Maswali na Majibu ya Dondoo Katika Mapambazuko ya Machweo

Share via Whatsapp

Utangulizi

Hati hii ina maswali ya Mapambazuko ya Machweo na majibu.

Waweza kupata maswali na majibu ya Mapambazuko ya Machweo in PDF kwenye tovuti ya EasyElimu au The EasyElimu Study App.

Hadithi zote katika kitabu cha Mapambazuko ya Machweo zimenakiliwa.

Unaweza kupata mwongozo wa hadithi zote ikijumuisha:

  • Fadhila za Punda
  • Msiba wa Kujitakia
  • Mapamazuko ya Machweo
  • Harubu ya Maisha
  • Mzimu wa Kipwerere!
  • Kila Mchezea Wembe
  • Kifo cha Suluhu
  • Ahadi ni Deni
  • Toba ya Kalia
  • Nipe Nafasi
  • Nilitamani
  • Pupa
  • Sabina

Pata maswali ya mapambazuko ya machweo pdf download hapa.

Pia, pata Mapambazuko ya Machweo summary notes pdf.

Swali 1

Kifo cha Suluhu maswali na majibu
...iwapo penzi hili litatia doa,basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa penzi langu kama jongoo na mti wake..."

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika  dondoo hili. (alama 4)
  3. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)
  4. Eleza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti. (alama 6)

Majibu

"...iwapo penzi hili litatia doa, basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa penzi langu kama )ongoo na mti wake...

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    • Haya ni maneno ya Suluhu kwa Abigael kama yanavyokumbukwa na Abigael. Walikuwa katika chumba walichozoea kwenda kuzituliza nafsi zao wakiwa na Suluhu. Aliyakumbuka maneno haya wakati alikuwa amekwisha kichomoa kisu kwenye mfuko alionunuliwa na Suluu huku akitaka kumuua.
  2. Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika dondoo hili. (alama 4)
    1. Nahau - tia doa.
    2. Tashbihi - kulitupa penzi langu kama jongoo na mti wake.
  3. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)
    • 'Ni muasherati - japo ana mke ana wapenzi wa kando kama Abigael.
    • 'Ni katili alifikiria namna ya kumuangamiza mkewe abaki na Abigael.
    • 'Ni msaliti - anaisaliti familia yake kwa kuitelekeza.
    • .Ni mlezi mbaya- anamwachia mkewe Bi. Suluhu mzigo wa kuwalea watoto wao na kumwambia ni wake pekee.
    • .Ni kiongozi mbaya - haleti maendeleo katika eneobunge lake kw alitumia pesa za umma kuwalipa mabinti wa Chuo kikuu kwa kula uroda nao.
  4. EIeza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti. (alam 6)
    • Msemewa ni Abigael.
    • Kupitia kwa Abigael tunaonyeshwa namna Bw. Suluhu alivyokuwa ameoza kitabia kwa kula uroda na mabinti wa Chuo kikuu.
    • Kupitia kwa Abigael tunajua kuwa Bwana Suluhu alikuwa tajiri mwenye mali na pesa nyingi zilizosababisha utovu wa amani kwa mkewe.
    • Kupitia kwa Abigael kuisoma barua ya Bi. Suluhu tunajua kuwa Bwana Suluhu alikuwa ameitelekeza familia yake na kumtwika Bi. Suluhu mzigo wa kuwalea wanawe.
    • Kupitia kwa barua aliyoisoma Abigael, tunajua kuwa Bwana Suluhu alinyakua shamba la mamake Abigael na kumuua.
    • Kupitia kwa Abigael kuisoma barua ya Bi. Suluhu kwa bwanake tunajua Suluhu alikuwa na nakama.
    • KupitiakwaAbigael tunaonyeshwabaadhiyamatatizoyanayowakumba wanafunzi wa Chuo kikuu kama ukosefu wa chakula, uozo wa jamii, utegemezi n.k.

Swali 2

Sabina maswali na majibu
Swala la elimu limepewa kipaumbele katika hadithi ya Sabina. Jadili (alama 20)

Majibu

  • Sabina ni mwanafunzi wa darasa la none. Jumapili ya mwisho kabla ya Elimu mtihanai wa kitaifa, Sabina anaonekana mwenye hisia mseto moyoni. (uk. 34)
  • Anawaza kuhusu mtihani huo ambao iwapo angepita ungemwezesha kupata ufadhili katika Shule ya upiti ya bweni. (uk. 34)
  • Anawaza vilevile, iwapo angefeli mtihani huo, hatima yake ingekuwa ipi? (Uk. 34)
  • Sabina anakumbuka maneno ya mwalimu mkuu kuwa mizizi ya elimu ni chungu ila matunda yake ni matamu. (uk. 34)
  • Kauli ya mwalimu mkuu pia inashauri kuwa ikiwa mtu anataka kuonja matunda ya elimu lazima atie bidii. (uk. 34)
  • Sekta ya elimu inakumbwa na changamoto mbalimbali kwa mfano mimba za mapema. Nyaboke - mamake Sabina- alimzaa akiwa kidato cha pili. (Uk. 35)
  • Changamoto nyingine ni kuacha Shule kabla ya kuhitimisha kiwango fulani. Nyaboke anapojifungua anakatiza masomo yake ili kuanza ulezi. (uk. 35)
  • Vilevile baadhi ya desturi potovu za jamii kama kuwaoza wanao mapema huweza kukatiza masomo ya watoto. (uk. 39)
  • Elimu huwahakikishia watu mustakabali mwema maishani. Wazazi wake Nyaboke wanakata tamaa ya maisha mazuri kwa sababu mwanao waliomtegemea kusoma hadi Chuo kikuu anakomea kidato cha pili. (uk. 35)
  • Binamu yake Sabina, Mike, anasomea katika Shule ya msingi ya bweni. Alizoea kubeba vitabu vya kudurusu ambavyo walidurusu na Sabina wakiwa katika kazi yao ya uchungaji. Hii inaashiria tamaa yao ya kutafuta elimu. (Uk. 36)
  • Werevu wa Sabina haukutiwa doa na hali yake ya ujakazi. Kila muhula aliibuka wa kwanza darasani kana kwamba nafasi hiyo ilikuwa imetengwa kwa ajili yake.
  • Mwalimu mkuu anawahutubia watahiniwa ukumbini kama sehemu ya maandalizi kabla ya mtihani wa kitaifa. (uk. 37)
  • Majukumu mengi nyumbani wanayopewa watoto hueza kutatiza masomo yao.
    Kazi ya kuuza maziwa inamfanya Sabina kuchelewa shuleni mara
  • Wanahabari wanamtafuta Sabina hadi nyumbani kwao ili kumhoji kwa kufanya vyema katika mtihani. Anaibuka mwanafunzi wa nane bora nchini. (uk. 39)
  • Kufanya vyema katika mtihani kunafanya kila mtu kujinasibisha na Sabina akiwemo Yunuke na Ombati. (uk. 40)

Swali 3

Fadhila za Punda maswali na majibu

“Isije ikawa mwenye nyumba kuja na yeye mpangaji akachelewa kumfungulia mlango; itakuwa balaa bin beluwa”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (ala 4)
  2. Jadili umuhimu wa mwenye nyumba anayerejelea (ala 6)
  3. Maisha yalikuwa balaa bin beluwa kwa mpangaji. Thibitisha ( ala 10)

Majibu

“Isije Ikawa mwenye nyumba kuja na yeye mpangaji akachelewa kumfungulia mpangaji itakuwa balaa bin beluwa.”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
    • Maneno ya msimulizi
    • Anarejelea Lilia
    • Lilia alikuwa nyumbani
    • Lilia anamngojea mumewe Luka huku akiwa na mawazo mengi kutoka mateso ambayo amepitia kutoka kwa Luka.
  2. Jadili umuhimu wa mwenye nyuMba anayerejelea. (alama 6)
    • Anabainisha maudhui ya unyanyasaji wa kijinsia – Luka anamchapa Lilia.
    • Anaendeleza maudhui ya uongozi mbaya kwa kutotimiza ahadi alizowapa wananchi.
    • Pia anachimuza maudhui ya usaliti kwani analiuza kanisa aliloachiwa na babamkwe Lee Imani.
    • Pia anaendeleza maudhui ya elimu kwa kuwa yeye na mkewe Lilia wanasoma katika chuo kimoja.
    • Anaendeleza maudhui ya ukandamizaji hasa katika kituo cha polisi. Ana marafiki kituoni wanaomjuza kuhusu kwenda kwa mkewe pale.
    • Ni kielelezo cha wanaume katili licha ya mkewe kuwa na ujauzito, Luka anataka waandamane naye katika siasa.
    • Ni kiwakilishi cha viongozi wanaotumia mamlaka yao vizivyo. Baada ya kuwa gavana anasema kuwa ana uwezo wa kufanya haki kuwa batili na batili kuwa haki.
      (zozote 6 x 1)
  3. Maisha yalikuwa balaa bin beluwa kwa mpangaji.Thibitisha.
    • Ana mawazo na wasiwasi – mumewe harejei nyumbani.
    • Kutusiwa na mumewe anamfananisha na nguruwe anapokataa kuandamana naye katika siasa.
    • Anakanwa na mumewe kuwa akiwa kazini yeye si mumewe.
    • Kupigwa – Luka anampiga Lilia si mara moja tu. Anamshika nywele na kumbururura, anapopigwa teke tumboni….
    • Kuharibikia kwa mimba – Mimba yake inaharibika na hili linamliza sana.
    • Anakatazwa kufika ofisini.
    • Ana hofu ya kutochukua simu inapopigwa.
    • Wakati alipigwa na kuanguka chini, alikuwa anashindwa ampigie nani.
    • Baada ya kufiwa na wazazi wote anahisi hana mtetezi.
    • Lilia alikuwa na wasiwasi wakati Luka aliingia kanisani na kuketi karibu naye.
    • Alikuwa na wasiwasi kwa wale waliomtembelea Luka hospitalini kwani hakukuwa na jamaa yeyote.
    • Lilia alikuwa na wasiwasi kuhusu yule mgonjwa,”Luka’ aliyetambulika na mamamkwe lakini yeye hakumjua.
      (zozote 10 x1)

Swali 4

Msiba wa Kujitakia Maswali na Majibu

  1. Machoka alikumbuka kauli ya jirani yake, Zuhura, aliyeishi kumkumbusha, “wetu ni wetu, hata akiwa mbaya … wetu. Hatuna budi ila kumchagua yeye. Lisilobudi hubidi. Awe amesoma ama hajasoma, angali wetu.”leo hii hata Zuhura mwenyewe alikuwa anajutia kumchagua huyo wetu.

