Wednesday, 11 October 2023 09:53

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term 3 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo.
Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Ni jambo la ___1____ kumfunza mtoto maadili___2____. Jamii __3____mapema huja___4___ baadaye na matendo ya mtoto huyo. Ndiposa wahenga wakasema___5___ Kitendo cha baadhi ya wazazi kuwaachia walimu jukumu la kuwarekebisha watoto___6__kwani huonyesha ukosefu wa___7____katika malezi. Watoto nao wasiwe___8__, ___9___wakionywa wakubali kubadili mienendo yao.

   A
 1.  dharura  muhali   muhimu   hiari 
 2.  tangu  hadi   angaa   lau 
 3.  wasipomfunza  lisilomfunza   isiomfunza   isipomfunza 
 4.  kuathirika  kuathirirwa   kuathiri   kuathiria 
 5.  kambare mkunje angali mbichi.  mwacha mila ni   mtumwa  asiyesikia la mkuu   huvunjika guu  jaza ya hisani ni   hisani.
 6.  halifai  haifai   hakifai   hakufai 
 7.   ukandamizaji  uwajibikaji  uchangamfu  utulivu
 8.  wali wa daku  wategemea nundu  wenye pupa  sikio la kufa
 9.    :  .  ''  ;

 

Amani ni hali inayofaa___10___ na kila__11____ humu nchini mwetu. Ukosefu wa usalamahuwa na gharama kubwa___12___ katika taifa lolote lile.__13____ madhara ya ukosefu wa usalama ni kupungua kwa wawekezaji __14_____ wengi wengi wao huhofia kupoteza mali yao.
Uchumi wa nchi nao huzidi__15____.

 10   kudunishwa     kubezwa    kuenziwa  kudhalilishwa
 11  mzalendo     mlowezi    msaliti  mhafidhina
 12  lisilolipika     isiolipika    usiolipika  isiyolipika
 13  Baadhi ya     Kati ya    Mithili ya  Fauka ya
 14  ambayo     ambapo    ambavyo  ambaye
 15  kuchuchumaa     kuimarika    kunawiri  kudidimia

