Thursday, 13 July 2023 09:58

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 2 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 hadi 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua lifaalo zaidi.

Mawasiliano ni sekta mojawapo __1__hatua sana __2__ kuvumbuliwa kwa teknolojia mpya. Siku hizi hata __3__ wanaohifadhi faili na kupokea simu ofisini wamepunguzwa. Ulimwengu umekuwa duara __4__ tu __5__ habari huweza kuenea __6__ katika muda mfupi sana. __7__, hakuna kizuri kisicho na dosari. Watu wenye __8__ mbaya wanatumia fursa hiyo kusambaza uvumi. Wengine husambaza picha zisizofaa __9__. Tusipochukua tahadhari tutaishia kujiuma kidole kwani
__10__.

   A   B   C   D 
 1.   zilizopiga   yaliyopiga   tulizopiga   iliyopiga 
 2.  hadi  tangu   kuliko   kama
 3.  matarishi  masogora   wahazili  mabawabu 
 4.  ndogo  dogo0     kidogo   mdogo
 5.  ingawa  mathalani   lau   madhali 
 6.  zote  kote   yote  lote 
 7.  Labda  Vilevile   Hata hivyo   Isitoshe 
 8.  nia  lengo  madhumuni   kusudi
 9.  redioni  magazetini   dunaini  mitandaoni
 10.   baada ya dhiki ni faraja    majuto ni mjukuu   mstahimilivu hula mbivu    dalili ya mvua ni mawingu 


Tangu siku zake za ujanani, Kiburi hakujua maana ya jirani __11__ siku moja __12__ na ya kumfika. Alikuwa __13__ watu ambao waliamini kuwa wakipatwa na __14__ ndugu atawasaidia. Alisahau kuwa __15__.

   A   B   C   D 
 11.   mpaka   baada ya   kisha   hadi 
 12.  alipofikia   alipofikwa   alifikiwa   alifikwa 
 13.  miongoni ya   katikati ya   kati ya   baina ya  
 14.  siha  adhabu   maarubu   adha 
 15.    fimbo ya mbali haiui nyoka   mtegemea cha nduguye hufa maskini   heri nusu shari kuliko shari kamili   akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki

 

Kutoka swali la 16 hadi 30 jibu kulingana na maagizo.

  1. Neno mwanahewa lina silabi ngapi?
    1. Tisa
    2. Tano
    3. Nne
    4. Nane
  2. Genge ni kundi la watu linalofanya kazi pamoja ilhali kenge ni;
    1. ndege mwenye sura kama ya paka
    2. mnyama wa porini afananaye na mbuzi
    3. samaki afananaye na nyoka
    4. mnyama kama mamba mdogo
  3. Ikiwa jana ilikuwa Alhamisi, mtondo ilikuwa;
    1. Jumatatu
    2. Jumapili
    3. Jumatano
    4. Jumanne
  4. Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
    Mama: Mwanangu, utanyolewa kesho jioni.
    1. Mama alimwambia mwanangu angenyolewa kesho jioni
    2. Mama akamwambia mwanawe atanyolewa siku iliyofuata jioni.
    3. Mama alimwambia mwanawe kuwa angenyolewa siku iliyofuata jioni.
    4. Mama alimwuliza mwanawe kama atanyolewa kesho.
  5. Joka la indimu ni kwa inda ilhali mkono wazi ni kwa;
    1. ukarimu
    2. uchoyo
    3. ujanja
    4. uvivu
  6. Ni maelezo yapi sahihi?
    1. Tathlitha ni shairi lenye mishororo minne kila ubeti.
    2. Ngonjera ni shairi la historia.
    3. Malenga hutunga mashairi na nyimbo.
    4. Tarbia ni shairi lenye mishororo miwili kila ubeti.
  7. Ki imetumiwaje katika sentensi? Mwalimu alipoingia tulikuwa kukiimba.
    1. Kuonyesha udogo.
    2. Kuonyesha kuendelea kwa kitendo. 
    3. Kuonyesha masharti.
    4. Kuonyesha namna.
  8. Miongoni mwa sehemu hizi za mwili, ni ipi iliyo tofauti na nyingine?
    1. Pafu
    2. Paja
    3. Kiganja
    4. Goti.
  9. Ni methali ipi yenye maana sawa na 'usiache mbachao kwa msala upitao'?
    1. Usione kwenda mbele kurudi nyuma kazi.
    2. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
    3. Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.
    4. Bura yangu sibadili na rehani.
  10. Tambua maneno yaliyopigwa kistari. Mwalimu mgeni atajiunga nasi mwakani.
    1. Kielezi, kihusishi
    2. Kivumishi, kiunganishi
    3. Kivumishi, kielezi
    4. Kiwakilishi, kivumishi.
  11. Ni jina lipi la makundi lisilofaa?
    1. Bunda la nyuki.
    2. Shehena ya mzigo.
    3. Chane ya ndizi.
    4. Kilinge cha wachawi.
  12. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo.
    Karani na wifi walifika jana.
    1. Makarani na wifi walifika jana.
    2. Karani na mawifi walifika jana. 
    3. Makarani na mawifi walifika jana. 
    4. Akina Karani na wifi walifika jana.
  13. Ni sentensi gani iliyotumia kwa kuonyesha sababu?
    1. Amekula wali kwa mchuzi.
    2. Alifurahi kwa kufikia utu uzima.
    3. Tatu kwa tano ya wanafunzi ni wavulana.
    4. Maria ataenda kwa shangazi yake kesho.
  14. Ni nomino zipi zilizo katika ngeli ya I-I?
    1. Maji, marashi
    2. Meza, dawati
    3. Mkate, maembe
    4. Mvua, chumvi
  15. Ni nahau ipi yenye maana ya kupata taabu au shida?
    1. Kula mwata
    2. Kata kamba
    3. Piga mbiu
    4. Laza damu.

