0 votes
650 views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by
  1. Mwalimu Mstaafu- (Dumu Kayanda)
    “Hiari na mukhitari ni juu yako. Lakini yeye kafika nyumbani”. Eleza mambo makuu ambayo mwandishi anayaibua kabla na baada ya kutolewa kwa usemi huu.
  2.  Ndoto ya Mashaka- (Ali Abdulla Ali)
    Anwani "Ndoto ya Mashaka” inaakisi barabara yaliyomo kwenye hadithi. Fafanua.    

1 Answer

0 votes
by
  1.  
    1. Utu- Jamii ya Mwalimu Mstaafu kumzawadi Mwalimu Mosi alimiminiwa sifa na waliohutubu kwenye sherehe ya kumuaga.
    2. Ubaguzi-Wanyonge hawakupewa nafasi ya kuhutubu kwenye sherehe ya kumuaga Mwalimu Mosi. Aidha hawakutengewa mahali maalum pa kukaa kama wastaarabu walioketi kwenye hema.
    3. Utabaka- Kuna watu matajiri katika jamii hii. Kwa mfano, wanafunzi wa zamani wa Mwalimu Mosi wanaendesha magari ya kifahari. Kuna watu maskini walitamauka kama vile Jairo anayeingia jukwaani na mavazi yaliyochanikachanika (uk.121)
    4. Unafiki. Kati ya wale waliotoa hotuba kumhusu Mwalimu Mosi, wote walimsifia sana. Walimuona kama mtu kamilifu asiye na taksiri (uk. 126) walimuona kama Mungu.
    5. Ufisadi- Rais alipokuja kuchangisha pesa kwenye shule ya upili ya Wangwani, pesa hizo zililiwa na wakora. (uk. 122)
    6. Anasa- Jairo hunywa pombe na kulewa sana. Hata anatembea bila viatu kutokana na ulevi wake.
    7. Ubabedume/taasubi ya kiume- Mwanamke kufuata amri ya mumewe bila ya kukaidi- mkewe Jairo anakubali kutolewa kwake na kukabidhiwa Mwalimu Mosi kama zawadi pasi na kupinga. Anasema, “Ni amri ya mume. Ndivyo nilivyolelewa na kufundishwa. Sharti nimutii mume wangu.” (uk. 127) Baadaye
    8. Ushirikiano - Mkewe Jairo kujumuika pamoja na Bi. Sera katika kazi zote shambani na hata nyumbani. Walikuwa na mlahaka mwema.
    9. Utu - Mwalimu Mosi analazimika kuikimu familia ya Jairo. Kwa mfano, kuwaelimisha wanawe. 
    10. Umbeya - Watu kumwambia Jairo kuwa Mwalimu mosi alitorokea mjini na bintiye Sabina ili kumfanya mkewe (uk, 128-129). Hizi zilikuwa ni tuhuma tu kwa sababu Mwalimu Mosi alimpeleka kwenye shule ya bweni naye akarejea nyumbani anakoendelea kuuguzwa.
    11. Ukatili- Jairo kwenda kwa Mwalimu Mosi akiwa na nia ya kumuua kwa kumtorosha bintiye na kumfanya mkewe. (uk. 129-130)
  2.  
    1. Ukosefu wa lishe- makuzi ya Mashaka yalikuwa ya tikiti maji na tango ya kuponea umande (uk. 70)
    2. Mashaka kuachwa yatima baada ya mamake kufa muda mfupi baada ya yeye kuzaliwa. Vilevile, babake aliaga dunia baadaye kidogo. Ililazimu Mashaka kuielewa na Biti Kidege- mwanamke mzee, maskini na tena mgonjwa.
    3. Kushiriki katika ajira katika umri mdogo- Mashaka alifanya kazi za kibarua ili kujikimu binafsi pamoja na mlezi wake Biti Kidege.
    4. Mashaka kusoma kwa taabu hadi akamaliza chumba cha nane. Punde tu baada ya kukamilisha masoma yake ya msingi, mamake mlezi akaaga dunia.
    5. Mashaka kufungishwa ndoa ya lazima na Mzee Rubeya kwa kusubuhiana na bintiye Waridi. (uk. 74) Mzee Rubeya alifanya hivi ili kujiondolea aibu na baada ya hapo akamahia Yemeni. Hii ilikuwa ni ndoa ya kimaskini kwa sababu ilikosa harusi.
    6. Kuishi katika makazi duni- baada ya kuoana na Waridi, waliendelea kuishi kwenye chumba kile kile kibovu- paa lilikuwa ni la madebe na lilivuja wakati wa mvua.
    7. Kuishi kwenye mazingira ya uchafu- pale kwao hapakuwa na vyoo, mifereji ya maji taka ilitema uchafu wake kwenye mito na uvundo ulikirihi. Mambo yalikuwa mabaya zaidi wakati wa mafuriko. (uk. 75)
    8. Kuzaa idadi kubwa ya watoto- (watoto saba)- nafasi ya kuwahifadhi haikutosha. Binti zao walibanana na mama yao kwenye chumba hicho usiku na wavulana walilala jikoni mwa Chakupewa kama nyau.
    9. Mashaka kufanya kazi duni – alikuwa mlinzi wa usiku. Aidha hakuwa na nafsi ya kutosha kushiriki kikamilifu malezi ya watoto wao.
    10. Mshahara duni- Mashaka anasema mshahara ulikuwa ni mkia wa mbuzi (uk. 76) Haungemwezesha kununua vitu vingi.
    11. Waridi kumtoroka Mashaka- Aliondoka pasi na kuaga. Mashaka anaporejea kutoka kazini, anawakosa nyumbani na hata baada ya kuwatafuta anaambulia patupu. (uk 76)
    12. Mashaka kutamauka- Hata baada ya kuachwa na mkewe, alikuwa na matumaini kuwa mambo yangekuwa mazuri. Anasubiri hadi anakata tamaa.(uk. 79)
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...