0 votes
6.6k views
in Chozi la Heri by

Tathmini umuhimu wa mbinu zifuatazo katika kuijenga riwaya ya Chozi la Heri

 • Nyimbo

1 Answer

0 votes
by
 1. Wimbo wa Shamsi unaonyesha ukengeushi,
 2. licha ya elimu aliyo nayo, Shamsi ameshindwa kukabiliana na changamoto za maisha. Anaingilia matumizi mabaya ya pombe.
 3. Unabainisha ukosefu wa uwajibikaji, badala ya kutafuta mbinu ya kukabiliana na hali duni ya maisha, analalamika kwamba wenye nguvu hawakumpa kazi walizoziahidi.
 4. Unakashifu unyakuzi wa ardhi za wanyonge. Shamba la kina Shamsi linachukuliwa na Bwana Mabavu.
 5. Unachimuza ufisadi – Bwana Mabavu anawaonyesha hati miliki bandia na kuwafukuza shambani mwao
 6. Unaendeleza maudhui ya ukoloni mamboleo – Mabavu anamiliki shamba la Baba ya Shamsi na kuwageuza kuwa maskwota.
 7. Unaangazia ukiukaji wa haki za binadamu – Shamsi na wenzake wanafutwa kazi kwa kuwazia kugoma.
 8. Inaonyesha umaskini wa familia ya Shamsi – Babake Shamsi anakufa kwa kula mizizi mwitu wenye vijaasumu
 9. Unakashifu unyonyaji wa wafanyikazi – Shamsi na wenzake wanalipwa mishahara duni.
 10. Unasawiri tatizo la matumizi mabaya ya vileo- Shamsi anaingilia ulevi baada ya kufutwa.
 11. Wimbo wa Shamsi unaoghaniwa na Ridhaa
 12. Wimbo wa majigambo unaosawiri tabia ya Shamsi – anajivunia na kusema kuwa anaogopwa kwa kutoka katika jadi tukufu.
 13. Unamfanyia tashtiti Shamsi kwa kujisifu kwa kuzua mikakati ya kukabiliana na hali ya uhitaji na hali mwenyewe ni mlevi.
 14. Unaonyesha uovu wa jamii – wauza pombe wanatia vijaasumu ili iwe tayari haraka bila kuwazia madhara ya watumia wayo.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...