Thursday, 09 March 2023 07:44

Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 1 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Kusikiliza na kuzungumza

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5

G4swaT1T23002P1

Chichi:   (akibisha mlango) Hodi!
Jabari:   (kwa furaha) karibu! Ni nani tafadhali?
Chichi:   Rafiki yako Chichi.
Jabari:   Karibu sana sahibu. Nimekungojea sana ufike ili tushinde pamoja leo.
Chichi:   Asante kwa makaribisho. Sebule yenu inafurahisha sana.
Jabari:   Namshukuru Mungu kwa kuwasaidia wazazi wangu kununua meza ya kisasa, makochi, televisheni, mazulia na mapazia mazuri.
Chichi:   (Akiangalia juu) Balbu zenu za stima zinapendeza sana.
Jabari:   (akiwasha umeme) Tazama, zina rangi tofautitofauti.
Chichi:   (akiikagua meza) Matendegu haya ya meza yametengenezwa kwa ufundi sana.
Jabari:   Seremala aliyeyatengeneza ni hodari. Pia alitengeneza fremu ya mlango wetu. Angalia vile inavutia.
Chichi:   Kusema kweli nyumba yenu inapendeza. Kabla sijarudi kwetu leo nitakusaidia kuipiga deki.
Jabari:    Asante Chichi. Usafi ni kitu muhimu.
(wote wanaketi na kupanga shughuli za siku hiyo)

  1. Ni jambo gani la heshima ambalo Chichi alifanya alipofika kwa rafiki yake?
    1. Kubisha hodi
    2. Kufurahi
    3. Kukaribishwa
    4. Kungojewa
  2. Kulingana na mazungumzo haya neno rafiki ni sawa na:
    1. Chichi
    2. Jabari
    3. Sahibu
    4. Karibu
  3. Sebule ya akina Jabari ina vitu hivi vyote isipokuwa?
    1. Makochi
    2. Balbu
    3. Meza
    4. Picha
  4. Gani kati ya vitu hivi huwa na matendeguu?
    1. Zulia
    2. Pazia
    3. Meza
    4. Balbu
  5. Ni shughuli gani ambayo Jabari na Chichi watafanya ili kutunza usafi?
    1. Kupiga deki
    2. Kuketi
    3. Kupanga shughuli za siku
    4. Kula pamoja

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali 6-9    

G4swaT1T23002P2

Chui na punda walikuwa marafiki wa chanda na pete. Walikuwa wakiishi msituni. Wakati mwingine walikuwa wakitofautiana kuhusu mambo fulani.

Siku moja Punda alimwambia Chui kuwa nyasi ni za rangi ya samawati. Chui alimpinga na kusema kuwa nyasi ni za rangi ya kijani. Walizozana sana kuhusu rangi ya nyasi mpaka
wakakosana.

Ili kupata suluhisho walienda kwa Simba ambaye alikuwa mfalme wa wanyama. Punda alikimbia mbele ya Chui na kumwambia Simba, "Nyasi ni za rangi ya kijani, kweli ama si kweli?" Simba akasema ni kweli. Chui naye akaja na kusema, "Nyasi ni za rangi ya kijani." Simba akamuuliza, "Ni nani hajui hivyo?"

Chui aliposikia hivyo alifurahi sana na kumwomba Simba amwadhibu Punda. Simba alimwadhibu Chui licha ya kuwa alisema ukweli. Aliadhibiwa kwa sababu ya kuzozana na punda ambaye alichukuliwa kuwa mnyama mjinga kuliko Chui.

  1. Punda na Chui walitofautiana kuhusu nini?
    1. Mfalme na wanyama
    2. Rangi ya nyasi
    3. Msituni
    4. Chakula
  2. Kulingana na kifungu mfalme wa wanyama alikuwa nani?
    1. Simba
    2. Chui
    3. Punda
    4. Nyasi
  3. Ni wanyama wangapi waliotajwa katika kifungu hiki?
    1. Mmoja
    2. Wawili
    3. Wanne
    4. Watatu
  4. Kulingana na kifungu hiki tunajifunza nini?
    1. Hatufai kuzozana na Punda kwani tunaweza kuadhibiwa na Simba.
    2. Mtu akiwa mwerevu kuliko mwingine anaweza kuadhibiwa.
    3. Simba, Chui na Punda ni wanyama wa msituni.
    4. Hatufai kuzozana na watu wasioelewa mambo kwani tunaweza kuingia hatarini.

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali 10-12   

Siku moja Jawabu aliambiwa na wazazi wake aeleze kuhusu nidhamu ya mezani. Pia aliambiwa aeleze faida zake. Aliwaomba kwa heshima wamruhusu aandike kwenye karatasi.

 Tabia yenye nidhamu   Faida zake 
 Kumshukuru Mungu  Huonyesha heshima kwa Mungu  
 Kunawa mikono kabla ya kula   Kuepuka magonjwa
 Kula kwa utaratibu  Huwezi ukatapika
 Kula bila kuongea  Hutachafua chakula cha wengine 
 Kunawa mikono baada ya kula   Kutunza usafi wa mtu binafsi

Wazazi wake waliposoma walifurahi sana kwa sababu mtoto wao anaelewa nidhamu mezani na umuhimu wake.

  1. Jawabu aliambiwa na wazazi wake aeleze kuhusu nini?
    1. Nidhamu
    2. Nidhamu mezani
    3. Nidhamu ya mezani na faida zake.
    4. Mezani
  2. Mtu akikosa kunawa mikono kabla ya kula atapata hasara gani?
    1. Atatapika
    2. Atachafua nguo zake
    3. Hatashiba
    4. Anaweza kunata maad
  3. Ni tabia gani nyingine ambayo Jawabu angeongeza kwenye orodha yake?
    1. Kutazama runinga ukila chakula.
    2. Kutumia simu wakati wa kula.
    3. Kula ukiwa umeketi vizuri na kutulia.
    4. Kula ukisoma kitabu cha hadithi.