Kuanzia nambari 16 mpaka 30, chagua jibu lifaalo zaidi

  1. Andika usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo:
    "Mtawapeleka ng'ombe machungani kesho," baba alimwambia mwanawe.
    1. Baba alimwambia mwanawe kuwa watawapeleka ng'ombe machungani kesho.
    2. Baba alimwambia mwanawe kuwa angewapeleka ng'ombe machungani siku ambayo ingefuata.
    3. Baba aliwaambia wanawe kwamba wangewapeleka ng'ombe machungani siku ambayo ingefuata.
    4. Baba alimwambia mwanawe kwamba wangewapeleka ng'ombe machungani siku ambayo ingefuata.
  2. Chagua maelezo yaliyo sahihi kati ya haya.
    1. Karadha ni pesa za ziada anazopata mkopeshaji.
    2. Ujira ni malipo anayopewa mfanyakazi mwishoni mwa mwezi.
    3. Bahashishi ni zawadi anayopewa mhudumu kwa huduma njema.
    4. Ridhaa ni malipo anayopewa mtu aliyesababishiwa hasara.
  3. Zipi ni nomino za ngeli ya U-YA 22 pekee
    1. ua, upishi
    2. ugonjwa, wembe
    3. ugali, ubaya
    4. ubele, ulezi
  4. Badili katika hali ya wingi:
    Waraka ulioupokea ulitumwa kutoka kijijini.
    1. Nyaraka ulizozipokea zilitumwa kutoka vijijini.
    2. Nyaraka mlizozipokea zilitumwa kutoka vijijini.
    3. Nyaraka mliyoipokea ilitumwa kutoka vijijini.
    4. Nyaraka walizozipokea zilitumwa · kutoka vijijini.
  5. Konokono ni kwa kombe ilivyo kuku kwa
    1. kizimba
    2. Zeriba
    3. kichuguu
    4. kitala.
  6. Chagua sentensi yenye nomino ya dhahania
    1. Kuimba kuzuri kulimfanya apate tuzo
    2. Huyo anathaminiwa kwa uaminifu wake.
    3. Mazingira yakitunzwa vizuri yatapendeza.
    4. Alishambuliwa na bumba la nyuki akilima.
  7. Neno daktari lina silabi ngapi?
    1. Nne
    2. Saba
    3. Tatu
    4. Sita
  8. Tambulisha sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
    1. Wanafunzi wengi (wale waliofanya mtihani) wamejiunga na shule za Dupili.
    2. Wachezaji walioshiriki walitoka katika nchi mbalimbali; Uhabeshi, Misri, Uganda na Moroko.
    3. Ukifika mjini, "akaniambia,"utafute zilipo afisi za wizara ya elimu.
    4. Watu wengi, wanajua kusoma, na kuandika; humu nchini.
  9. Kutokana na kitenzi vumilia, tunapata nomino;
    1. vumiliana
    2. vumilivu
    3. vumilika
    4. uvumilivu
  10. Unganisha sentensi zifuatazo kwa usahihi:
    Bakari alitoka nje ya darasa. Bakari hakuomba idhini ya mwalimu.
    1. Bakari alitoka nje ya darasa licha ya kuomba idhini ya mwalimu.
    2. Bakari alitoka nje ya darasa fauka ya kuomba idhini ya mwalimu.
    3. Bakari alitoka nje ya darasa minghairi ya kuomba idhini ya mwalimu.
    4. Bakari alitoka nje ya darasa dhidi ya kuomba idhini ya mwalimu.
  11. Tambulisha matumizi ya kiambishi ka katika sentensi.
    Kaka alienda shambani akapalilia mahindi.
    1. kuonyesha kuendelea kwa vitendo.
    2. kuonyesha kufuatana kwa vitendo.
    3. kuonyesha kutegemeana kwa vitendo.
    4. kuonyesha kukamilika kwa vitendo.
  12. Watu wakiagana bila matumaini ya kuonana kwa muda mrefu huambiana je?
    1. Buriani
    2. Makiwa
    3. Ashakum
    4. Inshallah
  13. Chagua methali yenye maana tofauti
    1. Damu ni nzito kuliko maji.
    2. Zimwi likujualo halikuli likakumaliza.
    3. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
    4. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
  14. Dungu ni ushindi upatikanao katika mchezo wa mpira. Dungu aidha ni
    1. maziwa ya kwanza ya mnyama baada ya kuzaa.
    2. tunda la mkanju ambalo bado ni bichi.
    3. sehemu anamokaa rubani katika ndege.
    4. angusha chombo cha angani kwa bomu au risasi.
  15. Tegua kitendawili kifuatacho;
    Nzi hatui juu ya damu ya simba.
    1. Maji
    2. Moto
    3. Nyuki
    4. Mbu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40

Enco la Mafuko lilipakana na mbuga ya wanyama ya 'T'unza. Wakazi wengi walikuwa wakulima na wafugaji. Sehemu hiyo ilijaliwa udongo wenye rutuba na mvua ya kutosha msimu baada ya msimu. Mimca ya kila aina ilinawiri na kushiba rangi ya chanikiwiti iliyokoza. Wazee kwa vijana walijawa na siha kutokana na lishe bora. Ukarimu wa wenyeji hawa ulipigiwa mfano karibu na mbali.

Chambilecho wahenga hakuna masika yasiyokuwa na mbu. Licha ya neema iliyoletwa na hali nzuri ya anga, wakazi walikabiliwa na changamoto moja. Wanyamapori walifika kijijini mara kwa mara na kuharibu mazao shambani. Ilibidi wakazi wakeshe mashambani mwao ili kuwinda ndovu, nyani, na viboko waliotoka mbugani kuja kujichumia mashambani humo. Mgogoro huo wa binadamu na wanyamapori haukusababisha uharibifu wa mali tu bali pia majeraha na mauaji ya wakazi. Ilibidi hatua mwafaka zichukuliwe ili kukabiliana na hali ile.