    Kwa muda mrefu, Machoka na Zuhura walikuwa kama fahali wawili hawakai katika zizi moja. Kisa na maana, ni wafuasi wa watu wawili tofauti. Leo hii kinachowaleta pamoja Machoka na Zuhura ni udhikinifu, hali ngumu ya maisha, mfumuko wa bei za bidhaa muhimu na kutozwa ushuru wa kiwango cha juu na serikali hiyo hiyo ya ‘watu wao’. Zuhura alisuta nafsi yake.

    Alikuwa akiitazamia nchi nzuri na maisha bora baada ya uchaguzi. Alitazamia ‘watu wake’ wangezitimiza ahadi walizozitoa wakati wa kampeni zao. Leo hii imebakia kujuta. Kujuta ghya ya kujuta! Tayari alikuwa amekwishafanya kosa. Kosa ambalo alifahamu lilikuwa la kujitakia. Ulikuwa mwiba wa kujidunga usiokuwa na kilio wala kuambiwa pole. Maji yalikuwa yashamwagika, katu hayangeweza kuzoleka…”
    Chambua maudhui katika dondoo hili. (ala 12)
  2. Eleza sababu nne zinazochangia jimbo la Matopeni kutoshuhudia maendeleo ya kisiasa tangu nchi kupata uhuru . (ala 8)

Majibu

  1. Maudhui katika dondoo
    • Mgogoro- Machoka na Zuhura walikuwa fahali wawili hawakai zizi moja.
    • Ukabila – “Wetu ni wetu, ata akiwa mbaya….wetu.
    • Umoja – Leo hii kinachowaleta pamoja Machoka na Zuhura ni udhikinifu, hali ngumu ya maisha.
    • Hali ngumu ya masiha – mfururiko wa bei za bidhaa muhimu na kutozwa ushuru wa kiwango cha juu.
    • Majuto – Leo hii hata Zuhura mwenyewe alikuwa anajutia kumchagua huyo wetu.
    • Utamaushi – Maji yalikuwa yashamwagika, katu hayangeweza kuzoleka…
    • Usaliti- waliochaguliwa kama watu wao walikosa kuendeleza uongozi wenye manufaa.
    • Unafiki – Ahadi zilizotolewa kwa kampeni hazikutimizwa.
      (zozote 6 x 2)
  2. Sababu za matopeni kutoshuhudia maendeleo.
    • Usaliti – Jimbo la Matopeni linawachagua viongozi kwa matumaini ya kuboresha maisha ya wananchi.
    • Viongozi wanapochagulia wanatupikia mbali ahadi walizotoa kama vile kuimarisha sekta ya afya, kutengeneza barabara, kuimarisha ukulima n.k.
    • Ukabila na unasaba- Wakati wa kampeni Zuhura anamwambia Machoka kuwa wanastahili kumchagua mtu wao. Matopeni imetawaliwa na familia moja; Sugu Senior na Sugu Junior.
    • Ujinga – kutoshuhudia maendeleo ndiyo malipo ya kumpigia kura kiongozi kwa kutumia matumbo yao badala ya akili.
    • Ufisadi – Wanamatopeni wanawachagua viongozi kwa sababu wakati wa kampeni, wanaowania wanawanunulia unga, khanga, sukari na mafuta.
    • Viongozi kuendeleza udikteta na ukoloni mamboleo. Kahindi Mlalama anadai kuwa vizingiti hivi haviishi daima matopeni licha ya kuwa bado wana ndoto ya kesho njema.
    • Ubadhirifu wa mali ya umma, mali ya umma inayotumiwa kugharamia safari za ndege za viongozi wa majimbo jirani.
    • Utabaka – Viongozi kwenye hafla ya kuapisha Sugu Junior wameketi vyema kwenye hema zilizotandikwa vyema, ilhali wananchi wameketi kwenye jua kali.
    • Uvunjaji wa sheria- kupiga kura si kazi, kazi ni kuhesabu kura.
    • Wanasiasa kukosa sera za kimaendeleo.
    • Wananchi kutuwazia sera za wanasiasa.
    • Propaganda – Wananchi kushindwa kufikiria ahadi za wanasiasa.
      (zozote 8 x 1)

Swali 5

Msiba wa Kujitakia Maswali na Majibu

  1. Fafanua mbinu za kimtindo katika dondoo lifuatalo. (alama 6)
    "Jimbo la matopeni lilikuwa limegeuzwa ngome ya watu fulani binafsi. Watu wenye ushawishi mkubwa serikalini! Watu wasiojali maisha ya wapiga kura kama Machoka na Zuhura. Wapiga kura walioamka siku hiyo asubuhi ya majogoo, wakastahimili baridi kali ya bukrata. Wakavumilia jua kali la mchana. Zuhura alikumbuka namna yeye na wenzake walivyotunga foleni ndefu kwenye vituo vya kupigia kura. Yote haya wakiwa na matumaini ya maisha bora ya baadaye, si bora maisha! Kumbe wajinga ndio waliwao! Mzigo mzito wa maisha haukuwatisha wala kuwakosesha usingizi viongozi wao. Ama kweli, mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi. "
  2. Onyesha namna wanamatopeni wanavyokumbwa na madhila kwa kurejelea hadithi ya "Msiba wa kujitakia" (alama 14)

Majibu      

  1.                                      
    1. Takriri - watu, wapiga kura.
    2. Nidaa/siyahi - hawajui leo wala kesho!
    3. Tashbihi - Maisha ya Wanamatopeni yalikuwa kama mchezo wa karata.
    4. Msemo - asubuhi ya majogoo.
    5. Mbinu rejeshi - Zuhura anakumbuka namna yeye na wenzake walivyotunga foleni ndefu.
    6. Methali - Wajinga ndio waliwao.
      • mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
    7. Jazanda - Mzigo mzito wa maisha. (zozote 6 x 1 =6)
  2.                    
    1. Maisha ya udhikifu
    2. Mfumuko wa bei
    3. Kutozwa ushuru wa kiwango cha juu na serikali.
    4. Uamuzi wa mpiga kura hauheshimiwi.
    5. Kupewa mishahara duni.
    6. Mishahara inachelewa kulipwa
    7. Wanatawaliwa na viongozi wasio na sera bora.
    8. Shughuli za uchaguzi zinaendeshwa kwa njia isiyo huru wa haki.
    9. Ndoto na nia za vijana zimebanwa, zikafinywa na kuzimwa.
    10. Njaa - Machoka hajatia chochote kinywani tangu asubuhi kiasi matumbo yake kushindwa kuhimili makali ya njaa.
    11. Ukosefu wa ajira - Machoka anatafuta kibarua mchana kutwa bila mafanikio.
    12. Ukabila – Zuhura anampigia kura Sugu Junior kwa sababu ni wa kabila lao.
    13. Viongozi waliochaguliwa hawawatimizii raia ahadi walizotoa.
    14. Ufisadi - wapiga kura wanahongwa kwa kupewa khanga, sukari, unga wa sima, mafuta na visenti vya kununua tembo.
      (zozote 7 x 2 = 14)

Swali 6

Fadhila za Punda Maswali na Majibu

. “Katika hali ile ya uchungu, kilio na mtanziko wa mawazo, akaiona simu yake imeanguka chini ya kitanda….. Haidhuru hata kama atamuunga mkono mwanawe.”

  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Fafanua mbinu ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Eleza sifa nne za anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 4)
  4. Eleza jinsi “taasubi ya kiume” inavyoshughulikiwa na mwandishi wa “fadhila za punda”. (alama 10)

Majibu

  1. Msemaji ni mwandishi.
    • Anayerejelewa ni Lilia
    • Mahali ni nyumbani kwa Luka/Lilia.
    • Ni baada ya kupigwa na mumewe kwa kumripoti katika kituo cha polisi. (alama 4)
  2. Taswira (hisi) - hali ya uchungu/ kilio /mtanziko
    • Nahau/msemo - unga mkono (alama 2)
  3. Sifa za Lilia
    • Mwenye mapenzi ya dhati - anampenda mumewe
    • Ni mtiifu - anawacha kazi baada ya kushauriwa na mumewe.
    • Ni mwaminifu - mbele ya mumewe
    • Ni mwenye heshima - anamwita mama mkwe kwa heshima.
    • Ni mwenye huruma - anamtetea mumewe kupewa ufadhili.
    • Mtulivu - hapendi ugomvi.
    • Mwenye bidii - anasoma hadi chuo.
      (za kwanza 4 x 1 =4)
  4. Taasubi ya kiume
    • Luka anampiga mkewe Lilia kwa ngumi, teke, kofi na hata kumfokea.
    • Baada ya kuanza uzinzi na hawara zake, Luka anakuwa mkali kwa mkewe.
    • Luka anashinikiza Lilia kuacha kazi kwa madai kuwa anamhitaji kudhibiti fedha za kanisa.
    • Lilia hana usemi nyumbani mbele ya Luka.
    • Luka anampuuza Lilia anapomshauri asiingilie siasa.
    • Luka analiuza kanisa lao bila kumshauri wala kumwuliza mkewe Lilia.
    • Luka kurithi mali ya babake Lilia badala ya bintiye (Lilia)
    • Luka haoni umuhimu wa kuandamana na mkewe; anamwacha kijijini.
    • Luka kutaka miadi kabla ya kutembelewa na mkewe.
    • Wanawake hawafai kuwastaki waume zao. Lilia anahofia kujulikana kwamba alikuwa na nia ya kumshtaki mumewe.
    • Luka kuwa na hawara. Kitendo hiki kinamkosesha Lilia hadhi yake katika ndoa.
      (zozote 5 x 2 = 10)

Swali 7 

Fadhila za Punda Maswali na Majibu

“Yu wapi kirukanjia wako? Wajua yuko wapi? Uliacha mbachao kwa msala upitao. Atakutunza nani, maana kwako fadhila za punda ni mashuzi!”

  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Taja mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Bainisha toni ya dondoo. (alama 1)
  4. Fafanua sifa zozote tatu za mzungumziwa. (alama 3)
  5. Kwa kurejelea hadithi “Fadhila za punda” onyesha ukweli wa kauli kuwa fadhila za punda ni mashuzi kwa mifano mwafaka. (alama 10)

Majibu

“Yu wapi kirukanjia wako? Wajua yuko wapi? Uliacha mbachao kwa msala upitao. Atakutunza nani, maana kwako fadhila za punda ni mashuzi!”

