0 votes
758 views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by
Mbinu za uandishi katika Mwalimu Mstaafu.

1 Answer

0 votes
by

Kuorodhesha

Mwandishi anatumia mbinu ya kuorodhesha mfano;
Uk 120: Wanafunzi waje wote hao wanafunzi wake hawamsahau kwa nasaha zake,kwa insafu yake, kwa huruma zake, kwa hekima zake, kwa ustaarabu wake, kwa uadilifu wake…
Uk 121:Wanafunzi wake waliokuwa bado wanasoma kwenye shule hiyo waliimba tele, nyimmbo za jamii mbalimbali, wakacheza zeze,mariamba, lelemama, mdundiko, violoni.
Uk 122:…sikwambii haya madude makubwa waliokuja kututisha nayo akina Bariki,Festo, Mshamba ,Nangeto na hali kadhalika.

Tabaini

Uk 124:Si matoroli,si vijiko vikubwa vya kuzola mchanga,si makubadhi ,si meza na samani aina aina, si fedha
Uk 124:Si matoroli,si vijiko vikubwa vya kuzolea mchanga,si makubadhi,si meza na samani aina aina,si fedha.

Takriri/Uradidi

Uk 126:Wanafunzi wako wote hao wanafunzi wake.
Uk 128:Jairo aliambiwa , akaambiwa na kuambiwa na wajuao.

Tashbihi

Uk 120:…mvi zimemkaa kwa haiba kama theluji kwenye mlima Kilimanjaro.
Uk 121:…walifurika kwenye kiambo cha shule kama mashabiki wa mchuano.
Uk 122:Kichwa chake chenye upana killing'aa utosini kama sufuria kwenye duka la Buniani.
Uk 125:…wakapokeza hotuba hio kama huizi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Uk 129:…kimenawiri kama ua linalotimbuka kudamu.
Uk 129:Aliona madodo yamesimama kifuani kama kanzi mbili za mwanamasumbwi.
Uk 129:…kiuno kimechukua umbo mduara kama cha nyigu.

Tashhisi

Uk 120:Alijaaliwa mvi nyeupe zilizojianika kwenye kichwa chake kidogo.

Methali

Uk 121: Anayo maneno ya kuweza kumtoa nyoka pangoni.
Uk 123: : Kuwashia pofu taa si kuharibu mafuta.
Uk 128:Alikuwa ametuma jongoo na mti wake.

Jazanda

Matumizi ya maneno yenye maana fiche.
Uk 121:…wenzao hao waliokuwa wamekua watu.
Uk 121:…lakini nadhani ni jambo la busara kutotia mchanga kitumbua.
Uk 129:Walitafuta kitabu cha maisha na kuanza kuandika kurasa mpya za maisha yao pamoja.
Uk 124:…kusubiri hadi ndio ndipo kuchuna ngozi.

Kinaya

Kinyume cha matarajio

Uk 123: Ni kinaya kwa Jairo hakuona sifa nzuri ya Mwalimu Mesi. Yeye anamuona kama kikwazo kikubwa kwake. Kama yeye Jairo anaishi maisha duni kwa sababu ya Mwalimu Mesi.
Uk 126:Ni kinaya Mwalimu Mesi kumpongeza Jairo kwa hotuba yake kumhusu ambayo ilijaa kumlaumu Mwalimu kisha Mwalimu Mesi anamueleza akifa mwanzo azungumze siku ya mazishi yake.
Uk 126:Ni kinaya Jairo anapopeleka mke wake na watoto kwa Mwalimu Mesi kama zawadi.

Uk 127:Ni kinaya kwa mkewe Mwalimu Mesi (Bi Sera)kumkaribisha mke na watoto wa Jairo kwao “Mwachie akae huyu binti na watoto wake, tutawatunza.”

Msemo

Uk 121:Wanafunzi wake wa zamani waliopewa kisogo na dunia
Uk 126:Hakuna mwanamke anayejua kumeza mate machungu.

Mdokezo/Kauli isiyokamilika

uk 120:kisa na maana ni huyo Mwalimu Mesi.
uk 123:kwamba kuwashia pofu taa si kuharibu mafuta.
UK 125:…umefanya makosa makubwa sana.
Uk 125:…hamna mwendawazimu wala mahaka kati yetu.
Uk 126: “Badala ya ngojera nyingi za huyo anayemwita si siri au siri sijui.

Sadfa(matukio mawili yanayotokea kwa pamoja).

Inasadifu kuwa baada ya Mwalimu kuondoka na kile kisichana kununua kitabu hakuonekana tena. Watu wakafikiri eti Mwalimu alikua amekioa kile kisichana.

Kumbe wakati huu Mwalimu alikua akiugua na alikua ndani(nyumbani) wakati wote huo na ndio sababu hakuonekana.

Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.3k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...