Wednesday, 15 March 2023 06:00

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 4

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya uliyopewa.

Tunapotia guu katika __1__ __2__, walimu wetu wapendwa wanaendelea kutupa__3__huku tukifunzwa mengi kama vile __4__ ambavyo hutoa taarifa kuhusu vitenzi, vivumishi na hata vielezi. Huku hayo yakiendelea, tumepata __5__ kufahamu akisami pia, __6__, __7__ ambayo ni sehemu moja ya saba. Kwa moyo wa shukrani, __8__ kuwapa kongole mzomzo.

   A   B   C   D 
 1.   kidato cha nane    darasa la kwanza   kidato cha kwanza   darasa la nane 
 2.  mwakani  mwaka ujao   mwaka huu   mwaka kesho 
 3.  motisha  vitisho   mazoezi   talaka 
 4.  viarifa  vibadala   viwakilishi   vielezi 
 5.  nafsi ya  fursa ya   nafasi wa   wasaa ya 
 6.  mathalani  mithili ya   mifano   madhali 
 7.  tusui  sudusi   subui   humusi 
 8.  haitulazimu  hatuna budi  ina bidii  tuna budi


Kristina alipojiangalia tena__9__ kioo, aligundua kuwa uso wake uliokuwa __10__na kufanya mabaka sasa ulianza kurudisha unyevuunyevu wa awali. __11__ mauti ya mume wake yapata majuma mawili __12__ yalimdhoofisha, __13__ kuwa __14__. Kwa vyovyote vile, ilimpasa kuyazika ya kale na kuendelea na safari ya maisha japo kwa kuuma __15__.

   A     B      C    D 
 9.   ndani ya   katikati ya   na   kwa 
 10.  ukimeremeta   umenawiri   umesawijika   umeiva 
 11.   hata hivyo  Hata ingawa   Hivyo   Kwa hivyo 
 12.  zilizopita  yaliyopita   yalipita   zilipita 
 13.  alijipa moyo  alipiga mwayo   alikonga roho   alipiga mtindi  
 14.  mavi usioyala wayawingiani kuku?  mavi ya kale hayanuki   kuchamba kwingi ni kuondoka na mavi   mavi ya kale hayaachi kunuka
 15.  meno   shida   ulimi   chanda 

 

Kutoka swali la 16 hadi 30, jibu swali kulingana na maagizo   

  1. Chagua maelezo yaliyo sahihi. 
    1. Arafa: ujumbe wa maandishi unaotumwa kwa simu.
    2. Kipepesi: chombo cha kutuma na kupokea barua.
    3. Kikokotoo: chombo cha kutuma ujumbe kwa sauti.
    4. Mtandao: mfumo wa mawasiliano kupitia tarakilishi.
  2. Chagua silabi.
    1. Sh
    2. Dha
    3. Ng
    4. Th
  3. Upi ni usemi halisi wa sentensi ifuatayo?
    Mwalimu kwa hasira aliwaamuru wanafunzi wote wapige magoti na kumaliza kazi yao ya ziada. Mwalimu
    1. alifoka, "Pigeni magoti na mmalize kazi yenu ya ziada!"
    2. alisema, "Mpige magoti na mmalize kazi yenu ya ziada."
    3. alifoka, "Malizeni kazi yenu ya ziada na mpige magoti!"
    4. alisema wanafunzi wote wapige magoti na wamalize kazi yao ya ziada.
  4. Tambua sentensi yenye kivumishi cha idadi.
    1. Mtumwa huyu ni mtiifu sana. 
    2. Kitabu cha kasisi si cheusi.
    3. Jino langu linauma sana.
    4. Kiatu cha kwanza hakifai.
  5. Ni jozi gani iliyokosewa?
    1. Skrubu - bisibisi.
    2. Mpini - jembe.
    3. Mchi - kinu.
    4. Mkufu - kipini.
  6. Ni kiunganishi gani kisichoweza kukamilisha sentensi ifuatayo?
    Kauleni aliadhibiwa vikali ________________________ kufukuzwa shuleni.
    1. licha ya
    2. fauka ya
    3. bighairi ya
    4. pamoja na
  7. Tambua sentensi yenye a unganifu.
    1. Cha walimu ni safi.
    2. Kitabu cha mwalimu kimeanguka.
    3. Msipoziba nyufa mtajenga kuta.
    4. Nilimwona alipokuwa akienda maktabani.
  8. Ni kundi gani lenye nominoambata?
    1. Maji, marashi, mate.
    2. Njugumawe, batamzinga, askarikanzu.
    3. Safu ya milima, umati wa watu, kichala cha matunda.
    4. Kenya, Juma, Agosti.
  9. Nomino maskani huwa katika ngeli gani?
    1. PAKUMU
    2. YA-YA
    3. U-YA
    4. LI-YA
  10. Paka huyu ndiye alaye buku katika wingi ni paka hawa
    1. ndiyo walaye buku.
    2. ndio walao buku.
    3. ndiyo walao mabuku.
    4. ndio walao mabuku.
  11. Tambua sentensi yenye kielezi.
    1. Katika debe tanna maji.
    2. Kilichosimama ni hiki.
    3. Niliitika kwa sauti.
    4. Mtoto aliyesimama kando ya mto ni mwoga.
  12. Banati ni kwa msichana kama vile ___________________________ ni kwa kaptura.
    1. kinyasa
    2. bombo
    3. mvuli
    4. mshipi
  13. Chagua nahau iliyo tofauti kimaana.
    1. Aga dunia
    2. Kata kamba
    3. Konga roho
    4. Enda na ulelengoma
  14. Kamilisha methali: Wema
    1. haiozi.
    2. haigombi.
    3. hauozi.
    4. haukomi.
  15. Kitendawili:
    Mzungu analala na ndevu ziko nie.
    1. Mwiko.
    2. Hindi.
    3. Mvi.
    4. Unga