  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake.
    • Ni maneno ya mamake Luka.
    • Anamwambia Luka.
    • Yumo katika hospitali (Luka).
    • Ni baada ya gavana Luka kuhusika kwa ajali na yule kirukanjia wake akakosa kuja kumwona baada ya kumsaliti Lilia alipokuwa gavana.   Zozote 4x1=4
  2. Taja mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili.
    • Methali – usiache mbachao kwa msala upitao.
    • Swali la balagha – yu wapi kirukanjia wako?
    • Takriri - …wapi…wapi
    • Nidaa - …mashuzi! 2x1=2
  3. Bainisha toni ya dondoo.
    • Huzuni, Majuto, uchungu.
    • Dhihaka,dharau 1x1=1
    • Umuhimu wa toni ni kuonyesha hisia za mzungumzaji.
  4. Fafanua sifa zozote tatu za mzungumziwa.
    • Mwenye bidii.
    • Ni laghai.
    •  Msaliti.
    •  Mzinzi.
    • Ni katili.
    •  Mnafiki.
    • Ni msomi.
    • Mwenye dharau. Zozote 3x1=3
  5. Kwa kurejelea hadithi “Fadhila za punda” onyesha ukweli wa kauli kuwa fadhila za punda ni mashuzi kwa mifano mwafaka.
    • Luka anaachiwa kanisa na pastor Lee Imani baadaye anauza kanisa ili awanie gavana.
    • Lilia anampenda Luka na anamshawishi babake akubali kuwabariki lakini Luka anamsaliti Lilia anapokuwa gavana kwa kumpiga makofi na teke la tumbo.
    • Luka anamsaliti pastor Lee baada ya kumkubali na kufadhili elimu, baadaye anakuwa na uhusiano na mtoto wake anayemtesa baadaye.
    • Luka anawasaliti waumini kwa kuuza kanisa na kuingia siasani.
    • Luka anamtendea uovu mkewe anapokosa kuandamana naye kwenye kampeni na kumtusi kuwa amenona kama nguruwe na kwamba wanawake ni wengi.
    • Luka anawasaliti wananchi waliomchagua kwa kutotimiza ahadi alizowatolea wakati wa kampeni.
    • Luka anamsaliti mkewe kwa kuwa na uhusiano ka kiruka njia.
    • Kirukanjia anamsaliti Luka kwa kukosa kumtembelea hospitalini baada ya kujulishwa na daktari huenda asiweze kutembea tena licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.
    • Lilia anamsaliti babake kwa kuacha kazi ya meneja wa benki baada ya babake kumsomesha na kupata kazi ili awe akipokea wageni wa Luka.
    • Lilia anamsaliti babake kwa kushinikiza aolewe na Luka, ingawa babake hakutaka.
    • Lee anamsaliti Lilia kwa kumrithisha Luka Kanisa 10x1=10

Swali 8

Huku ukirejelea hadithi zifuatazo tano jadili maudhui ya migogoro kwa kutoa mifano maridhawa. (alama 20)

  1. Fadhila za punda
  2. Msiba wa kujitakia
  3. Mapambazuko ya machweo
  4. Harubu ya maisha

Majibu

Huku ukirejelea hadithi zozote tano jadili maudhui ya migogoro kwa kutoa mifano maridhawa.

  1. Fadhila za punda
    • Lilia na Luka wana mgogoro unaosababisha vita k.m anapojitazama kwenye kioo anaona kovu shavuni na donda.
    • Mapenzi ya Lilia na Luka yanaleta mgogoro kati ya Lilia na babake-hapendi uhusiano ule.
    • Kuna mgogoro wa kinafsia kwa babake Lilia anayemshuku Luka kuwa na uhusiano na mwanawe Lilia.
    • Luka kumvamia mkewe na kumvuta nywele kumwelekeza kwenye chumba cha kulala, ambapo anampiga ngumi na mateke.
    • Luka anamtawisha Lilia na hata kumlazimisha kuandamana naye kwenye kampeni na hii inawafanya wakosane – Luka anamwambia wanawake ni wengi.
  2. Msiba wa kujitakia
    • Kati ya viongozi na raia ambao wako tayari kupigania haki zao-hawapewi huduma na viongozi.
    • Zuhura na Machoka-Zuhura angependa kumchagua kiongozi kwa misingi ya kikabila kinyume na Machoka.
    • Sugu Junior na Fumo Matata – Fumo anaona dai la serikali kwamba kuna maendeleo ni porojo tu.
    • Mgogoro kati ya tume ya uchaguzi na wananchi.
    • Mgogoro wa ushindi wa Sugu Junior dhidi ya Fumo matata.
    • Kati yam zee Sugu Senior na Zuzu Matata; ambapo mzee Sugu senior alitwaa uongozi baada ya kuondoka kwa wakoloni.
  3. Mapambazuko ya machweo
    • Mzee Makutwa kumtifulia mzee Makucha vumbi na kumdhihaki kuhusiana na kazi yake.
    • Bi Macheo anajikuta katika mgogoro na mumewe kwa vile hapendi jinsi mzee Makutwa anavyomfanyia stihizai mumewe.
    • Mzee Makucha anakuza mgogoro anapomwitia polisi mzee Makutwa kwa kuwahujumu vijana.
    • Mzee Makutwa ana mgogoro na sheria kwa vile anaendesha biashara haramu.
    • Migogoro kati ya vijana waliosoma na serikali kwa mfano Sai alidai kuwa vijana wanaachiwa kazi za hadhi ya chini.
    • Mzee Makutwa na polisi wakijaribu kumwingiza pangoni.
    • Mzee Makucha na shirika la reli-kukataa kumlipa pesa.
  4. Harubu ya maisha
    • Mama Mercy amtaka mumewe aeleze sababu ya kutofika ilhali motto anaelekea kulala. Mama Mercy analalamika kuwa mumewe hatimizi wajibu wake.
    • Familia ya Kikwai ina mgogoro na fundi wa nyumba hajalipwa kwa mwezi mzima.
    • Kikwai anagongana na Bosi kwa kuacha gari nyumbani kwa kukosa mafuta.
    • Nilakosi ana mgogoro wa mpangishaji wake kwa vile hajamlipa na mwezi unaenda kuisha.
    • Kikwai kutoleta chakula.
    • Kikwai kufika amechelewa.
    • Mercy kulalamikia njaa na upweke.

Swali 9 

Nipe Nafasi Maswali na Majibu

  1. Eleza tafsiri mbalimbali za kichwa cha hadithi hii, ‘Nipe Nafasi’ (alama 7)
    Pupa (F. M. Kagwa)
  2. Fafanua umuhimu wa mandhari ya Chenga-ways katika kujenga hadithi Pupa. (alama 5) Toba ya Kalia
    (Douglas Ogutu)
  3. “Ni kutokana na mchango wako kupitia twitter na facebook katika maswala mbalimbali ambapo iliamuliwa upewe fursa ya kuzungumza moja kwa moja na watazamaji wetu.”
    Eleza nafasi ya vijana kwa mujibu wa hadithi Toba ya Kalia. (alama 8)

Majibu

Nipe Nafasi – Mzamane Nhlapo

  1. Eleza tafsiri mbalimbali za kichwa cha hadithi hii, ‘Nipe Nafasi’ (alama 7)
    • Kuchukua nafasi ya kuboresha maisha yake. Kazili anapoona mumewe amemdhalilisha vya kutosha, anaamua kuondoka. Hajali kuomba ruhusa kama anavyotakiwa. 
    • Kuchukua hatua wanapoona waume zao hawawajibiki. Bi. Kazili anajisemea kuwa atarudi kufanya kazi kuwakimu, na siku hiyo lazima wale chajio.
    • Nafasi ya kuishi atakako. Kazili anawakumbusha wanaume kuwa yeye ni raia halali wa Lesotho kupitia kwa ndoa, na hakuna anayeweza kumlazimisha kurudi Swaziland, hata mumewe.
    • Kupinga maamuzi kuhusu maisha yake ambayo hajahusishwa kufanya. Mama Kazili anakana maamuzi ya wanaume kwenye kraal ambayo awali yanachukuliwa kuwa sheria isiyoweza kupingwa.
    • Wanawake kupewa nafasi na nyadhifa. Kazili anaeleza jinsi wanawake wanavyohiniwa nafasi na wadhifa katika jamii kwa kusingizia Biblia, kuwa mwanamke anafaa kuwa mnyenyekevu.
    • Nafasi ya kuheshimiwa. Kazili anapinga swala la mwanamke kuchukuliwa kama mtoto ambaye anafaa kuomba ruhusa kwa kila kitu kutoka kwa mumewe.
    • Nafasi ya ajira na kazi. Mwisho wa mwaka huo, Kaizili anafanya kazi ya ualimu bila ruhusa kutoka kwa yeyote, na wanawe wanapata chakula kila siku.
    • Kupatiwa nafasi ya usemi. Wanawake wa makamo wanakubaliana na rai ya Kazili, wanaona kuwa amaesema ukweli mchungu. Wako tayari kubadili mkondo huu wa dhuluma dhidi yao.
    • Kufanya maamuzi ya kibinafsi. Mama Kazili anawambia wanaume kwamba aliondoka bila kuomba ruhusa kwa mumewe kwa sababu alijua hangekubaliwa. Anawajuza kuwa hawezi kukaa tu kuwatazama wanawe wakihangaika kwa njaa.
    • Nafasi ya kusema ukweli. Wanaume wanahisi kwamba Kazili amewatusi, na kwamba lazima arudi kwao Swaziland kwa kuwakosea heshima. Hatarajiwi kusema ukweli.
      Pupa (F. M. Kagwa)
  2. Fafanua umuhimu wa mandhari ya Chenga-ways katika kujenga hadithi Pupa. (alama 5)
    • Kufichua mitandao ya uhalifu inavyofanya kazi / biashara haramu zinazoendeshwa katika jamii na madhara yake.. Ni danguro.
    • Kusawiri maudhui ya masaibu yanayoandama mtoto wa kike katika jamii.
    • Kuendeleza ploti. Baadhi ya matukio yanatokea katika mandhari haya. 
    • Kuwaibusha wahusika na sifa zao kama Mashaka.
    • Kuchimuza matabaka katika jamii. Kuna tabaka la wateja matajiri na wanyonge kina Mwakuona, Mashaka ambao ni bidhaa ya matajiri
      Toba ya Kalia (Douglas Ogutu)
  3. “Ni kutokana na mchango wako kupitia twitter na facebook katika maswala mbalimbali ambapo iliamuliwa upewe fursa ya kuzungumza moja kwa moja na watazamaji wetu.”
    Eleza nafasi ya vijana kwa mujibu wa hadithi Toba ya Kalia. (alama 8)
    • Kukuza vipaji. Jack na Siri wanashiriki katika shindano linaloandaliwa na wahandisi kutoka Uchina na kuibuka katika nafasi tatu za kwanza. Jack anaandaa kazi ya kupigiwa mfano na hata fomyula zake zinaingizwa kwenye vitabu, japo kwa jina la Siri
    • Kuendeleza lugha na utamaduni. Jack akiwa Uchina anaendeleza elimu ya lugha ya Kiswahili kwa wakazi wa huko, na anasema kwamba baadhi yao wanapata umilisi hata kuliko wazungumzaji wa nchi yake ya nyumbani.
    • Ujasiriamali. Jack anapokamilisha masomo yake ya shule ya upili kukosa karo anaanzisha biashara ya kuuza nguo.
    • Siri huwasiliana na wazazi wake kupitia skype, na Jack ndiye huwaunganishia mitambo kuhakikisha mawasiliano yanafaulu vizuri. Wanapatana naye vyema akiwa Uchina.
    • Urafiki wa dhati. Urafiki wake na Siri ni wa kipekee. Wanasaidiana sana, hata wanawafikiri kuwa ndugu. Hata kuhiniwa fursa yake na kupewa Siri hakuwatenganishi.
    • Usamehevu. Anawasamehe wote waliomkosea mwishoni.
    • Kukuza teknolojia kupitia kwake Jack , nafasi ya teknolojia na mawasiliano inabainika.
    • Kukuza uzalendo. Siri anakipigania Kiswahili na kukifunza Uchina.
    • Ushauri. Mwishoni mwa kipindi, Siri anawapa watazamaji wosia kuwa wasiwadhulumu mayatima na maskini
    • Siri na Jack wanawakilisha teknolojia ya mawasiliano na umuhimu wake katika kuunganisha jamii.
    • Watetezi imara wa haki na ukweli. Siri
    • Kukuza mahusiano ya kimataifa na umuhimu wake katika jamii unadhihirika. Siri