Soma kifungui kifuatayo kisha ujibu maswali 31 hadi 40.

Subira alikuwa barobaro ambaye hakujimudu kimasomo. Alikuwa kisubutu masomoni. Hata hivyo, alijaliwa kipawa katika riadha. Alionekana kila asubuhi akifanya mazoezi ya kukimbia. Wapo waliomhurumia kuwa huenda hakuwa na akili razini. Weng walisikika wakisema alikuwa akiadhibiwa na Mungu. Akiwa mkembe walidai kuwa alitumwa na nyanya yake gulioni lakini akakataa.

Watu wengi walijisaili mbona akaanza kukimbia miaka mitano baada ya nyanya yake kutembelewa na Izraili wa kaputi. Baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, Subira alianza kushiriki katika mashindano mbalimbali. Aliposhiriki mara ya kwanza, alishika nanga licha ya mazoezi ya bidii nyingi.

Aliendelea kufanya mazoezi pasi na kwenda nguu. Alivyozidi kujitahidi katika mazoezi ndivyo wengi walivyoendelea kumbeza. Hakubwaga silaha kamwe. Aliamini lisani ya wahenga isemayo kuwa atafutaye hachoki na akichoka keshapata. Mwaka uliofuata akiwa na umri wa miaka kumi na sita alishiriki tena katika mbio za masafa marefu. Alipata mwamko mpya alipofahamu kuwa ingawa hakushinda hali yake ilizidi kuimarika.

Alizidi kujiongeza maarifa. Akawa na matumaini kama tai kuwa siku moja angeibuka kifua mbele. Nusu mwaka baadaye, Subira alichaguliwa kuwa miongoni mwa wawakilishi wa nchi yao katika mbio za masafa marefu duniani. Huo ukawa ndio mwanzo mkoko unaalika maua. Nyota yake ikaanza kung'aa na mambo yakaanza kumwendea mserego. Aliamini lisani ya wahenga isemayo kuwa papo kwa papo kamba hukata jiwe.

