Wednesday, 05 July 2023 13:22

Kiswahili Questions and Answers - KCPE 2023 Prediction Papers Set 1

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa

Kila mzalendo wa nchi yetu hii tukufu, ___1___   ____ 2___ mashine ___3___  huwa na kazi ___4___ kufanya. ___5___
mzalendo mmoja atashindwa kutekeleza jukumu ____6___ ,wengine___7___. Ni muhimu mzalendo kuitunza nchi yake asije akaishia ___8____ atakapopata shughuli zake zimekwama.

   A   B   C   D 
 1.   mfano   zaidi   kama   sawa 
 2.  iliyo  ilivyo   ilipo   iliko 
 3.  :  ,  ;  __
 4.  inayohitajika   anayohitajika   wanaohitajika   zinazohitajika 
 5.  Maadamu  Ingawa  Ikiwa  Angalau 
 6.  aliyotengewa  alilotengewa   zilizotengewa   ilivyotengewa 
 7.  wataathiriana  wataathirikia   wataathiria   wataathiriwa 
 8.  kujikwaa ulimi   kujifia kikondoo   kujitia shemere   kujiuma kidole 


Sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa dada yangu ___9___. Tuliamka alfajiri na mapema ___10___. Tulikuwa na hamu kuu ya kuona binamu na bintiamu wetu wa toka nitoke yaani; ___11___ wetu. Baada ya kupata kisebeho, ___12___ kuelekea sokoni ___13___ tulinunua mboga za kila aina. Si mchicha, si kabeji, si ___14___ sukumawiki ___15___ alimradi tulikuwa na vingi vya kununua.

   A   B   C   D 
 9.   itakuwa ikiwadia   ikiwa iliwadia   ikawa inawadia   ilikuwa imewadia 
 10.   kuzitayarisha  kuwatayarisha   kujitayarisha   kupatayarisha 
 11.  wakoi  wanuna   masomo   maumbu 
 12.  tulishika zamu  tulishika kani  tulishika usukani   tulishika tariki 
 13.  ambayo  ambako   ambalo  ambao
 14.  mtungo wa  tita la  kicha cha  chane ya 
 15.  ___  ...  !  :


Kutoka swali la 16 - 30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Kanusha
    Mtamba aliyenunuliwa jana ameuzwa tena.
    1. Mtamba aliyenunuliwa jana hakuuzwa tena.
    2. Mtamba ambaye hakununuliwa jana hakuuzwa tena.
    3. Mtamba hakununuliwa wala hakuunzwa tena.
    4. Mtamba aliyenunuliwa jana hajauzwa tena.
  2. Neno 'mtakimbiliana' lina silabi ngapi?
    1. 7
    2. 13
    3. 6
    4. 8
  3. Ni maelezo yapi yaliyo sahihi?
    1. Mloto ni mshororo wa pili katika ubeti wa shairi.
    2. Tarbia ni mashairi yenye beti nne
    3. Ngonjera ni shairi linalozungumzia historia ya mtu fulani.
    4. Mwandamizi ni kipande cha pili katika mshororo wa shairi.
  4. Ipi ni nomino nadhania?
    1. Kionjamchuzi.
    2. Kikosi.
    3. Uhodari.
    4. Mchanga.
  5. Sentensi: "Nyumbani mwao mlishiba watu na kuwatapika wengine nje", imetumia tamathali gani za usemi?
    1. Tashhisi, chuku.
    2. Tashbihi, kinaya.
    3. Sitiari, nahau.
    4. Sitiari, chuku.
  6. Andika wingi wa
    Wakala alikutatulia shida uliyokuwa nayo
    1. Nyakala waliwatatulia shida mlizokuwa nazo.
    2. Wakala waliwatatulia shida mlizokuwa nazo.
    3. Mawakala waliwatatulia shida mlizokuwa nazo.
    4. Mawakala walimtatulia shida mlizokuwa nazo.
  7. Chagua sentensi yenye kiwakilishi halisi
    1. Watu wale walieleza haja zao ila wanyonge ndio waliosaidiwa kwanza.
    2. Vijana hodari walipongezwa lakini wengine walikashifiwa.
    3. Daktari alimtibu mgonjwa wa kwanza lakini yule wa pili hakutibiwa.
    4. Tulitembea mjini kwa uangalifu ila mmoja wetu aliteleza na kuanguka.
  8. Ni nini maana ya kujipalia makaa ni?
    1. Kujiletea jambo
    2. Kujiwekea makaa
    3. Kujiletea madhara
    4. Kujisababishia jambo.
  9. Kitita ni kwa pesa. Tano ni kwa ______________________________
    1. funguo
    2. ndizi
    3. chokaa
    4. ngozi.
  10. Kucha ni kwa binadamu, mapezi ni kwa
    1. ndege
    2. wanyama
    3. wadudu
    4. samaki.
  11. Chagua jibu lenye kivumishi kilichoundwa kutokana na kitenzi
    1. Mpishi - mapishi. 
    2. Babaika - babaifu
    3. Angaza - mwanga
    4. Samehe - msamaha.
  12. Ni senteni ipi ambayo imetumia 'kwa' ya kuonyesha sababu ya jambo fulani kutokea? 
    1. Mwanafunzi amemwamkua mzazi wake kwa heshima.
    2. Mwalimu alimtuza alama nane kwa kumi.
    3. Wazee kwa vijana walipinga mswada huo wa fedha.
    4. Mkimbizi alituzwa kwa kushinda mbio hizo.
  13. Ni sentensi ipi inayoonyesha hali ya kutegemea?
    1. Msaidieni kuuinua dawati hilo.
    2. Mwalimu akija atawapeleka uwanjani.
    3. Mulika alisikiliza ushauri akaokoka.
    4. Changarawe ambayo ilisombwa iliuzwa.
  14. Chagua sentensi sahihi
    1. Alifua samaki wengi.
    2. Alifua samaki nyingi.
    3. Alivua samaki wengi.
    4. Alivua samaki nyingi.
  15. Chagua kihusishi katika sentensi hii Najua tofauti baina ya mazingira na mazingara.
    1. najua
    2. na mazingara
    3. tofauti
    4. baina ya