Swali 10 

Nilitamani (Phibiana Muthama) na Kifo cha Suluhu – Dominic Maina Oigo

Nilitamani Maswali na Majibu

  1. “Wakati anaongea kwa simu, nikawa najifungua mkanda. Nikafaulu. Nikajaribu kufungua mlango. Duh! Ulikuwa ushatiwa loki. Sijui nilipata wapi nguvu za kupitia juu yake! Nikaponyoka pyu! Nikakimbia mguu niponye. Nilikimbia nisijue niendako. Nikakimbia. Sitaki kuangalia nyuma kwa kushtukia yaliyonikuta. Nilikata katikati ya misitu sijui nielekeako ila mbali na Romeo na pepo yake. Nimekaza mwendo huku nahema, pumzi si zangu! ”
    1. Fafanua aina za taswira zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 5)
    2. “Tamaa mbele mauti nyuma.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi: Nilitamani. (alama 7)
      Kifo cha Suluhu – Dominic Maina Oigo
  2. “Aliyaacha machozi yamtoke shibe yake kwani asingeweza kujizuia. Barua ile ilimfichulia siri si haba
    Thibitisha kauli iliyopigwa mstari ukirejelea hadithi Kifo cha Suluhu. (alama 8)

Majibu

Nilitamani (Phibiana Muthama)

  1. “Wakati anaongea kwa simu, nikawa najifungua mkanda. Nikafaulu. Nikajaribu kufungua mlango. Duh! Ulikuwa ushatiwa loki. Sijui nilipata wapi nguvu za kupitia juu yake! Nikaponyoka pyu! Nikakimbia mguu niponye. Nilikimbia nisijue niendako. Nikakimbia. Sitaki kuangalia nyuma kwa kushtukia yaliyonikuta. Nilikata katikati ya misitu sijui nielekeako ila mbali na Romeo na pepo yake. Nimekaza mwendo huku nahema, pumzi si zangu! ”
    1. Fafanua aina za taswira zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 5)
      • Taswira sikivu – Wakati anaongea kwa simu
      • Taswira mguso – nikawa najifungua mkanda / Nikajaribu kufungua mlango / Duh! Ulikuwa ushatiwa loki.
      • Tasira mwendo – Sijui nilipata wapi nguvu za kupitia juu yake! Nikaponyoka pyu! Nikakimbia mguu niponye. Nilikimbia nisijue niendako. Nikakimbia.
      • Taswira oni – Sitaki kuangalia nyuma kwa kushtukia yaliyonikuta. Nilikata katikati ya misitu sijui nielekeako ila mbali na Romeo na pepo yake.
      • Taswira hisi - Nimekaza mwendo huku nahema, pumzi si zangu!
    2. “Tamaa mbele mauti nyuma.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi: Nilitamani. (alama 7)
      • Tumaini, anaondoka kwao Kenya hadi nchi ya Wabongo kwa kutamani maisha mazuri.
      • Tumaini anatamani kuwa na milki na mali kama ya Nina. Anagundua kwamba alimwonea gere Nina.
      • Tumaini anapoishi na Nina anaanza kuwaonea wivu na kutamani kuwa na mume kama huwa Nina.
      • Tumaini anahama kwa Nina, kwa matumaini ya maisha mazuri bila mpangilio maalum: anaishia kuteseka zaidi.
      • Tumaini anapanda kutoka kiwango cha kutamani na kuanza kutaka. Anataka maisha mazuri, anataka mume wake waoane na kupata watoto wazuri.
      • Kwa tamaa yake, Tumaiini anamwona Romeo, kama mwanamume mtanashati aliyemwaza kwenye lile shairi lake. Nusra kumtoa kafara na analazimika kutoroka.
      • Matatizo ya kisaikolojia. Tumaiini anatamani kila kitu. Katika ushairi mawazoni, Tumaini anatamani kuwa na kasri afurahie, kazi ajikimu, na gari la kifahari. Anatamani maisha yawe mepesi na kumpa burudani.
      • Tuamini yuko katika ndoa ya kisaikolojia. Anatamani sana kupata mume mzuri amwoe, waishi maisha mazuri. Anajiona akiwa ameolewa, huku wamejaliwa watoto ambao wanawalea kwenye misingi ya kidini na kuwakuza vyema.
      • Unafiki wa kidini. Anapoona mambo yake yameenda kombo, anamgeukia Mungu na kumpa ahadi ya kumtumikia milele iwapo atamfungulia milango.
      • Ulaghai. Romeo anamhadaa Tumaini kwa kisingizio cha mahaba, lakini ukweli ni kwamba anataka kumtumia kwa matambiko yake.
      • Maamuzi mabaya. Tumaini anaamua kuondoka kwa Nina, japo hana pa kuishi. Ni ajabu kuwa anachoka kufadhiliwa hali hana hanani.
      • Maisha bandia. Tumaini anapopata hela kutoka kwa Nina, anaamua kwenda kudanganya moyo Coco Beach. Ananunua kaukau za mihogo na soda ya pepsi. Anavinjari kama mwenye vyake hali anateseka.
        Kifo cha Suluhu Maswali na Majibu
  2. “Aliyaacha machozi yamtoke shibe yake kwani asingeweza kujizuia. Barua ile ilimfichulia siri si haba”
    Thibitisha kauli iliyopigwa mstari ukirejelea hadithi Kifo cha Suluhu. (alama 8)
    • Matatizo katika asasi ya ndoa. Suluhu anamsababishia mkewe uchungu kwa kutengana naye na hapati fursa ya kuzungumza naye.
    • Ukatili wa suluhu, ikiwemo kumwua mamake Abigael.
    • Usuli na Mabadiliko. Anamkumbusha kazi yake ya kuuza makaa ilivyofika hatima ya ghafla, kisha akatwaa ubunge kwa mbinu azijuazo.
    • Uumilivu wa Bi. Suluhu. Amevumilia kwa ajili ya watoto na kuwalea, na wa kwanza amekamilisha darasa la nane.
    • Uaminifu wa Bi. Suluhu. Anasisitiza jinsi anavyompenda mumewe, wala hajawahi kumwendea kinyume.
    • Bi. Suluhu anaonyesha thamani ya ndoa ya kuweka siri kwa kumhakikishia mumewe kuwa hajawahi wala hatatoa siri zake anazojua.
    • Ufisadi na kutowajibika. Suluhu haleti maendeleo kwa kuwa anawalipa wasichana wa vyuo vikuu na kula nao uroda. Pesa anamlipa Bwana Ngoma aliyefadhili siasa zake.
    • Ushauri. Anamuasa akome tabia zake kwa kuwa hali yake ni bayana.
    • Shukrani za Bi. Suluhu. Anamshukuru kwa mema aliyomtendea kabla ya kubadilika, na yale aliyotendea wazazi wake.
    • Athari za kutowajibika. Bi. Suluhu anamlaumu mumewe kwa kifo chake anachotarajia kutokana na kukosekana nyumbani na uzinzi, vinavyomletea msongo wa mawazo.
    • Utamaushi. Bi. Suluhu anakiona kifo kama suluhu.
    • Kufichua yaliyofichika. Barua hii inategua kitendawili cha kifo cha mamake Abigael aliyepatikana ameuawa.
    • Kuonyeha mustakabali wa jamii mpya. Abigael anajuta kuingilia ndoa ya Suluhu. Anaona kifo cha Suluhu hakitafaa lolote. Kifo kifaacho ni cha maovu na kupalilia utu. Anafanya uamuzi wa kutia bidii kujipa riziki na kumwachia Mungu wajibu wa hukumu.

Swali 11

Mume wangu, hebu zivute fikra zako miaka kumi na mitano iliyopita tulipoingia katika mkataba wa ndoa. Kwa nini unataka kujitia hamnazo kuhusu ahadi ulizozitoa? Umesahau namna tulivyohangaika, tukachekwa na watu, tukakosa hata marafiki na hatimaye tukabandikwa majina ya ajabu? Umesahau, mume wangu? Umesahau namna kazi yako ya kuuza makaa ilivyofika hatima ya ghafla baada ya serikali kupiga marufuku ukataji wa miti katika eneo la Dafrao? Naomba ukumbuke. Ninaamini huenda umesahau! Ama cheo chako cha ubunge ulichokipata kwa mbinu nizijuazo mimi kimekulevya na kukufanya uisahau familia yako?

