0 votes
1.5k views
in Chozi la Heri by

“Dada Umu, Di, ni mimi, Ni ndugu yenu. Ni hai . Auntie Sauna alishikwa na polisi.”

  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. 
  2. Fafanua sifa tatu za msemaji 
  3. Taja tamathali moja iliyotumika katika dondoo. 
  4. Kwa nini Auntie Sauna alishikwa na polisi? Eleza kikamilifu. 

1 Answer

0 votes
by
  1. Maneno haya yalisemwa na Mwaliko.Alikuwa akiwaambia Umulkheri na Dick . Tendio hili lilitukia katika mkahawa na Mjaliwa walipokutana kisadfa. Hii ni baada ya mwaliko kumepeleka babakemlezi maeneo yale kusheherekea siku ya kuzaliwa kwake.
  2.  
    1. Mwenye maadili mema, Mwaliko alipolelewa mwangemi na Neema aliinuka kuwa ghulamu ya hali ya juu akiwaheshimu wazazi na majirani na kuwatii wazazi.
    2. Mwenye shukrani- Mwaliko aliamua kumnunulia babake chakula cha mchana siku yake ya kuzaliwa kwenye hoteli ya Majaliwa .
    3. Mwenye bidii- Alifanya bidii masomoni hadi kufikia chuo kikuu . Alisajili kwa shahada ya uzamili katika taaluma ya mawasiliano na kuhitimu . Mwaliko anafanya kazi yake kwa bidii ya mchwa.
  3. Kuchangaya ndimi –Auntie
  4. Baada ya Umu kupiga ripoti kwenye kituo cha polisi kuwa nduguze wanuna wamepotea, polisi walifanya uchunguzia wao na kujua kuwa walitekwa nyara. Aliyetekelea kitendo hiki ni kijakazi Sauna . Sauna alikuwa akimfanyia biashara Bi Kangara. Polisi walipojua mahali alikokuwa akijificha Bi Kangara, walishika jia hadi nyumbani kwake ambako waliwatia mbaroni. Bi Kangara na Sauna Walifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la ukiukaji wa haki za watoto hivyo basi wakafungwa miaka saba gerezani na kazi ngumu.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...