Thursday, 30 March 2023 07:42

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 12

Share via Whatsapp

Kuanzia nambari ya 1 hadi 15, soma vifungu vifuatavyo kisha ujibu kwa jibu lifaalo zaidi.

Uwajibikaji ni jambo __1__ kwa mja __2__ yule. Kila mmoja ana jambo la kufanya maishani mwake kuwajibika __3__ faida __4__.
Mojawapo ya faida __5__ ni ufanisi. __6__  uwajibikaji humpa mtu fursa ya kujifunza zaidi kutokana na jambo __7__. Mja razini hastahili __8__  yaani kutegemea wengine kwa kila kitu. Iwapo tunataka kupiga hatua maishani, __9__kujukumika kwani __10__

   A   B   C   D 
 1.   mbora   mzuri   aula   nzuri 
 2.  wowote   yeyote   yoyote   yenyewe 
 3.  ina  zina  kuna  inayo
 4.  belele  mingi  zingine   mengi
 5.  hiyo   huo  nyingine   hizo
 6.  Maadanu   Iwapo  Aidha  Ila
 7.  analolitekeleza   anayotekeleza   anapotelekeza   analolitelekeza 
 8.  kukaa pweke  kula mumbi  tia mrija  kula mwata
 9.  shati  tuna budi  budi  hatuna budi
 10.   vyote viowevu si maji   ajizi nyumba ya njaa   penye nia pana njia   ndugu ni kufaana si kufanana 


Uandishi wa insha __11__ kuandika ili kujaza karatasi au __12__ wa maneno tu __13__. Insha bora sharti iwe ya kumvutia __14__ anayeisoma na kukutuza alama. Mwanafunzi alenge __15__ ambayo ni sehemu iliyo na alama nyingi bila kupotoka.

   A   B   C   D 
 11.   siyo   si   sio   ndio 
 12.  kupachika   upachiki   upachishi   upachizi 
 13.  kivoloya  kimantiki    kwa mpango   kimaelezo 
 14.  mtahini  mtahiniwa   mwanagenzi   mwadhiri 
 15.  mtindo  mtiririko   maudhui   msuko 

 

Kuanzia nambari 16-30, jibu kulingana na maagizo.

  1. Neno "tulimpokea" lina silabi ngapi?
    1. 10
    2. 5
    3. 4
    4. 6
  2. Chagua jibu lisiloambatanishwa vyema.
    1. kiwavi - kifukofuko
    2. konokono - gamba
    3. simba - pango
    4. kasuku - tundu
  3. Chagua kundi lililo katika ngeli ya U-YA.
    1. maamuzi, unyoya, mabua 
    2. maji, marashi, mandhari
    3. mawele, mazingira, ndwele
    4. ute, uga, maua
  4. Chagua wingi wa:
    Ua huu una waya wa umeme.
    1. Maua haya yana nyaya za meme. 
    2. Nyua hizi zina waya za umeme. 
    3. Nyua hizi zina nyaya za umeme.
    4. Maua hizi zina nyaya za meme.
  5. Rahma alikuwa akielekea shuleni asubuhi. Kivuli chake kilikuwa upande wa kushoto. Je, shule ilikuwa upande gani?
    1. Mashariki
    2. Magharibi
    3. Kusini
    4. Kaskazini
  6. Kutaka kesi isikilizwe upya ni
    1. kuruka kesi
    2. kukiri mashtaka
    3. kukata kesi
    4. kukata rufaa.
  7. Chagua ukubwa wa sentensi hii
    Kiti kibovu kilimwangusha mzee yule.
    1. Jiti mbovu lilimwangusha jizee lile
    2. Jikiti bovu liliangusha jizee lile. 
    3. Kijikiti kibovu kilikiangusha kizee kile.
    4. Jiti bovu liliangusha jizee lile.
  8. Baraza ni la wazee au mawaziri.
    Genge ni la wezi au
    1. wahamaji
    2. wachezaji
    3. polisi
    4. vibarua.
  9. Chagua sentensi ambayo imetumia kihisishi ifaavyo.
    1. Hoyee! Timu yetu imeshindwa
    2. Ala! Kumbe unakula nyoka?
    3. Alhamdulillahi! Tumenusurika kifo.
    4. Pukachaka, nimesahau mkoba wangu!
  10. Chagua usemi taarifa wa
    "Nitawanunulia zawadi kesho," mwalimu alituahidi.
    1. Mwalimu aliwaahidi kuwa atawanunulia zawadi kesho. 
    2. Mwalimu alituahidi kuwa angetununulia zawadi siku ifuatayo.
    3. Mwalimu alituahidi kuwa atatununulia zawadi kesho.
    4. Mwalimu aliwaahidi kuwa angewanunulia zawadi siku inayofuata.
  11. Tambua maneno yaliyopigiwa mistari.
    Mtoto huyu ni mwadilifu lakini yule amekosa sana.
    1. kivumishi, kiwakilishi, kielezi 
    2. sifa, kiashiria, kitenzi
    3. kivumishi, kiashiria, kitenzi
    4. nomino, kiwakilishi, kielezi
  12. Chagua orodha yenye visawe pekee. 
    1. jukumu, dhima, madhumuni
    2. somo, rafiki, adui
    3. busara, hekima, tabasuri
    4. shida, tabu, wajibu
  13. Chagua sentensi iliyotumia o-rejeshi tamati.
    1. Kiatu kilichoshonwa si kipya.
    2. Mdudu anayeuma ni hatari.
    3. Basi lililowasili ni jipya.
    4. Kipi kikusikitishacho?
  14. Kiambishi "na" kimetumikaje?
    Wake wenza wanachukiana sana.
    1. Kuonyesha kuunganisha sentensi.
    2. Kuonyesha mtendaji
    3. Kuonyesha kauli ya kutendeana
    4. Kuonyesha nafsi.
  15. Chagua maelezo sahihi
    1. Utenzi ni shairi la malumbano.
    2. Ukwapi ni kipande cha pili cha mshororo.
    3. Mloto ni mshororo wa tatu katika shairi
    4. Mwandamizi ni kipande cha tatu katika mshororo.

