Wednesday, 26 April 2023 07:26

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 1 Exams 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata,
GRD4DSTICNKISWQN1

Fanaka ni mwanafunzi mzuri sana. Mwaka huu wa 2023, amejiunga na gredi ya nne. Fanaka anapendwa na marafiki zake kwa sababu ana tabia nzuri. Hii ndiyo sababu Fanaka ana marafiki wengi katika darasa lao. Vilevile, Fanaka anapendwa na walimu wote katika shule hiyo kutokana na nidhamu aliyo nayo. Fanaka hufanya kazi zote anazopewa na walimu wake. Kila anapoamka asubuhi, saa kumi na mbili kamili, Fanaka huomba ili kumshukuru Mungu kwa kumlinda usiku wote. Baada ya kupiga dua, yeye huingia msalani kwa haja kisha akatoka. Fanaka husugua meno yake kwa mswaki na dawa ya meno. Kisha yeye huingia hamamuni na kuoga akitumia sabuni, maji safi na dodoki. Yeye hujipaka mafuta, akazichana nywele zake kisha akavaa sare yake. Fanaka huondoka na kuelekea langoni pao ambapo yeye hupanda basi la shule na kuelekea shuleni.

  1. Kutokana na nidhamu ya Fanaka,
    1. ana marafiki wengi.
    2. anapendwa na walimu wengi.
    3. .anapendwa na walimu wote.
    4. anapendwa na wanafunzi wote.
  2. Kulingana na ufahamu, Fanaka ni mwanafunzi mwenye tabia gani?
    1. mwenye bidii
    2. mzembe
    3. asiyetii
    4. anayesumbua
  3.  Kwa nini Fanaka anapendwa na marafiki zake?
    A. Anajua kucheza
    B. Huwabebea chakula
    C.Wanaishi pamoja
    D. Ana tabia nzuri
  4. Kifungu kinaeleza kuwa Fanaka huamka saa ngapi?
    1. 12:00 
    2. 8:00
    3. 6:00
    4. 7:00
  5. Kulingana na kifungu, Fanaka alikuwa katika gredi ya tatu mwaka gani?
    1. .2023
    2. 2021
    3. 2022
    4. 2020
  6. Kwa nini Fanaka huomba anapoamka?
    1. Kumshukuru Mungu kwa kumlinda mchana wote
    2. Ili Mungu amlinde mchana wote
    3. .lli Mungu amlinde usiku wote
    4. .Kumshukuru Mungu kwa kumlinda usiku wote
  7. Unadhani Fanaka hufanya nini baada ya kutoka msalani?
    1. Hunawa mikono yake
    2. Hujipaka mafuta
    3. Hupangusa mikono yake
    4. Hujipaka sabuni
  8. Nini ambacho Fanaka huwa hatumii anapoenda kuoga?
    1. sabuni
    2. mswaki
    3. maji
    4. dodoki

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
GRD4DSTICNKISWQN2

Maadili ni tabia nzuri katika maisha ya mtu. Mtu mwenye tabia nzuri ni mtu mwadililifu. Tabia nzuri ni nyingi katika maisha. Tabia hizo ni kama vile bidii, upendo, heshima, uzalendo, ushirikiano na uvumilivu. Uzalendo ni tabia ya kuipenda nchi yako sana. Kila mmoja wetu anafaa kuipenda nchi ya Kenya kwa moyo wote. Ukiipenda nchi yako, basi wewe utakuwa mzalendo. Bidii nayo ni muhimu sana katika maisha. Bidii humsaidia mtu kufaulu katika kila sehemu. Bidii inahitajika katika michezo, masomo, kilimo na sehemu nyingine. Ushirikiano nao una faida sana. Mambo mengi huhitaji umoja na ushirikiano ili kufaulu. Ni vyema uishi kwa kushirikiana na wanafunzi wenzako katika shughuli mbalimbali. Kujifanyia mambo pekee yako kila mara si vizuri. Hii ni kwa kuwa umoja ni nguvu, utendano ni udhaifu.

