0 votes
4.1k views
in Fasihi by
Taja aina za watendaji katika fasihi simulizi.

2 Answers

0 votes
by

Wahusika ni viumbe wa sanaa ambao hutumiwa katika kazi ya fasihi kuwasilisha maswala mbalimbali.

  • Fanani-anayetunga na kuwasilisha fasihi simulizi. 
  • Hadhira-kusikiliza, kutazama, kushiriki wa kuimba, kuuliza maswali, kutegua vitendawili, kupiga makofi, n.k. kuna aina mbili za hadhira: (i) hadhira tendi/hai na (ii) hadhira tuli.
  • Wanyama-wanaofanya kama binadamu na kuwakilisha sifa kama vile ujanja, ulaghai, tamaa na ujinga na wanaobakia wanyama tu. 
  • Binadamu 
  • Mazimwi na majitu-viumbe vyenye matendo na maumbile ya kutisha kama vile jicho moja, vichwa viwili au zaidi, nusu mtu na nusu myama, wenye tamaa iliyokithiri ya kuweza kumeza kila kitu, kuhifadhi na kutunza binadamu ananyoyapendeza. 
  • Wahusika vitu (visivyo na uhai) mawe, miti, vijaluba, vibuyu-hutumiwa kuibua imani za kidini. 
  • Mizimu-roho za waliokufa-hutembea, hula na huathiri binadamu. 
  • Miungu-viumbe vyenye uwezo mkubwa dhidi ya binadamu k.m. katika mighani na visasili.
0 votes
by
Mtambaji Ni wa hadithi
Mhenga Ni wa semi
Manju Ni wa nyimbo
Malenga Ni wa shairi
Mlumbi Ni wa mazungumzo
Msanii Ni wa maigizo

Related questions

0 votes
3 answers
0 votes
2 answers
asked Aug 21, 2023 in Fasihi by 0746074XXX
0 votes
0 answers
asked Dec 29, 2023 in Fasihi by 0794158XXX
0 votes
1 answer
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...