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 5)
  2. Fafanua mbinu za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili. (alama 6)
  3. Tambua toni iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
  4. Fafanua umuhimu wa ujumbe alitoa mnenaji wa maneno haya. Tumia hoja nane. (alama 8)

Majibu

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    • Maneno haya ni ya Bi. Suluhu kwa Bwana Suluhu katika Barua aliyoitoa Abigael mfukoni mwa Bwana Suluhu. Bwana suluhu na Abigael walikuwa wamekwenda kujistarehesha.
  2. Fafanua mbinu za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili. (alama 6)
    • nahau/msemo – kujitia hamnazo
    • Balagha – umesahau mume wangu?
    • Takriri/urudiaji – neno umesahau limerudia.
    • Nidaa – naamini huenda umesahau!
    • Uhuishi/Tashihisi – cheo kimekulevya
    • Mbinu rejeshi – Bi Suluhu anakumbuka maisha yao ya awali – m.f tulivyohangaika.
    • Usambamba – tukachekwa tukakosa tukabandikwa
    • Majazi – Dafrao (zozote 6 x 1 = 1)
  3. Tambua toni iliyotumika katika dondoo hili.
    • Toni ya unyenyekevu – naomba ukumbuke.
    • Toni ya mshangao– Bi Suluhu anastaajabu vipi mumewe amesahau maisha yao ya awali. (yoyote 1x2=2)
    • Toni ya huzuni -
  4. Fafanua umuhimu wa ujumbe alitoa mnenaji wa maneno haya. Tumia hoja nane.(alama 8)
    • tunafahamu uhusiano wao – hapo awali Bw. Suluhu alimpenda Bi. Suluhu na kutoa ahadi nyingi kwake. Uhusiano huu umedhoofika sasa.
    • Tunafichuliwa maisha yao ya hapo awali. Walikuwa maskini aliuza makaa kupata riziki.
    • Bwana Suluhu ni Mbunge na alipata cheo chake kwa njia isiyo halali.
    • Tunafichuliwa kuwa Bw. Suluhu ndiye aliyemwangamiza mamake Abigael ili ajifaidi na shamba lake.
    • Tunafahamu kuwa Bw. Suluhu hafanyi maendeleo katika eneo bunge lake kwa sababu anafuja pesa za wananchi kwa kuwalipa wasichana wa vyuo vikuu baada ya kula uroda nao.
    • Tunaambiwa kuwa Bw. Suluhu ana deni la Bw. Ngoma aliyemkopesha pesa za kampeni hivyo akakosa kufanya maendeleo kwa kuwa anatafuta mbinu za kulipa deni hili.
    • Tunafahamishwa kuwa Bw. Suluhu ni mgonjwa. Watu wanazungumza kuhusu kuabiri gari moshi.
    • Bi. Suluhu anahofia Suluhu asimwambukize Abigael nakama
    • Tunafahamishwa kuwa Bw. Suluhu alikuwa mwema hapo awali kwani alisaidia mamake Bi. Suluhu na familia yake.
    • Bi .Suluhu pia anatufahamisha kwamba anaugua msongo wa mawazo uliosababishwa na vitendo vya mumewe vya kihayawani.
    • Kupitia kwa barua hii tunafahamu kuwa Bw. na Bi. Suluhu wana watoto wawili ambao wanaumia kwa sababu ya matendo ya Bw. Suluhu.
      (za kwanza 8 x 1 = 8)

Swali 12

“Wewe mke sampuli gani usiyetaka kumuunga mkono mmeo?”

Kwa kurejelea hadithi hii na nyingine zifuatazo, jadili changamoto anazopitia mnenewa pamoja na wahusika wa jinsia yake. (alama 20)
Ahadi ni deni.
Hadithi ya Nipe nafasi

Majibu

  1. Fadhila za punda
    • Mwanamke kutawishwa, lilia anaachishwa kazi ya umeneja na mwishowe kutawishwa. Anaishia kukaa nyumbani na kutishwa asidhubutu kutoka nje ya lango.
    • Mwanamke anatishiwa – Lilia anapodhubutu kumshtaki mumewe anakumbushwa kuwa yeye ndiye Gavana na ana uwezo wa kufanya haki kuwa batili na batili kuwa haki.Utajua kichomtoa kanga manyoya.
    • Mwanamke anapokezwa vipigo. Lilia anapokea mapigo kutoka kwa mumewe anapoenda kuripoti kwa polisi.
    • Mwanamke kutusiwa: Lilia anaambiwa amenona kama nguruwe.
    • Mwanamke kudhalilishwa. Lilia annambiwa kuwa ana umbo kama nguruwe kwani kazi yake ni kula na kulala tu.
    • Mwanamke kuendewa kinyume na mumewe, katika ndoa, Luka anasemekana kuwa na kiruka njia ambaye waliandamana naye kila mahali. Lilia anapouliza ni nani anapokea kipigo kinachomlaza kitandani siku mbili.
    • Kuachishwa kazi. Lilia anaachishwa kazi na mumewe ili awe mpokezi wa wageni nyumbani.
  2. NIPE NAFASI
    • Wanawake kutosaidiwa katika malezi na waume zao. Mama Kazili hatumiwe pesa na mumewe yeye na watoto wake wanataabika kwa njaa.
    • Mwanamke kutosikilizwa. Wazazi wa mama Kazili wanadinda kusikiliza malalamishi yake kuwa mumewe ana mke mwingine migodini.
    • Kutopatiwa pesa za mahitaji – nyanyake msimulizi anakosa kumpa mamake pesa zinapotumwa na babake.
    • Kufiwa na jamaa zao. Mama Kazili anafiwa na mwanawe Mkhathini wakiwa katika safari yao kwenda Makongeni.
    • Wanawake kulaumiwa/kusingiziwa kusababisha kifo. Mama Kazili analaumiwa kusababusha kifo cha Mkhathini kwa sababu hakuomba ruhusa.
    • Wanawake kuuawa – mwanamke katika kijiji cha Habelo anatoroka na mwishowe maiti yake kufukuliwa na mbwa kondeni mwake. Hii ni baada ya kumuita mumewe mzembe.
    • Wanawake kudhalilishwa – wanawake wanaketi sakafuni nao wanaume wanaketi vitini.
    • Mwanamke kutopewa nafasi ya kujitetea. Mama Kazili ananyamazishwa na Matweba anapojitetea kwa wazee.
    • Kutengwa kwa misingi ya kitaifa. Mama Kazili anaambiwa lazima arudi kwao Swaziland.
    • Mwanamke kuchukuliwa kama mtoto anayetarajiwa kuwa chini ya uelekezaji na utunzi wa mwanamume katika jamii ya Belo.
    • Jamii na serikali imewanyima wanawake uhuru. Wanahitajika kuomba ruhusa kwa kila jambo wanalolihitaji kufanya.
  3. Ahadi ni deni
    • Kutoonana na jamaa zao kwa muda mrefu. Fadhumo anakaa kwa muda wa mihula mitatu bila kuonana na wazazi na jamaa zake.
    • Kufiwa na wazazi, Fadhumo anafiwa na babake katika ajali na mamake pia anafariki baadaye.
    • Kuacha masomo – Fadhumo anaacha masomo yake kwa sababu ya ukosefu wa karo. Anaachia kidato cha pili.
    • Kulazimishwa kuwa kimada. Jamaa ya babake Fadhumo anamwambia kuwa ikiwa anataka kusoma sharti awe kimanda wake.
    • Mwanamke kulazimishwa kuolewa akiwa mchanga Fadhumo anaolewa na Adan akiwa mchanga.
    • Mwanamke kutwikwa majukumu. Fadhumo anajukumika kuwalea na kuwasomesha nduguze ingawa ni mchanga.
    • Mwanamke kufanya kazi kunachukuliwa kama kuzurura. Adan anaulizwa na watu kwa nini mkewe anaenda kazini ilhali anafaa kukaa nyumbani na kutunza nyumba na watoto.
    • Mwanamke kutoruhusiwa kusoma; mjombake Adan anamwambia kuwa masomo yatamfanya mkewe kuwa jeuri.
    • Mwanamke kusingiziwa; mjombake Adan anamwambia Adan kuwa Fadhumo anaweza kutoroka na walimu wake au wanafunzi wenzake (zozote 20 x 1 = 20)

Swali 13

Nipe Nafasi Maswali na Majibu

  1. Baridi ilizidi kututafuna kadri tulivyokazana kupanda Milima ya Maloti. Vidole vyangu vya miguuni vilikufa ganzi. Mashavu yetu yaliadhibika kwa upepo baridi huku vipande vya theluji vikitupiga kwenye nyuso zetu.Miili yetu iliathirika;tulihisi njaa na uchovu. Nikatamani tufike kwa jamaa ya baba yetu ambako tungepata angalau mchuzi wa papa kabla ya kulala. Bidii ya mama ilitutia moyo wa kuendelea na safari.
    1. Tambua nafsi ya usimulizi iliyotumika katika hadithi hii na uthibitishe jibu lako. (alama 2)
    2. Eleza umuhimu wa mwandishi kutumia  nafsi uliyotaja hapo(i) juu. (alama 2)
    3. Bainisha mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili (alama 2)
    4. “Mamake Msimulizi (Richman) ni kielelezo cha wanawake jasiri””Thibitisha kwa kutolea mifano mwafaka (alama 7)
  2. Hadithi “Toba ya Kalia” inahimiza uwajibikaji. Jadili. (alama 7)

