- Ratiba ni orodha ya mpangilio wa namna mambo yatakavyofuatana katika shughuli fulani.
- Lengo lake ni kuhakikisha wakati unatumiwa vizuri ili mambo fulani yasije yakakosa kutendwa kutokana na upungufu wa wakati.
- Ratiba hutumika katika sherehe, mikutano, mazishi, hafla, tamasha, n.k
Sehemu za Ratiba
- Kichwa
- Kichwa cha ratiba hutaja mambo yafuatayo:
- Shughuli yenyewe - Taja jina la tukio ambalo unaandalia ratiba. Kwa mfano Harusi ya Bwana na Bi Arusi, Siku ya Zawadi
- Tarehe ya shughuli - je shughuli hiyo itafanyika lini?
- Mahali- Taja mahali ambapo shughuli hiyo itafanyikia. kwa mfano katika uwanja wa michezo wa Kasarani, kanisa la St. Mtakatifu
- Mfano wa kichwa cha ratiba:
- Ratiba ya Hafla ya Ukimwi katika Bustani la Uhuru tarehe tano Januari.
- Ratiba ya Mazishi ya Dkt. Marehemu tarehe 20/12/1923 Kijijini Vikwazoni
- Kichwa cha ratiba hutaja mambo yafuatayo:
- Mwili
- Mwili wa ratiba hujumuisha mambo mbalimbali yatakayofanyika katika mpangilio maalum, saa mbalimbali. Ni vizuri kuzingatia vipengele vifuatavyo:
- Saa - Onyesha saa ambazo tukio limepangiwa kuanza hadi linapotakiwa kumalizika
- Mahali - Ikiwa shughuli tofauti zinafanyika katika mahali mbalimbali kama vile vyumba tofauti, inapaswa hutaje mahali ambapo kila jambo litafanyikia.
- Wahusika - Taja mtu au watu waliopewa wajibu wa kutekeleza jambo fulani. Hii huwasaidia kujitayarisha ipasavyo.
- Mwili wa ratiba hujumuisha mambo mbalimbali yatakayofanyika katika mpangilio maalum, saa mbalimbali. Ni vizuri kuzingatia vipengele vifuatavyo:
Mfano wa Ratiba
RATIBA YA MAZISHI YA MZEE MAUTI TAREHE 20/12/1923 KIJIJINI MIZUKANI
SAA | SHUGHULI |
07: 00 | Marafiki wa Mauti watoa mwili kutoka SlowDeath Hospital |
10: 30 | Maombi katika kanisa la G.I.Z.A yakiongozwa na Pst. Muna Fiki |
11: 15 | Mwili kuwasilishwa nyumbani, familia ya Mauti |
12: 00 | Kupakuliwa kwa chakula na Bi Kamafisi, Bi Mwachafu na wapishi walioteuliwa |
1: 10 | Kukusanyika kwa umati |
2: 00 | Maombi ya kuanzisha shughuli za mazishi |
2: 30 | Shuhuda zikiongozwa na Mzee Siachwinyuma |
3: 00 | Ushuhuda wa serikali na Chifu Mtesi |
3: 40 | Kuteremshwa kwa mwili kaburini na vijana walioteuliwa |
4: 00 | Shukrani za Mwisho, na Mwenyekiti wa Chama cha Kufa Tukusaidie |
6: 00 | Kugawana mali ya marehemu, na wazee wa kijiji |
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Insha ya Ratiba - Kiswahili Insha Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students