0 votes
2.2k views
in Chozi la Heri by

“…Nimeonja shubiri ya kuwa mtegemezi kihali na mali.lakini katika yote hayo, nimejifunza mengi…”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili 
  2. Bainisha tamathali ya usemi inayojitokeza katika kauli hii. 
  3. Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kumrejelea mzungumzaji. 

1 Answer

0 votes
by
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili 
    • maneno ya Ridhaa
    • akimwambie mwanawe Mwangeka
    • wamo kwenye nyumba yao iliyochomwa
    • anamwelezea dhiki ambazo amepitia tangu ghasia za baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya kuzuka.
  2. Bainisha tamathali ya usemi inayojitokeza katika kauli hii. 
    • msemo/nahau-onja shubiri 
  3. Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kumrejelea mzungumzaji. 
    • Kubomolewa kwa nyumba mtaani Tononokeni bila kufidiwa
    • Kutapeliwa na raia wenzake fisadi wanaomuuzia ardhi katika eneo lililotengewa ujenzi wa barabara
    • Kuchomekewa na nyumba-jengo lake la kibiashara linachomeka kutokana na hitilafu ya moto
    • Kufiwa na familia yake katika moto, Mzee Kedi anafariki, hata nduguye Makaa anachomeka katika mkasa wa moto.
    • Kuitwa mfuata mvua akiwa shuleni kwa sababu ya kuwa mwanafunzi mlowezi katika eneo la msitu wa Heri
    • Kutengwa mchezoni akiwa shuleni
    • Kusimangwa na wanafunzi wenzake
    • Kusingiziwa wizi wa kalamu
    • Kubakwa kwa wapwake Lime na Mwanaheri wanapovamiwa na wahuni
    • Dadake Subira anavamiwa na wahuni na kukatwa kwa sime
    • Kula mizizi-mwitu kwa kukosa chakula katika kambi ya wakimbizi
    • Kuugua shinikizo la damu baada ya kupoteza aila yake. 
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...