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 - 40.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumeshuhudiwa mabadiliko makubwa ya kijamii katika taifa letu. Miongoni mwa mabadiliko hayo ni kule kuendelea kwa taifa kuwa changa. Hii ina maana kuwa wananchi vijana walio na miaka chini ya thelathini na mitano ni wengi zaidi ya wale wenye umri mkubwa kuliko huo. Kwa sababu ya juhudi kubwa ya serikali, kufikia takriban miaka thelathini na mitano iliyopita, mbinu ya kujua kusoma na kuandika huchukuliwa kuwa kitu cha kawaida kama vile kuvaa nguo.

Tukitupa macho nyuma kabla ya utawala wa kikoloni kuingia huku kwetu yapata karne moja tu iliyopita, tutaona kuwa hali ilikuwa tofauti kabisa. Jumuiya zilizoishi katika sehemu ya bara hazikuwa zimeona wala kusikia mtu akiandika wala kusoma. Angetokea mtu awasomee makala wangemwona kama mwehu anayeboboka ovyo, kwani hicho kilikuwa kioja kikubwa.

Jumuiya za pwani zilikuwa na hali tofauti. Karne kadhaa hapo awali, wananchi hawa walikuwa wametembelewa na Waarabu kwa sababu ya kufanya biashara na kuwahubiria dini ya Kiislamu. Maingiliano haya yaliwanufaisha wananchi kwa njia ambayo labda haikukusudiwa. Walipata ujuzi wa kusoma na kuandika hati ya kiarabu ili waweze kusoma Koran katika lugha ya Kiarabu. Baadaye walitumia hati hiyo kuandika lugha zao za kienyeji. Maandishi mengi yalikuwa na lengo la kuhifadhi mafunzo ya dini ya Kiislamu.

Tukizingatia wazo hili la kuzichunguza baadhi ya jumuiya zilizoishi bara, tutaona kuwa zilikuwa na aina ya uandishi. Katika jumuiya mojawapo, kwa mfano, mgeni aliposema angekuja kutembea baada ya siku kumi, wenyeji wake walichukua ukambaa. Wakatengeneza mafundo kumi. Kila fundo liliwakilisha siku moja. Kila kulipokucha waliondoa fundo moja, mpaka fundo la kumi. Hii ikiwa njia mahususi ya kuhifadhi habari na ililingana na ile ya kuandika. Tunaweza kusema kuwa ilikuwa Wakoloni hawakuwa na mfumo mpya, labda kufikia sasa jumuiya hiyo ingekuwa imevumbua njia nyingine ya uandishi

