Tuesday, 28 February 2023 11:23

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 1

Share via Whatsapp

INSHA    

Andika insha ya kusisimua ukimalizia kwa maneno yafuatayo:

.....................................................................................................Baada ya kisa hicho cha kuatua moyo, wanakijiji waligundua umuhimu wa kushirikiana.

 MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Wanasiasa wa humu nchini sasa wametulia utadhani ___1___. Kila mwanajamii anasubiri kwa hamu na hamumu ___2___ kwa miradi mbalimbali waliyokuwa ___3___na ___4___ wao mwaka jana. Ni kweli kuwa kunao wale ambao wataziheshimu na ___5___ ahadi zao. ___6____, kunao wale ambao hata kuonekana kwao katika maeneo wanayoyawakilisha kutakuwa sawa na kuliona ___7___ hadi miaka mingine ___8___ ipite.

   A   B   C   D 
 1.   upepo wa tufani   maji ya mtungi   moto wa kifuu   maji ya bahari 
 2.  kuteketezwa  kutekelezwa   kutelekezwa   kutekelezewa 
 3.  wameahidiwa  wametendewa   wameahirishiwa   wameamuliwa 
 4.  washikadau  wapiga kura   wananchi   wawakilishi
 5.  kuzidunisha  kuziacha  kuzidhalilisha  kuzidumisha 
 6.  Kwa hivyo  Hivyo basi  Hata hivyo     Sasa basi
 7.  tone la maji    kaburi la baniani   vumbi la jangwani    ghubari la vumbi 
 8.  mitano  miwili  saba  tisa


Mchuano wa kombe la dunia mwaka uliopita ___9___ mataifa mengi ya humu barani na ya ___10___ Timu nyingi zilionyesha umahiri huku makocha wao wakizitolea maagizo. Hakuna kocha aliyetaka timu yake ___11___kwani___12___. Kipute hicho kilichoandaliwa nchini Qatar kilidhihirisha kuwa mchezo wa ___13___ huwa na mashabiki wengi zaidi. Hivi ni kutokana na ___14___ mkuu uliokuwa uwanjani. Mwisho wa kinyang'anyiro hicho, wanasoka wa Ajentina ___15___ washindi.

   A   B   C   D 
 9.   uliyavuta   uliyavutia   liliyavutia  liliyavuta 
 10.   ughaibuni   mbali   Kenya   Afrika 
 11.  ishinde   icheze   ishindwe   iongoze 
 12.  mcheza kwao hutuzwa   kazi mbi si mchezo mwema   angurumapo simba hucheza nani?  mwamba ngoma huvutia kwake 
 13.  kadanda  shoka  ngozi  kabumbu 
 14.  mlolongo  watu  timu  umayamaya
 15.  waliibuka  waliepuka  walilipuka  walikurupuka


Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu kulingana na maagizo

 1. Mwanafunzi mkaidi alionywa ingawa hakusikia. Maneno yaliyopigiwa mistari ni 
  1. kiwakilishi, kiunganishi.
  2. kiunganishi, kiwakilishi.
  3. kivumishi, kiunganishi. 
  4. nomino, kiwakilishi.
 2. Chagua sentensi iliyo katika wakati uliopo.
  1. Mzazi alimnunulia mwanawe sare mpya.
  2. Bwana Ngao amelilima shamba lote.
  3. Wanafunzi hawaimbi darasani.
  4. Hatutasafiri hadi wiki ijayo.
 3. Bata amemdonoa duduvule katika hali ya wingi ni
  1. mabata wamewadonoa duduvule. 
  2. bata wamewadonoa duduvule. 
  3. mabata wamewadonoa maduduvule.
  4. bata wamewadonoa maduduvule.
 4. Mgomba huzaa ndizi, nao mbuni huzaa
  1. mikahawa.
  2. buni.
  3. mbuni
  4. karakara.
 5. Sehemu ya mwili inayosafirisha damu ni
  1. moyo.
  2. figo
  3. mifupa.
  4. mishipa.
 6. Chagua orodha ya vimilikishi pekee. 
  1. wa, cha, vya, la.
  2. huyu, hao, kile, huo. 
  3. yangu, kwangu, lake, lao.
  4. piga, cheza, lima, simama.
 7. Kamilisha tashbihi:
  Wanafunzi hawa ni wasiri kama
  1. kaburi.
  2. giza
  3. kondoo.
  4. mchana.
 8. Sungura ni kwa kitungule. Bata ni kwa
  1. kisuse.
  2. kisui.
  3. kiyoyo.
  4. kifaranga.
 9. Kanusha sentensi ifuatayo:
  Ungekuwa mgonjwa ungetibiwa.
  1. Hungekuwa mgonjwa hungetibiwa.
  2. Hangekuwa mgonjwa hangetibiwa.
  3. Usingekuwa mgonjwa usingetibiwa.
  4. Usingalikuwa mgonjwa usingalitibiwa.
 10. Watoto 12 222 kwa maneno ni watoto 
  1. kumi na wawili elfu, mia mbili ishirini na wawili.
  2. kumi na mbili elfu, mia mbili ishirini na mbili.
  3. kumi na wawili elfu, mia mbili ishirini na mbili.
  4. kumi na mbili elfu, mia mbili ishirini na wawili.
 11. Ni ipi hapa ni zana ya vita?
  1. Kayamba.
  2. Firimbi
  3. Nyambizi.
  4. Mkuki.
 12. Akina Pendo hupenda kujifunika 
  1. tiki.
  2. gubigubi.
  3. chekwachekwa
  4. mkikimkiki
 13. Tumia kiulizi pi kwa usahihi.
  Manukato ya mama ni
  1. ipi?
  2. yapi?
  3. zipi?
  4. upi?
 14. Tumia-ingine na -enyewe kwa usahihi.
  Ubao ________________ ulianguka sakafuni ________________.
  1. mwingine, wenyewe
  2. mwingine, yenyewe
  3. wengine, penyewe
  4. nyingine, wenyewe
 15. Je, ni neno gani lililo na silabi changamano?
  1. Mbwa
  2. Mbu
  3. Mtu
  4. Mbweha

Soma kifungu kisha ujibu maswali 31 hadi 40.   

Ilikuwa Jumamosi yenye baridi shadidi na umande uliotanda. Mashaka aliamua kuingia afisini. Aliingia bila woga wala wasiwasi, utoke wapi? Kilichomkaa akilini ni wingi wa maswali. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Moja alikuwa na hakika nalo: hakuna tamaa ya heri.

Alipoingia, alisimama mkabala na mwenye afisi, "Shikamoo bwana," akamwamkia. Aliyemwamkia hakutikisika wala kugeuka ila aliinamia jalada fulani akawa anatafakari au anasoma kitu fulani. Lo! Ishara mbaya kwa Mashaka ambaye alijikuta katikati ya chumba pasi na mwenzi wala mwenyeji. Akawa mgeni katika chumba ambacho zamani alizoea kukiingia. Alimtumbulia macho baba yake na kushangazwa na tabia yake ya kujitia hamnazo.

Hali katika afisi ilimkumbusha Mashaka siku zile alipokuwa shuleni. Kulikuwa na mwalimu mmoja mkorofi ambaye kila alipopelekewa hesabu kusahihisha, akiwa na kazi yake ya kusoma au kuandika mezani, ungesimama kwa muda mrefu kabla hajalipokea daftari lako kulisahihisha. Kisha alipolichukua kulisahihisha, ikatokea kuwa umekosea hata hesabu moja tu, basi huenda asingaligusa kabisa daftari lako. Hayo ya mwalimu yalikuwa afadhali. Bwana Juba hakumtambua hata mwanawe wa kumzaa.

Bwana Juba aliinama kwa muda jicho lake kali nyuma ya miwani-miwani iliyosimama juu ya uti wa pua-iliyoenda sawia na karatasi alizozifunua kwenye jalada. Naam, ukweli ni kuwa, Mashaka alizubaa zubezube na kuduwaa waa, asijue la kufanya. Alisimama mbele ya Bwana Juba kama mlingoti, hatikisiki, huku mikono yake kaifumbata na huku akimkagua Bwana Juba ambaye alikuwa kamvalia mwenziwe miwani ya mbao kama vile hakuwa mle afisini..