Majibu

  1.  
    1. Nafsi ya kwanza
      • Vidole vyangu vya miguuni..
      • Nikatamani tufike kwa jamaa ya baba yetu.....
      • Kututafuna kadri tulivyokazana...nk. (Nafsi-1, Mfano-1)
    2. Umuhimu wa nafsi ya kwanza:
      1. Msimulizi humleta msomaji karibu na yeye/masafa baina ya msomaji na msimulizi yanaf upishwa.
      2. Msimulizi hudhihirisha hisia zake kwa wasomaji na kuwateka hisia zao
      3. Msimulizi huongezea kisa chake uhalisia ikilinganishwa na kama kisa kingesimuliwa kwa namna ya kuripotiwa
    3. Mbinu za kimtindo;
      • Tashihisi/uhuishi (uhaishaji- Baridi ilizidi kututafuna/vipande vya theluji vikitupiga
      • Msemo/ Nahau - vilikufa ganzi/ilitutia moyo
      • Taswira - miili yetu iliathirika / tulihisi njaa na uchovu
      • Usimulizi - dondoo lote limesimuliwa
    4. Mamake msimulizi (Richman) kama kielelezo cha wanawake jasiri;
      • Mama Kazili anapoamua kuwapeleka wanawe Makongeni bila idhini ya mumewe na wakwe zake.
      • Licha ya mumewe kukosa kumtumia pesa kwa zaidi ya mwaka sasa, anajikaza kuwalea wanawe
      • Mama Kazili anatoa dukuduku lake la kutaka apewe nafasi ya Kuikimu familia yaka kwa ukoo wa Belo bila woga
      • Mama Kazili anamweleza Msimulizi waziwazi sababu za kuenda Makongeni baada ya Msimulizi kumuuliza.
      • Vilevile, alianza kufanya kazi kama mwalimu wa shule ya msingi bila ruhusa kutoka kwa mumewe wala ukoo wa Belo.
      • Anaingiliana vyema na mama aliyemkopesha pesa za nauli ya gari ili kusafiri milimani
      • Aidha, alijibidisha kupanda milima ya Maloti licha baridi na utelezi kuwapeleka wanawe Makongeni wasife njaa.
      • Anamlenga Matweba usoni sawasawa na kumjibu licha ya Matweba kumkemea.
      • Licha ya kumpoteza mwanawe Mkhathini anaendelea na safari huku akiwa amembeba.
      • vilevile, alijua fika kuwa ukoo wa Belo ungem laumu kwa kusababisha kifo cha Mkhathini..
      • Mama Kazili anawaeleza jamaa ya mumewe kuwa yeye ni raia halali wa Lesotho kupitia kwa ndoa na hakuna yeyote anayeweza kumlazimisha kurudi Swaziland ikiwemo mumewe.
      • Anawaeleza wazee kuwa yuwajua Biblia namna mwanamke anapaswa kuwa mnyenyekevu na kuwa sheria za kijamii zinamchukulia mwanamke kama mtoto aliyepaswa kuwa chini ya utunzaji na uelekezi wa mwanaume.
      • Anaikashifu serikali kwa hila kwa kudai kwamba wamechaguliwa na wanawake.
      • Anasema kuwa kabla hajafa, apewe nafasi ya kuyaboresha maisha yake na yale ya mwanawe.
      • Anakataa kuomba msamaha kwa wazee wa ukoo wa kwa Belo kusema kuwa alimaanisha kile alichokisema.
  2. Uwajibikaji katika hadithi ‘Toba Kalia’
    1. Jack anawekeza pesa zake zote kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo.
    2. Jack anawajibika anapowaunganishia wazazi wa Siri mitambo ili kuwasiliana na mwanao Siri kwa njia ya ‘skype’
    3. Licha ya kuhiniwa nafasi yake katika mashindano na Bwana Kalia, Jack anampa mkewe Kalia zawadi yake ya hundi za shilingi elfu kumi amhifadhie
    4. Jack anajitengenezea kitanda na kuweka shati lake chini ya mto ili kunyooka .
    5. Siri anaidhamini lugha ya kwao licha ya kuwa Uchina na hata amewafundisha Wachina wengi lugha ya kwao Kiswahili.
    6. Siri akiwa Uchina kila mwezi, husoma riwaya mbili, tamthilia mbili na angalau diwani ya mashairi kila baada ya miezi miwili kuendeleza ugwiji wake katika lugha ya Kiswahili
    7. Bi. Mshewa (Mamake Siri) anafundisha Kiswahili katika Shule ya Upili ya Kayole.
    8. Siri amewafundisha Wachina wengi Kiswahili
    9. Wadhamini ambao ni wataalamu wa uhandisi kutoka Uchina wanachangia katika elimu kwa kutoa tuzo kila mwaka kwa shule za maeneo mbalimbali
    10. Bw. Kalia anakosa kuwajibika anaposhirikiana na Mkurungenzi wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia katika kubadilisha matokeo ya mashindano ya somo la Sayansi.
    11. Wazazi wa Siri hawakutimiza ahadi waliyotoa kwa wazazi wake Jack walipofariki katika ajali ya barabarani kwamba wangemtunza Jack hadi afikie kilele cha masomo yake.
    12. Wazazi wa Siri walikuwa na uwezo wa kumpeleka Jack chuo kikuu bila ufadhili wowote lakini Bw Kalia anampoka Jack aliyefiwa na wazazi
    13. Bi. Mshewa anakosa kuwajibika anapoona Jack anaanza kuimarika katika biashara yake na kumtaka awalipe nusu ya faida ya kila mwezi.
    14. Siri anawajibika anapozungumzia uovu waliomtendea Jack katika runinga ili dunia nzima ipate kujua.
    15. Siri anatoa mshahara wake wa mwaka kufadhili Masomo ya Jack ya chuo kikuu.
    16. Jane Gatoni anawájibika anapompa Siri fursa ya kumpeperusha siri yake studioni.
    17. Jack anawajibika katika biashara yake ya kuuza viatu na kuimarika.
    18. Jack anawajibika anapowasamehe wote katika familia ya Bwana Kalia na kumshukuru Siri kwa kusema ukweli
    19. Bw. Kalia anakosa kuwajibika anapojaribu kumpigia simu Siri kumwonya asipasue mbarika na akatize mahojiano ya runinga.
    20. Jack anawajibika anapoiweka siri ya kutomwambia Bwana Kalia mpango wa Siri wa kutoa ujumbe muhimu kwa nchi nzima.

Swali 14

Fadhila za punda

“Nitapata wapi mwandani kama mkee wangu marehemu?“

  1. Eleza mukthatha wa dondoo hiili ? (alama 4)
  2. Fafanua sifa tatu za msemaji. (alama 6)
  3. Tambua na ufafanue maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
  4. Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa kwenye dondo hili. (alama 2)

Majibu

  1. Muktadha: Pastor Lee Imani akijiwazia mwenyewe baada ya kupata shinikizo la kuoa mkw mwingine baada ya kifo cha mkewe. Anaeleza kuwa hangeoa kwa kuwa hayupo anayelingana na marehemu mkewe 1x4 = 4
  2.  
    • Mcha Mungu - anaanzisha na kuendeleza kanisa
    • Mkarimu - anampa mamake Luka ajira
    • Mdadisi - Anamwita Luka na kumuuliza nia yake kwa bintiye 
    • Mwenye mapenzi - Alimpenda marehemu mkewe pia bintiye
      za kwanza 2x3=6
      Tanbihi"
      1. kadiria majibu mengine ya mwanafunzi, maelezo ya sifa yaafikiane na sifa yenyewe
      2. Akikosea msemaji katika (2a) asituzwe sehemu hii.
  3.  
    1. Ndoa na mapenzi
    2. Kifo/mauti za kwanza  2x2=4
      Alama 1 kutaja, 1 ufafanuzi wa kweli
  4.  
    1. Swali balagha
    2. Tashbihi
      za kwanza 2
      Atoleee maelezo ya kila mbinu, asipoeleza asituzwe chochote.

Swali 15

Sabina

  1. Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo; (alama 6)
    ‘Athari ya mawazo yake ilijiandika dhahiri shahiri usoni mwake. Alianza kwa kuachia tabasamu pana mithili ya msafiri aliyefika salama. Baada ya dakika chache machozi yalianza kumtoka njia mbilimbili huku kajishika tama. Alifikiria kuhusu mtihani uliodhamiriwa kuanza siku ya Jumanne. Mtihani ambao ungemwezesha kupata ufadhili katika shule ya upili ya bweni ikiwa angepita vyema. Hili ndilo wazo lililozua tabasamu. Lakini, angefeli je?Hatima yake ingekuwa ipi? Maswali haya yalimliza yakamwacha akisinasina kama mgonjwa wa mafua. Akiwa katika hali hii, aliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu, ‘‘mizizi ya elimu ni michungu ila matunda yake ni matamu. Ikiwa mnataka kuyaonja matunda ya elimu, lazima mtie bidii kwani mtaka cha mvunguni sharti ainame.”
  2. Bainisha mbinu mbili zinazoweza kutumiwa kutambua sifa za mhusika Sabina kwa kurejelea hadithi Sabina. (alama 2)
  3. Taja na ueleze aina mbili za taswira zinazojitokeza kwenye dondoo hili. (alama 2)
  4. Kwa kutolea mifano mwafaka eleza matatizo yanayomkumba mwanamke katika hadithi Sabina. (alama 10)

Majibu

  1.  
    1. Ayasemayo mhusika
    2. Matendo ya mhusika
    3. Wayasemayo wahusika wengine
    4. Maelezo ya mwandishi kuhusu mhusika mwenyewe
    5. Uhusiano wake na wahusika wengineMbinu za kimtindo
  2.  
    1. Taswira – athari kujiandika
    2. Msemo- kajishika tama
    3. Tashbihi- mithili ya msafiri
    4. Balagha- angefeli je?
    5. Mbinu rejeshi- aliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu
    6. Jazanda- mizizi ya elimu
    7. Methali- mtaka cha mvunguni sharti ainame
    8. Tashihisi- maswali yakamwacha…
    9. Takriri- mtihani, mtihani
  3. Aina za taswira kwenye kifungu
    1. Oni- usoni mwake
    2. Mwendo- msafiri aliyefika salama
    3. Hisi- kujishika tama
    4. Usikivu- alifikiria
    5. Onji- mizizi ya elimu ni michungu (Za kwanza2x1)
  4. Matatizo yanayomkumba mwanamke
    1. Mimba za mapema- Nyaboke
    2. Kukatiza masomo- Nyaboke
    3. Kufanyishwa kazi nyingi- Sabina
    4. Kukataliwa na wanaowadunga mimba- Nyaboke kukataliwa na janadume lililompachika mimba
    5. Kujukumizwa ulezi wa mapema- Nyaboke
    6. Kukatisha wazazi tamaa
    7. Kukosa malezi ya baba mzazi- Sabina
    8. Kufanya kazi za sulubu ili mtoto apate mahitaji ya kimsingi
    9. Kifo cha mzazi-Sabina
    10. Kifo cha walezi- babu na nyanyake Sabina
    11. Kutelekezwa na wanakijiji –Wanakijiji kuapa kukaa mbali naye baada ya kushuku familia hiyo imelaaniwa.
    12. Kutengwa – Sabina anatengwa na watoto wa mjomba wake (Ombati)
    13. Dhiki za kisaikolojia-Sabina anapoitwa na mwalimu mkuu
    14. Kushukiwa- mwalimu mkuu anamshuku Sabina anapinga adhabu ya kuchelewa kufika shuleni.
    15. Kuchapwa/kuteswa- Sabina anapigwa na shangazi yake.(Yunuke)
    16. Matusi- Sabina anatusiwa kiokote na Yunuke
    17. Kunyimwa vifaa vya kimsingi vya matumizi- Yunuke anamzimia Sabina kibatari alipokuwa akisoma, rinda la Sabina ni kuukuu.

Swali 16

.“...majira ya magharibi pevu, nilifika tena pale mzimuni. Kama ilivyo ada yangu , nilivaa guo jeupe lililonifunika kama maiti. Nikaangalia huku na huko, sikuona mtu. Hapo nikasogea karibu zaidi na ule mzimu. Nilipofika nikauimba ule wimbo wote. Nilipomaliza tu nikajitoma kichakani mle bila hofu wala kimeme. Mara nikajikuta nimo ndani, kiza tororo! Nikatoa tochi yangu nikaanza kumulika hukuna huko. Nilichokiona humo, sikuamini macho yangu! Mle ndani ya mzimu mlikuwa na makanda na makasha ya tumbaku, unga wa kilevi na bang ikwenye marobota. Kulikuwa na mapipa yaliyojaa chang’aa na tembo ya mnazi. Humo pia, mlikuwa na kitanda cha besera kilichotandikwa
vizuri. Juu ya kitanda hicho, palitupiwatupiwa asumini na maua ya mlangilangiyaliyonukia harufu za mahaba kuliko harufuya mapambo ya harusi ya kiharuni! Mle mvunguni mwa kitanda kile mlikuwa na chetezo kilichojaa udi wa mawaridi. Nikabaki kinywa wazi kwa bumbuazi na butwaa la uduazi! Butwaa ambalo kwa hakika lilifanya akili yangu isimame kufikiri kwa muda wa sekunde kadhaa.”