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 hadi 40.

Hadithi! Hadithi! Hapo zamani za kale kabla ya majabali kukauka, kuku na mwewe walikuwa marafiki wa dhati. Usahibu wao ulikuwa ule wa kufa kuzikana. Waliishi pamoja kwa miaka na mikaka. Walishirikiana na kusaidiana katika lolote lililotokea, la furaha na la majonzi.

Walifanya kazi pamoja. Kila mmoja alijitahidi kadiri ya uwezo wake. Walishirikiana kama kinu na mchi. Bega kwa bega, walifanya kazi zao. Mwewe alijitwika jukumu la kulisha familia zote mbili naye kuku alikuwa na jukumu la kuwalinda watoto wao. Kuku alihakikisha wameshiba na kutulia.

Ndege hawa waliishi kwa amani na utulivu bila kukumbwa na tatizo lililowashinda kutatua. Urafiki wao ulifanya wakati mwingine walale njaa ili watoto wao washibe.

Siku moja walipata barua ya ualishi kutoka kwa ndege wenzao. Karamu ya kukata kwa shoka ilikuwa iandaliwe. Mwewe aliwatayarisha wanawe kwa sherehe. Kuku aligundua kuwa vifaranga wake walikuwa na kucha ndefu zilizowaaibisha. Hivyo, aliamua kumwomba mwewe wen.be. Mwewe alimpa wembe bila kusita kisha akamwambia, "Hakikisha kwamba umerudisha wembe wangu mara moja."

Kuku alitekeleza wajibu wake kwa haraka. Muda si muda, familia hizo mbili zikang'oa nanga kwa furaha. Karamun, kila mmoja na watoto wake alibugia mapochopocho. Vinywaji vilikuwa tele. Baada ya sherehe, walirejea nyumbani.

Siku iliyofuata, mwewe alimtuma mtoto wake kwa kuku kuuchukua wembe ili wanyolewe. Kuku alipigwa na butwaa alipogundua kwamba wembe wa mwewe haukuwapo. Wasiwasi ulimvamia mara moja. Huku na kule, alianza kuchakurachakura. Jasho lilimtiririka lakini wapi! Juhudi zake hazikumfaa.

Mtoto wa mwewe aliripoti haya kwa mama yake. Bila kungoja, mwewe alifika nyumbani kwa kuku. "Aka! Hujui wewe kuwa wembe huo ni mmoja kama moyo? Lazima nitwae fidia. Nitawala vifaranga wako mmoja mmoja hadi unirejeshee wembe wangu." Maneno hayo yalimchoma kuku moyoni kama mkuki. Tangu siku hiyo, kuku huchakurachakura huku na kule akiutafuta wembe wa mwewe. Naye mwewe huruka juu akiwasaka vifaranga wa kuku.

