0 votes
4.9k views
in Chozi la Heri by

Tathmini umuhimu wa mbinu zifuatazo katika kuijenga riwaya ya Chozi la Heri

  • Barua

1 Answer

0 votes
by
  1.  Barua ya Lunga
    • Barua ya kustaafishwa kwa Lunga inaonyesha dhuluma kwa wafanyikazi. Lunga anafutwa kwa kutetea wanyonge dhidi ya kuuziwa mahindi hatari kwa afya.
    • Inaonyesha uadilifu wa Lunga anavyosema Afisa Mkuu Mtendaji
    • Inakashifu ukatili wa waajiri – Lunga anafutwa bila hali yake kuwaziwa
    • Inaonyesha mbinu-hasi za uongozi – Viongozi wanawaangamiza wanaowapinga njama zao za kiufisadi.
    • Kuonyesha uongo/ unafiki wa waajiri- kusingizia kuwa shirika linapunguza wafanyikazi kutokana na changamoto za kifedha kutokana na gharama ya uzalishaji mali ilhali Lunga anafutwa kwa kukashifu kutaka kuuza mahindi yaliyoharibika. (hoja 5)
  2. Barua ya Subira
    • Inaonyesha ukosefu wa uwajibikaji wa Subira – anaondoka bila kuwazia hali ya baadaye ya watoto wake.
    • Inadokeza maudhui ya malezi – Subira anamuusia Mwanaheri amtunze mnuna wake na pia wamtii baba yao.
    • Inakashifu ubaguzi – Subira analalamikia kubaguliwa na mavyaa Inaonyesha uwajibikaji wa mzazi kwa watoto wake japo Subira anaondoka anawaachia wanawe ujumbe kwamba ameondoka na kuwashauri
    • Anakashifu ukiukaji wa haki za kibinadamu – anasimangwa na kuitwa mwizi.
    • Inajenga tabia ya wahusika – imesawiri udhaifu wa nia wa Kaizari. Hamtetei mkewe dhidi ya dhuluma ya mavyaa. Inakuza ukatili wa mavyaa kwa kumwita muuki na mwizi.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...