0 votes
1.2k views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by
recategorized by
  1. "Naomba radhi mfawidhi ... lakini nadhani ni jambo la busara kutokitia mchanga kitumbua .. . "
    • Eleza muktadha wa dondoo hili .      
    • Bainisha toni ya dondoo hili.           
    • Kwa kurejelea hadithi hii jadili kwa kutoa hoja kumi namna mhusika Jairo alivyokitia kitumbua mchanga.
  2. Bainisha vipengele vya kimtindo katika dondoo lifuatalo: 
    "Alijaaliwa mvi nyeupe zilizojianika kwenye kichwa chake kidogo kilichosimama jadidi kwenye shingo yake nyembamba. Alijaaliwa mvi kwa vile zilikuja mapema wakati akiwa bado ana umri wa miaka thelathini. Watu wakasema hekima hiyo kutabasuri huko. Kwa hiyo, hakujisumbua kujipaka rangi nyeusi kuung'ang'ania ujana uliotishia kumwondoka mapema ... mvi zimemkaa kwa haiba kama theluji ... "

1 Answer

0 votes
by
edited by
  1.  
    •   
      • Mzungumzaji ni Mwalimu Mustaafu, Mosi.
      • Anazungumza na hadhira ambayo imekuja kumuaga/mfawidhi
      • Yuko shuleni
      • Mwalimu mstaafu aligundua baadhi ya wasemaji walibaguliwa.
    •  
      • Toni ya kuonya  kutahadharisha - si vizuri kukitia kitumbua mchanga
      • kunyenyekea/unyenyekevu - Naomba/upole
      • Masikitio/huzuni.
      • Kejeli
        (dondoo limetolewa uk.121)
    •  
      • Kuwadhalilisha wenzake kama vile Baraka, Festo mshamba na Nangeto anapoonyesha hali yao mbaya ya awali.
      • Kufichua njama za kifisadi- anasema pesa zilizochangishwa na rais zililiwa na wakora kama vile akina Festo
      • Anapewa nafasi na Mwalimu Mosi kuhutubu lakini anamuaibisha anasema anafurahia kuondoka kwa Mwalimu Mosi
      • Kutotambua mchango wa Mwalimu Mosi -anasema Mosi ataondoka shule ipumzike
      • Anashindwa kustahimili changamoto shuleni. Kim hasomi-uzumbukuku k.m Kim kufeli mtihani.
      • Anajidhalilisha kwa kusifia suala kama vile utapeli na wizi, hajiamini -  anajiita zumbukuku asiyeweza kuimarika.
      • Anakosa kuyawajibikia maisha yake. Analaumu Mwalimu Mosi anasema umaskini uwake ulisababishawa na Mwalimu Mstaafu/Kukatazwa kunywa pombe
      • Anakosa kuwajibikia familia yake. Hatekelezi majukumu yake kama mume na mzazi.
      • Kutelekeza familia- hakuwahi kupita kwa Mwalimu Mosi kuwajulia hali wanafamilia wake. (uk. 128)
      • Kumharibia Mwalimu jina kwa kusema kuwa amekioa kitoto chake (uk. 130)
      • Jairo kutaka kujiua kujinyonga /kitanzi/kujitosa majini.
  2.  
    • Taswira-uoni-nyeupe, nyembamba
    • Tashihisi-mvi kujianika
    • Takriri/urudiaji-Alijaaliwa mvi
    • Tashbihi-kama theluji
    • Taashira-mvi-ishara ya hekima
    • Kinaya-mvi kuashiria busara- kujaliwa mvi mapema
    • Usimulizi - Kifungu chote ni usimulizi
    • Chuku/udamisi-mvi kujianika
    • Mdokezo-kama theluji...
      (dondoo limetolewa uk.120)   
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...