Alasiri moja, Bwana Chifu aliwaita wakazi katika mkutano. Mbiu ya mgambo ilipigwa nao wakazi wakaitikia kwa kauli moja mwito wa kiongozi wao. Yamkini walifahamu fika kuwa mtu hakatai mwito bali aitiwalo. Waliketi chini ya miti iliyokuwa uwanjani wakatega masikio yao ndi.

Bwana chifu alianza kwa kuwapa wananchi nafasi ya kueleza shida zao. Walitaja mambo mengi kama vile ukosefu wa maji safi, kuzagaa ovyo kwa mabiwi ya taka na uharibifu uliosababishwa na wanyamapori. Hatimaye Bwana Chifu aliwaomba wapendekeze suluhisho mwafaka kwa masaibu yao. Wengi walisimama kadamnasi na kuongea kwa ukali, "Serikali imezembea! Kwa nini tukiwaua wanyama tunatiwa mbaroni ilhali binadamu akiumia hatua za dharura hazichukuliwi? Tangu lini mnyama akawa na thamani kuliko binadamu? Lazima tulipwe fidia! Fidia!" Hapo umati ulilipuka kwa makofi.

Ni katika hali hiyo ambapo kijana mmoja aliunyosha sana mkono wake. Kwa idhini ya Bwana Chifu, akapewa nafasi ya kueleza hoja zake. "Wakazi wenzangu, ninasikitika kwa masaibu yanayotusibu. Hakika eneo letu limefikwa na changamoto chungu nzima katika siku za hivi karibuni. Hata hivyo, ashakum si matusi, dhiki zetu ni kama mwiba wa kujichoma ambao hauambiwi pole." Hapo alitua kidogo kutazama athari ya maneno kwa hadhira.

Baada ya muda aliendelea, "Hebu tujiulize, mabiwi ya taka tunayolalamikia yanatapakazwa na nani? Ukitokea utovu wa usalama, wahalifu wanatoka wapi? Tena, ni kina nani wanaovunja ua ulioizingira mbuga ili waingize mifugo, kukata kuni na kuchoma makaa kiholela? Majangili wanaowaangamiza ndovu, vifaru,chui na mbogo wanatoka wapi? Tukiweza kuyajibu maswala haya tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika kuiondolea mbali dhiki inayotukumba". Kijana alihitimisha kauli yake hadi akatembea taratibu hadi lilipokuwa kundi la vijana wenzake. Umati ulimzindikiza kwa macho kimyakimya kisha makofi, shangwe, vifijo na nderemo zikafuatia...

Maneno ya kijana yalizua mjadala mkali miongoni mwa wakazi. Mwishowe waliafikiana kuchukua hatua zifaazo badala ya kuilalamikia tu serikali. Walielewa kuwa mambo ni kikoa. Halikadhalika, walikubaliana kuwafichua wote walioonyesha mienendo ya kutiliwa shaka miongoni mwao.

Bwana Chifu alijiunga kwa kuchangia ajenda ya siku hiyo kwa uwazi.Alihaidi kuwa ofisi yake isingelegeza kamba katika kuwachukulia hatua wote walioshiriki maovu yaliyotishia kuiangamiza jamii. Hatimaye, umati ulifumukana huku kila mmoja akijiahidi kimoyomoyo kufanya jambo lifaalo,