  1. Aya ya kwanza inaudokezea kwamba
    1. urafiki wa mwewe na kuku ulikuwa wa unafiki.
    2. mwewe na kuku walitengana sana.
    3. urafiki wa ndege hawa haukuwa wa ukweli.
    4. kuku na mwewe walipendana sana
  2. Neno lililopigiwa mstari mwishoni mwa aya ya kwanza lina maana sawa na
    1. huzuni.
    2. ufanisi.
    3. furaha.
    4. ugomvi.
  3. Katika kifungu ulichosoma, ni nani aliyekuwa akitafuta chakula?
    1. Kuku.
    2. Mwewe.
    3. Wote wawili.
    4. Watoto wao.
  4. Mwewe na kuku walishirikiana kama kinu na mchi. Methali inayoafikiana na hali hii ni
    1. bendera hufuata upepo.
    2. baniani mbaya kiatu chake dawa.
    3. kidole kimoja hakivunji chawa.
    4. adui mpende.
  5. Ni nini ambacho kinaonyesha kuwa ndege hawa waliwajali watoto wao?
    1. Kuwatafutia chakula kila siku. 
    2. Kuwatetea kila siku.
    3. Kulala njaa ili watoto washibe.
    4. Kwenda karamuni pamoja.
  6. Barua waliyoipata mwewe na kuku
    1. iliandikiwa watoto wao.
    2. iliwaalika katika karamu.
    3. iliwafurahisha sana.
    4. iliwaletea chakula.
  7. Ni kweli kuwa
    1. mwewe alikuwa mwaminifu.
    2. kuku hakuwapenda watoto wake.
    3. watoto wa mwewe walikuwa wachafu.
    4. kuku alikuwa mzembe.
  8. zikang'oa nanga..." ni sawa na
    1. zikaanza safari.
    2. zikakamilisha safari.
    3. zikafika sherehení.
    4. zikasherehekea.
  9. Kulingana na kifungu ulichokisoma, ni nini kilichomtia kuku wasiwasi alipogundua kuwa wembe haukuwapo? 
    1. Kuvunjika kwa urafiki wao.
    2. Kunyakuliwa kwa watoto wake.
    3. Onyo alilokuwa amepewa awali.
    4. Kukosa kuhudhuria karamu.
  10. Tabia ya mwewe ya kuruka juu ili kuwasaka vifaranga wa kuku inaonyesha tabia ya
    1. kuonyesha mapenzi. 
    2. kutoa onyo.
    3. ulafi.
    4. kulipiza kisasi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 hadi 50.

Je, ni mnyama yupi mwenye nyayo kama za kasuku, awezaye kutazama pande zote kwa wakati mmoja na mwenye ulimi wenye kasi isiyomithilika? Si ndege, si chura bali ni kinyonga. Kwa makini ukichunguza vidole vya kinyonga, utagundua kuwa, kiaina, vinafanana na vya kasuku. Kila mguu unavyo vidole vitano vyenye upekee wa kuyakamata matawi sawasawa. Aidha, kila kidole kinao ukucha, hivyo, kuwafanya vinyonga wakwezi hodari.

Si miguu yao tu ambayo huajabiwa katika miili yao. Kwa mtazamo wa makini, itadhihirika kuwa katika kila moja ya macho yao, ukope wa juu na wa chini hukaribiana kiasi cha kuacha nafasi ya mboni pekee. Kinyume na binadamu, kinyonga huweza kutazama na kuona pande mbili tofauti mara moja, kwa wakati mmoja. Hili humwezesha kuona kwa nyuzi mia tatu na sitini bila tatizo. Vile vile, wao huwa na uwezo mkubwa wa kuona hususan wakiyaelekeza macho yao yote mawili katika azma moja. Wana uwezo wa kuwaona wadudu wadogo wadogo hata wakiwa mbali. Hili huwasaidia sana wakati wa mawindo.

Ili kulipiza katika utaratibu wao wa kutembea, vinyonga huwa na ndimi ndefu ajabu. Wakati mwingine, ndefu kuliko urefu wa miili yao kwa jumla! Yasemekana kuwa ndimi hizo zao huwa na kasi kiasi kuwa ni vugumu binadamu kuufuatilia mwondoko huo kwa macho. Ni kwa vipi ambavyo ndimi zao huwa na kasi hivyo? Hakika, ndimi zao huwa kama upote na mshale au manati. Jinsi ambavyo upote hurusha mshale ndivyo ambavyo ulimi wa kinyonga hutoka na kuingia kinywani mwake na hivyo kumsaidia kulinasa windo lake.