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31 - 40.

Uhifadhi wa mazingira ni jitihada zinazofaa kuwekwa na kila mja ili kuhakikisha kwamba ulimwengu anamoishi unamfaa yeye wenzake wa kizazi cha leo na vizazi vya kesho. Ni dhima yake kujituma katika harakati za kuboresha mazingira yake. Vilevile ni jambo aula kuhamasisha wenzake kuweka juhudi za kuyathamani makao yao kwa kuyatunza. Kwa njia hizo tutakuwa na dunia ambayo inampendeza muumbaji hata zaidi.

Adinasi aliye na akili razini anastahili kutunza mazingira yake kwani akiyachafua ataandamwa na masaibu si haba. Ni kujichoma mwiba matokeo yake unayafahamu. Mlipuko wa ndwele kama vile walea. homa ya matumbo na mengine mengi huchangiwa na uhawayani waja wasiojali. Wengi wameamua kuyaziba masikio yao na kufumba macho wasione na kusikia mawi yanayotendeka. Wamesahau kuwa mtego wa panya hunasa waliomo na...

Mazingira huweza kuundwa na vitu aina ainati. Kwanza kuna yale ya asili. Haya ni yale yaliyoumbwa na Mola. Kunayo yenye maji kaama vile bahari, maziwa, mito na chemichemi za aina zake. Mengine ni milima, mabonde na misitu. Haya yote ni muhimu sana kwani huwa ni maliasili ambayo huweza kutumiwa kuzalishia nchi utajiri na kuinua uchumi.

Aidha kuna yale ya kujitengenezea. Binadamu kwa uwezo wa Mola amevumbua mengi na kujitengenezea mazingira kama vile viwanda, majengo ya kifahari, vyombo vya usafiri na hata misitu penye jangwa. Kukata miti kiholela imepelekea ukosefu wa mvua. Huku ni kuchafua vyanzo vya maji na kupelekea hata wanyama kugura makazi yao ili kutafuta hifadhi kwingineko. Binadamu naye anabaki jangwani kifo kikimkodolea macho.

Pia kutokana na ukataji miti ovyo, kumechangia kuanguka kwa kilimo ulimwenguni. Matokeo yake ni waja kugugunwa na njaa katika baadhi ya maeneo kame. Vilevile joto linalizidi kuongezeka na kupanda sana na kupelekea vifo. Tambiko la ozoni ni hatari kwa viumbe. Tatizo hili limesafirisha waja lukuki jongomeo.

Ni dhahiri kuwa sote tunafahamu umuhimu wa maji katika kuendesha maisha ya wanadamu, wanyama na viumbe wengine. Ni ukweli usipopingika kuwa viumbe vyote vinategemea maji ili viweze kuishi. Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vimetunzwa kwa njia muafaka. Kwanza ni kuepuka kurundika takataka katika vyanzo vya maji. Licha ya hayo, ni kuepusha taka za viwandani kuingia katika vyanzo vya maji. Aidha, ni kuwahamasisha wavuvi kuhusu njia salama za uvuvi.

Kijana, mzee amka, zinduka kutoka gonezini. Angalia vitu vinavyokuzunguka. Piga mbiu kila. mja ajue na kufahamu kuwa kizazi cha leo na cha kesho kinategemea bidii zetu sasa. Tujengee wana wetu, wajukuu na vitukuu mustakabali.

