0 votes
923 views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by
Jadili matatizo yanayowakumba wakazi wa madongoporomoka katika Tumbo Lisiloshiba.

1 Answer

0 votes
by
  1. Wanamadongoporomoka wanadharauliwa na kutwaliwa ardhi yao.
  2. Kuporwa aridhi yao imenyanyaswa na tabaka la mabwanyenye.
  3. Wanawatoa katika ardhi yao na kuvunja vibanda vyao pasipo hata kuwalipa fidia.
  4. Unyanyasaji huu unafanywa kwa wakazi hawa kwa kuwa hawana mtetezi.Haki imenunuliwa na wenye nacho.
  5. Wanabomolewa vibanda vyao ilhali hawajaonyeshwa mahali mbadala pa kweda kuishi.
  6. Ukosefu wa haki: Watu wa mandogoporomoka hawana haki wenye fedha wanawaona wakazi hawa kama takataka tu.
  7. Ardhi ya madongoporomoka inaponyakuliwa na wenye nacho wanashindwa kupata mtetezi . wanasheria wamenunuliwa na matajiri ni vigumu kupata mwanasheria mwaminifu. Mzee Mago anashauriana na wenzake namna ya kurukaviunzi hivi vya kisheira.
  8. Makazi duni : Wakazi wamadongoporomoka wanaishi katika makazi yenye mandhari chafu. Kulikuwa na mashonde ya vinyesi.Wanaishi katika vibandachwara vinavyozungukwa na uozona bubujiko la maji machafu. Hakuna mamlaka yoyote ya maji taka inayojishughulisha nao.
  9. Wakazi madogoporomoka wananyimwa fidia inayolingana na thamakni ya makazi yao yaliyopokonywa na mambwanyenye.
  10. Watu wa madongoporomoka wanaachwa njaa baada ya jitu kubwa kula chakula chote . Jitu linaingia katika mkahawa mshenzi na kuagiza kila chakula kilichopo kiletwe . jibu linabugia chote huku watu waliokuwa wamesubiri chakula hicho wakibakia njaa.
  11. Wakazi wa madongoporomoka wanabaguliwa sehemu wanaoishi hakuna maendeleo yoyote kuna uchafu mwingi sana sehemu hii ilipaswa kusafishwa ili walau ifafanane na sehemu nyingine za mji ho.
  12. Wanamadongoporomoka wamekosa usalama. Wanaishi kwa wasiwasi sana. Wanaamshwa kwa vishindo vya mabuldoza .
  13. Askari wa baraza la mji wanaangusha vibanda vyao na kuwatimua waliokuwa bado wamelala. Jeshi la polisi linawapa ulizi askari kwa mirau na bunduki Mali zao duni zinaharibiwa.
  14. Wanadongoporomoka wanalia na kulalamika kwa kukandamizwa na vyombo vya ulinzi. Wanakandamizwa kwa sababu ya umaskini wao . Matajiri wanawakandamiza.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...