Talanta nyingine maarufu ya kinyonga ni uwezo wake wa kubadilibadili rangi ya ngozi yake. Anao uwezo wa kujibadili hadi rangi zote za upinde wa mvua na hata zambarau, waridi, nyeusi na hudhurungi. Uwezo huu huwasaidia kujificha kwa kujifananisha na mazingira waliyomo. Hata hivyo, sababu kuu ya uwezo huu huwa kudhibiti kiwango cha joto mwilini na kuelekeza hisia zao. Wao hutumia mabadiliko haya ya rangi kuonyesha hali ya kutamalaki na utetezi katika maeneo wanamoishi. Mabadiliko haya ya rangi aidha hutumika kuwavutia vinyonga wa jinsia tofauti.

Vinyonga wengi hupatikana Afrika. Hata hivyo, matabaka mengine machache yamewahi kushuhudiwa kwingineko kama vile Asia na pia majangwani. Maadamu vinyonga hawana masikio, wao hutumia hisia za mirindimo katika mazingira yao. Hayo yote ya kuajabia kuhusu kinyonga humfanya awe mwanajamii wa kuvutia mno miongoni mwa wanyama jamii ya mamba na mburukenge.

  1. Ni gani hapa si kweli kuhusu kinyonga?
    1. Anao ulimi wenye kasi ya juu.
    2. Nyayo zake hufanana na za kasuku.
    3. Huweza kutazama pande nyingi kwa wakati mmoja.
    4. kwa kiwango fulani, hufanana na chura.
  2. Badala ya kutumia neno lililopigiwa mstari katika aya ya kwanza, mwandishi angetumia
    1. kenge.
    2. lumbwi.
    3. ngwena.
    4. nyoka
  3. Ni nini huwafanya vinyonga kuwa wakwezi hodari?
    1. Miili yao miembamba.
    2. Vidole vyao vitano. 
    3. Kucha zao.
    4. Utaratibu wao katika kutembea.
  4. Kwa maoni yako, nafasi za mboni hubakia kwa nini? Ili
    1. kudhibiti kiwango cha nuru. 
    2. kuwawezesha vinyonga kuona. 
    3. kutenganisha kope za juu na za chini.
    4. kuajabiwa na mwanadamu.
  5. Ni uwezo gani wa vinyonga ambao mwanadamu anaweza kuiga?
    1. Kutazama pande kadhaa kwa wakati mmoja. 
    2. Kasi ya ulimi.
    3. Kujibadili rangi.
    4. Utaratibu katika kutembea.
  6. Je, ni gani hapa si sababu ya vinyonga kujibadili rangi?
    1. Kutambulisha hisia zao.
    2. Kupima viwango vyao vya jotomwili.
    3. Kujitofautisha na mazingira wanamoishi.
    4. Kutafuta wenza.
  7. Mwandishi ametaja mambo mangapi ya kuajabia kuhusu kinyonga?
    1. Manane
    2. Saba
    3. Matano
    4. Sita
  8. Sababu kuu ya kinyonga kubadilibadili rangi ni
    1. kujifananisha na mazingira.
    2. kuvutia jinsia tofauti. 
    3. kuonyesha hisia zao.
    4. kudhibiti jotomwili.
  9. Mwandishi ametaja uwezo gani wa vinyonga unaowafanya kuwa maarufu?
    1. Uwezo wao wa kukwea miti. 
    2. Kasi ya ndimi zao.
    3. Uwezo wao wa kujibadili rangi.
    4. Urefu wa ndimi zao.
  10. Kulingana na msemaji, vinyonga huweza kupatikana katika mabara yapi?
    1. Majangwani na misituni.
    2. Asia na Marekani.
    3. Asia, Afrika, Marekani, misituni na majangwani.
    4. Asia na Afrika.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Andika insha ya kusisimua ukianzia kwa maneno haya:

Baada ya kupata maakuli, kila mmoja wetu alielekea ukumbini ili kupata burudani ya muziki. Kufunba na kufumbua,......................................................................



MARKING SCHEME

  1. D
  2. C
  3. A
  4. D
  5. B
  6. A
  7. C
  8. B
  9. D
  10. C
  11. B
  12. B
  13. A
  14. B
  15. A
  16. A
  17. B
  18. A
  19. D
  20. D
  21. C
  22. B
  23. B
  24. B
  25. D
  26. C
  27. B
  28. C
  29. C
  30. B
  31. D
  32. A
  33. B
  34. C
  35. C
  36. C
  37. D
  38. A
  39. A
  40. D
  41. D
  42. B
  43. C
  44. B
  45. D
  46. C
  47. D
  48. D
  49. C
  50. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 4.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students