ya mahakama kuu
      Hoja zozote10*2=20

SEHEMU YA C; Tamthilia ya Bembea ya maisha na Timothy Arege

  1. Kila binadamu hukabiliana na mabadiliko katika maisha yake.Thibitisha kauli ukirejelea Tamthilia ya Bembea ya maisha.(alama 20)
    • Sara anapolemewa kupika anamwita Dina amsaidie
    • Yona anapokuwa mlevi na kupoteza kazi yake Sara anawasomesha watoto wake
    • Jamii inapomsema Sara kuhusu kutopata watoto katika ndoa yake anavumlilia
    • Yona anapokuwa mlevi sana Sara anamvulilia na kumwita ‘mlevi wangu’
    • Sara napokuwa mjini kwa sababu ya matibabu ,Yona anashughulika nyumbani
    • Uhaba wa chakula unamfanya Kiwa asipende kula sana
    • Asna anapokosa kazi baada ya kumaliza masomoyake ya chuo kikuu anajikaza kutafuta tafuta vijikazi mjini
    • Bunju anapokataa mamamkwe Sara kulala kwake kwa sababu ya utamaduni, Neema anampeleka kwa Asna dadake
    • Ghararama ya maisha inapopanda Bunju anatafuta njia mbadala ya kupata pesa kando na kazi yake ya kuajiriwa
    • Tatizo la msongamano wa magari mjini linamfanya Neema kutoka mapema kila siku kwenda kazini
    • Kuajiriwa kazi kwa Neema kunamfanya amwandike kijakazi Bela ili amsaidie na kazi za nyumbani
    • Ukosefu wa hospitali nzuri kijijini ni sababu mojawapo ya Neema kuja kumchukua mamake na kumpeleka mjini kuliko na madaktari wataalamu wa kumsaidia
    • Neema na Bunju baada ya kugombana kuhusu mchango wake kwa matibabu ya Sara anaamua kumuelewa hivyo ndoa yao kuendelea vyema
    • Maradhi ya moyo yalipomlemea Sara kiasi cha kukata tamaa,Neema anamsaidia kupata matibabu na kurejesha matumaini yake
    • Yona anapoona kuwa ulevi wake na kutojali kwake kunaangamiza familia yake anaapa kutolewa tena,
    • Mgogoro kati ya Yona na Sara unaisha anapoachana na utamduni na kuingia jikoni na kumpikia mkewe kiamsha kinywa.
    • Mgogoro kati ya Neema na Yona unaisha anapomshukuru kwa mengi mema aliomfanyia akiwa mtoto msichana
    • Yona anapomwomba Sara msamaha kwa kumsababishia ugonjwa wa moyo hali hii inaleta utulivu katikati yao.
    • Yona na Beni walipotofautiana kuhusu watoto wao ,Luka anafaulu kuwatuliza na wazee hawa wanaendelea na sherehe yao.
    • Neema anapolalamikia ubahili wa Bunju Sara anampa sababu ya kuona uzuri wa Bunju hivyo kumtuliza
      Zozote 20*1=20
      AU
  2. ”Mwanangu binadamu mchoyo kwa lake lakini mkarimu ajabu kwa la mwenziwe.
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
      • Maneno ya Dina
      • Anamwambia Kiwa
      • Yuko nyumbani kwa Dina
      • Dina alikuwa akimwambia Kiwa kuhusu magumu ambayo Sara amepitia katika maisha.
