0 votes
2.3k views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by

Eleza maudhui yafuatayo kama yalivyojitokeza katika hadithi ya Mame Bakari

  1. Uwajibikaji 
  2. Ukatili

1 Answer

0 votes
by
  1. Uwajibikaji 
    • Beluwa anawajibika katika kazi yake anapomwagiza Sara kwenda hospitalini kupimwa akiwa na ujauzito wa miezi sita. Sara anawajibika anapotunga mimba, ingawa alikuwa amebakwa, hakuavya mimba ila aliamua kuilea. Wazazi wa Sara wanapojua kuwa ana ujauzito, waliwajibika kwa mtunza vyema n ahata baada ya kujifungua wanamfanyia sherehe.    
  2. Ukatili 
    • Lile janadume bakaji lilikuwa na tabia ya kuwanajisi wasichana wadogo kama vile Sara. Sara alihofia kuwaeleza wazazi hali yake kwa kuhofia ukatili wa baba yake ambaye angemfurusha nyumbani iwapo angegundua ujauzito wa Sara. Umati unampiga yule mbakaji kwa hasira hadi kifo  
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...