0 votes
783 views
in Chozi la Heri by
“Haidhuru kuwa huenda wimbo huu unawaghasi waliolala. Atakalo mwimbaji huyu ni kutakasa hisia zake.” Bainisha jinsi mrejelewa alivyotakasa hisia zake kwenye wimbo wake kwa mifano mwafaka.

1 Answer

0 votes
by
  1. Ulevi kumpa utulivu uliosababishwa na kuwepo kwa shinikizo kutoka kwa wenye uwezo- Majabali (uk. 129) ulevi kwake ni suluhisho la kuyakimbia matatizo.
  2. Kubaguliwa na mahasidi wenye uwezo/tabaka la juu kumbagua.
  3. Kuchekwa na matajiri wakiwa kwenye roshani za nyumba zao. Walikuwa wamekula na kushiba (uk. 130) Wanamkejeli kwa kumuita Bwana Dengelua.
  4. Watu wanamkejeli tu pasi na kutaka kujua ni nini kilichosababisha uraibu wake wa pombe.
  5. Kutwaliwa kwa shamba lao la asili na Bwana Mabavu ambaye anahalalisha wizi huo kwa hatimiliki bandia. Wao walishindwa kumpinga (uk. 131)
  6. Ananwonea babake huruma kwa kumenyeka kwa kazi za sulubu ili apate riziki na karo.
  7. Yeye alifanya bidii chuoni ili kuivua aila yake kutoka kwenye umaskini. Alipohitimu alikosa kazi.
  8. Nafasi za kazi zilitolewa kwa mapendeleo ya kinasaba. (uk. 133)
  9. Kazi aliyoipata ni duni – ya kufutia mchozi na mshahara wake ulikuwa mdogo. (uk. 133)
  10. Wanapodai nyongeza ya mshahara, mwajiri wao anawarejelea kama 'unskilled labourers' hivyo waridhike na mshahara duni waupatao.
  11. Walipoandamana kuomba wafikiriwe kama wataalamu wengine kazini na kutaka wapandishwe cheo, walifukuzwa walikokaa mabandani na kufutwa kazi.
  12. Babake Shamsi kufanya kazi ya sulubu hata katika umri wake mpevu bila kuonewa imani na mwajiri wake. (uk. 131)
  13. Babake 'anaaga dunia kwa njaa - alilazimika kula vijasumu vilivyomuua.
  14. Mfumo duni wa afya- hamna hospitali pale kijijini. Babake alikosa matibabu ya dharura hivyo kuaga dunia.
  15. Wanaomcheka kutokana na ulemavu wa mali, bila shaka hata nao yatawafika.
  16. Chakula kinapatikana kwa taabu. Shamsi ana matumaini kuwa Bi. Halua ameambulia kibaba cha unga kutokana na ujira mdogo.(uk.135)
  17. Kuna watu wanaomsifu kwa kuwa wa kwanza kuhitimu masomoni na hivyo kuwa mwanga wa jamii- hilo halikutimia.
  18. Ndoto zake za ujana zimezimwa na watu waliomzidishia umaskini. (uk. 137)
  19. Anabahatika hakupofuka wala kufa kutokana na unywaji wa pombe haramu kama wenzake.
  20. Wagema kuitia pombe haramu vijasumu ili iive haraka- matokeo yake ni upofu na vifo. Shamsi anawalaumu kwa hilo.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...