  1. Kwa nini taifa letu linaweza kuitwa changa?
    1. Halikui kwa sababu ya vijana wengi.
    2. Kwa sababu si la zamani sana.
    3. Hakuna wananchi wenye umri mkubwa. 
    4. Idadi kubwa ya wananchi ni vijana.
  2. Watu wengi nchini wanajua kusoma na kuandika kwa sababu
    1. kumekuwa na utulivu nchini.
    2. wananchi wanaona faida ya kujua kusoma na kuandika.
    3. wananchi wenyewe wamefanya bidii.
    4. kumekuwa na mpango uliotekelezwa kwa miaka thelathini na mitano.
  3. Kwa mujibu wa taarifa hii, neno jingine lenyenmaana sawa na mbinu ni
    1. mafunzo
    2. wazo
    3. stadi
    4. hati.
  4. Ukoloni uliingia lini huku kwetu? 
    1. Miaka mia mbili iliyopita.
    2. Karibu miaka mia moja iliyopita.
    3. Karibu miaka hamsini iliyopita. 
    4. Miaka mia tatu iliyopita.
  5. Ni nini maana ya neno kioja?
    1. Ghasia.
    2. Ajabu.
    3. Maarifa.
    4. Wendawazimu.
  6. Ujuzi wa kusoma na kuandika ulifika pwani
    1. wakati wa kuingia kwa ukoloni
    2. muda mrefu kabla ya ukoloni
    3. muda mfupi baada ya ukoloni
    4. muda mrefu baada ya ukoloni.
  7. Chagua kifungu kilicho sahihi zaidi kukamilisha sentensi hii:
    Wenyeji wa pwani walitumia hati ya Kiarabu
    1. kusomea na kuandikia Koran na lugha zao.
    2. kusomea na kuandikia Kiarabu na lugha zao.
    3. kusomea na kuandikia Kiarabu.
    4. kusomea na kuandikia Kiswahili.
  8. Shabaha kuu ya kuandika wakati huo wa zamani ilikuwa
    1. kuhifadhi mafunzo ya dini za wenyeji
    2. kuendeleza lugha ya Kiarabu
    3. kuendeleza hati ya Kiarabu
    4. kuhifadhi mafunzo ya Kiislamu.
  9. Chagua jibu lililo sahihi zaidi
    Mwandishi analinganisha kuandika na kule kutengeneza mafundo kwa sababu
    1. shughuli zote mbili zilifanywa kwa mikono
    2. shughuli zote mbili zilikuwa zikifanywa kwa wakati mmoja
    3. shughuli zote mbili zilikuwa na lengo la kuhifadhi habari
    4. shughuli zote :nbili zilifanywa na wataalamu.
  10. Katika aya ya mwisho, maoni ya mwandishi ni
    1. kuja kwa Wakoloni kulibadilisha utaratibu bora wa uandishi
    2. kuja kwa Wakoloni kulibadilisha matumizi ya mafundo
    3. kuja kwa Wakoloni kuliendeleza njia ya uandishi
    4. kuja kwa Wakoloni kuliendeleza matumizi ya mafundo.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 - 50.

Baada ya uhuru, Kenya ilihitaji kuikweza lugha moja ya kiasili kuwa lugha ya taifa. Wakenya hawakutaka kuitumia lugha ya Kiingereza kama lugha ya taifa. Hii ilionekana kuwa lugha ya kikoloni na kigeni. Hali ya kuwepo lugha nyingi nchini ilitatiza uchaguzi wa lugha moja. Kila kabila lilitarajia lugha yake kuchaguliwa, jambo ambalo lilikuwa gumu. Kuchagua Kiingereza hakungefaa kwani, mbali na wasomi, raia wengi hawakukijua. Hata sasa wananchi wengi bado hawajakimudu.

Serikali ilishughulikia suala hili la uteuzi. Hatimaye, Kiswahili kilitunukiwa hadhi ya kuchaguliwa. Kama lugha ya taifa, Kiswhili hutumika katika maongezi ya kawaida, mawasiliano ya kibiashara na kadhalika. Kiswahili kilichaguliwa kwa sababu kadhaa. Kwanza, baadhi ya wasomi walifikiria kuwa lugha hii ilikuwa na asili ya Kiarabu. Kwa sababu hii walifikiria kuwa, Kiswahili hakikuwa lugha ya kabila lolote. Pili, wengine waliamini kwamba Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha za kiafrika. Hivyo kingekubaliwa na makabila yote. Hata hivyo, wasomi wengine walishikilia kuwa hii ilikuwa ni lugha ya Kiafrika asilia bila mchanganyiko wowote.