  1. Kando na taswira, tambua mbinu zingine za kimtindo katika dondoo hili. (alama 5)
  2. Ainisha taswira katika kifungu hiki. (alama 3)
  3. Chambua maudhui yanayojitikeza katika kifungu hiki. (alama 4)
  4. Eleza umuhimu wa Msimulizi katika mujibu wa hadithi husika. (alama 8)

Majibu

  1. Kando na taswira, tambua mbinu zingine za kimtindo katika dondoo hili.
    1. Tashbihi - nilivaa guo jeupe lililonifunika kama maiti.
    2. Tanakali za sauti - mara nikajikuta nimo ndani, kiza tororo!
    3. Nidaa - sikuamini macho yangu!
    4. Msemo - nikabaki kinywa wazi kwa bumbuazi na butwaa la uduazi!
    5. Utohozi - tochi
    6. Tashihisi - butwaa ambalo kwa hakika lilifanya akili yangu isimame kufikiria kwa muda wa sekunde kadhaa (alama 5)
  2. Ainisha taswira katika kifungu hiki.
    1. Taswira oni - nilichokiona humo, sikuamini macho yangu!
    2. Taswira sikivu - nikauimba ule wimbo.
    3. Taswira mnuso - yaliyonukia harufu za mahaba kuliko harufu ya harusi ya kiharuni.
    4. Taswira hisi - butwaa ambalo kwa hakika lililofanya akili yangu isimame kufikiri kwa muda sekunde kadhaa. (3x1=3)
  3. Chambua maudhui yanayojitikeza katika kifungu hiki.
    1. Utamaduni/itikadi - nilipofika nikauimba ule wimbo wote.
    2. Matumizi ya mihadarati/madawa ya kulevya - kulikuwa na mapipa yaliyojaa chang’aa na tembo ya mnazi.
    3. Anasa/uzinzi - humo pia mlikuwa na kitanda cha besera kilichotandikwa vizuri. Juu ya kitanda hicho,palitupiwatupiwa asumini na maua ya mlangilangi yaliyonukia harufu za mahaba kuliko harufu ya mapambo ya harusi ya kiharuni!
    4. Ujasiri/uwajibikaji/ufichuzi - hapo nikasogea karibuzaidi na ule mzimu. Nilipofika nikauimba uke wimbo ... (4x1=4)
  4. Eleza umuhimu wa Msimulizi kwa mujibu wa hadithi husika.
    1. Ni kielelezo cha ujasiri na umuhimu wake katika jamii.
    2. Anadhihirisha migogoro kati ya vijana na wazee hasa kuhusiana na masuala ya utamaduni.
    3. Kupitia kwake, mchango wa vijana/watoto katika kujenga na kuboresha jamii unadhihirika.
    4. Anaonyesha umuhimu wa upelelezi katika kuwafichua wahalifu miongoni mwa wanajamii.

Swali 17

Mzimu wa Kipwerere Maswali na Majibu

…akikiomba radhi kile kitawi cha mti kilichonasa kwenye kazu yake ya rangi ya udongo  iliyoficha kiwingu cha nongo kwa kukosa kuoshwa tangu ainunue! Nikauacha mpambano ule kati ya mzimu na mwenye dhamana ya mzimu ambao sina shaka ulidumu hadi asubuhi pale wanakijiji walipofika kushuhudia siri nzito iliyomezwa na mzimu ule waliokuwa wakiogopa na kuamini kiasi cha kuabudu kwa unyenyekevu na uchaji uliotukuka!
  1. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
  2. Fafanua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili. (alama 4)
  3. Fafanua mbinu za kimtindo katika dondoo. (alama 4)
  4. Onyesha jinsi itikadi ilivyomwezesha ‘mwenye dhamana ya mizimu’ na wenzake kuwafanya wanakijiji kuogopa na kuamini mzimu wa Kipwerere kiasi cha kuabudu kwa unyenyekevu na uchaji uliotukuka. (alama 8)

Majibu

  1. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
    1. Ni maneno ya msimulizi
    2. Anamrejelea Salihina
    3. Walikuwa katika Mzimu wa Kipwerere
    4. Msimulizi alikuwa amewafumania Bishoo na Salihina katika mzimu na wakati Salihina alipokuwa akitoroka akashikwa na kitawi cha mti hivyo akapiga mayowe akiomba msamaha. 4 x 1 = 4
  2. Fafanua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili. (alama 4)
    1. Kubainisha mgogoro katika hadithi – mgogoro uliopo unaotokana na itikadi unaotumiwa na kina Salihina kuwalaghai wanakijiji.
    2. Kuwatambulisha wahusika: Salihina na Bishoo
    3. Kuchimuza maudhui: unafiki – Salihina anajifanya kuwa mdumishaji wa maadili ilhali yeye ndiye alikuwa akilangua dawa za kulevya.
    4. Kutambulisha sifa za wahusika: Bishoo anabainika kuwa mwongo kwa kuwa anamdanganya mumewe kuwa alikuwa akienda kumwona mtoto mgonjwa ilhali alikuwa anaenda kwa Salihina.
    5. Kuibua dhamira ya mwandishi: Kuonyesha madhara ya ushirikina na itikadi: imani kuhusu Mzimu wa Kipwerere unawatia wanajamii hofu ilhali hakukuwa na mizimu au mashetani yoyote katika kichaka hicho.
    6. Kuendeleza ploti – kusuluhisha taharuki kuhusu kuwepo kwa mashetani katika mzimu kwa kuonyesha kuwa hakukuwa na shetani yeyote ila wajanja kama kina Salihina. Zozote 4 x 1 = 4
  3. Fafanua mbinu za kimtindo katika dondoo. (alama 4)
    1. Tashihisi/uhaishaji - akikiomba radhi kile kitawi cha mti
    2. Taswira - kilichonasa kwenye kazu yake ya rangi ya udongo iliyoficha kiwingu cha nongo kwa kukosa kuoshwa tangu
    3. Nidaa - ainunue! uliotukuka!
    4. Kejeli - Nikauacha mpambano ule kati ya mzimu na mwenye dhamana ya mzimu
  4. Onyesha jinsi itikadi ilivyomwezesha ‘mwenye dhamana ya mizimu’ na wenzake kuwafanya wanakijiji kuogopa na kuamini Mzimu wa Kipwerere kiasi cha kuabudu kwa unyenyekevu na uchaji uliotukuka. (alama 8)
    1. Kuna itikadi kuhusu chanzo cha kichaka cha Mzimu wa Kipwerere – inaaminika kuwa kichaka hicho kilitokana na kaburi la mwanamke aliyeitwa Kipwerere.
    2. Inaaminika kuwa yeyote aliyekiuka miiko kuhusu kutoingia katika mzimu angetolewa kama kafara kwa mizimu.
    3. Wanajamii wa eneo la Mzimu wa Kipwerere wanaamini kuwa Salihina angeweza kuwasiliana na mizimu. Hivyo, wanapotaka kuandaa sherehe kama vile jando wanamtuma Salihina kuzungumza na mizimu.
    4. Wanajamii wa eneo la Kipwerere kutoruhusiwa kupita kichaka hicho saa sita mchana na usiku wote. Wanajamii hawakupewa sababu zenye mashiko za kuwanyima ruhusa ya kupitia kichaka hicho bali walitishiwa tu kuwa wangetolewa kama kafara kwa mzimu.
    5. Kuamini kwamba taa zilizowaka usiku katika Mzimu wa Kipwerere ziliwashwa na shetani wa mzimu ili kuwapa watoto wake chakula.
    6. Kuamini kwamba mwanamke na mwanamume waliozungumza walikuwa shetani na mkewe. Inadaiwa kuwa waliungumza wakati watoto wao walikuwa wamelala.
    7. Mashetani wanavuta sigara - Kuamini kwamba harufu ya sigara iliyotoka katika mzimu ilitokana na shetani aliyekuwa akivuta sigara.
    8. Kuamini kwamba kulikuwa na wimbo uliokuwa kama ufunguo wa kuingia katika mzimu.

Swali 18

“Mike! Mike! Mike! Njoo! Nilijua utafanya vyema mwanangu…”

  1. Tambua na ueleze toni ya dondoo hili. (alama 2)
  2. Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Eleza sifa nne za msemaji wa dondoo hili. (alama 4)
  4. Eleza mbinu mbili ulizozitumia kutambua sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 4)
  5. Tambua na ufafanue madhila yanayomsakama mhusika mkuu katika hadithi hii ya “Sabina”. (alama 8)