Mashaka alichukua nafasi hiyo kuukagua utukufu wa bwana yule, nao si haba! Isitoshe, jinsi afisi yenyewe ilivyopambwa, makochi ya kisasa yenye matakia manene ya kahawia, katikati meza ndogo iliyochutama na kubeba bakuli kubwa la maua, vitabu, majarida na magazeti machache yaliyopangwa hapo kwa madoido. Na matendegu je? Yalisimama tisti kwenye zulia jekundu lenye mapaku ya maua ya kutupiatupia ya manjano ambalo lilifunika sakafu nzima.

 1. Mashaka aliingia afisini akiwa
  1. ameaibika.
  2. na woga.
  3. jasiri.
  4. dhaifu.
 2. Kulingana na ufahamu, mwenye afisi alikuwa nani?
  1. Mashaka.
  2. Ndugu wa Mashaka.
  3. Baba wa Mashaka.
  4. Rafiki wa Mashaka.
 3. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza  ni
  1. nahau.
  2. methali.
  3. istiara.
  4. tashbihi.
 4. Ni jambo gani halikuwa la kawaida? Mashaka
  1. kupuuzwa na mwenye afisi.
  2. kutambuliwa na mwenye afisi.
  3. kuanza kuizoea afisi.
  4. kumpata asiyemjua afisini.
 5. Kulingana na Mashaka, mwalimu wao wa Hesabu alikuwa
  1. mvumilivu.
  2. mkorofi.
  3. nadhifu.
  4. makini.
 6. Mashaka alipojaribu kumwamkia mwenye afisi,
  1. Bwana Juba alikuwa akilala.
  2. kulikuwa na wageni afisini.
  3. Bwana Juba alikuwa ameinamia jalada fulani.
  4. kulikuwa na kazi nyingi zilizokuwa zikifanywa.
 7. Mashaka aliduwaa kwa sababu
  1. Bwana Juba alikuwa amehuzunika.
  2. hakuna aliyekuwa akiongea naye. 
  3. uchafu ulikuwa umetapakaa afisini. 
  4. alikuwa amepoteza matumaini.
 8. Yaelekea Mashaka alienda afisini kufanya nini?
  1. Kuonana na wafanyakazi wake.
  2. Kuongea na Bwana Juba.
  3. Kumaliza kazi yake.
  4. Kumjulia hali baba yake.
 9. Neno zulia kama lilivyotumika linaleta dhana ya
  1. kitambaa cha kupambia dirisha.
  2. aina ya kiti.
  3. kataza mtu kufanya jambo.
  4. tandiko la sakafuni.
 10. Afisi inayozungumziwa ilikuwa na
  1. viti vikuukuu.
  2. viti visivyo na thamani.
  3. pesa nyingi.
  4. viti vyenye thamani.

Soma kifungu kisha ujibu maswali 41 hadi 50.   

Utalii ni kati ya sekta muhimu sana zinazochangia ukuaji wa uchumi katika taifa la Kenya. Tunajivunia utalii, hali ya kusafiri kutoka kwako au kwenu ili kwenda kwingine kujifurahisha nafsi au hata kujifunza mambo mageni. Kuna aina mbili za utalii; utalii wa kitaifa na ule wa kimataifa. Wapo watalii wanaozuru nchi zao kujiburudisha na kujielimisha na wengine wanaovuka mipaka ya nchi zao.

Humu nchini, Mola ametutunukia mengi, mengi zaidi ya nchi nyingi duniani, hata ingawa kila nchi inacho angalau cha kujivunia. Kivutio kikuu humu nchini ni tamaduni zetu na wanyamapori. Wanyama hawa ni fahari ya nchi yetu. Wamechangia pakubwa katika ujenzi wa taifa kutokana na pesa za kigeni. Baadhi ya vivutio vingine ni maliasili mengi tuliyonayo.

Wanyama tunaojivunia nchini ni pamoja na twiga, simba, ndovu, kifaru, viboko na kadhalika. Wanyama hawa hususan huwa wanatengewa sehemu maalumu. Sehemu hizi aghalabu humilikiwa na serikali. Ili kuingia na kuwaona wanyama hawa, mtu hulazimika kulipa kiwango fulani cha pesa. Hakuna cha bwerere eti!