    2. Jadili namna msemaji na wenzake wa jinsia ya kike walivyosawiriwa kwa njia chanya katika tamhilia hii.(alama 6)
      • Mwanamke ni mkarimu-Neema anatumia mshahara wake kuwalipia karo wanuna wake
      • Ni mwenye bidii-Sara anatia bidii ya kuwasomesha wanawe Yona alipopoteza ajiar
      • Mwajibakaji-Neema anawatafutia wafanyikazi wazazi wake wawe wakiwasaidia
      • Wenye utu-Dina anaitikia wito wa Sara kwenda kumsaidia na upishi
      • Watiifu-Bela anatii anapoelekezwa na Neema
      • Mwenye busara-Sara amaamshauri Neema kuwa maisha ya ndoa ni kama bembea
        Zozote 6*1=6
    3. Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya msemaji na msemewa katika tamthilia ya Bembea ya maisha
      (alama 10)
      • Yanaibua maudhui ya uwajibikaji-Kiwa amekuja kumjulia hali mamake
      • Yanachimuza sifa za Sara-mvumilivu-alivulimilia masimamgo kutka kwa jamii kwa sababu ya kutoata watoto
      • Mgogoro katika ndoa-Yona alikuwa akimpiga Sara kwa kutopata mtoto mvulana
      • Kuonyesha sifa za Neema-akili kama sumaku
      • Maudhui ya umbea-wanajamii walimsema sana Sara
      • Sifa ya Yona –ana msimamo dhabiti-hakuoa mwanamke mwingine ili ampe mtoto kijana kama vile jamii ilivyomsukumia
      • Kujali kwa Dina-anataka kujua mbona mtoto wake Kiwa amekonda sana
      • Maudhui ya mila na utamaduni-umuhimu wa mtoto kijana kama mrithi wa jamii
      • Dhamira ya mwandishi-kupinga tamaduni zinazomthamini mtoto wa kiume na kumdunisha mtoto wa kike
      • Usasa-tambo la mwili halionyeshi kufaulu maishani ila akili
        Zozote10*1=10

SEHEMU YA D.MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI ZINGINE

  1. Jinsia ya kike imesawiriwa kuwa dhaifu na inazidi kudhulumiwa kila uchao.Thibitisha kauli kutoka hadithi zifuatazo;(alama 20)
    1. Nipe nafasi
      • Ameachiwa jukumu la malezi-Mama Kazili ameachiwa jukumu la kuwalea wanawe wakati Moshi anapotelea kazini kule Afrika kusini
      • Mke haaminiwi katika ndoa –Moshi humtumia mamake pesa badala ya kumtumia mkewe.
      • Anaachwa wakati anaoa mke mwingine kule Afrika kusini
      • Anapitia mateso ya kuona vifo-Mama Kazili anamwona mwanawe akifa na kumbeba maiti yake kwa jamaa ya mumewe
      • Mke anatolewa hukumu ya kumdhulumu-Matweba anamtolea Kazili hukumu ya dhuluma ya kumwamuru abebe maiti ya mwanawe ili aende naye nyumbani azikwe
        (alama 5)-kadiria jibu la mwanafunzi
    2. Sabina
      • Mwanamke amepewa kazi nyingi-Sabina anafanyishwa kazi nyingi nyumbani katika umri wake
      • Ananyimwa haki ya kupata elimu bora-Sabina analazimika kufanya kazi ngumu asubuhi kabla ya kwenda shuleni
      • Ananyimwa haki ya kupata elimu-Ombati na mkewe hawataki Sabina aendelee na masomo hadi wanapanga kumuoza kwa mwendesha pikipiki ili wapate mahari walionyimwa na Nyaboke mamake Sabina.
      • Nyaboke anaachiwa jukumu la ulezi-Janadume lililofaa kuitwa babake Sabina lilimkana Nyaboke peupe mchana,
      • Mwanamke anachukuliwa kama chombo cha kuchumia mali-Ombati alitarajia kutajirika kupitia kwa mahari ya Nyaboke na Sabina.
        Zozote 5*1=5)
    3. Fadhila za punda
      • Mwanamke anapigwa na mumewe- Luka anamdhulumu mkewe Lilia kwa kumpiga na kumjeruhi kila uchao
      • Mwanamke anatusiwa –Luka anamtusi mkewe anapomtembelea ofisini mwake
      • Anasalitiwa kimapenzi-Luka alimsaliti mkewe Lilia alipoanza uhusiano nakirukanjia wake akiwa mke
      • Mwanamke anapewa nafasi ya pili katika ndoa-Luka anabaki mjini kikazi na anamwacha mkewe Lilia na kukosa kufika nyumbani
      • Mwanamke analazimika kufanya mambo asioyapenda ili kumfurahisha mumewe-Lilia anamsaidia bwanake katika siasa ingawa haipendi
        ( Zozote 5*1=5)
    4. Kifo cha suluhu
      • Mwanamke ameachiwa jukumu la malezi-Suluhu amemwachia mkewe majukumu hayo
      • Ametumiwa kutimiza ashiki za mwanamume-Suluhu anahusika kimapenzi na Abigael licha ya kuwa ana mke na familia
      • Mwanamke anauliwa-Suluhu anamuua mamaye Abigael kwa kutishia kuchukua hatua za kisheria ili kupinga kunyakuliwa kwa shamba lake
      • Bi Suluhu anajitoa uhai badala ya kukabilana na hali yake moja kwa moja
      • Kila wakati Abigael alipopata mimba alitafuta njia bora ya kuavya mimba hiyo ili aendelee na ufska wake
        (Zozote 5*1=5)
        AU
  2. PAULINE KEA:Kila mchezea wembe
    1. Eleza nafasi ya mbinu zifuatazo za lugha katika kuendeleza hadithi:
      1. Barua
        • Barua ya Tembo kwa mkewe Emmi akimweleza yote aliyoyafanya na kumwomba msamaha
        • Barua hii inaandikwa na Salim kwani Tembo haongei na hawezi kusonga naye mkewe alimuacha kwa kukataa kufuata ushauri wake wa kuacha pome
        • Barua inaendeleza ploti
        • Inachimuza maudhui ya ujutivu na athari za matumizi ya pombe
          (alama 4)
      2. Majazi
        • Jina la Tembo ni majazi lenye maana ya pombe. Mhusika anapenda kunywa pombe kupita kiasi.