Majibu

  1. Tambua na ueleze toni ya dondoo hili. (al 2)
    • Toni ya furaha- Ombati anamwita mwanawe Mike kushangilia matokeo ya mtihani akidhani ni yake.
  2. Changanua mtindo katika dondoo hili. (al 2)
    • Nidaa- mike!
    • Mdokezo-mwanangu…
  3. Eleza sifa nne za msemaji wa dondoo hili. (al 4)
    • Ni mwenye tamaa. Ananuia kujinufaisha kutoka kwa dadake kupitia kwa mahari yake. Anapoyakosa, anaamua kutumia bintiye, Sabina, kwa kumwoza baada ya darasa la nane ili kupata mifugo.
    • Ni mtamaduni. Anaendeleza mifumo ya kijamii kama vile ubidhaaishaji wa wanawake. Anataka kupata mahari kupitia kwa Nyaboke na anapoyakosa, anaamua kumwoza bintiye, Sabina, katika umri mchanga na kumwandalia sherehe. Anasemekana kumlaani Nyaboke kwa kumkosesha mahari.
    • Ni kigeugeu. Maripota wanapofika kumhoji Sabina, anaungana naye huku akijisifia jinsi alivyomlea na alivyo mwerevu, licha ya kuwa awali anamtelekeza. Anawafukuza waliokuja kumposa Sabina na mifugo wao.
    • Ni mwongo/mzandiki/mnafiki. Anamhadaa mwalimu mkuu kuwa Sabina anapata muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya mtihani. Anadanganya kuwa Sabina anapenda kazi za shambani hali analazimishwa.
    • Msaliti- anaisaliti jamaa yake kwa kumwacha Yunuke kumtesa mwana wa dadake Nyaboke.
    • Mbaguzi- anabagua kati ya wana wake na mtoto wa dadake Sabina. Sabina anatumikizwa huku wanawe wakikaa starehe.
  4. Eleza mbinu mbili ulizozitumia kutambua sifa za msemaji wa dondoo hili. (al 4)
    • Usawiri wa mwandishi
    • Maneno ya wahusika wengine
    • Maneno yake mwenyewe
    • Matendo yake kwa wahusika wengine
  5. Tambua na ufafanue madhila yanayomsakama mhusika mkuu katika hadithi hii ya “Sabina”. (al 8)
    • Kufiwa na mamake Nyaboke na kuachwa mikononi mwa babu na nyaya yake.
    • Babu na nyanyake kufariki akiwa darasa la tano. Hili linamfanya achukuliwe na mjaombake Ombati na Yunuke.
    • Alitumikizwa sana nyumbani kwa mjombake ambako alifanya kazi za kila nui.
    • Anapokea kichapo kutoka kwa Yunuke baada ya kuchelewa kutoka shuleni.
    • Anatusiwa sana Yunuke. Anaitwa baradhuli, kiokote,mjalaana n.k.
    • Kusingiziwa. Subira anasingiziwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume Fulani.
    • Kubaguliwa. Binamu zake wanasomea shule za bweni huku yeye akisomea shule ya kutwa.
    • Kunyimwa nafasi ya kudurusu. Yunuke anazima kibatiri hivyo kumnyima Sabina nafasi ya kumalizia kusoma alichokuwa amebakisha.
    • Kuozwa.mjombake Ombati anapanga kumuoza kwa kijana mwendesha pikipiki hivyo kuzima ndoto yake ya kuemdelea na masomo.
    • Kupuuzwa- yunuke na Ombati waliziona juhudi zake masomoni kama za bure.
    • Kukosa malezi ya wazazi wote. Babake anamringa mimba mamake Nyaboke na kumtoroka.

Swali 19

“Poko! Ukiumwa na nyuki haina haja ya kujitwika jukumu la kuharibu mizinga yote ya asali. Hujui faida ya nyuki ulimwenguni? Uliamua kurina asali ya nchi.”

  1.  
    1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
    2. Tambua tamathali mbili za usemi zilizotumika katika dondoo hili. (alama 2)
    3. Onyesha matokeo ya kuharibu mizinga yote ya asali ukirejelea hadithi Mapambazuko ya Machweo.
  2. Jadili maudhui ya ukiukaji wa haki za watoto katika hadithi ya; 
    1. Mapambazuko ya Machweo   (alama 10)
    2. Sabina  (alama 10)

Majibu

  1.  
    1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
      • Maneno ya Makucha kwa Makutwa mgodini baada ya MAkutwa kukamatwa kwa kosa kufuja raslimali ya nchi.
    2. Tambua tamathali tatu za usemi zilizotumika katika dondoo hili. (alama 2) 
      • Taswira fiche. Ukiumwa na nyuki-kuajibishwa kwa kuhujumu uchumi wa nchi. Dhihaka. kujitwika jukumu la kuharibu mizinga yote ya asali.
      • Jazanda. Uliamua kurina asali ya nchi - kuhujumu uchumi wa nchi
    3. Onyesha matokeo ya kuharibu mizinga yote ya asali ukirejelea hadithi Mapambazuko ya Machweo.    (alama 7)
      • Makutwa anafanya biashara ya kimagendo ya kuchimba vito katika mgodi kisiri. Hii ni raslimali ya serikali ambayo mtu anafaa kupata leseni ya kuchimba
      • Ukoloni Mamboleo. Mzee Makutwa anawasomba ijana kwenda kuwafanyisha kazi ya kusaka vito vya thamani katika mgodi wake. Wanafanya kazi hii katika mazingira mabovu na kufungiwa mle ndani, wasiwe na nafasi ya kutokea.
      • Makutwa analipoka taifa nguzo yake muhimu kwa kuwachukua vijana mabarobaro na kwenda kuwatumikisha katika mgodi wake. Vijana hawa wanafaa kuwa wakiendesha shughuli nyingine muhimu za kujenga jamii.
      • Ajira ya watoto. Vijana kadhaa, ikiwemo watoto wadogo wanafanya kazi ya kudondoa vijiwe vidogovidogo vinavyong'aa. Wanasimamiwa na wanyapara wanaowaamrisha kwa sauti za kutisha.
      • Mazingira mabovu ya utendakazi. Vijana mgodini wanakumbwa na hali ngumu ya kimaisha, kwani huko wanakoishi hakuna hali nzuri. Hewa si safi na kazi wafanyazo ni za sulubu.
      • Ukosefu wa ajira. Sai na Dai pia wanawakilisha hali ya vijana ambao baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, hawajapata kazi wala hawana matuamini. Wanashinda kuzurura mitaani.
      • Wafanyakazi kutimuliwa bila fidia. Mzee Makucha anafanya kazi na shirika la reli ambalo linamtimua kwa ajili ya kupunguza idadi ya wafanyakazi wake. Baadaye linasambaratika, hivyo anakosa marupurupu yake.
      • Umaskini. Mzee Makucha anaanguka kwenye lindi la umaskini baada ya kuachishwa kazi katika shirika la reli bila marupurupu, kwani shirika hilo linasambaratika pia.
      • Kazi duni. Makucha analazimika kuchuuza vitafunio kando ya barabara kujipatia riziki. Mkewe naye anauza kaimati na vitumbua kwenye veranda ya nyumba yao.
      • Kukimbilia ndoa. Riziki, anawatoroka wazaziwe na kuolewa na Mhindi ili kuepuka urumo.
  2.  
    1.  
      1. Haki ya kuishi/ jasho- hakuna hewa mgodini
      2. Ajira ya watoto- watoto wadogo na vijana kuchimba mchanga na kusomba kwa mikokoteni.
      3. Afya – hakuna miale ya jua kwenye mgodi
      4. Kutishwa na wanyapara- walinzi katili
      5. Mazingira duni
      6. Kuchimba gizani- taa za vibatari
      7. Kulala kwenye mabanda
      8. Kutoruhusiwa kuondoka- walinzi wakali, mbwa wakubwa na nyua za stima
      9. Kukatiziwa masomo- vijana na watoto wadogo
      10. Wanakusanywa barabarani kwa probox ya Makutwa
      11. Kufanywa kuwa watumwa- Sai na Dai
    2. Sabina
      1. Kunyimwa haki ya kusoma- anaambiwa anaharibu mafuta na Yunuke
      2. Kukatiziwa masomo- Nyaboke kuacha shule katika kidato cha pili
      3. Ndoa za mapema – Nyaboke kukataa posa za wanaume/ Sabina kuozwa siku ya kutangaza matokeo
      4. Kufanywa mtumwa- kazi zinazozidi umri wa Sabina/ miaka 14
      5. Mavazi kuu kuu- Sabina kutoka shambani akiwa na rinda kuu kuu
      6. Mateso- matusi ya Yunuke, kumzimia taa, kumkashifu kwa kutouuza maziwa Itumbe
      7. Kuchelewa kufika shule- anafika saa tatu na nusu
      8. Kudhalilishwa – kukama ng’ombe, kuwapeleka malishoni, kuzoa kisonzo, kuuza maziwa asubuhi,kuandaa chajio, kuwafunga ng’ombe zizini
      9. Kutolindwa dhidi ya hatari – watu kuambaa familia ya Nyaboke/ laana
      10. Kudharauliwa na binamu zake Sabina/ Mike ndiye anambebea vitabu wakiwa malishoni.
      11. Kujaribu kumnyima bahati kwa kumwita Mike kuhojiwa na wanahabari.

Swali 20

Siku moja alipokataa katakata kuandamana na mumewe, jungu lilifoka. “Wewe mke sampuli gani usiyetaka kumuunga mkono mmeo?” Haya kaa nyumbani. Kula na kulala tu, hujui jingine. Ona umbo lako sasa, kama nguruwe. Si mke mrembo niliyeoa! Wanawake ni wengi…”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Bainisha vipengele vinne vya kimtindo katika dondoo hili (alama 4)
  3. Fafanua nafasi ya mwanamke katika hadithi hii. (alama 12)

Majibu

  1.  
    1. msemaji ni Luka
    2. msemewa ni Lilia
    3. nyumbani kwao
    4. Luka alimtaka mkewe kuandamana naye katika kampeni – taswira ya kiongozi anayethamini ndoa na familia ili achaguliwe kuwa gavana, (alama 4x1)
  2.  
    1. Balagha – wewe mke sapuli gani?
    2. Nahau = katakata, unga mkono
    3. Taswira – ona sasa
    4. Tashbiha – kama nguruwe
    5. Masimango – kama nguruwe
    6. Nidaa – niliyeoa!
    7. Mdokezo – wengi…
  3. Fadhila za punda
    1. Mwanamke kutawishwa- lilia anaachishwa kazi ya umeneja na mwishowe kutawishwa.
    2. kukaa nyumbani na kutishwa asidhubutu kutoka nje ya lango.
    3. Mwanamke anatishiwa – Lilia anapodhubutu kumshtaki mumewe anakumbushwa kuwa yeye ndiye Gavana na ana uwezo wa kufanya haki kuwa batili na batili kuwa haki.Utajua kichomtoa kanga manyoya.
    4. Mwanamke anapokezwa kichapo cha mbwa-  Lilia anapokea mapigo kutoka kwa mumewe anapoenda kuripoti kwa polisi.
    5. Mwanamke kutusiwa-  Lilia anaambiwa amenona kama nguruwe.
    6. Mwanamke kudhalilishwa-  Lilia annambiwa kuwa ana umbo kama nguruwe kwani kazi yake ni kula na kulala tu.
    7. Mwanamke kuendewa kinyume na mumewe katika ndoa-  Luka anasemekana kuwa na kiruka njia ambaye waliandamana naye kila mahali. Lilia anapouliza ni nani anapokea kipigo kinachomlaza kitandani siku mbili.
    8. Kuachishwa kazi. Lilia anaachishwa kazi na mumewe ili awe mpokezi wa wageni nyumbani.
    9. Ni chombo cha starehe-
    10. Wasaliti – kunyanganywa bwana
    11. Kunyimwa uhuru wa kutangamana
    12. Kutohusishwa katika maamuzi ya familia
    13. Mwajibikaji – mamake gavana
    14. Mwaminifu – Lilia kwa mumewe
    15. Mwenye mapenzi ya dhati-  Lilia
    16. Mvumilivu- Lilia na mavya wake
Join our whatsapp group for latest updates

Download Maswali na Majibu ya Dondoo Katika Mapambazuko ya Machweo.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?