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza
    1. dunia haimpendezi Mungu
    2. tunaishi katika mazingira yasiyo bora 
    3. sio waja wote wanaotunza mazingira
    4. mja ameonyesha kuthamini mazingira.
  2. Kulingana na aya ya pili si kweli kuwa
    1. mwanadamu hana akili razini
    2. yakini shida zitamwandama mja asipotunza mazingira
    3. kutotunza mazingira huleta maradhi mbalimbali
    4. watu wanayaharibu mazingira wenyewe.
  3. Ni orodha gani iliyo sahihi kulingana na aya ya tatu?
    1. ziwa, bahari, mabonde
    2. makavazi, milima, mito
    3. makavazi, minara, nyumba
    4. mabonde, nyumba, misitu. 
  4. "Wengi wameamua kuyaziba masikio na kuyafumba macho" Kauli hii inaonyesha
    1. kujifanya kutoona na kutosikia
    2. kukemea uharibifu
    3. kuchangia uharibifu
    4. kuupuza wanayoyaona. 
  5. Mwandishi anazungumzia aina ngapi ya mazingira?
    1. Moja
    2. Tatu
    3. Mbili
    4. Nne
  6. Chagua orodha ya mazingira ambayo ni maliasili pekee.
    1. madini, maziwa, mabonde
    2. majengo, maji, miti
    3. vyombo vya usafiri, makavazi, mito
    4. mito, mimea, zaraa
  7. Ukataji miti huchangia haya yote isipokuwa
    1. kupoteza watalii
    2. kuathirika na tambiko la ozoni
    3. kusababisha jangwa
    4. kuongezeka kwa hayawani.
  8. Kulingana na kifungu, ni wazi kuwa
    1. wengi hawafahamu umuhimu wa kutunza mazingira
    2. kila mmoja anawajibika kuweka mazingira sawa
    3. watu wanatumia maliasili kuzalisha utajiri wa nchi
    4. kudidimia kwa miti ndiko kunaleta madhara makubwa zaidi.
  9. "Binadamu naye anabaki jangwani kifo kikomkodolea macho" ni
    1. methali
    2. nahau
    3. tashihisi
    4. chuku.
  10. Ni methali gani haifai kifungu hiki?
    1. Mtego wa panya huingia waliomo na wasiokuwemo.
    2. Mchimba kisima huingia mwenyewe.
    3. Mwiba wa kujidunga hauna pole.
    4. Tahadhari kabla ya hatari.

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 41 - 50.

Jumanne alfajiri mbichi, nilijihimu na kudamka ili nisije nikalimatia shuleni. Nilielewa barabara maana ya methali chelewa chelewa utamkuta mwana si wako. Naam, sikutaka kumkosa huyo mwana. Niliyakumbuka maneno ya Bwana Busara, mwalimu mkuu wa shule yetu ya Bidii. Siku iliyotangulia alikuwa ametuonya dhidi ya uzembe hasa wakati huo ambapo tulikuwa katika hatua za mwisho katika masomo ya msingi. Kila mwanafunzi alikuwa amelitega sikio lake ndi ili ajizolee lulu za mwalimu.
Baada ya nasaha kemkem, kila mmoja alishika njia moja kwa moja kuelekea nyumbani. Masikio yetu yalikuwa yameshiba.

Staftahi iliyoandaliwa na mpishi hodari, mamangu ilinikaribisha mezani. Nilibugia huku mawazo yamenitinga akilini mwangu. Mseto wa mawazo kuhusu shoka la mtihani wa kitaifa ambalo lilikuwa laning'inia kichwani pangu. Sikupata uhondo wa mlo huo ilivyokuwa desturi kila asubuhi. Nina aliniaga na kunitakia heri za Mola.

Saa thenashara, nilikuwa nimeshika njia na kuchapua milundi kuelekea shuleni. Kimya kilishamiri kote, pote na mote njiani. Giza la usiku lilikuwa limeanza kutokomea huku likipisha miale ya jua la mathlai. Miale nayo ikafukuza umande ambao ulipaa mithili ya moshi. Baada ya kutembea kwa kitalifa cha kilomita tatu, hatimaye nilifika njia panda. Hapo ndipo tuliafikiana kuonana ana kwa ana na Asiya. Tuliamkuana na kutaniana kisha tukaendelea na safari yetu. Mikono iliyosheheni matopa ya vitabu ilitutiririsha si haba. Si kwapani, si kipajini si kwenye uti wa mgongo. Tukaloa chepechepe. Zilikuwa zimesalia kilomita mbili.

Mazungumzo yetu yalikuwa kuhusu mitihani. Tukayadadafua maswali na kujaribu kukisia yale ambayo yangetahiniwa. Asiya alinitia moyo. Hii ni baada ya kunikumbusha kwamba maswali mengi tulikuwa tumeyashughulikia katika muhula wa tatu. Jakamoyo ikaniyeyuka. Nikahisi mshindi wa washindi.

Baada ya takribani dakika sitini tulikuwa tumewasili. Lango la shule likatukaribisha. Tukaingia na. kuanza kudurusu. Asiya akakisumbua kichwa changu kwa maswali. Ingawa nilikuwa nimelemewa sikukata tamaa. Nilijua hisabati ndilo lilikuwa somo lililotia jekejeke, lakini wa zama waliamba kuwa papo kwa papo kamba hukata jiwe. Watahiniwa wengine walianza kuingia mmoja mmoja, wawili wawili au makundi. Walimu nao wakafuata. Saa mbili kamili mkirizi wa kengele ulisikika. Ishara tosha kwamba ni wakati wa gwaride. Sote tukakusanyika pale. Walimu wakaongea. Ushauri na maagizo yakatolewa, kisha kila mmoja akaingia katika chumba cha mtihani. Madarasa manne, kila chumba na watahiniwa ishirini.

Karatasi nyeupe pepepe ikatua usoni pangu. Nilikuwa nimetuona ingawa kuna wale walioonekana kuhaha. Nilijiamini siku ya kwanza ikakamilika nikiwa mwingi wa bashasha. Ya pili na tatu mtindo ukawa ni uleule.

Sekunde ziliunda dakika. Dakika nazo zikawa saa. Saa zikawa siku. Hatimaye matokeo yakatangazwa. Sikuyaamini macho na masikio yangu. Jina langu lilikuwa kwenye orodha ya wanafunzi kumi bora nchini. Macho ya furaha njia mbilimbili, kutahamaki, nikaona umati ukiingia ukiongoza na kamera.

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza si kweli kuwa
    1. maneno ya Bwana Busara yalimfanya mwandishi arauke
    2. Bwana Busara alikuwa mwalimu mwenye nasaha
    3. yamkini wanafunzi wengine walikuwa wazembe
    4. wanafunzi walikuwa wakijiandaa kuukalia mtihani wa kitaifa. 
  2. Aya ya pili inatudokezea kuwa
    1. mseto wa mawazo ulitokana na rai za mwalimu
    2. shoka lilikuwa lamngoja mwandishi
    3. chakula kilikuwa chapwa siku hiyo
    4. mamake mwandishi alikuwa amewajibika.
  3. Kutoka kwa mwandishi hadi shuleni ni umbali wa
    1. mita tatu
    2. kilomita nne
    3. kilomita tatu
    4. mita mia moja.
  4. "Hapo ndipo tuliafikiana kuonana ana kwa ana". Hii ni fani gani?
    1. Nahau
    2. Chuku
    3. Tasbihi
    4. Msemo
  5. Jasho lililowatoka ilichangiwa na
    1. uchovu
    2. mwendo mrefu
    3. uzito wa vitabu
    4. woga.
  6. Kutoka kiamboni hadi shuleni, mwandishi alitembea kwa
    1. saa moja
    2. zaidi ya dakika sitini
    3. karibu saa moja
    4. saa mbili.
  7. Somo la hisabati
    1. lilimfanya mwandishi kuingiwa na wasiwasi
    2. lilimlemea siku ya mtihani
    3. lilimfanya atie bidii kwa mazoezi
    4. lilifanya wakutane na Asiya
  8. Ni kauli gani iliyo sahihi?
    1. Watahiniwa wote walikuwa themanini.
    2. Watahiniwa walikuwa na jekejeke.
    3. Kengele iliashiria mwanzo wa mtihani.
    4. Mtahiniwa hakuwa na matumaini ya kupasi.
  9. Yamkini furaha ya mwandishi ilitokana na
    1. kufanya mtihani wa kwanza 
    2. kusaidiwa na rafikiye kwenye chumba cha mtihani
    3. kuona wepesi wa maswali
    4. kupata majibu yote ya mitihani.
  10. Kichwa mwafaka kifaacho habari hii ni
    1. Shule ya Msingi
    2. Mtihani wa kitaifa
    3. Papo kwa papo kamba hukata jiwe
    4. Bidii haindoi kudura

INSHA   

Malizia insha yako kwa maneno haya;

...................Hapo ndipo nilipoamini kuwa chanda chema huvikwa pete.

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. C
  4. A
  5. D
  6. C
  7. A
  8. C
  9. D
  10. B
  11. C
  12. D
  13. A
  14. A
  15. C
  16. D
  17. B
  18. A
  19. C
  20. D
  21. D
  22. B
  23. D
  24. C
  25. B
  26. A
  27. C
  28. D
  29. C
  30. D
  31. B
  32. A
  33. C
  34. D
  35. C
  36. A
  37. D
  38. D
  39. C
  40. B
  41. A
  42. D
  43. B
  44. D
  45. B
  46. C
  47. C
  48. A
  49. C
  50. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 12.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students