  1. Kulingana na aya ya kwanza,
    1. Mvua ilinyesha katika eneo la Mafuko wakati wote.
    2. Wakazi wa Mafuko walikuwa wenye bidii, ardhi yao ilikuwa na mbolea ya kutosha.
    3. Kupakana na mbuga ya wanyama kuliwaletea neema wakazi wa Mafuko.
    4. Vijana walipigiwa mfano na watu waliopakana na eneo la Mafuko.
  2. Methali hakuna masika yasiyokuwa na mbu jinsi ilivyotumika ina maana kuwa;
    1. kila inaponyesha mvua kubwa huwa kuna mbu.
    2. hakuna jambo lisilowezekana hata liwe gumu vipi.
    3. hata jambo lionekanalo baya huwa na manufaa yake.
    4. kila jambo zuri huwa na matatizo yake.
  3. Ni maafa yapi yaliyosababishwa na wanyamapori?
    1. Kuharibu mimea na kusababisha vifo.
    2. Kuwajeruhi watu na kuharibu ua wa mbuga.
    3. Kuharibu miti na kusababisha vifo.
    4. Kuwakosesha watu usingizi na kuharibu makazi.
  4. Badala ya kusema, mbiu ya mgambo ilipigwa, mwandishi pia angesema
    1. taarifa ilitumwa.
    2. watu walienda mbio.
    3. tangazo lilitolewa.
    4. mkutano uliitishwa.
  5. Si kweli kusema kuwa;
    1. matatizo yote ya wakazi yalisababishwa na wanyama.
    2. Bwana, Chifu anayajali maslahi ya wakazi wake
    3. wakazi waliendeleza uharibifu wa mazingira.
    4. baadhi ya watu waliofika mkutanoni walijawa uchungu moyoni,
  6. Wakazi wanailaumu serikali kwa.
    1. kuwalinda wanyama
    2. kutosikiliza maoni yao
    3. kuleta mbuga kwenye makazi
    4. kupuuza hasara yao.
  7. Hoja alizotoa kijana katika makala zilionyesha,
    1. upuuzaji wake
    2. ukomavu wake
    3. ujana wake
    4. ukaidi wake
  8. Kijana alianza, maelezo yake kwa kusema ashakum si matusi'; Bila shaka, kauli hii inaonyesha kuwa
    1. anaomba usikivu wa hadhira ile 
    2. anakubaliana na yaliyosemwa na watangulizi wake.
    3. anawaomba wasikilizaji wake. msamaha
    4. anapinga kauli zilizotolewa awali na wenyeji
  9. Chagua maelezo sahihi kulingana na aya ya sita
    1. wakazi walishindwa kuyajibu maswala ya kijana
    2. maafa yaliyowasibu wakazi yalichangiwa na matendo yao.
    3. serikali iliwakabili vikali waliojitafutia malisho mbugani
    4. ilichukua muda mrefu kwa umati kumwelewa kijana.
  10. Mtazamo wa mwandishi wa makala haya kwa jumla ni kuwa;
    1. shida nyingi hutokana na kutoafikiana wananchi na serikali.
    2. wanaopakana na mbuga za wanyama hupitia changamoto nyingi.
    3. wananchi wenyewe kwa kiasi kikubwa huwa na suluhisho la shida
    4. serikali huwa haina suluhisho kwa matatizo ya wananchi.

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia nambari 41 mpaka 50

Je, umewahi kuwaza kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira? Pengine jibu lako kwa swali hili ni 'ndiyo'. Hata hivyo, nikikuuliza kuhusu mchango wa vijana katika kuyahifadhi mazingira utatatizika kujibu swali hili. Hii ni kwa sababu vijana, hususan watoto wa shule hudhani kwamba shughuli za uhifadhi wa mazingira zinahitajika kuendelezwa na serikali au watu wa makamo.

Ni dhahiri kwamba watoto wa shule wana nafasi bora ya kuyatunza mazingira. Wakiwa shuleni, wanaweza kujihusisha katika shughuli ndogondogo za kuyanadhifisha mazingira yao. Mathalani, wanaweza kukata nyasi, kukusanya na kuchoma taka, kufagia na kupiga deki madarasa yao. Halikadhalika, wanafunzi wanaweza kuanzisha vyama ambavyo vitaendeleza shughuli za kupambana na uharibifu wa mazingira. Hakika wapo wanafunzi ambao, kwa kuelekezwa na walimu walezi, wameanzisha vyama vya walinda mazingira. Wanafunzi hawa hutenga muda wao wa mapumziko kusafisha mazingira si shuleni mwao tu bali pia katika ujirani wa shule. Isitoshe, kwa vile wanafunzi wana ushawishi mkubwa ya hulka kwa wenzao, wanaweza kuwazindua na kuwahamasisha wengine dhidi inayopalilia uharibifu wa mazingira.

