0 votes
2.5k views
in Kigogo by
Utawala wa jimbo la Sagamoyo umejaa sumu ya nyoka.”Jadili usemi huu.

1 Answer

0 votes
by
  1. Unyakuzi wa ardhi. Majoka na mshauri wake wajitwalia eneo la soko la chapakazi ili wajenge hoteli ya kitalii jambo hili linasababisha madhara makubwa kwa wananchi waliokuwa wakitegemea soko hii kukimu familia zao.
  2. Mauaji ya watu : vijana watano wanauwawa wakati wa maandamano na wengine wanaumia.
  3. Kuna vitisho. Wanaharakati wanaopinga utawala wa majoka wanatishwa, kuna vikaratasi vinavyo rushwa katika makazi yao ili wahame.
  4. Kuangamiza wapinzani wake; Jabali aliuwawa kwa njama za Majoka na chama chake kikasambaratika . Tunu kiongozi wa wanaharakati wa kudai haki nusura auawe. Yule aliyetumwa kutekeleza mauaji yake hakutimiza lengo lake.
  5. Ukosefu wa utu. Majoka hadhamini utu/uhai wa mtu. Majoka anaamlisha watu wapigwe risasi bila kujali kuwa wana haki ya kuchagua viongozi wanaotaka.
  6. Tengatawala: katika jimbo la Sagamoyo kuna sumu ya nyoka: yaani uhasama unapendwa na viongozi ili kuwagawa wananchi kwa mfano Sudi ana uhasama na Boza ambaye ni mchonga vinyango mwenzake . Sababu ya uhasama wao ni kwa kuwako katika milengo tofauti ya kisiasa. Aidha , Ngurumo na kundi lake la walevi tayari wameshatiwa sumu na utawala wa majoka, hivyo wanahasimu wanaharakati, Tunu na sudi.
  7. Kuzorota kwa maendeleo. Jimbo la sagamoyo limetimiza miaka sitini ya uhuru lakini bado liko nyuma kimaendeleo.
  8. Rushwa: Mamapima anatoa hongo ya uronda kwa Ngurumo ili apate mladi wa kukata keki ya Uhuru. Vilevile Boza na kombe wanapokea kipande cha keki kutoka kwa Kenga ili wawe wafuasi wa utawala wa majoka vivyo hivyo kwa ngurumo , ukataji wa miti.
    • utakaji wa miti
    • kufunga soko
    • Kubomoa viosiki
    • Kuongeza kodi
    • Kutoa kibali cha kuuza pombe haramu
  9. Mapendeleo Mama pima anapewa mradi wa kuoka keki.
  10. Uzalishaji wa dawa za kulevya
  11. Ukwame wa majoka kwa kunyemelea Ashwa.
  12. Anasa ya Husda kwa kujipondoa
  13. Kutozingatia usafi wa soko/maziangira
  14. Ukabila: Siti na kombe wanapata vijikaratasi wahame Sagamoyo.
  15. Kudorora kwa kiwango cha ellimu ; Wanafunzi wa majoka academy wamekuwa makabeji.
  16. Matumizi ya vyombo vya usalama /askari/polisi kuzima maandamano
  17. Kudhibiti vyombo dola na kuweka watu kwa seli bila hatia.
  18. Matumizi mabaya ya raslimali/mikopo. 
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...