0 votes
1.6k views
in Kigogo by

Sitaki kazi za uchafu hapa Sagamoyo."

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.   
 2. Kwa hoja kumi na sita, onyesha jinsi kazi za uchafu zinavyoendelezwa kwenye jimbo la Sagamoyo."

1 Answer

0 votes
by
 1.  
  1. Msemaji ni Majoka .
  2. Anamwambia Ashua
  3. Walikuwa ofisini mwa Majoka
  4. Ashua alikuwa akiomba soko lifunguliwe ili wafanye biashara na wajikimu. Majoka alisema takataka za soko hilo zinaharibu sifa nzuri za jimbo lao.
 2.  
  1. Kutengeneza sumu ya nyoka
  2. Uuzaji wa pombe haramu
  3. Kushambuliwa na kujeruhiwa na vikosi vya usalama
  4. Kuuwawa kwa wapinzani kwa mfano Jabali
  5. Kunyakuliwa kwa ardhi ya soko- Majoka alitaka kujenga hoteli kwenye uwanja wa soko . Ulanguzi wa dawa za kulevya hali inayosababisha wanafunzi kufeli masomoni
  6. Kandarasi muhimu kutolewa kwa njia ya mapendeleo- Ngurumo na Asiya kupewa kandarasi ya kuoka keki za kuliwa siku ya sherehe ya uhuru .
  7. Ushauri potovu- Kenga kupanga jinsi ya kumwadhibu Sudi kwa kukataa kuchonga kinyago cha Ngao. Aidha alishiriki kupanga mashambulizi ya Tunu.
  8. Raia kutishiwa kufurushwa jimboni- Hashima anaeleza kuhusu vijikaratasi vilivyosambazwa vikiwataka wahame Sagamoyo.
  9. Bei ya bidhaa kuongezwa maradufu kwenye kioski cha kampuni
  10. Kufungwa kwa soko mahali ambapo wachuuzi na wachongaji vinyago hupata riziki
  11. Uzinifu- Majoka kumtamani sana Ashua kimapenzi ilhali ana mke. Ngurumo anahusiana kimapenzi na Asiya ambaye ni mkewe Boza.
  12. Kudhulumiwa kwa wafanyabiashara- wanasema wanatozwa kodi na kitu juu yake.
  13. Matumizi ya hila- Majoka kupanga kuwaongezea walimu na wauguzi pesa huku akipandisha kodi. Kukandamizwa kwa vyombo vya habari, kwa mfano runinga ya Mzalendo kutishiwa kufungwa baada ya kupeperusha taarifa za maandamano.
  14. Kumfungia Ashua kizuizini bila hatia.
  15. Kutishia kumfuta kazi Kingi bila kujua kazi yake imelindwa kikatiba.
  16. Majoka kutoa kibali cha kukatwa kwa miti hali inayosababisha ukame na mazao kupungua.
  17. Ubadhirifu wa mali ya umma- Majoka ana magari mengi- mkewe anafika pale kwake ofisini kisha dereva anaagizwa kumpeleka nyumbani kwa gari jingine.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...