0 votes
4.3k views
in Chozi la Heri by

“Vipi binadamu anavyoweza kuyazoa maji yaliyomwagika?"

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.  
 2. Taja na kufafanua tamathali ya usemi iliyotumiwa kwenye dondoo hili. 
 3. Onyesha jinsi baadhi ya wanajamii katika jumuiya ya Chozi la Heri
  walivyomwagikiwa na maji.

1 Answer

0 votes
by
 1.  
  1. Haya ni maneno ya Mwanaheri
  2. Alikuwa akiwaambia Kairu, Zohali na Umu.
  3. Walikuwa katika shule ya upili ya Tangamano.
  4. Ni baada ya wao kukutana na kusimuliana kuhusu masaibu yaliyowaleta pale.
 2.  
  1. Jazanda 
  2. Kuyazoa maji yaliyomwagika 
  3. Kurekebisha mambo yaliyoharibika au hata kwenda kombo. Hapa Mwanaheri anarejelea masaibu yaliyomfisha mamake. 
 3.  
  1. Lunga anaachwa na mkewe Naomi hali inayomletea kihoro na maradhi baadaye.
  2. Umu na nduguze wanaachwa mayatima wakati Lunga anapofariki. Hali hii inampa kijakazi Sauna upenyu wa kuisambaratisha familia hii kwa kuwatenganisha.
  3. Ridhaa anaipoteza aila yake katika kisa cha kuteketezwa isipokuwa Mwangeka aliyenusurika kwa sababu alikuwa nje ya nchi.
  4. Mwangeka kumpoteza mkewa na mwanaye katika shambulizi lililowateketeza.
  5. Zohali kutungwa mimba katika umri mdogo na kusababisha kukatizwa kwa masomo yake kwa muda na kisha kuteswa na wazazi wake.
  6. Waafrika kukatazwa na wakoloni kulima mazao yaletayo fedha huku wakilazimika kufanya vibarua. Baadhi ya vijana wa rika la Tauma wanaaga dunia baada ya kupashwa tohara.
  7. Wagonjwa kwenye hospitali za umma kukosa huduma za dawa, ukosefu wa vifaa na mwangaza kutokana na usimamizi mbaya wa hospitali. Wakazi wa Msitu wa Mamba wanaharibikiwa pale wanapofurushwa huku mazao waliyolima yakiibiwa na viongozi.
  8. Vijana barobaro wanaotumiwa na wanasiasa kuandamana, wanamiminiwa risasi vifuani na kuuawa na walinzi.
  9. Kitoto kilichookotwa na Neema kilimwagikiwa na maji pale kilipotupwa na mamake mzazi badala ya kukilea.
  10. Ridhaa kubomolewa nyumba zake kwenye mtaa wa Zari- hakupewa fidia. Wale waliowauzia ardhi hiyo haramu waliingia mitini.
  11. Lunga kufutwa kazi na mkurugenzi kwa kupinga mradi wa ununuzi wa mahindi.
  12. Lime na Mwanaheri kubakwa na genge la majabazi kadamnasi ya baba yao.
  13. Lemi kudhulumiwa na umati wa watu kwa kuchomwa moto baada ya kusingiziwa wizi wa rununu ya mwanamke mmoja.
  14. Rehema kudhulumiwa kimapenzi na mwalimu wake Fumba akiwa kidato cha tatu na kutwikwa mimba katika umri mdogo.
  15. Selume kutengwa na mumewe kwa misingi ya kikabila - mumewe anaoa mke wa kikwao.
  16. Tauma anapashwa tohara hali iliyosababisha yeye kuugua na kulazwa hospitalini.
  17. Pete anahatarisha maisha yake anapomeza vidonge vya kukiangamiza kitoto chake kilichokuwa tumboni.
  18. Mambo yanawaendea vibaya walevi wakati ambapo watu sabini wanakufa na wengine kunusurika kifo kama vile Kipanga kutokana na unywaji wa pombe haramu.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...