Licha ya kuwa wanyama hawa huletea nchi yetu sifa na faida chungu nzima, wao husababisha madhara pia. Mara kwa mara, simba wamekuwa wakitoroka mbugani. Madhara huwa wazi na huwa hayakadiriki. Simba na raia hupoteza maisha yao huku mifugo wakiwa hatarini kwani hufanywa kitoweo. Ndovu na viboko hawajaachwa nyuma. Wao huyavamia mashamba na kusababisha uharibifu mkubwa. Hali hii huleta njaa. Licha ya hali hii, tunalo jukumu la kuwalinda wanyama hawa. Tusiwe majangili tunaotafuta pembe za ndovu, na iwapo utakutana na mmoja, basi usikose kumripoti. Unahimizwa kupiga ripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu au kupiga simu kwenda nambari 999. Moto unaowashwa misituni pia ukomeshwe. Vilevile, ukulima unaoendelezwa mbugani pia ukomeshwe. Sote tuungane pamoja tuwalinde wanyama wetu.

 1. Kulingana na aya ya kwanza,
  1. utalii ndiyo sekta ya pekee inayokuza uchumi.
  2. utalii haukuzi sana uchumi.
  3. wakenya wengi aghalabu hawajivunii utalii.
  4. utalii ni mojawapo ya sekta zinazokuza uchumi.
 2. Kulingana na kifungu,
  1. watalii ni wazungu wanaokuja nchini. 
  2. watalii hutoka nje na ndani ya nchi. 
  3. watalii daima huleta tabia mbaya nchini.
  4. hatuna mengi nchini ya kutalii.
 3. Taarifa yasema kuwa kivutio kikuu cha watalii ni
  1. maliasili na tamaduni.
  2. wanyamapori na tamaduni.
  3. wanyamapori na maliasili.
  4. tamaduni pekee.
 4. Mwandishi anaposema kuwa wanyama watengewe sehemu maalumu, bila shaka anarejelea
  1. mbuga.
  2. nyika.
  3. misitu.
  4. pori.
 5. Neno chungu kama lilivyotumika katika ufahamu lina maana ya
  1. chombo cha kupikia.
  2. inayouma.
  3. isiyo tamu.
  4. nyingi.
 6. Ni methali gani inayofaa kutoa mukhtasari wa mwanzo wa aya ya nne?
  1. Hakuna masika yasiyokuwa na mbu. 
  2. Zimwi likujualo halikuli likakuisha. 
  3. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
  4. Mtaka unda haneni.
 7. Hasara zinazosababishwa na wanyama si pamoja na
  1. kuvamia mashamba.
  2. kuangamiza mifugo.
  3. kusababisha vifo.
  4. kubuni nafasi za ajira.
 8. ...pembe za ndovu ni sawa na
  1. vipusa. 
  2. tembo. 
  3. mikonga.
  4. mabori.
 9. Mwandishi asema kuwa
  1. wanyama wanaovamia mashamba wanaweza kuuawa.
  2. ili kuwaona wanyama, mtalii hulipa kiingilio.
  3. nchi nyingine hazina kivutio chochote cha watalii.
  4. mifugo huwala wanyama wanaowavamia.
 10. Mwisho kabisa, msemaji anamalizia kwa
  1. lawama.
  2. kero
  3. ombi.
  4. shime.


MARKING SCHEME

 1. B
 2. B
 3. A
 4. D
 5. D
 6. C
 7. B
 8. A
 9. B
 10. A
 11. C
 12. D
 13. D
 14. D
 15. A
 16. C
 17. C
 18. A
 19. B
 20. D
 21. C
 22. A
 23. C
 24. C
 25. D
 26. D
 27. B
 28. B
 29. A
 30. D
 31. C
 32. C
 33. B
 34. A
 35. B
 36. C
 37. B
 38. C
 39. D
 40. D
 41. D
 42. B
 43. B
 44. A
 45. D
 46. A
 47. D
 48. D
 49. B
 50. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students