Fauka ya hayo, wanafunzi wanaweza kushiriki katika shughuli za upanzi wa miti shuleni na hata katika maeneo mengine. Hili litasaidia katika kuhifadhi misitu na vyanzo vya maji. Kupitia kwa upanzi wa miti, wanafunzi wanashiriki katika juhudi za serikali za kuchangia utoaji wa chakula kwa binadamu na wanyama. Vilevile, upandaji huu wa miti utasaidia kuyafanya mazingira kuwa ya kuvutia kwa wanafunzi na hata wanajamii wengine. Ikumbukwe pia kuwa juhudi za wanafunzi za kupanda miti zitawahakikishia wanyama kama vile tumbili makao.

Juu ya hayo, wanafunzi wanaweza kuanzisha miradi ya kuyatunza mazingira ili kuifaidi jamii. Kwa mfano, wanaweza kupanda vitalu vya miche ambayo watawauzia watu. Pia, ikiwa kuna vijito na vidimbwi shuleni mwao, vinaweza kunadhifishwa na kutumiwa kufugia wanyama wa majini kama vile samaki. Hii ni njia mufti ya jamii kujiinua kiuchumi. Wanafunzi wanaposhiriki katika shughuli hizi hujifunza stadi za kujitegemea maishani. Kadhalika, wanafunzi wawa hawa wana nafasi kubwa ya kuhifadhi wanyama wadogo wa kufuga. Wanaweza kuanzisha chama cha ufugaji wa kuku, bata na hata sungura. Litakuwa jambo la kuchangamsha kumpata kijana mdogo akionea fahari idadi kubwa va yeye na wenzake wamefuga chini ya uelekezi wa mwalimu wao haitakuwa ajabu hata wao katika maonyesho ya kimataifa ya kuwaona wanafunzi hawa wakiwapeleka kilimo!

Manaa kuu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira huhitaji kusambazwa na kurithishwa. Nyimbo na mashairi yanayotungwa na wanafunzi ni nyenzo kuu za kutekeleza hayo. Wanafunzi wanaposhiriki katika tamasha za muziki hubuni nyimbo zinazosifu mbinu chanya za uhifadhi wa mazingira. Nyimbo hizi pia hutumiwa kukashifu wale ambao wanaendeleza uharibifu wa mazingira. Kwa mfano, zipo nyimbo ambazo huonya dhidi ya kuendeleza kilimo kinachochangia katika mmomonyoko wa udongo. Pia, katika hafla hizi, wanafunzi hutumia uigizaji kuonyesha madhara ya uwindaji haramu, uchomaji wa misitu na upandaji wa miti itakayokausha vyanzo vya maji.

Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha nina, Nao wanajamii hawana budi kuwa kielelezo chema kwa vijana. Ikiwa watu wazima ndio vigogo wa uharibifu wa mazingira, kwa manufaa yao, juhudi za vijana zitaambulia patupu