  1. Ufahamu unaeleza kuwa maadili ni nini?
    1.  tabia maishani
    2. tabia mbaya maishani
    3. tabia nzuri maishani
    4. tabia nyingi maishani
  2. Kulingana na ufahamu, mtu mwenye tabia nzuri ni;
    1. mwaminifu
    2.  mwadilifu
    3. mvumilivu
    4. mtiifu
  3. Gani si maadili kwenye orodha ifuatayo?
    1. uchoyo 
    2. upendo
    3. heshima
    4. uzalendo
  4. Mtu anayeipenda nchi yake sana
    husemekana kuwa yeye ni;
    A. Mvumilivu
    B. Mwenye bidii
    C.Mzalendo
    D. Mtulivu
  5. Mtu anayehitaji kufaulu katika kila sehemu lazima awe na nini?
    1. bidii
    2. upendo
    3. heshima
    4. uvumilivu
  6. Wapi ambapo hatuhitaji bidii katika maisha?
    1. masomo
    2. kulala
    3. michezo
    4. kilimo
  7. Tunafaa kushirikiana kwa kuwa umoja ni nguvu,
    1. ushirikiano ni muhimu.
    2. utengano haufai.
    3. utengano ni udhaifu.
    4. ushirikiano unafaa.

Chagua jibu linalofaa ili kujazia kila nafasi iliyoachwa.

Kijana        16        alitoka nyumbani kwao asubuhi na mapema. Jina        17          kijana huyo lilikuwa Kamau. Kamau alikuwa akienda katika shule      18         kwa sababu ilikuwa siku ya michezo. Siku    19        Kamau na wenzake walicheza michezo kama vile kandanda, kibemasa, jugwe na kadhalika. Wakati wa      20        ulipofika, wote walirudi nyumbani kwa furaha.

16  A kimoja  B. moja  C. mmoja  D. wawili 
 17  . A. cha  B. ya  C. la  D. wa
 18  A. yao  B. lao  C. zao  D. mwao
 19  A. huo B. hiyo  C. hilo  D. hicho
 20  A. alfajiri  B. usiku  C. asubuhi  D. jioni

Jibu maswali yanayofuata kulingana na maagizo.

  1. Tambua nomino kwenye sentensi ifuatayo. Mwanafunzi ameingia ndani ya darasa. 
    1. mwanafunzi, darasa
    2. ameingia, ndani ya
    3. mwanafunzi, ndani ya
    4. ameingia, darasa
  2. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
    Mtoto huyu anacheza, yule analala.
    1. kivumishi, kiwakilishi
    2. kiwakilishi, kivumishi
    3. kivumishi, kivumishi
    4. kiwakilishi, kiwakilishi
  3. Mchoro ufuatao unaonyesha nini?
    GRD4DSTICNKISWQN23
    1. mafiga 
    2. tumbuu
    3. balbu
    4. kinu
  4. Jibu gani linaloonyesha kitenzi?
    1. mama
    2. kikubwa
    3. polepole
    4. soma
  5. Tambua sehemu ya tarakilishi iliyoonyeshwa kwa herufi 'Y'
    GRD4DSTICNKISWQN3.
    1. kiwambo
    2. kitengo kikuu cha uchakataji
    3. bodidota
    4. kebo
  6. 'Lo!, Ala!, Salaala!' ni mifano ya.
    1. vihusishi 
    2. vivumishi
    3. vihisishi
    4. vitenzi
  7. Jaza nafasi kwa jibu linalofaa zaidi.
    Mtoto ameanguka              hajalia.
    1. lakini
    2. na 
    3. kwa sababu
    4. tena
  8. Unapokutana na nyanya yako wakati wa jioni, utamwamkuaje?
    1. hujambo
    2. habari ya jioni
    3. salaam aleikum
    4. shikamoo
  9. Onyesha kihusishi kwenye sentensi ifuatayo.
    Paka amesimama juu ya meza.
    1. meza
    2.  juu ya
    3. amesimama 
    4. paka
  10. Tegua kitendawili; Nifungue nikufunike.
    1. viatu
    2. mwavuli
    3. kofia
    4. macho

INSHA 

Andika insha ya wasifu kuhusu ; 

MWALIMU WANGU 



MARKING SCHEME 

  1. C
  2. A
  3. D
  4. C
  5. C
  6. D
  7. A
  8. B
  9. C
  10. B
  11. A
  12. C
  13. A
  14. B
  15. C
  16. C
  17. C
  18. A
  19. B
  20. D
  21. A
  22. A
  23. A
  24. D
  25. C
  26. C
  27. A
  28. D
  29. B
  30. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 1 Exams 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students