Ulimwengu mzima ulishuhudia Subira akinyakua nishani ya dhahabu katika michezo hiyo duniani. Subira aliyekuwa akidhalilishwa na kupakwa tope akawa anasifika kote. Jina lake likawa kibwagizo midomono mwa wengi. Miaka michache baadaye akawa tajiri wa kutajika. Waliomcheka wakakosa pa kuziweka nyuso zao. Walipata funzo kuwa dhamira ni dira na nia zikiwa pamoja, kilicho mbali huja karibu.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, ni kweli kusema kuwa;
    1. Subira alikuwa wembe shuleni
    2. Subira alifanya mazoezi ya kukimbia machweo
    3. Subira alihurumiwa na wanakijiji wote
    4. Subira hakujiweza sana masomoni
  2. Baadhi ya wakazi walisema kuwa Subira alikuwa akiadhibiwa kwa sababu;
    1. hakuwa na akili timamu
    2. akiwa mdogo alitumwa na bibi yake lakini akakataa
    3. hakuwa mcha Mungu
    4. mienendo yake haikuvutia
  3. Neno gulioni lina maana gani kulingana na kifungu?
    1. Sokoni
    2. Dukani
    3. Mtoni
    4. Shambani
  4. Ni methali ipi mwafaka kuelezea tabia za Subira baada ya kushindwa katika jaribio la kwanza?
    1. Mbio za sakafuni huishia ukingoni
    2. Asiyekujua hakuthamini.
    3. Kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi.
    4. Mtegemea nundu haachi kunona.
  5. Ni nini maana ya alishika nanga kulingana na kifungu?
    1. Alipoteza matumaini
    2. Alikuwa wa mwisho.
    3. Alibadili nia.
    4. Alikuwa wa kwanza.
  6. Kushinda kwa Subira hatimaye kulitokana na;
    1. ujuzi, bidii na tamaa
    2. umri, ujana na utepetevu
    3. laana, maarifa na bidii
    4. bidii, ulegevu na ujuzi.
  7. "Akawa na matumaini kama tai." Hii ni mfano wa fani ipi ya lugha?
    1. Kinaya
    2. Chuku
    3. Istiara
    4. Tashbihi.
  8. Subira alikuwa akishiriki michezo katika dunia nzima. Hii inamaanisha alikuwa;
    1. hadhi yake ya kimichezo ilipanda 
    2. mtalii wa kutembelea mataifa
    3. mweledi wa kusafiri miji mikubwa
    4. mpenda anasa za dunia.
  9. Ni nini maana ya kupakwa tope kulingana na kifungu?
    1. Kutegemewa
    2. Kuharibiwa jina
    3. kuaibishwa
    4. kuchukizwa.
  10. Kichwa kinachofaa kifungu hiki ni kipi?
    1. Juhudi si pato.
    2. Tusiwe wa kutegemea wengine.
    3. Uvumilivu hutamausha maishani.
    4. Tusikate tamaa.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 hadi 50.

Kila mwanadamu ameumbwa akiwa na uwezo wake maalum. Mungu alifanya hivyo makusudi kabisa. Hebu fikira ulimwengu wenye watu ambao kila mmoja anajitosheleza. Yaani kila mtu anaweza kujifanyia kila kitu apendavyo. Ulimwengu usingehitaji watu wanaosomea kazi mbalimbali wala watu wasingetegemeana. Upendo na huruma vingekuwa havipo dunaini.

Mungu aliwaumba watu na vipawa vyao mbalimbali. Hata wanaofikiriwa kuwa hawana vipawa, ukiwachunguza vizuri utaona kuwa wana upekee fulani katika jambo wanalolimudu vizuri. Wakati mwingine, sio lazima jambo hilo liwe kubwa sana kiasi cha watu kulizungumzia. Kuna watu wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi lakini waliobarikiwa kwa uwezo wa kuzungumza vizuri au uwezo wa kuwashauri wengine wenye mahitaji mbalimbali. Hili linatukumbusha kuwa hata vipawa tunavyofikiri kuwa si vikubwa vina thamani kubwa ajabu.

Ingawa kila mtu ana kipawa chake, kuna watu wengi wasioweza kutambua vipawa vyao. Sababu moja inayowafanya washindwe kutambua vipawa hivyo ni kule kutokuwa na mtu wa kuwaongoza na kuwahimiza kuandama safari ya vipawa vyao. Sababu nyingine ni kwamba watu wengine hawaviamini wala kuvithamini vipawa vyao. Kwa mfano mtu anaweza kuwa na kipawa cha kucheza kandanda lakini akawa anataka kuwa daktari hata kama huo udaktari haumo katika damu yake. Mtu anapopuuza kipawa chake na kukifuata kingine tofauti huwa hana hamy na raha ya kufanya kazi ambayo hatimaye atakuwa amechagua kuifanya.

Wakati mwingine watu hupotishwa kuviacha vipawa vyao. Jamaa na marafiki huweza kumshawishi mtu kukiacha kipawa chake na badala yake kukifuata kile cha wale wanaomshauri. Mara nyingi wanaomshawishi mtu kuacha kipawa chake huwa hata hawajauelewa uwezo wa wanayemshauri. Japo watu wengine hufanikiwa kwa kuelezwa kufuata njia ambayo haikuwahusu, wengine hushindwa kufanikiwa, huwa kuna asilimia kubwa inayojilazimisha kuifanya kazi amambo haihusiani na talanta yao moja kwa moja.

Ni vizuri kutambua kwamba kuwa na kipawa tu hakutoshi. Kipawa cha mtoto ni mche unaohitaji maji, mwanga na mazingira mazuri yasiyo na magugu ili uweze kuimarika na kustawi, la sivyo utanyauka na kukauka. Mwenye kipawa anafaa kukilea kwa kukifanyia mazoezi ili kukiboresha. Anafaa kuwa na nidhamu ya kukiendeleza hadi kitakapokomaa. Anahitaji kufuata ushauri na mwongozo wa watu wengine ambao wamekitumia vizuri kipawa sawa na chake.