        • Mamapima-ni mama anayewapimia walevi pombe ya viwango tofauti katika biashara yake
        • Mwanaheri-analeta heri kwa Tembo anapomtembelea hospitalini na kukubali kuwa tarishi wa kupeleka barua kwa Emmi. (alama 3)
      3. Usimulizi
        • Usimulizi wa nafsi ya kwanza umetumika ambapo Tembo anasimulia matukio yaliotendeka nayo yanaandikiwa mkewe aende kusomewa kana kwamba wanawasiliana moja kwa moja.
        • Usimulizi wa kisa cha mkufu ulong’ang’aniwa hata baada ya kupata tope na mate unadhihirihsa kuwa kitu kizuri hakipotezi thamani yake.
        • Usimulizi huu unachimuza maudhui ya urafiki   (alama 3)
    2. Katika hadithi ya Msiba wa kujitakia na D.W.Lutomia athari za uteuzi mbaya wa viongozi zinaoenkana wazi.Zitambue(alama 10)
      • Ukosefu wa ajira-Machoka anatafuta kibarua mchana kutwa na anaambulia patupu
      • Njaa/ukosefu wa chakula-matumbo ya Machoka yanateta kwa kushindwa kuhimili njaa
      • Utabaka-maisha ya wapiga kura na wapigiwa kura ni tofauti
      • Mfumuko wa bei za bidhaa-bei ya bidhaa iliongezeka kinyume na matarajio ya wanamatopeni baada ya uchaguzi
      • Kutozwa ushuru wa kiwango cha juu-serikali iliendelea kuwatoza wnamatopeni ushuru wa juu wa mishahara yao duni kuwasukumia kwa umaskini zaidi
      • Mshahara duni-mwandishi anasema kwamba mishahara yao duni ilikwakama huko kwenye udhalimu
      • Umaskini-siku za ukata ziliendelea kujikokota
      • Wizi wa kura-kwamba Matopeni kuhesabu kura ndio muhimu kushinda kupiga kura
      • Kulimbikiziwa viongozi-wanamatopeni hulimbikiziwa viongozi wasiowataka
      • Ubadhirifu wa mali ya umma-Sugu Junior anatumia mamlioni ya pesa ya umma kugharamia nauli ya ndege kwa viongozi wa majimbo.
        Zozote 10*1=10
  3. SEHEMU YA E: SHAIRI (alama 20)
    1. Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 4)
      • Mshairi anaeleza juhudi anazofanya mkulima akiwa kazini na matatizo anayopata katika kazi hiyo.
      • Ingawa mkulima najitahidi licha ya matatizo hayo bado anahujumiwa haki yake na hafaidiki
        (hoja 2*2=4)
    2. Kwa kutolea mifano tambua mifano miwili ya uhuru wa mshairi. (alama 4)
      • Inkisari-yendapo
      • Udondoshaji wa silabi-‘wiano-uwiano
        (Kutaja alama 1 mfano alama 1)
    3. Onyesha umuhimu wa matumizi ya ;
      1. Kihisishi (alama 2)
        • Nimeona,kijua kinawaka , kama jehanamu!-Kuonyesha ile dhana ya jinsi mkulima anavyofanya kazi katika hali ngumu ya jua kali mno.
      2. Kiulizi (alama 2)
        • Kwa nini?Nauliza mkulima:kwani?- Kuonyesha msimamo wa mshairi kuhusu unyanyasaji unaofanyiwa mkulima .Mshairi anashangaa na amekasirishwa na hali hii ya kumnyanyasa mkulima.
    4. Eleza mtindo wa lugha katika shairi hili. (alama 4)
      • Tashibihi-kama jehanamu
      • Maswali ya balagha-Kwa nini?
      • Takriri-nimeona –neno hili limerudiwa rudiwa
      • Taswira-Picha ya mkulima ambaye hana raha ;jasho linamwagika
    5. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi. (alama 4)
      • Mshairi anasema kwamba ingawa anamwona mkulima akitia juhudi zake aisaidie hali yake kuimarika ,anashangaa kuwa badala yake anachoona mkulima ni matatizo yake yakiongezeka.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 End Term 2 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest