Friday, 31 March 2023 06:08

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 7

Share via Whatsapp Written by
Rate this item
(0 votes)

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 1-5

Katee alimwalika rafiki Kilo wanywe chai mjini. Kilo aliomba waandamane na binamu yake koko. Basi Kilo alimwambia Koko ajiandae waende mjini Koko alifurahi sana na akajiandaa upesi.

Walipofika mjini, walimkuta Katee akiwasubiri katika hoteli iliyoitwa Fahari. Waliagiza chai na mandazi. Wakaletewa vikombe, sukari kwenye kikopo na vifuko vya majani.

Koko alichukua kifuko cha majani alikuwa tayari kukirarua ili ayatie majani kwenye kikombe Kilo alipoona vile alishtuka sana. Akashika bega na kumtuliza.

"Kaka kwanza tuiombee chai" Kilo alimsihi kwa sauti ya chini. Badala ya kuomba Kilo alimshauri Koko kwa lugha ya mama kuhusu jinsi ya kutumia kifuko kile cha majani. Hakutaka Koko awatie aibu pale hotelini.

  1. Kwa nini Koko alifurahi?
    1. Kwa sababu alikuwa aende mjini
    2. Alikuwa amepita mtihani wake
    3. Alikuwa ametumwa mjini
    4. Alikuwa amepewa zawadi na Kilo
  2. Vyote hivi vililetwa mezani kule mkahani ila
    1. sukari
    2. majani
    3. mandazi
    4. sharubati
  3. Neno hoteli liko katika ngeli ya
    1. I-I
    2. I-ZI
    3. LI-YA
    4. U-ZI
  4. Ni kweli kusema kuwa
    1. Katee na Kilo walimchukia Koko
    2. Koko hakufahamu jinsi ya kutumia kifuku. cha majani
    3. Koko ndiye aliombea chai
    4. Watatu hawa hawakupenda chai
  5. Kwani nini Kilo alimshauri Koko kwa lugha ya mama? Kwa sababu
    1. ndiyo lugha tu angeelewa
    2. hakufahamu vyema Kiswahili
    3. alitaka watu wengi wasisikize alivyomweleza jinsi ya kutumia mayai
    4. ndiyo lugha ya taifa

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu swali 6-10.

Nina rafiki mmoja, mwenye mguu mmoja
Tunapokuwa pamoja, mimi huona kioja
Anasema ngoja haja, napiga hatua moja
Fumbo hili ni la haja, jibu lake hilo laja.

Rafiki huyo mmoja, mwenye muundi mmoja
Ana jina lake moja, ni uyoga nalitaja
Nilimla siku moja, alipikwa na Khadja
Fumbo hili ni la haja, jibu lake hilo laja

Nina rafiki wa pili, nikila anajongea
Japo yeye hali, mezani amezoea
Rafiki huyo mkali machozi ananitoa
Matega kitendwali, fumbo ninakufumbia

Huyo rafiki wa pili, sasa namueleza
Ni kiungo cha halali, wengi wamekizoea
Kinaitwa pilipili, machoni kinasumbua
Nategua fumbo hili, jibu nimekupatia

  1. Mshairi ana rafiki mmoja mwenye mguu mmoja, rafiki huyo anaitwa?
      1. Bendera
      2. Uyoga
      3. Pilipili
      4. Kiungo
  2. Ni ipi ni sifa ya rafiki wa pili wa mshairi?
    1. Yeye humfanya atabasamu
    2. Humtoa machozi machoni
    3. Humtoa neno kinywani
    4. Ni mtamu kama hatua
  3. Shairi hili lina beti ngapi?
    1. Tano
    2. tatu
    3. Sita
    4. Nne
  4. Vina vya kati katika ubeti wa mwisho ni?
    1. a
    2. li
    3. u
    4. ja
  5. Neno kioja lina silabi ngapi?
    1. Tatu
    2. Nne
    3. Tano
    4. Mbili

Soma kifungu hiki kwa makini kisha uchagua jibu bora zaidi kujazia mapengo yaliyoachwa 11-15.

Katika shule ___11___ kuna duka. Duka hili ___12___ na wanaskauti. Bidhaa ___13___ huuzwa dukani humo ni ___14___ kalamu, madaftari, vichongeo na vifutio. Wanaskauti hutumia ___15___ inayotokana na maunzo ya bidhaa hizi kuwasaidia watoto wenye mahitaji ya kimsingi.

   A   B   C   D 
 11.   yetu   kwetu   sababu   petu 
 12.  linaposimamia   linasimamisha   linasimamiwa   linasimamika 
 13.  ambayo  ambazo   ambako   ambamo 
 14.  ,  !  ;  ?
 15.  riba  hisa   kodi   faida 

 

Kuanzia swali la 16-30. Jibu kulingana na maagizo.  

  1. Kati ya maneno haya chagua neno linalopatikana kati ngeli ya U-I
    1. mali
    2. nywele
    3. mpera
    4. kucheza
  2. Maneno yafuatayo hupangwa vipi kwenye kamusi gonga, ganda, gamba, godoro.
    1. ganda, gamba, godoro, gonga 
    2. gamba, gonga, ganda, godoro
    3. ganda, gamba, gonga, godoro
    4. gamba, ganda, godoro, gonga
  3. Andika kwa wingi
    Wavu wa mvuvi unastahili kuwa na shimo kubwa
    1. Nyavu za mvuvi zinastahili kuwa na shimo kubwa
    2. Nyavu za wavuvi zinastahili kuwa na mashimo makubwa
    3. Nyavu za wavuvi zinastahili kuwa na shimo kubwa
    4. Wavu za wavuvi zinastili kuna na mashimo makubwa
  4. Kanusha:
    Maseremala walitutengenezea madawati
    1. Maseremala hawakututengenezea madawati
    2. Maseremala hakutengeneza madawati
    3. Seremala alitulengenezea dawati
    4. Maseremala waliharibu madawati
  5. Ukubwa wa neno mlango ni
    1. Kilango
    2. jilango
    3. mlango
    4. lango
  6. Umesimuliwa hadithi na mlezi wako sasa ni wakati wa kulala. Chagua maagano utakayotumia kumwaga mlezi wako
    1. kwaheri
    2. alamsiki
    3. masalkheri
    4. buriani
  7. Changua methali inayotoa maana na maelezo kuwa mtoto huchukua tabia za walezi na watu walio karibu naye
    1. Mwana hutazama kisogo cha mamaye
    2. Mchelea mwana hulia mwenyewe
    3. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu 
    4. Mchimba kisima huingia mwenyewe
  8. Wachezaji wana nidhamu _______________________ huheshimu refarii.
    1. wao
    2. wewe
    3. yeye
    4. nyinyi
  9. Tunasema thureya ni kwa nyota. Tutasema ______________________ ni kwa nyuki.
    1. bunda
    2. bumba
    3. wingu
    4. mkusanyiko
  10. Levi ni wembe masomoni. Hii ina maana kuwa yeye ni _________________________
    1. mwenye subira
    2. jasili
    3. mwenye bidii
    4. mwerevu
  11. Ni sentensi ipi sahihi.
    1. Palipo na siafu hakukaliki
    2. Palipo na siafu hamukaliki
    3. Mlimo na siafu hapakaliki
    4. Kuliko na siafu hakukaliki
  12. Tegua kitendawili
    Niendapo hinifuata _______________________
    1. mauti
    2. kivuli
    3. jua
    4. nzi
  13. Kipi si kiungo cha mapishi?
    1. Sukari
    2. Bizari
    3. Unga
    4. Nyanya
  14. Kitenzi nawa katika kauli ya kutendesha ni
    1. navya
    2. nawisha
    3. nawishia
    4. nawia
  15. Tunda lilianguka sakafuni
    1. kacha!
    2. chubwi!
    3. pu!
    4. tifu!

MARKING SCHEME

  1. A
  2. D
  3. B
  4. B
  5. C
  6. B
  7. C
  8. D
  9. B
  10. A
  11. A
  12. C
  13. B
  14. C
  15. D
  16. C
  17. D
  18. B
  19. A
  20. D
  21. B
  22. A
  23. A
  24. B
  25. D
  26. D
  27. B
  28. C
  29. A
  30. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 7.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 2713 times Last modified on Tuesday, 04 April 2023 07:33

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.