  1. Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza.
    1. labda msomaji amearifiwa kuhusu umuhimu wa vijana katika kuyatunza mazingira.
    2. angalabu watoto huwaachia waliokomaa shughuli za watunza mazingira.
    3. huenda msomaji ametafakari kuhusu faida za kuhifadhi mazingira.
    4. kawaida watoto hutarajia walio kwenye uongozi kuhimiza utunzaji mazingira.
  2. Kifungu kimebainisha kwamba,
    1. watoto wanawashinda watu wazima katika utunzaji wa mazingira.
    2. shule zina uwezo mkubwa zaidi wa kuonyesha utunzaji wa mazingira.
    3. madarasa yana mahali kwingi zaidi kwa kuendeleza utunzaji wa mazingira.
    4. wanafunzi wanaweza kushughulikia utunzaji wa mazingira zaidi ya watu wazima.
  3. Kulingana na aya ya pili,
    1. nasaha kutoka kwa marika huwezesha kuondoa mienendo inayochangia kutohifadhiwa kwa mazingira.
    2. uanzishaji wa vyama husaidia kutenga muda wa kunadhifisha maeneo.
    3. maelekezo ya walezi huyawezesha maeneo jirani kuwa safi.
    4. kushiriki kwa walimu kwenye mazingira huimarisha mikakati zaidi ya uzoaji taka.
  4. Chagua mifano ya kukithi miti kwa mujibu wa kifungu
    1. Kuhifadhi msisituni shuleni, kutunza kunakotokea maji
    2. Kujitosheleza kwa chakula, kuimarisha sura ya mandhari
    3. kushirikisha serikali, kutunza wanyama, kustawisha hali ya kuvutiwa kwa wanafunzi.
    4. kuwapa wanafunzi fursa kujihusisha, kuwa na makazi ya wanyama.
  5. Miradi ya kuyatunza mazingira inasaidia,
    1. kupunguza kuchafuliwa kwa vidimbwi shuleni
    2. kuwaelekeza wanafunzi kuhusu uanzishaji wa ukulima.
    3. kuimarishwa kwa akiba ya miti.
    4. kuwashirikisha wanachama katika maonyesho ya kutangazia bidhaa.
  6. Ni dhahiri kwamba shughuli za kuhifadhi mazingira,
    1. huhakikisha ongezeko la wanyama wa majini.
    2. husaidia kuzidishwa kwa shughuli za kutafuta pesa.
    3. huelekea kutoa ushauri kuhusu namna ya kuongeza idadi ya mifugo.
    4. huwapa vijana maarifa ya kuendesha maisha yao hata bila michango ya wengine.
  7. Tungo zinazobuniwa na wanafunzi,
    1. huelezea njia za kubuni mafunzo kuhusu mazingira
    2. huwahimiza wale wanaopendekeza njia nzuri za kutumia ardhi.
    3. huwaonya wale wanaopunguza idadi ya wanyama kwenye mazingira.
    4. hukosoa mitindo mibaya ya matumizi ya ardhi.
  8. Kulingana na aya ya mwisho,
    1. viongozi ndio wanaokwamiza juhudi za kusafisha maeneo.
    2. ubinafsi ndicho kichocheo kikuu cha uharibifu wa mazingira.
    3. wanajamii wanahitaji kuwaonya vijana dhidi ya kufanya mambo kujifaidi.
    4. uelekezaji unatakiwa kuhimizwa ili vijana watende kama
  9. Kisawe cha ''haitakuwa ajabu'' ni?
    1. ibra
    2. kosa.
    3. shida.
    4. nadra
  10. "Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha nina", ina maana kuwa,
    1. tabia ya mtu huathiriwa na wanaomzunguka kwao.
    2. mwenendo wa mtu huathiriwa na wanaomshinda madaraka.
    3. hulka ya mtu huathiriwa na wanaofunzwa pamoja.
    4. desturi ya mtu huathiriwa na wanaomtegemea kihali.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Endeleza insha ifuatayo kwa maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.
Mgeni alifika mapema kama ilivyotarajiwa. Kengele ilipigwa ili....

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. C
  2. A
  3. D
  4. B
  5. A
  6. C
  7. B
  8. D
  9. D
  10. C
  11. A
  12. D
  13. B
  14. B
  15. D
  16. D
  17. C
  18. D
  19. B
  20. A
  21. B
  22. C
  23. A
  24. D
  25. C
  26. B
  27. A
  28. D
  29. C
  30. B
  31. B
  32. D
  33. A
  34. C
  35. A
  36. D
  37. B
  38. C
  39. B
  40. C
  41. C
  42. B
  43. A
  44. B
  45. B
  46. D
  47. D
  48. B
  49. A
  50. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term 3 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students