Hivi leo hakuna ubishi wowote kuhusu asili ya Kiswahili. Hii ina maana kuwa Kiswahili kimekubalika kama lugha ya kiasili Afrika Mashariki. Pia ni kitambulisho cha utaifa wa nchi kama Kenya na Tanzania. Isitoshe, Kiswahili ni lugha mojawapo ya lugha za taifa nchini Kongo, Burundi na Rwanda.

  1. Ni nini kilichotatiza uchanguzi wa lugha ya taifa?
    1. Wakenya hawakutaka kuchagua lugha ya kikoloni.
    2. Makabila na lugha nyingi nchini Kenya.
    3. Hakukuwa na lugha maalum ya kiasili ambayo ingechaguliwa.
    4. Wakenya walijua lugha nyingi tofauti.
  2. Kwa nini haingefaa kuchagua Kiingereza? 
    1. Ilikuwa lugha ya wasomi na raia.
    2. Ilionekana kama lugha ngumu isiyoweza kueleweka.
    3. Si watu wengi walioweza kukiongea.
    4. Wenyeji walichukia wageni na lugha yao.
  3. Kulingana na taarifa, lugha ya taifa hutumika vipi nchini Kenya?
    1. Katika mawasiliano ya siasa na shughuli rasmi.
    2. Katika maongezi na mawasiliano ya serikali.
    3. Katika mawasiliano ya kawaida, biashara, siasa na dini.
    4. Katika maongezi ya kawaida na dini.
  4. Kwa nini Kiswahili kilichaguliwa hatimaye kuwa lugha ya taifa?
    1. Kwa sababu kilifikiriwa kuwa si lugha ya kundi lolote.
    2. Kwa sababu kilitumika kwingi barani Afrika.
    3. Kwa sababu uamuzi huo ulitolewa na wasomi.
    4. Kwa sababu kilifikiriwa tu kuwa ni lugha ya Kiarabu.
  5. Maana ya neno hatimaye ni
    1. mwishowe
    2. aghalabu
    3. tena
    4. mwanzoni.
  6. Uliposoma habari hii ulipata jumla ya maoni mangapi juu ya asili ya Kiswahili?
    1. Manne.
    2. Moja.
    3. Matatu.
    4. Mawili.
  7. Maana ya neno hadhi kama lilivyotumika katika kifungu ni
    1. ubora
    2. staha
    3. zawadi
    4. umaarufu.
  8. Lugha ya taifa nchini ni muhimu kwa kuwa 
    1. inapendwa na wananchi wote
    2. hutumika na watu wengi
    3. huimarisha amani na nchi jirani
    4. ni kitambulisho cha utaifa.
  9. Maana ya hakuna ubishi wowote ni
    1. hakuna kukubaliana tena
    2. hakuna jambo lisilo wazi
    3. hakuna jambo la kujadiliana
    4. hakuna pingamizi zozote.
  10. "Kiswahili ni lugha mojawapo ya lugha za taifa' inamaanisha
    1. ndiyo lugha pekee ya taifa
    2. ni lugha ya kimataifa
    3. ni lugha ya kiasili
    4. kuna lugha nyinginezo za taifa.

INSHA

Mwandikie rafiki yako barua huku ukimweleza namna ambavyo utatumia wakati wako wa likizo ili kujinufaisha.

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. B
  4. B
  5. C
  6. B
  7. D
  8. D
  9. D
  10. C
  11. A
  12. D
  13. B
  14. C
  15. B
  16. D
  17. A
  18. A
  19. C
  20. A
  21. C
  22. B
  23. C
  24. C
  25. D
  26. B
  27. D
  28. B
  29. C
  30. D
  31. D
  32. D
  33. C
  34. B
  35. B
  36. C
  37. A
  38. D
  39. C
  40. C
  41. B
  42. C
  43. C
  44. A
  45. A
  46. C
  47. B
  48. D
  49. D
  50. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - KCPE 2023 Prediction Papers Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students