0 votes
1.6k views
in Chozi la Heri by
Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika. Tetea kauli hii ukilejelea Chozi la Heri

1 Answer

0 votes
by
  1. Subira alitengwa na familia ya mume wake kwa kuwa wa kabila tofauti na lao
  2. Mwanaheri anatueleza kuwa mama yake alikuwa ametoka kwenye jamii ya mamwezi lakini babake alikuwa wa jamii tofauti. Kila mara subira aliitwa ‘muki’ au huyo wa kuja
  3. Kijana mmoja alimwita Ridhaa mfuata mvua jambo lilimuumiza sana Ridhaa.
  4. Mzee kendi alimtendea udhalimu Ridhaa na kuiteketeza aila yake licha ya wao kuwa majirani kwa miaka hamsini. Ridhaa alifanyiwa hivi kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye kabila tofauti na mzee kendi.
  5. Ndoa ya Selume ilisambaratika baada ya vita vya kutawazwa kwa kiongozi mpya.kuoa msichana wa kikwao.
  6. Tulia alimsaidia kaizari kufunganya na kumsidikiza hadi njia panda. Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi Mungu ndiye hupanga na nguvu na mamlaka pia hutoka kwake
  7. Uongozi mpya umezua uhasama kati ya koo ambazo zimeishi kwa amani kwa karibu karne moja.
  8. Subira aliweza kuvumilia kubaguliwa, kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyoyatenda, Mwishowe alihiari kujiondokea na kwenda mjini alikojinywea kinywaji kikali. 
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...