0 votes
1.4k views
in Chozi la Heri by
  1. "Mara moyo unaanza kumwenda mbio na vipapasio vya akili yake kusimama wima. Anajihisi kama anayetarajia kuanza kinyang'anyiro kikali cha upiganaji masumbwi. Kwa mbali anasikia mbisho hafifu ... Anatoka nje kwenda kuitikia mbisho huu ... Mara anasikia moyo wake ukimwambia, "Yako ya arobaini imefika," ...
    • Eleza muktadha wa dondoo hili.  
    • Jadili aina mbili za taswira katika dondoo hili.     
    • Bainisha vipengele vingine vinne vya kimtindo katika dondoo hili.     
  2. Jadili umuhimu wa mandhari katika kuijenga riwaya hii kwa kurejelea kituo cha afya cha Mwanzo Mpya. 

1 Answer

0 votes
by
  1.  
    •  
      • Haya ni maneno ya msimulizi✓/mwandishi
      • Yanamhusu Sauna✓.
      • Sauna yumo nyumbani✓ mwa Bi. Kangara.
      • Anahisi anakabiliwa na hatari✓ fulani ndipo moyo unamwenda mbio
      • Anapofungua lango anakumbana na polisi ana kwa ana
        (Dondoo limetolewa uk.153) 
    •  
      • Taswira hisi - anahisi/kikali
      • Mwendo - anatoka nje, moyo kumwenda mbio,kusimama.
      • Usikivu - mbisho hafifu/anasikia
      • Mguso - vipapasio 
    •  
      • Tashbihi - anajihisi kama anayetarajia kuwa na kinyang'anyiro cha upiganaji masumbwi.
      • Tashihisi - kusimama kwa vipapasio vya akili/ moyo ukimwambia.
      • Mdokezo /sehemu wa methali -yake ya arobaini imefika.
      • Kutumia usimulizi wa wakati uliopo- mara anasikia.
      • Nahau/msemo - kumwenda mbio.
      • Taashira - vipapasio, moyo kumwenda mbio
      • mdokezo wa kauli - hafifu .....imefika
  2.  
    • Kuonyesha changamoto zinaz kumba hospitali za umma. Selume anshangaa namna alivyoweza kustahili matatizo✓ kama vile ukosefu wa glavu hospitalini.
    • Kuangazia swala la ufisadi. Dawa✓ zilizotengewa hospitali zinauzwa na wasimamizi wa hospitali. (uk. 140). Ruzuku kutolewa kwa wasiostahili.
    • Kuonyesha ukosefu wa uwajibikaji wa wasimamizi wa taasisi✓ za umma. Hospitali haijalipa umeme. (uk. 140)
    • Kuendeleza ploti - kupitia sadfa. kituo kinakamilika wakati ambao Selume anajiuzulu; anapataka kazi✓, na mkondo wa matukio kubadilika.
    • Kuonyesha migogoro✓ inayosababishwa na tamaa ya rasilimali. Mgonjwa analemazwa katika mapigano ya kung'ang'ania ardhi. (uk 141).
    • Kujenga tabia✓ za wahusika. Kwa mfano,utu wa Ridhaa. anaanzisha kituo cha afya na kuwapa ajira Selume na Kaizari.
    • Kuonyesha athari za matumizi mabaya ya vileo✓.mwanafunzi anakufa kutokana na pombe haramu. (uk. 142).
    • Kuonyesha ukengeushi✓ . Wasomi wanashindwa kukabiliana na  matatizo/changamoto wanatumia mbinu hasi ili kujisahaulisha na hali ya duni.(uk 142).
    • Kuangazia changamoto zinazokumba sekta ya elimu✓. Halmashauri ya mikopo kutotosheleza mahitaji ya wanafunzi.
    • Kuonyesha umuhimu wa mshikamano✓ wa kifamilia katika maisha ya watoto. Kipanga anaingilia matumizi mabaya ya vileo kwa kukataliwa na aliyedhani ndiye babake.
    • Kuonyesha athari za kufuata mila✓ zinazorudisha nyuma maendeleo ya kijamii. Tuama anakasirika kwa kupashwa tohara.
    • Kuangazia swala la ukiukaji wa haki✓ za watoto. Mama yake Pete kutoshughulika kutambua kwamba binti yake amekua na mahitaji yake yamebadilika.
    • Kuonyesha jukumu la jamii katika kuwarithisha vijana mbinuishi. mwanzo mpya inawapa vijana kama vile Kipanga huduma za ushauri✓ nasaha unaosaidia kubadilisha tabia.
    • Kuangazia uozo✓ wa jamii. Uavyaji mimba - Pete anajaribu kuavya mimba.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...