Tunafaa kutambua kuwa vipawa ni vingi jinsi walivyo watu. Vilevile hata watu wenye kipawa kile kimoja wana uwezo tofauti. Kama wasemavyo wahenga akili ni nywele kila mtu ana zake. Tukumbuke kuwa hata vidole havilingani

  1. Kulingana na aya ya kwanza ni kweli kuwa;
    1. bila kuwa na elimu wanadamu hawawezi kusaidiana
    2. kila binadamu ana mambo maalum anayopenda
    3. watu wanaojifanyia kila kitu huwashangaza wanajamii 
    4. hali ya kutegemeana husaidia kujenga maadili.
  2. Kwa mujibu wa aya ya pili;
    1. watu wengi hudhani kuwa wengine hawana vipawa
    2. kuna vipawa vya thamani kuliko vingine
    3. wakati mwingine watu wenye vipawa hawagunduliwi
    4. wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi wamebarikiwa.
  3. Kifungu kinaonyesha kuwa watu wengi hawawezi kutambua vipawa vyao kwa sababu;
    1. hukosa mwongozo unaofaa wa kukuza vipawa vyao
    2. huwa hawafurahishwi na vipawa vyao kama wenzao
    3. huwaza kuwa kutambua vipawa kunachukua muda mrefu
    4. hufikiri kuwa kipawa cha udaktari ndicho bora maishani.
  4. Ni kauli ipi sahihi kulingana na kifungu?
    1. Wasiojua umuhimu wa kazi huwazuia wengine kushughulikia kazi zao
    2. jamaa na marafiki huweza kumnyima mtu fursa ya kukuza kipawa chake
    3. wanaotoa ushauri kuhusu vipawa huwa wanawajua wenye vipawa hivyo
    4. kubadilisha kazi huifanya isiwe ya kuvutia kwa wale wanaifanya
  5. Kifungu kimebainisha kuwa;
    1. watu hufanya vizuri kuwashauri wengine kuacha vipawa vyao
    2. ushawishi wa marafiki huwa mkubwa zaidi kuliko wa wenye kipawa
    3. baadhi ya wanaoshauriwa kufuata vipawa tofauti na vyao hufaulu maishani
    4. ukujazi wa vipawa hutofautiana kulingana na imani ya mtu kwa Mungu
  6. Ni maelezo yapi si sahihi kulingana na mwenye kipawa?
    1. Anahitaji kukifanyia mazoezi ili kukiboresha
    2. Anahitaji kuhakikisha amekiimarisha hadi kitakapokomaa.
    3. Anafaa kufuata mfano wa wengine wenye vipawa sawa na chake.
    4. Anafaa kuwategemea wengine kukijenga kipawa chake
  7. Ni neno lipi ni kisawe cha kipawa?
    1. Nishani
    2. Ilhamu
    3. Kipaji
    4. Dhima
  8. Maneno... kipawa cha mtoto ni mche unaohitaji maji." yametumia fani ipi ya lugha?
    1. Istiara
    2. Tashbihi
    3. Kinaya
    4. Majazi
  9. Katika kifungu maana ya methali "Akili ni nywele kila mtu ana zake' ni;
    1. watu wenye hamu ya kushirikiana hutofautiana
    2. viwango vya uwezo wa watu vinatofautiana
    3. mitazamo ya watu kuhusu vipawa ni tofauti
    4. watu wanaothamini vipawa hutofautiana.
  10. Ni nini maana ya wanalolimudu kama ilivyotumiwa katika kifungu?
    1. Wanaloweza kulifanya
    2. Wanalolipenda
    3. Wanaloliamini
    4. Wanalofurahia kulipenda.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.

Malizia insha yako kwa maneno haya.

................................................................................................................Hakika tukio la siku hiyo haliwezi kusahaulika maishani.

MARKING SCHEME

  1. D
  2. B
  3. C
  4. A
  5. D
  6. B
  7. C
  8. A
  9. D
  10. B
  11. D
  12. B
  13. C
  14. D
  15. A
  16. C
  17. D
  18. A
  19. C
  20. A
  21. C
  22. B
  23. A
  24. D
  25. C
  26. A
  27. C
  28. B
  29. D
  30. A
  31. D
  32. B
  33. A
  34. C
  35. B
  36. A
  37. D
  38. A
  39. C
  40. D
  41. D
  42. C
  43. A
  44. B
  45. C
  46. D
  47. C
  48. A
  49. B
  50. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 2 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students