0 votes
4.1k views
in Fasihi by
Zitaje changamoto zozote tano za miviga katika jamii yoyote ile.

1 Answer

0 votes
by
  1. Vifo- upashaji tohara kwa vijana unaweza kusababisha uvujaji wa damu nyingi na mwishowe vifo.
  2. Kusababisha magonjwa hatari ya kuambukiza mfano kupitia tohara
  3. Husababisha hofu miongoni mwa sehemu ya jamii kwa mfano katika sherehe za kufukuza mapepo.
  4. Baadhi huweza kukiuka haki za binadamu mfano tohara kwa wasichana.
  5. Baadhi huharibu mazingira- sherehe zinazohusu utoaji wa kelele mfano nyimbo mbalimbali zikiimbiwa mahali pasipofaa, zinaweza kusababisha kelele ambayo itachafua mazingira hayo.
  6. Kukinzana na malengo ya kitaifa na kidini mfano tohara kwa wasichana ni marufuku nchini. Shughuli ya maapizo huenda kinyume na mafundisho ya kidini. nk.
  7. Hugharimu pesa na raslimali nyingi mfano harusi
  8. Baadhi huhusisha imani za kishirikina ambazo zinaweza kuleta uhasama katika jamii. Mfano maapizo.

Related questions

0 votes
0 answers
asked Mar 16, 2022 in Fasihi by Judevasang
0 votes
1 answer
0 votes
2 answers
0 votes
1 answer
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

5.7k questions

7.4k answers

6 comments

590 users

...