Soma kifungu kifuataccho kisha ujibu maswali 13 - 15.  

G4swaT1T23002P3

Wekeza ni mfanyabiashara hodari katika Jiji la Mtaji. Ana duka kubwa sana la mavazi. Watu wote; wazee kwa vijana, matajiri kwa maskini, wanawake kwa wanaume hununua mavazi katika duka hilo.

Mavazi hayo yamepangwa ya kiume kando na ya kike kando. Sehemu ya mavazi ya kiume ina suruali, kaptura, mashati, tai, suti, soksi, chupi na mavazi mengineyo. Upande wa mavazi ya kike kuna; marinda, blauzi, chupi, suti, sketi, sidiria, mitandio na mengineyo.

Duka hilo pia lina mavazi ya wakati wa baridi kama vile makoti na sweta. Aidha kuna mavazi ya wakati wa kazi kama vile ovaroli. Isitoshe kuna sehemu ya viatu, mishipi, kofia, soksi na sare za wanafunzi.

Wanunuzi wengi huenda katika duka hilo kwani bidhaa huuzwa kwa bei nafuu.

  1. Duka lililoelezewa liko katika jiji gani?
    1. Hodari
    2. Mfanyabiashara
    3. Wekeza
    4. Mtaji
  2. Kulingana na kifungu ni mavazi gani yameambatanishwa vizuri na wanaoyavaa? 
    1. Blauzi-wanaume
    2. Shati- wanawake
    3. Sare- wazee
    4. Ovaroli-wafanyakazi
  3. Kwa nini wanunuzi wengi huenda katika duka la Wekeza?
    1. Lina bidhaa nyingi.
    2. Bidhaa huuzwa kwa bei nafuu.
    3. Duka liko jijini.
    4. Duka hilo lina mavazi yote.

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo Zaidi kati ya yale uliyopewa.

Nyumba ___16___ ni ___17___. Jikoni kuna mawe ___18___ ya kupikia yanayoitwa ___19___. Sisi huitunza nyumba yetu ___20___.

   A   B   C   D 
 16.   wetu   yetu   chetu   letu 
 17.  nzuri  mzuri   zuri   mizuri 
 18.  watatu   mitatu   tatu  matatu 
 19.  mchi  mvungu   mafiga   makochi 
 20.  nzuri  vizuri   mzuri   wazuri 

Kutoka swali 21-30, chagua jibu sahihi. 

  1. Ni maamkuzi gani ambayo hayajajibiwa vizuri?
    1. U mzima?- ni mzima
    2. Alamsiki-binuru
    3. Makiwa- tunayo au yamepita
    4. U hali gani?- nawe pia
  2. Ni kundi gani la maneno yaliyoambatanishwa sawasawa na aina yake? 
    1. Zuri, -baya-,refu, -fupi- vivumishi
    2. Soma, andika, keti, simama- nomino
    3. Mvungu, tumbuu, kizingiti, globu- viwakilishi
    4. Mimi, wewe, yeye, wao- vitenzi
  3. Ni sentensi gani haina kielezi?
    1. Nilikula wali jana.
    2. Mwalimu mzuri anafundisha.
    3. Wanafunzi wanacheza uwanjani.
    4. Mtoto alikula polepole.
  4. Ni kifaa gani cha nyumbani kimeambatanishwa sawasawa na jina lake?
    G4swaT1T23002P4
  5. Ni kundi gani lina mpangilio mzuri wa maneno kama yanavyofuatana katika kamusi?
    1. Kinu, kisu,mwiko,mchi
    2. Zulia,tumbuu,pazia,fremu
    3. Kula,nawa,pakua,pika
    4. Salamu, salama, salimu,sala
  6. Badilisha sentensi hii katika umoja: vyakula vyao vimepikwa.
    1. Chakula chake kimepikwa.
    2. Vyakula vyake vimepikwa.
    3. Chakula chao kimepikwa.
    4. Chakula changu kimepikwa.
  7. Ni sentensi gani si kitanzandimi?
    1. Baba alivua papa.
    2. Mama alitoa doa.
    3. Kuku alikula gugu.
    4. Jana aliandika jina.
  8. Unapoandika insha unafaa kuzingatia haya yote isipokuwa
    1. Anwani
    2. Mpangilio mzuri wa mawazo
    3. Hati safi
    4. Michoro mizuri
  9. Ni sentensi gani yenye kiulizi?
    1. Wewe una nidhamu mezani? C
    2. Seremala alitengeneza mtoto wa meza.
    3. Wacha kula ovyoovyo!
    4. Alifagia, akapiga deki na kupanga nyumba.
  10. Tazama picha kisha ujibu swali
    G4swaT1T23002P5
    Chombo hiki kinaitwaje?
    1. Tarakilishi
    2. Televisheni
    3. Redio
    4. Simu

INSHA

Kuandika (Alama 10)

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Andika insha juu ya:

                                                                       RAFIKI YANGU

______________________________________________________________________________________

MARKING SCHEME

  1. A
  2. C
  3. D
  4. C
  5. A
  6. B
  7. A
  8. D
  9. D
  10. C
  11. D
  12. C
  13. D
  14. D
  15. B
  16. B
  17. A
  18. D
  19. C
  20. B
  21. B
  22. A
  23. B
  24. C
  25. C
  26. C
  27. D
  28. D
  29. A
  30. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 1 Exams 2023 Set 1.

Tap Here to Download for 30/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students